WanaJamvi,
Cheap politics haisaidii. Balaa gani hiyo? Kama ni balaa Dr Slaa kilipaswa kumshukia baada ya List of Shame niliyoitangaza MwembeYanga,Temeke, dar-Es-Salaam Tarehe 25 September, 2007. Siku hiyo mbele ya Polisi wengi wa Makao Makuu, FFU waliokuwa wametanda kila mahali, Usalama wa Taifa wenye Radio Masikioni dakika zote nilitaja, kwa kushirikiana na Lisu, Mkurugenzi wa Sheria Chadema, Mafisadi 11, katika Listi hiyo akiwemo JK. Rostam Aziz na Lowasa walikuwa kwenye Listi hiyo. Wako walionitishia kunipeleka mahakamani wakashindwa(leo baadhi yao wako mahakamani kwa tuhuma hizo hizo),JK akatangaza hadharani kuwa kelele za DR Slaa ni kama "kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba kulala" na matambo mengine mengi-Leo JK mwenyewe anatumia msamiati "Mafisadi aliokuwa ameukataa muda wote, na leo ameanzisha usanii wa " Kuitaka CCM kujivua gamba" kwa ajili ya Ufisadi. Sasa balaa lipi mwenye kuanzisha thread hii anaiona. Kama ni nape simshangai, kwani inawezekana 2007 alikuwa mdogo, na kwa hiyo namsamehe bure. Nani anamtumia nani Dr Slaa aliyewatangaza hadharani wote hao miaka, Dr Slaa aliyewataja hdharani miaka mitatu iliyopita, au Nape aliyeteuliwa juzi na kulewa mara madaraka na kusahau historia na au kulewa siasa ya makundi ndani mwao wenyewe? Dr Slaa hasumbuliwi na uchafu ndani ya CCM, hayo ni mambo yao. Wavue gamba wasivue ni shauri lao. Dr Slaa ninayosema, ambayo nimeisema consistently, "walipe fedha zetu watanzania, na bila ubaguzi wapelekwe mahakamani na hjatimaye gerezani kama ambavyo watanzania wengi wana[pelekwa kwa ajili ya "vijisenti vichache tu. Ni dhahiri Nape haelewi anachoongea, na au hajui historia au makusudi anapotosha. Narudia tena Ufisadi ndani ya CCM hautusumbui ni wa kwao wenyewe, watajua wanavyofanyiana. Kinachotusumbua ni ufisadi uliofanywa na Wana CCM na CCM yao (kama nilivyohusisha vijimemo vya Mangula na Malecela kwa Dr Balali, aliyekuwa Governor wa BOT) kwa rasilimali na Fedha za Taifa au kwa manufaa yao binafsi au ya Chama chao. Wanakazi kweli, kujivua Gamba pekee hakutoshi labda "wabadili na damu",kama hata hiyo itawasaidia tulikofikia.