Balaa lingine lamwangukia Dr Slaa

Mujumba

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
853
306
Balaa lingine limemwangukia katibu mkuu wa chama cha CHADEMA,baada ya kutuhumiwa na chama cha mapinduzi kuwa anatumika na mafisadi,hii inaweza chukuliwa kirahisi lakini ni swala nyeti ikizingatiwa Slaa amekuwa akijifanya kuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi,Slaa hana budi kukanusha hizi tuhuma au kutoa maelezo ya kujitosheleza kwasababu kukaa kimya inaweza kuleta tasfiri tofauti kwa wafuasi wake( silence means yes)

HABARI KAMILI
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na chama chake, wanatumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi waliotakiwa kujiuzulu wenyewe ndani ya chama hicho.

Akihutubia umati wa watu katika viwanja vya Mwembe-Kisonge Zanzibar, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema kwa sasa watuhumiwa hao wameamua kutumia baadhi ya vyama vya siasa, magazeti na asasi za dini kujibu mapigo.

“Tumewapa miezi mitatu watuhumiwa wote wa ufisadi katika chama chetu wajiondoe wenyewe. Baadhi wanajaribu kupinga na kujibu mapigo kwa kutumia magazeti, vyama vya siasa na taasisi za dini...tunajua tutashinda na wao lazima waondoke,” alisema Nnauye.

Alisema, “Tumeandaa mkakati wa kusafisha chama kutoka ngazi za chini mpaka katika ngazi ya Taifa. Tumechunguza na tunajua wanaotakiwa kuondoka ndani ya chama chetu. Lakini baadhi ya watu wamejitokeza kutaja majina ya watuhumiwa ndani ya chama chetu, hiyo si kazi yao.”
 
Mbona hilo sio balaa? Hao mafisadi huyo Nape amewataja? ua ni maswaiba wake maana sidhani kama ana ubavu wa kuwataja. Ameshawaandikia barua za kiinteligensia. Blaa blaa hizi za akina Nape zitawatokea puani, shauri zao.

The boxers in the animal farm.:whoo:
 
mmmmmmmmmmmh MASKINI NAPE NAUYEEEEEEE na wewe umeingia katika huu mkumbo,Walahi ita ku cost kama Baba Ridhi1 na wenzake bora ujenge chama chenu cha magamba kivingine na wala usimjaribu huyu raisi wa Wananchi Dr.Slaa utapotea katika Anga za siasa za Bongo:rant::spy:
 
  • Thanks
Reactions: SpK
Huko ni kutapatapa kwa viongozi wa CCM.

Dr. Slaa amekuwa siku zote mwiba mkali katika kupambana na ufisadi si kwa maneno tu bali kwa vitendo. Mapambano haya yamekuwapo hata kabla CCM hawajivua gamba. Madai ya Nape yanahitaji uthibitisho kutoka kwake yeye mwenyewe na si Dr. Slaa, kwani the basic principle is that "He who alleges must prove". Dr. Slaa amekuwa aki- allege na kuwataja hadharani viongozi wa CCM ambao ni mafisadi na amekuwa akilithibitisha hilo. Sasa hizo tuhuma za Nape zahitaji kuthibishwa na yeye mwenyewe na si Dr. Slaa
 
  • Thanks
Reactions: SpK
...Dk Remmy Ongala (RIP) alipata kuimba "ukiwa mtenda mabaya kila siku utasema unaonewa..ukiwa mtenda mabaya kila mtu utasema m'baya". RA na kundi lake wameanza ku-hit back sasa kina Nappe wanaweweseka na kudhani RA anatumiwa na CDM/Slaa (PhD)!! kama Slaa anaweza kuwatuma kina RA na Chenge wazishambulie CCM then Slaa yupo juu.
CCM wanaogopa/wanakimbia kivuli chao
 
akili zako za kiTAMBWE HIZZA utazijua tu.

Dr. SLAA ametoa list na wote wale waliotajwa wana makosa ya wazi kama waliyonayo EL,RA ,AC sasa kazi kwa CCM kuchukua uamuzi wa kuwatosa hao jamaa pamoja na list mpya.
Kwa sasa CCM itabaki chafu kwani hakuna mwenye ubavu wa kuiondoa hiyo list ndani ya CCM.

Kumbuka JK alikuwepo kwenye list of shame kwa hiyo Sekretariet inataka kusemaje hapa?
(CCM walitaka kuwaondoa watatu tu EL,RA,AC halafu waanze kudai ni chama kisicho na mafisadi ila Dr. SLAA amewawahi)
 
Mbona sioni sehemu Dr.Slaa anatajwa?
NI kweli mafisadi wanatumia vyama vya siasa ila sio chadema!
CUF,NCCR,TLP ndo wanaotumiwa na nadhani hakuna asiye jua na ndo maana nape kasema alilosema!
Dr.Slaa anaingiaje hapo?
 
:panda:Mh!!!, nina wasiwasi na uwezo wa NAPE ktk kufikiria, amehisi hiyo ndio njia sahihi ya kuanza kukisafisha CHAMA? CCM wametoa gamba wameweka gamba,!!??.

mbona simwelewi kuwa mafisadi wanamtumia SLAA ili awachafue?, it does not make sense. :teeth:
 
Nape kaingia choo cha Kike.
watacheza sana ngoma ya CDM mwaka huu. Nia ni kuhakikisha wapo kwenye kuzuia wakati CDM wanashambulia goli.
Nape anatakiwa atafakari, apime, ashauriwe, na achuje kila anachosema. akiendelea na mwendo huu wa kuropoka ajue hana mwezi bendi itamshinda na santuri itakataa kuuza. Masikini kijana mdogo anacheza ngoma ya kulinda mafisadi. Mafisadi ndani ya CCM wamejipanga wakisaidiwa na mwenyekiti wao.
 
Kashaga, wanaotumiwa na mafisadi ni kina wewe pamoja na nape. maana Nape anawatetea kundi mafisadi na analishambulia lingine waTZ wanataka nape pamoja na mafisadi anaowashambulia na anaowatetea wapelekwe mahakamani.

Nape kapewa ulaji na mafisadi ili kuokoa boti sasa anaona boti zote mbili zinataka kuzama, amebaki kupiga kelele tu. Wote ni mafisadi tu kama hataki ahame CCM na kuanzisha chama cha.

CCM wanataka kujinasu kwa kuwatumia kina Nape wanafiki wao wasafi hakuna lolote.
 
kwani ile list of shame ya mafisadi 11 ya mwembe yanga mwaka 2007 dr alishinikizwa na mafisadi gani kuwataja?, kwa nini wakati huu ambapo ccm inavyosadikika kujivua gamba kwa sababu ya mafisadi halafu tena dr atumiwe na mafisadi hao hao walioko kwenye list yake. nadhani ni busara zaidi kama tukitenganisha uongo na ukweli kwani havikai pamoja.
 
Mbona hilo sio balaa? Hao mafisadi huyo Nape amewataja? ua ni maswaiba wake maana sidhani kama ana ubavu wa kuwataja. Ameshawaandikia barua za kiinteligensia. Blaa blaa hizi za akina Nape zitawatokea puani, shauri zao.

The boxers in the animal farm.:whoo:
Wakati mwiingine huwa unafikiria mkuu
 
Hiyo ni according to kashaga sio nape!!! Dr slaa sio mtu wa caliber hiyo ya kipuuzi kama unayoiongelea hapo juu hata nape analijua hilo na kwa uelewa wake hawezi kumtaja Rais halali wa JMT katika ujinga kama huo.
 
mmmmmmmmmmmh MASKINI NAPE NAUYEEEEEEE na wewe umeingia katika huu mkumbo,Walahi ita ku cost kama Baba Ridhi1 na wenzake bora ujenge chama chenu cha magamba kivingine na wala usimjaribu huyu raisi wa Wananchi Dr.Slaa utapotea katika Anga za siasa za Bongo:rant::spy:

Did u say Rais wa wananchi??..........lol:A S 465::A S 465:
 
hiyo ni according to kashaga sio nape!!! Dr slaa sio mtu wa caliber hiyo ya kipuuzi kama unayoiongelea hapo juu hata nape analijua hilo na kwa uelewa wake hawezi kumtaja Rais halali wa JMT katika ujinga kama huo

Sure,sijaona sehem yoyote anatajwa
 
Nape kaingia choo cha Kike.
watacheza sana ngoma ya CDM mwaka huu. Nia ni kuhakikisha wapo kwenye kuzuia wakati CDM wanashambulia goli.
Nape anatakiwa atafakari, apime, ashauriwe, na achuje kila anachosema. akiendelea na mwendo huu wa kuropoka ajue hana mwezi bendi itamshinda na santuri itakataa kuuza. Masikini kijana mdogo anacheza ngoma ya kulinda mafisadi. Mafisadi ndani ya CCM wamejipanga wakisaidiwa na mwenyekiti wao.


Bahati mbaya sana uwezo wa kufikiria hana,kama anao basi ume diffuse kwa sababu ya kua ndani ya chama cha majinga
 
Teh teh,kichwa cha habari hakiendani na unayoyaandika humu
eti "BALAA" wewe unajua maana yake au unajiandikia tu kama ulivyotumwa,na kwa jinsi mlivyozoea kuchakachua vitu na kiswahili nacho unachakichakachua
 
Back
Top Bottom