OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
Wakati wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania nafasi ya urais ikifika 32, mwasisi wa chama hicho, Balozi Job Lusinde amesema wimbi hilo ni ishara ya kupanuka kwa demokrasia, huku akisema Lowassa ni mtu safi na anayefaa kwa wakati huu...
Akizungumza jana katika mahojiano maalum na gazeti hili, Balozi Lusinde alisema kada huyo wa CCM ni kiongozi mchapakazi na mwadilifu... Alisema watu wanaopita katika maeneo mbalimbali nchini na kuchafua wagombea wengine wanastahili kuchukuliwa hatua kali sana, kwani tabia hiyo si nzuri...
"Ni Lowassa huyu huyu aliyefutilia mbali mkataba wa City Water baada ya kubaini ni wadanganyifu. Richmond ukiulizwa anahusika vipi huwezi kujibu kwa sababu hausiki. Edward Lowassa ni kiongozi mchapakazi kweli kweli na mwadilifu"..
"Lowassa anaadhibiwa kwa ubunifu wake, kwani alikuwa anahangaika kutafuta suluhu ya tatizo, kama Richmond ilikuwa na tatizo mbona tulinunua Dowans na Obama (Rais wa Marekani) akabariki," alisema Balozi Lusinde....
Huu ni muda wa chama kusimama imara, kuwa na umoja na mshikamao na sio kuwaachia baadhi ya wagombea wanaopita katika maeneo mbali mbali nchini na kuchafua makada wenzao.....
Mpaka sasa makada wa CCM ambao wamechukua fomu kuomba kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu hadi kufikia jana ni 32...
Jambo Leo... 14.06.2015...