BAKWATA iliundwa na nani?
tatizo kubwa wanakosa hierchial ya kiuongozi ndio maana leo utasikia shehe bungo, kundecha mara mkuu wao ponda kasema hili juu ya mufti n.k.

naomba wakajifunze mfumo.mzuri wa.utawala na uongozi kutoka kanisa katoliki.

hao wameibuka baada ya kuona wenye madaraka na BAKWATA wana tumia vibaya rasmali za baraza ndio maana wakaanza kusema ukweli na hapo sioni kama ni tatizo,
 
ukimjengea mtu nyumba unampa aishi kwa matakwa yake si kwa matakwa yako

unauhakika/ ushahidi gani kuwa wanaishi kwa matakwa ya serikali. Au ndio yaleyale ya conspiracy za unexisting mfumo kristo
 
hapa hatulaumu kama unavyotaka wewe hapa tunajadili waundaji wa baraza hilo na kwanini serikali iwe na mikono yake mpk leo

nafikiri waislamu mkiamua kama dini mnaweza, kwani serikali haina dini, tatizo ndani yenu kunawanafiki wengi, lakini mkijipanga mnaweza, mbona makanisa mengi nayaona yapo huru kutoka kwenye mikono ya serikali? Mkifuata sheria na kujenga hoja serikali itawaelewa, ila hofu yangu hapa ni moja harakati zozote zitakazoambatana na vurugu zitaipa serikali sababau ya kufutilia mbali hoja zenu hata kama ni za msingi!
 
na hii ni nukuu kutoka mwandishi Mohamed Said....

[SIZE=+2]Kuvunjwa kwa jumuia ya EAMWS[/SIZE] HII ni sehemu ya nane ya mfululizo wa makala ambazo ni sehemu ya muswada wa kitabu "Mwalimu Julius K. Nyerere, Kanisa Katoliki na Uislamu: Dola na tatizo la Udini Tanzania" kitakachotoka hivi karibuni. Kitabu hicho kimeandikwa na mwandishi maarufu wa masuala ya historia hasa ya Tanganyika BWANA MOHAMMED SAID.
MKUTANO wa Iringa ulipitisha katiba ya jumuiya mpya ya Waislam, katiba ambayo ilikuwa sawasawa na katiba ya TANU. Hivi ndivyo BAKWATA ilivyoundwa.
BAKWATA ikamchagua Saleh Masasi, Muislam tajiri na ambae alikuwa kama mwenyekiti wa mkutano ule kuwa Mwenyekiti wa Taifa na Adam Nasibu akawa Katibu Msaidizi. Nafasi zote za juu katika BAKWATA kama ilivyotegemewa zilichukuliwa na kundi la Adam Nasibu, kundi ambalo toka mwanzo lilikuwa likidai kuvunjwa kwa EAMWS.
Uongozi wa BAKWATA uliomba serikali itambue jumuiya hiyo mara moja na ipige marufuku EAMWS kama jumuiya isiyo halali na mali zake zizuiwe. BAKWATA ilitoa maazimio kadha lakini azimio namba nne ndilo hasa linafaa kuelezwa. Azimio hilo liliomba serikali, TANU na ASP kuwatazama na kufanya uchunguzi wa kina kwa viongozi wote wa EAMWS, hasa Rais, Makamo wa Rais, Katibu wao na baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya ambao wana chuki na hii jumuiya mpya.[SUP]70[/SUP] Uongozi wa BAKWATA katika ushindi wao hawakutaka salama na mawaelewano na Waislam wenzao katika EAMWS wala kuwaonea huruma kama Uislam unavyofundisha, bali ulitaka chama na serikali uwaandame, hasa wale waliokuwa viongozi.
Baada ya kuundwa BAKWATA, ili kuondoa wasiwasi na kuwarudishia imani Waislam, Katibu wa Tume ya Waislam, Mussa Kwikima alitoa taarifa iliyosema:
Hakuna anaeweza kutishia kuwepo kwa EAMWS isipokuwa wanachama wake, sheria na serikali, lakini si watu binafsihata ikiwa mikoa yote kumi na saba ikijitoa haitamaananisha kuwa jumiya imekufa kwa kuwa kuwepo kwake hakutokani na kuwepo kwa mikoa hiyo kama wanachama isipokuwa kuwepo kwa wanachama wake, Waislam.[SUP]71[/SUP]
Wakati ilipotoka taarifa hii BAKWATA ilikuwa bado haijaandikishwa rasmi na Msajili wa Vyama. Kisheria ilikuwa haiwezekani kwa kundi la Adam Nasibu kuunda jumiya mpya iliyokuwa na malengo sawa na jumuiya ambayo tayari ishaandikishwa. Kwa muda wa siku tatu BAKWATA na EAMWS zikawepo kwa wakati mmoja. Ilionekana kama kwamba EAMWS itashinda vitimbi vya serikali na vya kundi la Adam Nasibu.
Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA Cerificate of Exemption na kuifungia EAMWS.[SUP]72[/SUP] Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:
Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[SUP]73[/SUP]
Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.
Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS. Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama. Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza. Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam. Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA. Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe. Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu. BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa. Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa. Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine. Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.
Huu ndiyo ukawa mwisho wa kile kilichokuwa kikijulikana kama mgogoro wa Waislam ulivyomalizika. Mgogoro ambao ulianza pale mwalimu wa shule ya msingi asiyefahamika na yeyote alipofanya maandamano katika mitaa ya Bukoba akimuunga mkono Julius Nyerere na Azimio lake la Arusha na ukaishia kwa mwalimu huyu akiwa na nafasi juu katika jumuiya ya Kiislam ambayo ilikuwa ikichukiza machoni mwa Waislam. Mwalimu huyu ambae sasa amekuwa Makamu Katibu Mkuu wa BAKWATA alianza kazi yake kwa kuwashutua Waislam. Katika mkutano wa waandishi wa habari Adam Nasibu aliiomba TANU na ASP kujikinga na watu wanaohujumu umoja wa nchi kupitia dini. Akaendelea na kusema kuwa BAKWATA ni sawa na Baraza la Kikristo la Tanzania. [SUP]74[/SUP] Kwa kuwa Waislam walinyimwa fursa ya kujadili "mgogoro' hivi sasa kilichobaki na dhana tu, kuwa nini kingelitokea endapo wangeliruhusiwa kufanya mkutano ule ulioitishwa na EAMWS. Waislam wa Bukoba ambao ilitaarifiwa kuwa walifanya maandamano kuunga mkono Azimio la Arusha hawakutayarisha maandamano ya kuunga mkono BAKWATA. Dar es Salaam na katika miji mingi ya Tanzania, neno BAKWATA halina tofauti na tusi. Kumuita Muislam kuwa yeye ni mwanachama wa BAKWATA ni sawa na kumuita Mkristo mfuasi wa Yuda Iscariot, aliyemsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.
Mjumbe mmoja wa Tume ya Waislam inastahili kuelezwa habari zake - Mussa Kwikima. Mussa Kwikima mwaka 1968 alikuwa ameteuliwa kuwa jaji na Rais Nyerere. Yeye ndiye hasa alikuwa nguvu kuu katika tume ya Waislam. Wakati alipojitolea kuisaidia tume katika kupambana na kundi la Adam Nasibu, Waikela alimuonya kuhusu hatari ambayo itamkabili yeye mwenyewe binafsi na kazi yake. Kwikima alijibu kuwa umoja wa Waislam ni muhimu kuliko maslahi yake binafsi. Ilipoundwa BAKWATA na hapo kuwa ndiyo mwisho wa 'mgogoro', Kwikima alihamishwa kutoka Dar es Salaam na kupelekwa Mwanza kama Hakimu Mkazi na Rais Nyerere akamvua madaraka ya ujaji wake. [SUP]75[/SUP]
Kilichobakia baada ya kuvunjika kwa EAMWS ilikuwa ni kujaribu kuiweka BAKWATA katika mikoa kama jumuiya inayowakilisha Waislam wote wa Tanzania Bara. Mwaka mzima wa 1969 Adam Nasibu na kamati ya watu wanne walitembea katika mikoa wakiahidi msaada wa fedha kwa katibu yeyote wa zamani wa EAMWS ambae atashirikiana na BAKWATA makao makuu kuisaidia kufungua ofisi katika mkoa wake. Waislam waliipuuza BAKWATA.
Tabora ambayo haikujitoa katika EAMWS, serikali iliwaruhusu Adam Nasibu na kikundi chake kufanya mkutano wa hadhara. Kabla Adam Nasibu hajahutubia Waislam, Maulid Kivuruga mmoja wa wakongwe wa African Association na muasisi wa TANU Tabora, alipanda jukwaani kwa niaba ya Waislam wa Tabora na kuweka sharti kuwa Waislam watakuwa tayari kumsikiliza Adam Nasibu endapo Waikela mjumbe wa Tume ya Waislam iliyokuwa ikitafuta sulhu na yeye ataruhusiwa na serikali kuwahutubia Waislam ili aeleze upande wa pili wa kisa kile. Kivuruga alisema kuwa Waislam wanaomba sharti hili likubaliwe kwa sababu katika Uislam panapotokea mgogoro basi mpatanishi ni lazima asikilize pande zote mbili. Sharti hili lilikataliwa na BAKWATA na serikali. Palepale mbele ya waheshimiwa wa serikali na viongozi wa BAKWATA, Waislam wakaanza kuzomea huku wakitawanyika wakipiga takbir na wengine wakiitikia Allahu Akbar.
Siku chache baada ya tukio hili Waikela aliitwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai kusailiwa kwa nini anaipinga BAKWATA. Wakiwa ndani ya chumba cha Tabora Hotel, Geoffrey Sawaya, Mkrugenzi wa C.I.D, alimpiga maswali Waikela na kutaka kujua kwa nini yeye hayuko tayari kushirikiana na serikali kuipa nguvu na kuieneza BAKWATA. Sawaya akatoa hongo ya shilingi elfu arobaini kwa Waikela ili asaidie kuimarisha BAKWATA. Waikela kama istizai alimuuliza Sawaya kama fedha zile zilikuwa zimetoka bait mal. Waikela alikataa kupokea hongo ile. Sawaya akamtisha lakini Waikela hakutishika. Waikela aliwekwa ndani ya chumba kile akiulizwa maswali kwa kiasi cha saa nne na kisha akaamrishwa kuweka sahihi yake katika makaratasi fulani. Hili alilifanya. Waikela hakufuatwa tena na serikali. Ingawa kulikuwepo na juhudi za chinichini za kuipinga BAKWATA, juhudi hizi hazikushinda kwa kuwa BAKWATA iliweza kufungua matawi yake nchi nzima pamoja na Tabora. Wapo baadhi ya viongozi ambao hawakuweza kuhimili vishawishi vya kupokea ile hongo ya serikali na kwa ajili hii walishirikiana na serikali hivyo kuwezesha ofisi za BAKWATA kufunguliwa, hata kama zipo pale kwa jina tu. Kuangushwa kwa EAMWS kulisababishwa na watu watatu ambao wao ndiyo walikuwa mstari wa mbele kabisa - Adam Nasibu, Sheikh Kassim Juma na Abdallah Chaurembo[SUP]76[/SUP] - na njama hii ikaungwa mkono na Rashid Kawawa na Abeid Amani Karume. Mkono wa Julius Nyerere na Kanisa Katoliki katika njama hii haukuonekana kabisa kama ilivyo kawaida katika njama zote za kupiga vita Uislam na Waislam Tanzania

kwanza who is waikela?? KINGINE nilipofika kwenye maandishi haya mwili ukasisimka( Kuangushwa kwa EAMWS kulisababishwa na watu watatu ambao wao ndiyo walikuwa mstari wa mbele kabisa - Adam Nasibu, Sheikh Kassim Juma na Abdallah Chaurembo76 - na njama hii ikaungwa mkono na Rashid Kawawa na Abeid Amani Karume. Mkono wa Julius Nyerere na Kanisa Katoliki katika njama hii haukuonekana kabisa kama ilivyo kawaida katika njama zote za kupiga vita Uislam na Waislam Tanzania)
 
hata kama ni mgeni hamna lisilowezekana!

Kuangushwa kwa EAMWS kulisababishwa na watu watatu ambao wao ndiyo walikuwa mstari wa mbele kabisa - Adam Nasibu, Sheikh Kassim Juma na Abdallah Chaurembo76 - na njama hii ikaungwa mkono na Rashid Kawawa na Abeid Amani Karume. Mkono wa Julius Nyerere na Kanisa Katoliki katika njama hii haukuonekana kabisa kama ilivyo kawaida katika njama zote za kupiga vita Uislam na Waislam Tanzania
 
unauhakika/ ushahidi gani kuwa wanaishi kwa matakwa ya serikali. Au ndio yaleyale ya conspiracy za unexisting mfumo kristo[/QUOTupo]

upo kama serikali au upo kama nani,ushahidi unadaiwa mahakamani hapa ni hoja tu.
 
Ndugu, hii ishu ya BAKWATA, imekua kama jinamis!! waislam baadhi hawaitaki na kigezo ni kuwa ipo close na serikali!! Lakini kiundani ni kwamba BAKWATA ile ya mwanzo na uongozi wake, wameshindwa kufanya mabadiliko kwenda na wakati, idadi ya waislam imeongezeka, dunia imebadilika, wale mashekhe wamebaki rigid. Mabadiliko kwenye uislam yamepata nafasi, hivyo nchi za kiarabu, maana ndo zenye ushawishi na dini hiyo, zimeibuka na makundi, mfano ushia, answar sun nk umekua na kujitanua, hivyo bakwata ikajikuta haiweza kumeza mabadiliko hayo yote!!

Kuna watu hawataki bakwata, lakini hawaji na njia mpya ya kutatua tatizo wamebaki na maneno tena yale ya viongozi waliokataliwa na kisha kuizushia bakwata mabaya, bila jema hata moja, naamini ina mema yake.

Je Bakwata ndo tatizo? Jibu langu hapana, katika dini hii misikiti yote ni mali ya watu flan, ama aliye ujenga, au imamu wa pale au au....., hivyo organization structure ya uislam ipo ngumu kiasi. Mfano shekhe wa wilaya hana sauti na mamlaka ya kuchagua maimamu wa misikiti katika misikiti iliyopo eneo lake, na mkoa n,k nini madhara yake? hamna mwenye kumtii mwingine. shekhe mkuu hawezi mkanya/ adhibu au kumfukuza, shekhe/imamu wa mkoa, wilaya, au kata.
Hivyo yake kila msikiti umekuwa independent hivyo kufanya individual decisions, wakati mwingine zina kwanza Bakwata as organization.

Nini kifanyike? kuvunja Bakwata siyo suluhu, ila kuimodern ma kure-organize ikiwa na kureform institution ili iendane na wakati ni muhimu sana!! tatizo nani anafanya hivyo? je TAMPR, MAULAMAA, wasomi n.k wanafanya nini? nao walalama!!! ajabu na kweli!!! Kosa ambalo leo limefanywa ni kuwa na vitasisi vingii, vidogo vidogo vya kislaam kisha vina bishana venyewe, kisha vinatoa maoni kwa niaba ya waislam wote, ingawa wengine hawavitambui.

Nani aliunda BAKWATA jibu lake siyo suluhisho, BAKWATA ifanye kazi zake kwa ufanisi hilo ndo suluhisho!!, we never walk the dead, otherwise we shall never stop complains.
Sp

msingi wa nyumba ndio huishika nyumba isidondoke,vivyo hivyo waloiunda ni lazima wahakikishe inakuwa mikononi mwao kwa maslahi yao wenyewe......
 
Bakwata liundwa na waislam kwa msaada wa serikali.kwa sasa waislam wanataka waunde mahakama ya kadhi kwa masaada wa serikali.

Bakwata na EAMWS kipi kilianza? Jibu ni EAMWS, Je EAMWS kilianzishwa na nani? je kwa nini chombo hiki kilivunjwa?
 
Kusahihisha makosa si rahisi kwasababu mfumo aliouanzisha mwl juu ya bakwata ni uleule na watu ni waaina ile ile, kwa mfano shekhe mkuu wa mkoa wa dar es alaam ni shushu wa serikali na halina ubishi,
Na hao ndo aina ya watu waliopo bakwata na ndio maana serikali inawakumbatia na kuwakingia kifua
Huku hao watu wakitumikia mfumo kristo unaondesha serikali bila ya kujitambua.
 
hili ndiyo tatizo la waislamu, wakisaidiwa wanalalamika(NYERERE ALIWASAIDIA KUWAUNGANISHA KWA KUWAANZISHIA CHOMBO BAKWATA) wasiposaidiwa wanalalamika(KIKWETE KAKATAA KUWASAIDIA KUANZISHA MAHAKAMA YA KADHI) wananungunika kila siku! KWELI HAWA NI MAJANGA!

'mahakama ya KADHI kwa unavyojua imekataliwa na kikwete au unaropoka tu...'
 
nyie ndio wakuyatoa hayo mapandikizi, serikali haina dini itayatoaje? Au serikali inaratibu chaguzi za bakwata?

'kama haina DINI kwa nini inaing'ang'ania na kuikumbatia......................waislam hawamtaki sheikh mkuu serikali inaingilia kati,pia hawaitaki taasisi yenyewe bado serikali inazuia halaf unasema haina dini serikali?'
 
unavyo ongelea bakwata,nimfano wa ccm.kijana anae jitambua hawezi kuipenda ccm,hivyo hivyo kijana alie timamu hawezi kuipenda bakwata.ccm mafisad na bakwata nao mafisadi.
 
Kama tatizo lishajulikana ni bakwata & serikali ya ccm. Sasa waIslaam mmefanya nini kuondokana na hili tatizo...
 
Kama bakwata itakuwa tayali kufanya chaguzi ktk misikit.nakitaifa wataona moto wao.tunaomb serikal iyache hii bakwata ijiendesh yenyewe.viongoz wengi wabakwata elimu hawana.kuandika shida.bakwata imeshindwa hata kulipa maustadh wa madrasa.hawana mikakati yoyote ile ya kuendeleza dini yao.wao nikuendesha malumbano yahuyu kafuga ndevu ndefu,nahuyu kaswali nasuudia basi.taasisi nyingine zinamipango mizuri.lakin bakwata na serikali hazitaki kizitambua rasmi.nandio kilio kikubwa cha waislamu.
 
je hilo ndio lilikuwa dhumuni la BAKWATA???? kama ni kweli kwanini limekuwa liki lalamikiwa kila kona na waislamu wengi watoto kwa wakubwa??

Unaposema inalalamikiwa na Waislam wengi, what if na mimi nikisema inaungwa mkono na Waislam wengi? Swali hapa ni wangapi?

Ponda alipounda hiki kikundi chake cha ugaidi, amepata wapi ridhaa ya kusema anawawakilisha Waislamu?

Hapa kuna jambo moja la msingi unapaswa kujua. Uislam hauna hierarchy inayoeleweka kimataifa at the same time, Waislam wanataka sauti ya pamoja kama walivyo Roman Catholic. Hii ni ngumu. Ni ngumu kwa msingi kwamba, hata leo hii ikiondolewa BAKWATA, hakuna namna Waislam wanaweza kujiunda na kujiwekea chombo/taasisi. Mfano mzuri ni haya makanisa yanayochipuka kila leo kiasi mengine yana majina ya binadamu...Kanisa la Mwasota, Kanisa la Mpimbinjenje n.k, as far as hayana established central board, basi hakuna kukubaliana.

Wakati Ponda anaandaa harakati za kuing'oa BAKWATA, nataka nikukumbushe kuwa lilikuwepo kundi lingine la Waislam lililosema hawatanyamaza kuona Mufti anakosewa adabu na Ponda. Tell me brother, who will tell who, on who are Muslims and who are not?

Sunni hawawatambui Waislailiya kuwa Waislam na katika nchi nyingine wanawaua kabisa. Sunni na Shiite hawafungamani kama uonavyo Iraq, Syria, Iran na kwingineko, je wewe Sunni (mathalan), utakuwa radhi kuongozwa na Shiite?
 
Kama tatizo lishajulikana ni bakwata & serikali ya ccm. Sasa waIslaam mmefanya nini kuondokana na hili tatizo...
md25 yanayo msibu ponda nihayo yakukataa dhulma na uhuni unao fanywa na bakwata.hiki chombo kimekuwa kandamizi sana kwawaislam.mabwana zao ccm nao ndio wanao wapa kiburi.mchukue simba wa bakwata,umwambie huo umufti wake wagombee yeye na kishki,atapata aibu.bakwata ni janga kubwa,nandio wavuruga amani tanzania .viongozi wao niwanafki kupitiliza,wamejaa njaa natamaa.hawa ndio mashekhe ubwaba.nataman nimkamate mmoja nimtie bakora.
 
mwana mtoka pabaya
Ponda si gaidi,toka zaman bakwata wangekuwa naakili nao wangeaanzisha shule zao na hospitali zao.kama katoriki.nawangeweza kulipa mishara vizur tu.tatizo hawana mipango yoyote zaid yakuendeleza migongano isiyo na tija.
 
Back
Top Bottom