BAKWATA: Mgomo wa madaktari ni batili

Hatuelewi?
Hatuwezi kujadili uhalali au ubatili wa vitu bila kuhusisha dini na viongozi wa dini?
Uhalali au ubatili wa mgomo wa madaktari unapaswa kuwa mtizamo wako si wa kukopa kwa shehe au padri au mchungaji
Jadilini hilo
Bakwata au makanisa waseme kwa niaba yao si yako wewe
Wewe una akili timamu, changanua pumba na mchele na sema kile unachoamini kuwa sahihi na jaribu kuwaelimisha wanaopingana na wewe wakuelewe sio uwakashifu
Kukashifu Bakwata au Makanisa ni upumbavu wa hatari na wa kupingwa na nguvu zote
 
Kila siku Mnalalamika MOU,MOU,MOU..Kwani nyinyi mlikatazwa kuanzisha hospitali zenu ili na nyie mpokee hiyo ruzuku kama ya Mou? Acheni kupiga domo tu,kama vipi na nyie anzisheni hospitali zenu mtapewa ruzuku na serikali ya baba rizi1.

MoU= EPA = RICHMOND

Tutapiga kelele hadi kanisa liache ufisadi wa mali za umma: nitafafanua

a. Wanapokea pesa za Umma (waislam na wakristo)..unaudited ???

b. Hospitali wanatulipisha fee kubwa (diagnosis, dawa etc kupita hospital ya serikali) wote waislam na wakristo??? (biashara persee) huu ni uwizi

c. Wanapokea sadaka kutoka kwa waumini (hili hatuna shida nalo)..

A and B is unacceptable na UWIZI wa mchana..tutapiga kelele hata kama mmefunga masikio na kula bila kanawa shwan..
 
Mkuu hata hayo makanisa yanayopewa pesa na Serekali naona watumishi wao wanagoma. MOU useless in Tanzania. CCM iache kukumbatia makanisa kuwapa pesa badala yake pesa za watz *zilenge kuboresha mahitaji ya madaktari

Kwenye Hospitali za Makanisa kuna Watumishi wa Serikali ambao wamekuwa Seconded huko. Pia serikali imekuwa ikizihadaa hizo hospitali kwa kutopeleka madawa pamoja na vifaa kama walivyokubaliana kwenye MoU. Hospitali hizi zimekuwa zikiiomba serikali kama wameshindwa kupeleka madawa na vifaa basi wao wanunue kwa pesa zao alafu wapandishe bei ya huduma maana manunuzi ya vifaa na madawa wananua kwenye Open Market ambako bai ni kubwa kuliko bei za Medical Store Department (MSD), ambao kimsingi ndio mwakilishi wa serikali katika kusambaza madawa na hospitali nchini.

TUMBIRI (PhD, University of Hull - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Kwenye Hospitali za Makanisa kuna Watumishi wa Serikali ambao wamekuwa Seconded huko. Pia serikali imekuwa ikizihadaa hizo hospitali kwa kutopeleka madawa pamoja na vifaa kama walivyokubaliana kwenye MoU. Hospitali hizi zimekuwa zikiiomba serikali kama wameshindwa kupeleka madawa na vifaa basi wao wanunue kwa pesa zao alafu wapandishe bei ya huduma maana manunuzi ya vifaa na madawa wananua kwenye Open Market ambako bai ni kubwa kuliko bei za Medical Store Department (MSD), ambao kimsingi ndio mwakilishi wa serikali katika kusambaza madawa na hospitali nchini.

TUMBIRI (PhD, University of Hull - UK),
tumbiri@jamiiforums.com


Hospitali zinapewa ruzuku lakini bado bei kufanya diagnosis na madawa ni kubwa kupita hospitali za serikali...

Kwanini serikali ipeleke watumishi wake hospitali za kanisa wakati hospitali za serikali kuna upungufu wa madr.. (akili au matope??
 
Kila tamko linalotolewa na mwislam mnalichukulia kama ni tamko la Bakwata, huyo mnayemwita Katibu wa Vijana wala hatambuliki na bakwata!!! mbona kwn kipindi cha Jambo TBC1 leo asubuhi walikuwepo viongozi wawili wa dini m1 ni mkristo na mwingine ni sheikh wote walionekana kuwasihi madaktari kutokugoma na kuishauri pia serikali kusikiliza malalamiko ya madaktari
 
Pamoja na Uislamu wangu, napinga hili tamko la Katibu Mkuu wetu wa Vijana BAKWATA. Napinga pia shinikizo la kutulazimisha tusihesabiwe kwenye sensa. Hivi sisi Waislamu tuna tatizo gani? Kwa nini tunalalamikia mambo ambayo hayana mshono na Uislamu wetu?

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com

Bakwata imekuwa kama kikundi cha watu fulanifulani wachache ambao wanaamua mambo au kutoa matamko kwa kivuli cha uislam. Itafikia wakati waislam watachoshwa na haya na hapo ndipo kasheshe litakapoanzia. Kuna wakati waislam wanajiuliza haya matamko huwa wanamshirikisha nani hasa? je huwa wanapata baraka za haya matamko yao na waislam au wawakilishai wa Tanzania nzima?

Waslam ifike mahali sasa kupinga matamko yote ambayo yanaidhalilisha dini hii. mengi sana ya haya matamko ya wanaojiita bakwata ni ya aaibu tu.
 
Mods lugha hizi za kejeli,dharau na kuudhi natumaini kama mnazifuatilia. Kwa haiba nzuri ya furum hii naomba mchukue hatua dhidi ya kauli hizi na mtoa kauli hii.

Back to the nukta. Tukiondoa ushabiki wa dini, jambo gani baya walilotamka BAKWATA, hivi kutowataka madaktari kushiriki katika mgomo badala yake warudi makazini kwani uamuzi wao huu una athari kubwa sana kwa wananchi.

Naamini, ikiwa maamuzi yakuipinga BAKWATA hayakutawaliwa kisiasa inayolenga kuiangusha serikali iloiyoko madarani kwa kufanya nchi isitawalike. Leo Madaktari, kesho waalimu. Hivi nyie pro-CDM mbona mko kwenye the same line? Kutukana uislamu na taasisi zake sambamba na kuunga mkono maamuzi haya ya kinyama ya madaktari.

Umeanza vizuri ila umemaliza kwa namna ileile unayoipinga wewe,aliyekwambia wanaopinga tamko la BAKWATA ni pro CHADEMA ni nani? kauli kama yako hii ndo inaweza chochea kauli au maneno uliyowalalamikia mods kuwa ni ya kejeli na dharau! umakini unahitajika zaidi hapa na zisitumike hisia
 
Hospitali zinapewa ruzuku lakini bado bei kufanya diagnosis na madawa ni kubwa kupita hospitali za serikali. Kwanini serikali ipeleke watumishi wake hospitali za kanisa wakati hospitali za serikali kuna upungufu wa madr.. (akili au matope??

Mkuu Topical,
Ni kweli serikali pamoja na kukubaliana kupeleka madawa na vifaa, serikali pia inawajibu kupeleka Ruzuku na Bed Grants. Bahati mbaya ruzuku inayopelekwa mara nyingi inaanzia Million mbili hadi sita. Na kuna miezi baadhi ya hospitali zinatoka kapa kwa hoja kwamba serikali haina fedha. Sasa jiulize Hospitali haijapelekewa madawa, vifaa tiba na ruzuku haijaendea na bado unataka watoto, wazee, wazazi na wazee watibiwe bure. Alafu wakati huo huo bei za huduma kwa wagonjwa wengine zipunguzwe, watawazaje kuendesha?

Nimetembelea Hospitali nyingi za Mashiriki ya dini kuanzia Ilulu Hospital (DDH), Tosamaganga Hospital (DDH), Ilembula Hospital (VAH), Ikonda Hospital (VAH), Bulongwa Hospital (VAH), Lugarawa Hospital (VAH), Milo Hospital (VAH) na Bunda Hospital (DDH) ruzuku wanazopata ni chini ya Milioni 5 kwa mwezi na bado serikali haipeleki madawa na vifaa. Hilo la kwanza.

La pili. Swala la kwa nini serikali inapeleka watumishi kwenye hizo serikali ni miongoni mwa makubaliano walioingia na mashirika ya dini ili waweze kutoa huduma kwa bei nafuu. Vinginevyo wangeweza kuajiri wao wenyewe na kuwalipa mishahara wao wenyewe kama Agha Khan au Regency. Swali linakuja ni watanzania wangapi wangeweza ku-afford gharama za huduma??

Tanbihi:-
DDH - District Designated Hospital
VAH - Voluntary Agency Hospital

TUMBIRI (PhD, University of Hull - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Last edited by a moderator:
UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA.
MADAI
1. Kuboresha Huduma za afya hospitalini kwa vifaa vya upimiaji, madawa.
2. Kuboresha Mazingira Ya kazi (ukarabati wa majengo, uongezaji wa vitanda)
3. Posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) 5% kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote.
4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu 40% ( MEANING anayefanya kazi SAME, TANDAHIMBA, NYAMPULUKANO nk ni tofauti na akaaye MJINI)
5. Posho ya makazi 40% au nyumba kama ilivyo kisheria(since DOCTOR IS ENTITLED KUPATA, HII NI KATIKA SHERIA YAO WENYEWE)
6. Bima ya Afya(Green Card) kwa wafanyakazi wote wa sekta ya Afya.
7. Kuwaondoa viongozi wa juu wa W/Afya kutokana na ubadhirifu.
8. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi 30% au Chanjo(Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB)

MAKUBALIANO
1. Kuondolewa kwa viongozi na watendaji wa juu wa Wizara ya Afya
2. Kupewa nusu ya ombi la call allowance hadi pale baada ya mazungumzo(ktk kipindi cha mpito)
3. Kamati kujadili na kuona kiasi gani mshahara na posho zitaongezwa kwa kutengeneza(developing a formula)
4. Serikali kuongeza bajeti ya W/Afya ili kuongeza vifaa, na madawa.

HALI ILIVYO SASA
- HOSPITALINI: hakuna huduma za afya (matibabu, upimaji wala upasuaji), YAANI NI KWELI TUMEGOMA
- VYOMBO VYA HABARI: Kuna upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwa umma.
- MTAANI:Hofu na mashaka kwa wananchi kutokana na kutoelewa matamko yanayopingana kati ya Serikali na Tamko la madaktari

MTAZAMO
HEBU ANGALIA KATIKA MAKUBALIANO NI LIPI LIMETEKELEZWA HADI SASA?? THEN SERIKALI INAONGEZA MISHAHARA YA WABUNGE, HIVI KARIBUNI UTASIKIA SABASABA!!!
- Jumla ya madaktari wote ni chini ya 15,000 (na hapa namaanisha General practitioners and Specialists). Kwa uchache au wingi wetu tumekwisha kuona madhara ya migomo miwili iliyokwishatokea.Nashangwazwa na kuona baadhi ya watu wanaosema madaktari hatuna utu wala huruma na tunaweka maslahi yetu mbele, hivi mnajua kuwa katika nchi za East and Central Africa, Tanzania ndiyo yenye kulipa mishahara midogo kwa watu wa sekta ya Afya?? Rwanda juzi juzi(1994) walikuwa na vita lakini daktari analipwa 1500USD, au mnadhani hatujui kuna nchi za jirani na mbali tunaweza kwenda kama wenzetu (Mf. Rwanda, Botswana, Zambia, Lesotho, Egypt, SA, nk)???mnadhani kubaki kwetu Tanzania tuteseke kwa kauli eti "UDAKTARI NI WITO?", "WATANZANIA -WATOTO, KINA MAMA, NA WAZEE WATAKUFA IWAPO TUKIGOMA", "OOOH?? HATUTAKIWI KUGOMA"…tumeonyesha uzalendo wetu kwa kubaki hapa hapa na mazingira yetu magumu, lakini sasa IMEFIKA MWISHO..
Pediatrics(wodi ya watoto):Hakuna vifaa vya kuongezea maji/damu mwilini(cannula), hakuna mitungi ya gesi, OBGYN(wodi ya kina mama);hakuna pamba, mipira ya mikojo(urine bags), MOI, Mwaisela hakuna vitanda, Operating Theatre,OT; Hakuna gloves ,mask, kofia za kutosha, Huduma ya mionzi ya CT SCAN ni mwezi wa saba haifanyi kazi(huku mmiliki akiwa anaidai Wizara ya Afya mil.800/=Tsh)na haitakuwepo hadi atakapolipwa.
Kwa madai hayo, si lazima serikali itekeleze all at once, lakini Mshahara unazungumzika, wale mnaofanya interview, huwa hamuulizwi ni kiasi gani unategemea kuanza nacho na waajiri wenu? Doesn't this make salary being negotiable?? Then kwanini isiwe kwetu?
Hivi ulishawahi kusikia MASS RESIGNATION????? It takes ATLEAST 12yrs kumpata huyo specialist after elimu ya sekondari, Halafu nasikia mnasema eti tufukuzwe kazi?Then what??? Kwa wale wenye mtazamo mfupi mnadhani Serikali inaweza ku-import madaktari toka nje..kwa mfano
1.Ni nchi gani itakuazima madaktari?? Kwa mshahara upi na vifaa gani? CUBA-3000USD, RWANDA-1500USD!!!
2.Hypothetically speaking, wakikusaidia madaktari, watakupatia wangapi??
3.Apartment na transport allowances utawapa kiasi gani?
4.Hivi bibi aliye Tandahimba, asiyejua Kiswahili vizuri ataweza kuongea kiingereza na hao doctors??ama utahitaji wakalimani(translators), if so wangapi??? Utawalipa??
5.Then hao madaktari watakaa hapa milele??
Then NASIKIA MTATUPELEKA MAHAKAMANI.
Utawakamata madaktari wote nchini?? Kumbuka huu mgomo hauna kikomo na hauna kiongozi!!!..hypothetically speaking ukitupeleka, tutawatibu tukiwa huko gerezani?? Waliobaki mnadhani watarudi makazini?tukirudi mnadhani tutafanya kazi? Tukifanya kazi unadhani itakuwa katika kiwango kinachotakiwa? With demoralization unategemea tutaponyesha ndugu zetu kweli, au mortality kuwa juu??? Then kwa wanafunzi walio vyuo vya tiba kama MUHAS, WBUCHS, KCMC, UDOM, HKMU, IMTU..watafanya kazi hapa nchini kwa hali hii, ama Brain drain ndiyo itazidi!!
SIASA.
Wananchi walishazoea kudanganywa, na hii imezoeleka na viongozi Fulani kushindwa kufanya wajibu wao kusingizia wanasiasa kadhaa..Hapa HAKUNA siasa ila mkiileta tutawaachia tu kwani huko hatupawezi ila viongozi mjue hakuna tena rufaa ya kwenda nje(mf. INDIA) MUHIMBILI
Hivi wananchi mnajua viongozi wanalipwa kiasi gani wanapoenda nje kutibiwa na familia???
Eti kwa sababu sekta nyingine hawawezi kugoma, ndio na sisi tusigome? Eti kwa sababu askari anayetumia SMG na kupambana na jambazi anayetumia AK47, eti kwa sababu mishahara ya walimu inacheleweshwa, ndio tusigome??? Nani kasema??
HITIMISHO:
HAPA KAZINI HATURUDI…HII IELEWEKE VIZURI…HATURUDI….MGOJA NIIWEKE VIZURI HATURUDI, ACHA MEDIA IENDELEE KUDANGANYA, LAKINI UKWELI TUNAUJUA, MWISHONI MTARUDI TU, NA THIS TIME SI TENA YA KUTUMIA BUSARA ZETU KUWASTAHI VIONGOZI NA KISHA KWENDA PALE KUONGEA NA ‘WAZEE WA DSM"
"Doctors we might be slow walkers, but we never walk back" ..Solidarity Forever
 
BAKWATA wanahusika vipi kwenye mgomo wa madaktari?

CCM inawatumia BAKWATA kama toilet paper ikimaliza shida zake inawatupilia mbali ila Waislamu wenyewe hajijui kama wanatumiwa,CCM iliwatumia huko kwenye uchaguzi wa Igunga na nasikia hata huko Kusini inwatumia sana ili kufanikisha dhuruma zake.
Waislamu kwa nini hamuamki mnaona la sensa ndo la maana wakati hospitali zote ziko hoi bin taabani hata hao madaktari watafanya nini kama hospitalini hakuna vifaa na dawa???? Mbona hamsemi chochote wakati mafisadi wanatamba nchi nzima na wabunge wanapitisha Bajeti ya kumlemea Mtanzania???????
 
naapa kwammba......sitasiliza radio imaan ktk maisha yangu yote,eeh mwenyezi mungu naomba unisaidie

sio lazima usikilize kwani usiposikiliza unapunguza nini kwenye radio yetu ambayo haina mou kama hayo mahospitali ambayo yana mou lakini madaktari bado wanagoma na sasahivi kuna tv imaan nahiyo pia usiangalie makafiri wana matatizo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
bakwata inaongozwa na vilaza wanakurupuka na kuropoka,mlaaniwe bakwata.

kilaza ni wewe ambae hao madaktari wanatumia hela zako wakati wewe hizo hospitali za kanisa wewe huna hela ya kutibiwa njoo arusha nenda hospitali inayoitwa selian ni yakanisa lutheran kama utaweza kulipia gharama halafu kuna fungu la hela yako zinaingia hapo huo si ukafiri ni nini?
 
jamani naomba nipatieni frequency za hiyo redio imaaan kwa Dar, mimi huwa siipati
 
Back
Top Bottom