Sitachoka
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 3,030
- 1,303
- Thread starter
- #41
weka picha ya ushahidi wa jinsi pesa isivyoweza kushindwa na lolote.
Tunajipumbaza wenyewe na imani zetu, hakuna kinachoshindikana kwa maamuzi ya pamoja,
pesa ni makaratasi tu
Kama unaikumbuka habari hii! Utaamini kile ninachokisema
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi
Khamisi Kagasheki amemtuhumu Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa
wa Arusha (RCO), Diwan Nyanda,
kuhujumu operesheni `tokomeza
majangili', baada ya kudaiwa kuwatorosha majangili wawili raia wa
kigeni.
Tuhuma hiyo nzito ilitolewa na Balozi
Kagasheki, jijini Dar es Salaam jana,
wakati akitangaza kuanza kwa
operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili,
biashara haramu ya pembe za ndovu,
faru na maliasili ya misitu nchini kote.
Katika operesheni hiyo iliyopewa jina la
`tokomeza ujangili' alisema ilianza hivi
karibuni na inahusisha majeshi yote ya ulinzi na usalama.
Waziri Kagasheki alisema, kiongozi huyo
wa jeshi la polisi alisaidia kuwatorosha
watu wawili wenye uraia wa nchi ya
Saud Arabia ambao walikuwa
wakishikiliwa baada ya kukutwa wakiwa na silaha na baadhi ya
vithibitisho vinavyoonyesha walikuwa
majangili.
"Inasikitisha sana na inaturudisha nyuma
ikiwa kama kiongozi wa jeshi anayevaa
sare ya Watanzania, kwa makusudi anawaachia watuhumiwa wa ujangili na
kusaidia kuondoka nchini," alisema
Kagasheki.
Alisema katika tukio hilo, polisi
walifanikiwa kuwakamata watu hao
wakiwa na vithibitisho vyote vya kujihusisha na ujangili na kuwapeleka
kituo cha polisi Arusha kwa ajili ya
mahojiano.
Akielezea mchezo huo ulivyofanyika,
alisema kabla ya kuwekwa rumande,
watu hao walinyang'anywa hati zao za kusafiria ili kuwazuia wasitoroke. Lakini
katika hali ya kushangaza (RCO), Nyanda,
alihakikisha watu hao anawatoa nje
kwa dhamana na kisha aliwakabidhi hati
hizo kitu kilichosababisha watoroke
nchini.