...Balozi Khamis Kagasheki katika hili umeonewa hatia yako siioni bado

hujasikiliza wewe.

hata report ya kamati haikumu-implicate kagasheki kwenye upuuzi uliotokana na tokomeza, execution ilitolewa kabisa mikononi mwake, Kagasheki alipambana sana

Alipambana nini wakati mauaji yalitokea kwenye wizara yake. Alifanya nini kuzuia hayo mauaji na mateso akiwa kama waziri au ulimsikia wapi akiyapinga? Utaandamana mwenyewe kwa sababu watanzania waliopoteza ndugu zao na mali zao wamefurahi
 
Kagasheki HAJAONEWA kagasheki AMEWAJIBIKA!! Ukiwa waziri yote yanatotendeka chini yako unamamlaka na wajibu wa kuya oversee.. Watendaji walioko chini yako wakiharibu hatakama wewe nimzuri namna gani utaratibu sahihi nikuwajibika kisiasa.

Nahiyo haimaanishi kwamba wewe ndio uliofanya makosa

Therefore, kagasheki amefanya heshima kubwa kuwajibika kwa makosa ya watendaji wake japo yeye hakufanya kosa kimsingi.
 
mkumbuke kuna kiongozi alimtisha kumshtaki kwa jk kama angeendelea kuingilia maslah yao sababu alizuia ujangili wa tembo
 
Kakashegi alizaliwa waziri, na Atakua waziri hadi kufa..... mijitu mingine bana
 
Kagasheki anafaa kwa lipi? Yeye si ndio aliagiza majangili wauawe huko huko hata kama hakuna ushahidi? Matokeo yake sasa wananchi wengi wameuawa na kujeruhiwa kwa kisingizio hicho, huku wahusika wakidunda mitaani!
 
wewe umelipwa kiasi gani kwa kazi hiyo, kumbuka cheo ni dhamana usidhani kuna uwaziri wa maisha.

Ninaomba kwa umoja wetu tupeleke tweet kwa Rais wetu, twitter handle yake ni ..@jmkikwete na usisahau hashtag #KagashekiArudishwe

hii ni kwa sababu naamini kwamba kagasheki ni moja ya mawaziri 5 bora kwa sasa, na kwa hili najua siko peke yangu.

Kwa wale waliofatilia Bunge jana, na waliosoma ile report kwa ukamilifu wake watagundua tatizo la operesheni tokomeza lilikua kagasheki kuwa side lined wakati wa execution, hata ile plan ya mwisho ya opersheni hakupewa.

Wakati ninaamini Nchimbi na Nahodha ilikua sahihi kabisa kwa wao kustep down au kufukuzwa (vyovyote ilivyotokea) kwa kagasheki na labda mathayo david mathayo haikua fair.

Pamoja na kwamba ninahisi mathayo hakuhusika kabisa na hii operation tokomeza, sijaona utendaji wake kiasi nitamani tupigane arudi, kagasheki kazi yake imeonekana, anahitaji kuiendeleza
 
Nasupport,mimi niko tayari kuandamana!
Kumekuwa na mapungufu mengi sana katika operation hiyo lakini ukipitia ripoti iliyosomwa kuna vitu vingi sana vilichangia operation hiyo kutofanikiwa na wala sio Waziri Kagesheki!Waziri Kagasheki wewe ni mtendaji mzuri tunakupongeza na kuonyesha hilo wewe pekee ndiye ulichukua jukumu la kuresign wengine walisubiri kufukuzwa!Pole Kagasheki kwa kuwajibika kwa sababu ya makosa ya watendaji wengine!
 
Viongozi kama wale mazingira ya nchi zetu sio mazuri kwao kusurvive!! Unafki mwingi ukiwa patriotism unaonekana mbaya! Mi naomba wale tembo waishe tu tujue moja kwa sababu inauma sana hatujaingia gharama yoyote kuwa nao wangekuwepo bila hata mijitu tenye tamaa kuwepo!! Kagasheki we understand!
 
Ni kweli Kagasheki amewajibika nadhani tukisema kaonewa hatupo sahihi lakini wengine tunaangalia nje ya box jinsi alivyokuwa anapambana na uhujumu maliasili.
Wengine tunafahamu mziki wa maliasili na jinsi alivyotikisa "maboss" wake.Hivyo ni dhahiri hili tatizo limepata tu pakushikia.
 
Sijapendezwa hata Kidogo kwa
Kagasheki Kujiuzulu, Makosa ni kweli yalifanyika kwenye
Oparation hii.lakini amini nakwambia
waliofanya makosa ni kina Emanuel
Nchimbi,pamoja na Vuai Nahodha, Kwanini natafakari kwa huyu mzee
Kagasheki,kwanza amejitahidi
kupambana na Majangili kwa nguvu zote
mpaka kufikia kuomba msaada kwa Rais
amsaidie,maana majangili wana mtandao
mpana,najaribu kufikiria kwamba majangili inasemekana ni makada kutoka chama chake
.(Ccm) Je, kwa njia hizo uoni kwamba
Kagasheki ameingizwa tu kwenye hatia
apate kibano atolewe? Majangili yalikuwa
yamebanwa kiasi fulani,Kagasheki
alijitahidi mno kupambana na Majangili,hivyo majangili yalikuwa
yanatumia mpaka Wabunge wampinge
Kagasheki,Jamani mtandao wa Ujangili
una mikono mipana sana na mirefu,Je
kuondoka kwa Kagasheki mustakabali wa
pembe za ndovu itakuaje? Msimamo wangu Kagasheki amepatwa na
bahati mbaya ya kisiasa,lakini waliotakiwa
waondoke ni kina Mzengo Pinda,Nchimbi, Vuai, Chikawe, Mkuchika, ambao Wizara
zao ndiyo zenye kuhusika na matukio
makubwa sana ambao wananyooshewa
kidole na Wananchi,' kama kung'olewa macho Kibanda,Kuuwawa Mwangosi,Kung'o
lewa kucha Ulimboka,na mateso ya kila
aina ya raia,pamoja na mabomu kupigwa
wana Chadema kwenye mikutano yao,na
waziri akiendelea kufyatua tumbo tu
kama wanaokufa ni Dagaa,huyu Nchimbi alishapoteza uhalali wa kuwa waziri, Sasa kama Oparation ya maliasili,hawa
wanajeshi waliingiaje kuttoa vichapo?
Nakubali kabisa kuliandaliwa mazingira
ya Kuhujumu zoezi Jema la kupambana na
Majangili na kuishia kupambana na
Wafugaji.Mungu ttusaidie kwa hili, Hongera Kagasheki,nitaendelea kukupa
heshima yangu kwako,wewe ni Shujaa.

umenitangulia kidogo tu! ni kweli kabisa . nchi hii ukiwakamata wakubwa ..aka wazee wa meno ya tembo ...lazima ukatwe kidizaini fulani hivi! Ohhh mara mawaziri mizigo ...mara haki za binadamu ...daah..inji hii... hadi hawa hapa below nao watachunwa ngozi zikauzwe...maana tembo wana miaka kama 2 tu.. tz2.jpg
 
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge kwa kuisimamia vema serikali, kuhusiana na suala la operation tokomeza iliyokuwa maalum kwa kutokomeza majangili katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.katika hili pamoja na mapungufu yote liliyonayo bunge yakiwemo yakushindwa kujadili vifo vya wananchi mtwara kwenye sakata lagesi,la vifo vya wananchi kule arusha kwenye bomu la soweto na menginemengi.ila kwa hili mmejitahidi kufanya kazi ya wananchi badala ya kuwa mawakala wa serikali kama mfanyavyo siku zote.kubwa zaidi kwangu nikumpongeza aliyekua waziri wa maliasili na utalii balozi hamisi kagasheki.ninampongeza kwa sababu baada ya wabunge kujadili ripoti ya kamati ya lembeli mh kagasheki alikua wa kwanza kujieleza na kukubali maneno ya wabunge waliotaka mawaziri kujiuzulu,mh kagasheki alikubali mara moja kujiuzulu yeye mwenyewe bila kusubiri mamlaka ya uteuzi kumfuta kazi kama ilivyokua kwa ma waziri wenzie waliojaribu kujitetea kwa kutoa vijisababu visivyokua na maana.kwa kufanya hivyo mh kagasheki amaeonyesha kuwa
1.ni mtiifu kwa mamlaka iliyomteua na kwa wananchi(bunge)
2.anaheshimu utawala wa kisheria
3.ni muadilifu.
4.ni mzalendo
5.anajuamaana ya uajibikaji
6.ni mtu anayejitambua
7.alijua kua cheo na dhaman
8.ana element za uongozi
kwa machache hayo nimeona ni vema nichukue nafasi hii kumpongeza mh kagasheki,maana siku hizi ni nadra kumpata kiongozi kama mh kagasheki aliye tayari kutupa ulaji kirahisi namna hii.mnyongemnyongeni lakini haki yake mpeni.nawasilisha.
 
Back
Top Bottom