. Bila shaka ndiyo mwanzo mkubwa wa kusambaratika kwa CCM. Wapinzani kwa ujumla kwanini kusifanyike kwa maandamano nchi nzima ya kumuunga mkono aliyefichua bomu hili na kulaani vikali wizi na uzembe wa CCM?..
Sakata la BoT lilianza kufukuta kwa muda mrefu kupitia vyombo vya habari vilivyokua vikihoji hasa ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo na matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia mifuko na dhamana kwa wakopaji wakubwa ambao walianza kuonyesha dhahiri kuwa ukopaji wao ulikuwa wenye shaka kubwa.
Baada ya kujadiliwa kwa muda na vyombo vya habari, jina la BoT lilianza kuingia pole pole ndani ya vikao rasmi ikiwa ni pamoja na vikao vya Bunge ambako Mbunge wa Karatu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, aliongeza kasi ya waandishi wa habari kujua undani wa matumizi mabaya kupita kiasi ya fedha ndani ya Serikali kupitia Benki Kuu na Hazina.
Dk. Slaa alifikia hatua ya kutaka kuwasilisha hoja binafsi akitaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza matumizi mabaya ya kutisha ndani ya BoT, hoja ambayo iligonga mwamba hata kabla ya kuwasilishwa na badala yake kambi nzima ya Upinzani kuamua kuanza kutoa baadhi ya vipengele katika mikutano ya hadhara.
Hata hivyo, wakati Dk. Slaa akizungumzia BoT ndani ya Bunge, tayari Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Zakia, ilikwisha kutangaza kufanya uchunguzi wa kuhusu matumizi ya fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) lakini bila kufanya uchunguzi katika maeneo mengine pamoja na kuwa maeneo hayo yamekuwa yakichunguzwa na vyombo vya dola.
watu walidhani tunawatania.. chess.. juu ya chess.. watu waende kusoma raiamwema.co.tz pale juu kuna kaujumbe...
HABARI
Nakala chapishi
Mtumie mwenzio
Ndugu wamshinikiza Ballali kujibu mapigo ya Serikali
Mwandishi Wetu Januari, 16, 2008
Sasa anaweza kuzungumza
ALIYEKUA Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Ballali, ameanza kupata nafuu na anashinikizwa na ndugu ajibu mapigo ya tuhuma za Serikali zilizosababisha angolewe wiki iliyopita.
Taarifa za karibu na ndugu zake zilizopatikana wiki hii, zinasema sasa Dk. Ballali anazungumza baada ya kuwa amepoteza fahamu kwa muda mrefu, na matarajio ya wanafamilia yake ni kwamba muda si mrefu akiendelea hivyo, ataijibu Serikali.
Mmoja wa wanafamilia ameiambia Raia Mwema kwamba kuna shinikizo la familia na marafiki, la kumtaka ajisafishe dhidi ya tuhuma za ubadhirifu ndani ya BoT ambazo ndizo msingi wa kuondolewa kwake.
Kwa mujibu wa habari hizo, Ballali amekuwa akipata shinikizo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki ili aweze kujitokeza na kutoa maelezo ya nini kilichomsibu, hasa baada ya Serikali kushindwa kutoa taarifa halisi ya hali yake ya ugonjwa.
Mbali ya kuzungumzia hali ya afya yake, Ballali anashinikizwa pia azungumzie kuhusu hatima yake hasa baada ya mwenyewe kuomba kujiuzulu na kujikuta akitimuliwa akiwa mgonjwa badala ya kujibiwa barua yake ya kuomba kujiuzulu ambayo haijapata kutangazwa rasmi nchini.
Kwa mujibu wa habari hizo, yeye mwenyewe amekuwa akitoa kipaumbele kwa afya yake kwanza badala ya kuingia katika malumbano na wakuu wake, na kwa kuwa kimsingi hajaondolewa katika utumishi wa umma.
Taarifa za ugonjwa wa Ballali zimekua zikitatanisha, zikizongwa na usiri mkubwa kiasi cha kuibuka uvumi wa kuwa amekwisha kufa. Serikali haijatoa taarifa ya kina kuhusu hali yake.
Serikali kwa kawaida haiwezi kuzungumzia ugonjwa wa mtu bila ridhaa kwanza ya familia, na familia ndiyo inayoweza kutoa taarifa ama kuiomba Serikali itoe taarifa kwa kushirikiana nayo, na hili la Ballali ni katika mantiki hiyo, alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali.
Ofisa huyo alisema Ballali amekuwa akiumwa kwa muda mrefu sasa japo amekuwa akipata matibabu ndani na nje ya nchi na kwamba kabla ya kwenda Marekani aliwahi kutibiwa nchini Afrika Kusini.
Mkuu Halisi,
Bwana wee! makubwa haya!
Ila hii ya kwamba alitumiwa ni ujinga mtupu. Muhimu kama ameanza kuropka kama wale wasaidizi wa Saddam. Atatusaidia kumkamata the big fish.
Hapo mchezo utakuwa mtamu sana, kama JK anataka kuondoa corruption basi awe tayari ku bargain na Ballali ili kuhakikisha wengine wote wananaswa. Anaweza kumhakikishia japo msosi wa maana na matibabu akiwa Keko.
Unamjua aliyefichua hilo bomu kabla hujaiitisha maandamano! Au unakurupuka tu? Angalia quote hii kutoka page 2 ya thread hii!!!
Kwa mtindo huu watanzania tutakuwa tunazunguka katika mduara tu bila kufika popote.
Sasa tunataka Ballali 'a-bargain' kwa manufaa yake? Tunajuaje kuwa ufisadi haupo kwenye hiyo ofisi kubwa!
Tumwache Ballali ajitetee kivyake, bila ya kumning'inizia peremende zenye sumu ya panya.
JENGA HOJA ACHA MAJUNGU YA KUTAFUTA NANI KASEMA.aka KUWA NA TABIA ZA KIUME.Ni kichekesho mtu kukubali kufanya wizi wote huo kama alikuwa katumwa na kigogo flani,ina maana yeye hakuwa na maamuzi binafsi!!!!!!!!!!!!aliona nini kuresigne kama kweli analipenda taifa lake.mbona Mwakyembe alipoona kuwa NBC mambo hayaendi sawa alijivua ujumbe wa board?Na KWA NINI TUMWAMINI KUWA NI MKWELI WAKATI ALIDILIKI HATA KUMDANGANYA MAMA ZAKIA KUWA MALIPO NI HALALI WAKATI SIO KWELI?AKINGOJA MPAKA AFUKUZWE NDIO ASEME?ANAEKUFA HAACHI KUTAPATAPA.BALALI KUFA MWENYEWE HUSITAKE MKUCHAFUA BABA ZETU WAADILIFUI smell KADA MPINZANI in making. Yule aliyekuwa katika kundi la watu wa ajabu. Endelea FISADIST- I mean FISI DUST
Asha
JENGA HOJA ACHA MAJUNGU YA KUTAFUTA NANI KASEMA.aka KUWA NA TABIA ZA KIUME.Ni kichekesho mtu kukubali kufanya wizi wote huo kama alikuwa katumwa na kigogo flani,ina maana yeye hakuwa na maamuzi binafsi!!!!!!!!!!!!aliona nini kuresigne kama kweli analipenda taifa lake.mbona Mwakyembe alipoona kuwa NBC mambo hayaendi sawa alijivua ujumbe wa board?Na KWA NINI TUMWAMINI KUWA NI MKWELI WAKATI ALIDILIKI HATA KUMDANGANYA MAMA ZAKIA KUWA MALIPO NI HALALI WAKATI SIO KWELI?AKINGOJA MPAKA AFUKUZWE NDIO ASEME?ANAEKUFA HAACHI KUTAPATAPA.BALALI KUFA MWENYEWE HUSITAKE MKUCHAFUA BABA ZETU WAADILIFU
MNATUNGA SANA HABARI ZA MAFISADI LAKINA HAMKO CRITICAL NA WALA HAMNA DATA.NGOJA LEO NIWASAIDIE KUWAONYESHA NAMNA YA KUGUNDUA MAMBO.chukua gazeti la raia mwema la jana,angalia barua za zakhia kwa delloite,umeona barua ya kuwithdraw inafanana ref no na hio nyingine?maanake ni kuwa hio ya pili ni ya kuforge si kweli alikanusha anajisafisha.barua mbili tofauti hazifanani ref no ata siku mojaeti nilikuwa natumiwa? mpuuzi sana huyu na bora aje aseme ukweli tujue who/where is the money? akiwa mkweli wananchi tunaweza kumpa immunity maana atakuwa ametusaidia kuondoa mafisadi wengi sana
Kalamu,
Polisi yeyote wa maana hapa duniani atakuambia ukimkamata jambazi, kitu cha kwanza unamwambia yuko kwenye hot water, sasa aamue atapunguzaje maumivu yake.
Kwa habari alizo nazo Ballali, ningelikuwa JK, na kama kweli nataka kunasa kila mtu kwenye huo mtandao, ningekubali ku bargain naye.
Wenzetu ndivyo wanavyomaliza mitandao ya madawa na hata Italy ndivyo walivyoweza kuwapunguza sana Mafia.
Vinginevyo tutapata nusu ukweli na nusu uwongo.
Kama serikali ina kila kitu then hakuna haja ya ku bargain naye. Nina wasiwasi kwa serikali ya Kizembe kama yetu kama wanajua kila kitu.
bt msiseme nawageuka wazee wanguMNATUNGA SANA HABARI ZA MAFISADI LAKINA HAMKO CRITICAL NA WALA HAMNA DATA.NGOJA LEO NIWASAIDIE KUWAONYESHA NAMNA YA KUGUNDUA MAMBO.chukua gazeti la raia mwema la jana,angalia barua za zakhia kwa delloite,umeona barua ya kuwithdraw inafanana ref no na hio nyingine?maanake ni kuwa hio ya pili ni ya kuforge si kweli alikanusha anajisafisha.barua mbili tofauti hazifanani ref no ata siku moja