...Balozi Khamis Kagasheki katika hili umeonewa hatia yako siioni bado

Kaka hata mimi nakuunga mkono asilimia 150,Na nimeona hii vita ni ngumu sana,Kwa kazi aliyopiga katika hii vita binafsi nimetokea kumheshim sana Kagasheki, kapambana mpaka tone la mwisho kazi yake itakuwa respected moyoni mwangu ila bahati mbaya kazidiwa nguvu na mtandao wa Majangili ni uungwana alichoamua kukifanya,na mi nina maswali pia juu ya hatma ya Tembo wetu,natarajia Mhe. Rais ataweka mtu mwenye kasi ileile na atampangia Kagasheki majukumu mengine na mbeleni naamini atarudi kwenye post kubwa sana kwa mfano wa kupambana na uwajibikaji aliouonyesha,tuzidi kumuombea Afya njema na uzima ni mfano wa kuigwa.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Ahsante kwa kuliona ili nina wasiwasi kama mh. Rais nae hayumo katika mtandao wa kijangili? Kwanini hakuweza kumpa nguvu pale alipomuomba msaada juu ya mtandao wa majangili?
 
No comment for these saga akumbuke marehemu Baba askofu Laizer aliwahi kusema wakati wa kumpokea mh Lowasa Monduli wakati amejiuzulu/ amewajibika(collective responsibility) alitahadharisha wanasiasa Lowasa ni sawa na kuni ambayo imeungua jikoni lakini ziko kuni nyingine zitaungua tu hata kama ni mbichi lengo kutimiza matakwa ya wanasiasa na wahafidhina weusi wanaofanana na makaburu. kagasheki you have done your level best, you have to accept liability and challenges. welcome streets
 
Bado naamini kuwa waziri aliyejiuzulu, ni mtu muhimu sana ndani ya mapambano dhidi ya ujangili ulioundiwa ngome imara. Yawezekana Tanzania isimpate shujaa kama huyu milele. Ni shujaa aliyeangamizwa na oparesheni yake mwenyewe. Operesheni tokomeza majangili ikamgeuka na kuwa operesheni tokomeza Kagasheki. Nakutia Moyo shujaa uliyeuawa vitani. Wameua mwili wako lakini naamini wameshindwa kuua uzalendo wako mtukuka! Kwa tafakuri pevu, vita yako takatifu imenajisiwa na kuonekana si kitu. Bunge letu tukufu kwa kusukumwa na upofu wa kura za mwaka 2015 limeshughulikia matawi na sio tatizo lenyewe! Wakati kamati ya uchunguzi ilipaswa kuja na majibu ya kwa nini wale waliotumwa na kagasheki kupigana vita takatifu wameigeuza kuwa vita ya kishetani, tume hiyo imekuja na majibu ya matokeo ya uasi wa vita takatifu iliyoasisiwa na mheshimiwa Kagasheki. Wabuge wetu wakatumia bunge kama eneo la kuhakikishia usalama wa kura zao! Vita takatifu imepoteza udhu!
 
Acha kutetea upuuzi.....taarifa za unyamera wa watekelezaji wa operesheni zilimfikia lakini hakuchukua hatua...hii ina maana aliunga mkono.
Anastahili kunyongwa yeye na kina nchimbi
 
Imeniuma sana,kweli CCM inawenyewe Kagasheki ndiye waziri pekee aliyeanza kufichua wizi mkubwa wa pembe za ndovu. Maige alkuwa anacheza mchezo wa pasu kwa pasu. Muda wa kujiunga CUF kwa upande wangu naona umefika.
 
Tutambue amewajibika hata kama hana kosa bado ataheshimika ndani na nje ya nchi. ila bunge letu lisitumiwe kama genge la baadhi ya wahuni wakijinasibu wanatetea wananchi wakati wao wametumia mbinu chafu kusaliti operesheni yenyewe.
 
Tatizo la Kagasheki ni kukata mti wa tawi alilokalia. Tofauti na wachangiaji wengi hapa mimi namlaumu yeye mwenyewe Kagasheki. You can't go against the manifesto of your employer and expect to keep your job. Plain and simple.
 
Kweli huyu bwana ni mchapakazi na mzalendo wa kweli. Ndiyo hivyo tena siku ya kufa nyani miti yote uteleza.
 
Acha kutetea upuuzi.....taarifa za unyamera wa watekelezaji wa operesheni zilimfikia lakini hakuchukua hatua...hii ina maana aliunga mkono.
Anastahili kunyongwa yeye na kina nchimbi

ACHA UJINGA WEWE!Mbona huzungumzii askari waliouwawa na Majangili unazungumzia raia tu upande mmoja,Kagasheki ni Jembe kazi yake na ujasiri wake utaheshimika daima,kwa mapungufu hayo ya operesheni ndiyo maana akawajibika kisiasa ila hatuwezi kudharau wala kupuuza kazi nzito aliyoifanya,kapambana vya kutosha na kaacha Legacy kuwa alithubutu kuokoa wanyama wetu sema Majangili yana Mtandao mpana yakamgeukia,Pumzika Kagasheki ull always be respected.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Bado naamini kuwa waziri aliyejiuzulu, ni mtu muhimu sana ndani ya mapambano dhidi ya ujangili ulioundiwa ngome imara. Yawezekana Tanzania isimpate shujaa kama huyu milele. Ni shujaa aliyeangamizwa na oparesheni yake mwenyewe. Operesheni tokomeza majangili ikamgeuka na kuwa operesheni tokomeza Kagasheki. Nakutia Moyo shujaa uliyeuawa vitani. Wameua mwili wako lakini naamini wameshindwa kuua uzalendo wako mtukuka! Kwa tafakuri pevu, vita yako takatifu imenajisiwa na kuonekana si kitu. Bunge letu tukufu kwa kusukumwa na upofu wa kura za mwaka 2015 limeshughulikia matawi na sio tatizo lenyewe! Wakati kamati ya uchunguzi ilipaswa kuja na majibu ya kwa nini wale waliotumwa na kagasheki kupigana vita takatifu wameigeuza kuwa vita ya kishetani, tume hiyo imekuja na majibu ya matokeo ya uasi wa vita takatifu iliyoasisiwa na mheshimiwa Kagasheki. Wabuge wetu wakatumia bunge kama eneo la kuhakikishia usalama wa kura zao! Vita takatifu imepoteza udhu!
 
bado naamini kuwa waziri aliyejiuzulu, ni mtu muhimu sana ndani ya mapambano dhidi ya ujangili ulioundiwa ngome imara. Yawezekana tanzania isimpate shujaa kama huyu milele. Ni shujaa aliyeangamizwa na oparesheni yake mwenyewe. Operesheni tokomeza majangili ikamgeuka na kuwa operesheni tokomeza kagasheki. Nakutia moyo shujaa uliyeuawa vitani. Wameua mwili wako lakini naamini wameshindwa kuua uzalendo wako mtukuka! Kwa tafakuri pevu, vita yako takatifu imenajisiwa na kuonekana si kitu. Bunge letu tukufu kwa kusukumwa na upofu wa kura za mwaka 2015 limeshughulikia matawi na sio tatizo lenyewe! Wakati kamati ya uchunguzi ilipaswa kuja na majibu ya kwa nini wale waliotumwa na kagasheki kupigana vita takatifu wameigeuza kuwa vita ya kishetani, tume hiyo imekuja na majibu ya matokeo ya uasi wa vita takatifu iliyoasisiwa na mheshimiwa kagasheki. Wabuge wetu wakatumia bunge kama eneo la kuhakikishia usalama wa kura zao! Vita takatifu imepoteza udhu!

mkuu, tumekua tukiskia majangiri wakiiba nyara za serikari,ikiwemo pembe za ndovu na na wanyama km twiga kukunjwa kunjwa km karatasi na kupakiwa kwenye ndege kwenda nchi za wawekezaji

na haya yte yametokea kipindi ambacho uyo kagasheki ndiye waziri

lakin hata siku moja hajawai kuzungumzia hilo wala kuwataja wadau waloiba wanyama wetu,wala nyara yyte ya serikari.

Ni jambo la ajabu sana.

Mtanzania wa kawaida akikutwa ana winda sungura,kwaajiri ya kitoweo chake,kando kando mwa hifadhi au msitu anaitwa jangiri

wakati wageni kutoka nje ,wanakuja kubeba mpk wanyama wetu na kuwasafirisha kwenda nje, lkn wanaitwa wawekezaji

kagasheki si jasiri.
Amebeba mzigo alio stahiri
 
Imeniuma sana,kweli CCM inawenyewe Kagasheki ndiye waziri pekee aliyeanza kufichua wizi mkubwa wa pembe za ndovu. Maige alkuwa anacheza mchezo wa pasu kwa pasu. Muda wa kujiunga CUF kwa upande wangu naona umefika.

Ukiwa ndani ya ccm hutakiwa kuongea mabaya yake
 
Sijapendezwa hata Kidogo kwa
Kagasheki Kujiuzulu, Makosa ni kweli yalifanyika kwenye
Oparation hii.lakini amini nakwambia
waliofanya makosa ni kina Emanuel
Nchimbi,pamoja na Vuai Nahodha, Kwanini natafakari kwa huyu mzee
Kagasheki,kwanza amejitahidi
kupambana na Majangili kwa nguvu zote
mpaka kufikia kuomba msaada kwa Rais
amsaidie,maana majangili wana mtandao
mpana,najaribu kufikiria kwamba majangili inasemekana ni makada kutoka chama chake
.(Ccm) Je, kwa njia hizo uoni kwamba
Kagasheki ameingizwa tu kwenye hatia
apate kibano atolewe? Majangili yalikuwa
yamebanwa kiasi fulani,Kagasheki
alijitahidi mno kupambana na Majangili,hivyo majangili yalikuwa
yanatumia mpaka Wabunge wampinge
Kagasheki,Jamani mtandao wa Ujangili
una mikono mipana sana na mirefu,Je
kuondoka kwa Kagasheki mustakabali wa
pembe za ndovu itakuaje? Msimamo wangu Kagasheki amepatwa na
bahati mbaya ya kisiasa,lakini waliotakiwa
waondoke ni kina Mzengo Pinda,Nchimbi, Vuai, Chikawe, Mkuchika, ambao Wizara
zao ndiyo zenye kuhusika na matukio
makubwa sana ambao wananyooshewa
kidole na Wananchi,' kama kung'olewa macho Kibanda,Kuuwawa Mwangosi,Kung'o
lewa kucha Ulimboka,na mateso ya kila
aina ya raia,pamoja na mabomu kupigwa
wana Chadema kwenye mikutano yao,na
waziri akiendelea kufyatua tumbo tu
kama wanaokufa ni Dagaa,huyu Nchimbi alishapoteza uhalali wa kuwa waziri, Sasa kama Oparation ya maliasili,hawa
wanajeshi waliingiaje kuttoa vichapo?
Nakubali kabisa kuliandaliwa mazingira
ya Kuhujumu zoezi Jema la kupambana na
Majangili na kuishia kupambana na
Wafugaji.Mungu ttusaidie kwa hili, Hongera Kagasheki,nitaendelea kukupa
heshima yangu kwako,wewe ni Shujaa.[/QUOTEl .kagasheki afai kwa lolote.muonevu kwa watu wadogo
 
unaweza ukauona hivyo kwa sasa, na labda kwa sababu hujui jinsi pesa isivyoweza kushindwa na lolote

weka picha ya ushahidi wa jinsi pesa isivyoweza kushindwa na lolote.

Tunajipumbaza wenyewe na imani zetu, hakuna kinachoshindikana kwa maamuzi ya pamoja,

pesa ni makaratasi tu
 
Kweli huyu bwana ni mchapakazi na mzalendo wa kweli. Ndiyo hivyo tena siku ya kufa nyani miti yote uteleza.

kweli uyu bwana mchapa kazi asee

ndo mana ktk kipindi chake tumeshuhudia Wanyama kusafirishwa nje ya nchi

Tumeshuhudia,Meno ya Tembo kuwa Tittle kuu ktk vyombo vya Habari

Tumeshuhudia,akikaa kimyaa bila kuwataja majangili papa na majangiri nyangumi

ila kubwa zaidi tunamshukuru sana kwa sbb bila yy na wenzake tusingeweza kuwa na msamiati mpya ktk kamusi ya siasa
"WAZIRI MZIGO"

ametumia muda mwingi kurumbana na meya wa bukoba,ule mda angetumia kuwataja majina majangiri hata wa wili tu haya yte yasinge mkuta.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom