TANZIA Balozi Juma Mwapachu afariki Dunia

TANZIA Balozi Juma Mwapachu afariki Dunia

Balozi Juma Mwapachu, ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, amefariki dunia leo Machi 28, 2025 katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Balozi Mwapachu utasafirishwa kwenda Kijiji cha Pande, Kiomoni, Tanga kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumapili Machi 30, 2025

Mwapachu aliwahi kujitoa CCM Oktoba 2015 kuunga safari ya matumaini ya Edward Lowassa na kurejea chama hicho mwaka 2016 ikiwa ni miezi mitano baadaye

HISTORIA FUPI
Juma Volter Mwapachu (alizaliwa tarehe 27 Septemba 1942 huko Mwanza, Tanzania) ni mwanasiasa wa Tanzania na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aliyachukua nafasi ya Amanya Mushega wa Uganda, ambaye alimaliza muhula wake wa miaka mitano mnamo Machi 24, 2006.

Mwapachu aliteuliwa kwa nafasi hiyo na Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kilele cha Wakuu wa Nchi wa EAC mnamo Aprili 4, 2006. Kabla ya uteuzi huo, Mwapachu alikuwa Balozi wa Heshima na Mjumbe wa Kudumu wa Tanzania katika UNESCO.

Mwapachu ni mhitimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (alipata shahada yake mnamo 1969). Aidha, ana Stashahada ya Uzamili katika Sheria za Kimataifa, Taasisi za Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Kimataifa cha Sheria na Diplomasia cha India kilichopo New Delhi, India. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilimtunuku Shahada ya Udaktari wa Fasihi (Honoris Causa) mnamo 2005. Pia anashikilia Shahada ya Udaktari wa Heshima wa Fasihi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Udaktari wa Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda.

Balozi Juma V. Mwapachu ni mwanasheria kitaaluma na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika sekta za benki, maendeleo vijijini, diplomasia, na sekta binafsi.

Baadhi ya nyadhifa alizoshikilia kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa EAC ni:
  • Kufanya kazi na Wizara ya Serikali za Mitaa na Utawala wa Mikoa katika miaka ya 1970.
  • Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa kati ya 2002 - 2006.
  • Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania.
  • Mwenyekiti wa Bodi za Mashirika ya Umma, ikiwa ni pamoja na Benki ya Uwekezaji Tanzania.
  • Kamishna wa Tume ya Rais ya Marekebisho ya Sekta ya Mashirika ya Umma.
  • Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
  • Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Biashara ya Nje na Baraza la Usimamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  • Mjumbe wa Baraza la Usimamizi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa.
  • Mjumbe wa Tume kadhaa za Rais na mmoja wa waandishi wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025.
Alitupa raha sana Tanga, mid 90s kwa kutuletea lacasa chica
 
Mbona swali la kawaida sana.
Pole kwa msiba.
Kuuliza ''ni nani huko daslamu''.

Ni kauli ya utani wa kujifanya mjanja, iliyojaa dharau na kejeli.

Mara nyingi muulizaji anakuwa anajua, ila anauliza kujifanya kwamba yeye yuko bize sana hafuatilii mambo ya 'daslamu' kwa sababu anayapuuza.

Swali hili huulizwa sana wanapohusika waigizaji, wasanii au watu fulani wa social media.

Juma Mwapachu alikuwa kiongozi wa kitaifa.

Ni ujinga na ulimbukeni kuuliza kwa staili hiyo.
 
Niko msele kwanza
Dar mvua

Ova

Watu wa zamani na alio karibu nao ndio wanamjua, wengine hawamjui kabisa. Usipangie watu maswali.
Usifikiri kila kinachokuumiza kinaumiza wengine pia, utateseka sana.
 
Watu wa zamani na alio karibu nao ndio wanamjua, wengine hawamjui kabisa. Usipangie watu maswali.
Usifikiri kila kinachokuumiza kinaumiza wengine pia, utateseka sana.
Mbona nimefafanua vizuri.

Mimi sijaumizwa na chochote, nilikuwa naelezea uhalisia ulivyo.

Tatizo lako hauzingatii logic, unatumia hisia, labda ndivyo wanawake wengi mlivyo.
 
Wewe ndio unatumia hisia, ndio maana swali la kawaida kabisa unapanic.
Madam, ukawaida wa swali uko wapi?

Anapoongelewa mtu kisha unauliza, ''ndiyo nani huko daslam''

Kwani watu wote ni wa daslam?

Mtu humjui, halafu unakurupuka kusema ni wa ''daslam''

Huo ni ulimbukeni wa kishamba.

Kujifanya mjanja kumbe mjinga.
 
Hafu isitoshe maelezo yamemuleezea kwakina Marehemu,halafu anauliza ninani huko Dsm?
Kuuliza ''ni nani huko daslamu''.

Ni kauli ya utani wa kujifanya mjanja, iliyojaa dharau na kejeli.

Mara nyingi muulizaji anakuwa anajua, ila anauliza kujifanya kwamba yeye yuko bize sana hafuatilii mambo ya 'daslamu' kwa sababu anayapuuza.

Swali hili huulizwa sana wanapohusika waigizaji, wasanii au watu fulani wa social media.

Juma Mwapachu alikuwa kiongozi wa kitaifa.

Ni ujinga na ulimbukeni kuuliza kwa staili hiyo.
 
Nilitania tu; sijui asili yake ni wapi kwani majina ya Mwapachu unaweza kukuta ni ya Mbeya; ila Juma alizaliwa Mwanza. Sasa sijui wazazi wake walitokea wapi.
Kwao ni Tanga,Yeye alizaliwa Mwanza wakati baba Yao alipohamishiwa huko Mwanza ili kumuweka mbali na harakati za uhuru.
Bakari alikuwa wa Kwanza yeye wa pili
 
Madam, ukawaida wa swali uko wapi?

Anapoongelewa mtu kisha unauliza, ''ndiyo nani huko daslam''

Kwani watu wote ni wa daslam?

Mtu humjui, halafu unakurupuka kusema ni wa ''daslam''

Huo ni ulimbukeni wa kishamba.

Kujifanya mjanja kumbe mjinga.
Ujuaji fulani lakini mtu wa sampli hiyo huwezi kumwelewesha, itakua sawa na kumpigia mbuzi kitaa, better not to argue
 
Back
Top Bottom