...Balozi Khamis Kagasheki katika hili umeonewa hatia yako siioni bado

Mbaga Michael

Verified Member
Nov 17, 2011
2,883
1,250
Sijapendezwa hata Kidogo kwa Kagasheki Kujiuzulu, Makosa ni kweli yalifanyika kwenye Oparation hii lakini amini nakwambia waliofanya makosa ni kina Emanuel Nchimbi,pamoja na Vuai Nahodha.

Kwanini natafakari kwa huyu mzee Kagasheki,kwanza amejitahidi kupambana na Majangili kwa nguvu zote mpaka kufikia kuomba msaada kwa Rais amsaidie,maana majangili wana mtandao mpana.

Najaribu kufikiria kwamba majangili inasemekana ni makada kutoka chama chake (Ccm) Je, kwa njia hizo uoni kwamba Kagasheki ameingizwa tu kwenye hatia apate kibano atolewe?

Majangili yalikuwa yamebanwa kiasi fulani,Kagasheki alijitahidi mno kupambana na Majangili,hivyo majangili yalikuwa yanatumia mpaka Wabunge wampinge Kagasheki,Jamani mtandao wa Ujangili una mikono mipana sana na mirefu.

Je kuondoka kwa Kagasheki mustakabali wa pembe za ndovu itakuaje?

Msimamo wangu Kagasheki amepatwa na bahati mbaya ya kisiasa,lakini waliotakiwa waondoke ni kina Mzengo Pinda,Nchimbi, Vuai, Chikawe, Mkuchika, ambao Wizara zao ndiyo zenye kuhusika na matukio makubwa sana ambao wananyooshewa kidole na Wananchi,' kama kung'olewa macho Kibanda,Kuuwawa Mwangosi,Kung'olewa kucha Ulimboka,na mateso ya kila aina ya raia,pamoja na mabomu kupigwa wana Chadema kwenye mikutano yao,na waziri akiendelea kufyatua tumbo tu kama wanaokufa ni Dagaa.

Huyu Nchimbi alishapoteza uhalali wa kuwa waziri, Sasa kama Oparation ya maliasili,hawa wanajeshi waliingiaje kutoa vichapo?

Nakubali kabisa kuliandaliwa mazingira ya Kuhujumu zoezi Jema la kupambana na Majangili na kuishia kupambana na Wafugaji.Mungu ttusaidie kwa hili, Hongera Kagasheki,nitaendelea kukupa heshima yangu kwako,wewe ni Shujaa.
 

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,404
2,000
Kama ana jeuri ajiuzulu na Ubunge kabisa atuachie Bukoba yetu kuijenge badala ya malumbano yake na Meya wa Bukoba
 

ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Gambas, nakubaliana nawe 100%... Kagasheki kapambana vya kutosha, tunajua kuwa mtandao umesukwa na kusukika maana PM ni beneficiary wa madudu yote yanayotokea! anajiita motto wa mkulima lakini beyond façade he is a liar adulterer and big time cheater ... PM amekula madeal mengi sana yakiwemo yakijinga kabisa baina yake na ponjoro wa mwanza fisheries mr Bob wakachukua Bank 2.4B kisha huyo ponjoro akatimkia nchi jirani... Unlike the rest of ministers, Kagasheki amepambana kiume ila hakupata msaada wowote kutoka kwa Pinda ... Kama ningekuwa na mamlaka ya kuteua hakika Mhe Kagasheki ningemrejesha ulingoni amalizie ngwe yake ...
 

MwanaCBE

JF-Expert Member
Sep 23, 2009
1,773
2,000
Pokea pongezi huko huko uliko kwa uwezo wa kuona ipi pumba na upi mchele.

Naamini siku moja Kagasheki atarudi katika nafasi kubwa zaidi ya kisiasa kwa kazi nzuri aliyokuwa anaifanya kama waziri.
 

TabletFellow

JF-Expert Member
May 17, 2011
922
0
Unaweza ukauona hivyo kwa sasa, na labda kwa sababu hujui jinsi pesa isivyoweza kushindwa na lolote
kagasheki ametumia pes NYINGI tu kufika hapo alipo na kufanya anayofanya

hajaonewa, amewajibika

haya mambo ya emotions ndio yametufikisha hapa

maybe you dont know kagasheki
 

Muangila

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,920
2,000
Hata mimi nahisi Mh.Kagasheki ameondolewa na mtandao wa majangili kwa kuwa amekuwa mwiba kwao na huu ni ushindi mkubwa kwa majangiri,
Siipendi CCM lkn kagasheki alikuwa miongoni mwa mawaziri watendaji.
 

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,728
1,225
Kagasheki ameonewa, ametokomezwa yeye na majangili, nakumbuka majangili yalimwambia hutuwezi akabisha, mengine yalimshitaki mpaka kwa rais hakusikia, too bad mtu anaetetea maslahi ya nchi anaondolewa, akina type ya Mkuchika wanabaki.
 

Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,943
1,500
...hebu komaza akili yako kijana,wanaotafsiri hatia ni mahakama hapa kinachofanyika ni kufukuzwa kazi kama hujafikia malengo ya mamlaka ya uteuzi. Watanzania tujifunze kuwajibika kwa kutofikia au kwa makosa yanayofanyika ndani mwako(ofisi/wizara/kampuni n.k) ili kuhakikisha uwajibikaji situ mpaka wabunge waseme ndo uwajibike. No wonder watu hawaelewi kwa nini lowasa ajiuzuru. Binafsi nashangaa kumuona waziri mwinyi mpaka leo hajafukuzwa. Alipaswa kuwa wa kwanza kabla ya hawa wa sasa. Mabomu ya gongo la mboto na mbagala ilitosha kabisa kumuondoa ofisini. Ajali kama hizi ilitokea maramoja tu nadhani singapore na waziri akajiuzuru on the spot bila kusubiri tume...
 

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
382
250
Kaka hata mimi nakuunga mkono asilimia 150,Na nimeona hii vita ni ngumu sana,Kwa kazi aliyopiga katika hii vita binafsi nimetokea kumheshim sana Kagasheki, kapambana mpaka tone la mwisho kazi yake itakuwa respected moyoni mwangu ila bahati mbaya kazidiwa nguvu na mtandao wa Majangili ni uungwana alichoamua kukifanya,na mi nina maswali pia juu ya hatma ya Tembo wetu,natarajia Mhe. Rais ataweka mtu mwenye kasi ileile na atampangia Kagasheki majukumu mengine na mbeleni naamini atarudi kwenye post kubwa sana kwa mfano wa kupambana na uwajibikaji aliouonyesha,tuzidi kumuombea Afya njema na uzima ni mfano wa kuigwa.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Mbaga Michael

Verified Member
Nov 17, 2011
2,883
1,250
Gambas, nakubaliana nawe 100%... Kagasheki kapambana vya kutosha, tunajua kuwa mtandao umesukwa na kusukika maana PM ni beneficiary wa madudu yote yanayotokea! anajiita motto wa mkulima lakini beyond façade his liar adulterer and big time cheater ... PM yakiwemo amekula madeal mengi sana yakiwemo yakijinga kabisa baina yake na ponjoro wa mwanza fisheries mr Bob wakachukua Bank 2.4B kisha huyo ponjoro akatimkia nchi jirani... Unlike the rest of ministers, Kagasheki amepambana kiume ila hakupata msaada wowote kutoka kwa Pinda ... Kama ningekuwa na mamlaka ya kuteua hakika Mhe Kagasheki ningemrejesha ulingoni amalizie ngwe yake ...

Wengi wetu wanaangalia kwa karibu sana lakini ukweli ipo wazi! Kuna mchezo umefanywa na majangili
 

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,723
2,000
Ila ile ripoti inatisha jamani. Unaweza ukadhani hayatokei tanzania. Ukija kwenye topic, kagasheki ameadhibiwa kwa makosa yaliyotendeka chini ya wizara yake. Majangili wanafungua shampeni na kugonga cheerz.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom