'Balozi' ataka Rais Samia atengenezewe sanamu

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
276
476

Muktasari:​

  • Balozi wa utalii ataka Rais Samia atengenezewe sanamu kama kumbukumbu ya kuwa Rais mwanamke wa kwanza na aliyejitoa kwa dhati kuipambania sekta hiyo kwa kushiriki kutangaza utalii wa nchi.
Dar es Salaam. Wakati sekta ya utalii ikiendelea kuimarika na kuvutia idadi kubwa ya watalii Balozi wa utalii nchini Nangasu Warema amepongeza hatua zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta hiyo ambayo ilipitia mdondoko kufuatia athari za janga la Uviko 19.
IMG-20230208-WA0001.jpg

Balozi wa Utalii Nangasu Warema

Balozi huyu amesema jitihada kubwa zimefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kuhakikisha sekta hiyo inarudi kwenye mstari na kushauri kuwepo alama ya kuonyesha shukrani kwa kiongozi huyo.

“Naiomba Serikali kutengeneza sanamu ya Rais Samia iwekwe kama kivutio, kwanza kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke pili kwa jitihada zake ambazo amezifanya kuinuua sekta ya utalii ikiwemo kuwa muongoza watalii kupitia filamu ya Royal Tour.

Hii filamu imeweza kutangaza utalii na imewavutia watu wengi kuja nchini, hili halikuwahi kufanyika tangu nchi ipate uhuru hivyo naona kuna kila sababu ya kutengeneza kumbukumbu ya huyu mwanamke shupavu ambaye amesimama kidete kwa ajili ya sekta ya utalii na nchi yake kwa ujumla. Hii italeta chachu kwa vizazi vijavyo hasa wanawake kuwapa hamasa ya uongozi.

Januari 7 mwaka huu akizungumza katika mkutano wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) wa mashauriano baina ya sekta binafsi na sekta za umma katika sekta ya utalii, Waziri wa Maliasi na Utalii Dk Pindi Chana alisema sekta ya utalii nchini imeendelea kuimarika baada ya athari za janga la Uviko-19, ambapo mwaka 2022 watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.29 ikilinganishwa na watalii 922,692 waliokuja nchini mwaka 2021.

Ongezeko hili la watalii ni asilimia 71.02 kuanzia Januari hadi Novemba 2022, ambapo Serikali imeweka lengo kuwa ifikapo mwaka 2025 ipokee watalii milioni tano kwa mwaka na mapato kufikia Dola bilioni 6.

Waziri huyo alibainisha ongezeko hilo la watalii limetokana na jitihada za Serikali na wadau wa utalii, zikiwemo kukuza, kuendeleza na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa kutumia Programu ya ‘The Royal Tour sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya utalii, hudumaa na kuimarisha matumizi ya Tehama.
 
“Naiomba Serikali kutengeneza sanamu ya Rais Samia iwekwe kama kivutio, kwanza kwa kuwa rais wa kwanza mwanamke pili kwa jitihada zake ambazo amezifanya kuinua sekta ya utalii ikiwemo kuwa muongoza watalii kupitia filamu ya Royal Tour.
Naunga mkono hoja
P
 
Mada imebdadilika ghafla sasa anajadiliwa balozi badala ya mada yenyewe
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom