BAKWATA wafanya Maandamano kupinga Mapenzi ya Jinsia Moja, Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia na Mauaji

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
ushoga 1.jpg


Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Mwanza, limefanya maandamano ya amani kupinga mapenzi ya jinsia moja, Ushoga, ulawiti, ukatili wa kijinsia pamoja na mauaji.
---

Pia soma
- BAKWATA yawataka Watanzania kukataa ndoa za jinsia moja, Mufti ashangazwa wanaume kulawitiana ilhali wanawake wa kuolewa wapo

20230306_110443.jpg


bakwata.jpg


ushoga.jpg

Baraza kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata ) Mkoa wa Mwanza, limefanya maandamano ya amani kupinga mapenzi ya jinsia moja, Ushoga, ulawiti, ukatili wa kijinsia pamoja na mauaji.

Aidha Bakwata Mkoa wa Mwanza, wamesema wamepokea na kuunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt, Abubakari Zuber Bin Ally juu ya kupinga na kukemea vikali matendo yote haramu

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke ameishukuru Serikali kwa umakini wake wa kuchukua hatua za haraka pale tu inapobaini kuwepo na ulazima wa kupiga marufuku kuendelea kutumika kwa vitabu visivyo faa katika shule zetu nchini

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Alhaji Nuhu Jabir Mruma amelipongeza Baraza Kuu la Waislam Mkoa wa Mwanza kwa kuunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt, Abubakar Zuber Bin Ally juu ya kupinga na kukemea vikali viendo vyote haramu.

Mzawa
 
Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Mwanza, limefanya maandamano ya amani kupinga mapenzi ya jinsia moja, Ushoga, ulawiti, ukatili wa kijinsia pamoja na mauaji
 
Jambo zuri Mungu awabariki ndugu zetu katika imani, ila next time msiweke watoto kwenye masuala kama hayo. Maana baada ya hapo wataanza kuulizana nini maana ya jinsia moja na tutatengeza kizazi chakujaribu!

Yani wajaribu waone inakuwaje.
 
Wanazuga tu waonekane wanapinga. Approach wanayoitumia ni dhaifu, haina tofauti na NGs zingine. Wamejishushia hadhi, wakristo wasijaribu kuiga maandamano kama haya hawataeleweka wanapinga nini wakati biblia imepinga mambo hayo waziwazi.

Itakuwa ni uzembe wao kuhubiri ukweli uliobainishwa na biblia. Mambo mengine waachieni wanasiasa wapambane nayo na siyo wanasiasa kuwatupia mzigo uliowashinda kwa kukosa mbinu za kupambana nazo.

Hayo mambo ni dhambi, ni uzembe wa dini kuhubiri, wanasubiri wanasiasa wawakurupushe ndio wajitokeze kupinga? Ni unafiki mtupu
 
Back
Top Bottom