BAKWATA iliundwa na nani?
Ni muhimu kwa waislamu wote kuwa na baraza halisi linalowawakilisha kikamilifu ili waweze kuwa na sautimoja inayo wakilisha waislamu wote wa madhehebumbalimbali ili waweze kuangalia maslahi yao ,kuchangia katika ujenzi wa taifa, ustawi wa jamii, kuweka mawasiliano na kuimarisha uhusiano na dini nyinginezo. Inavyoonekana BAKWATA ilivyo sasa na tangu kuasisiwa haikufanya kazi yake na imekuwa chanzo cha mgawanyiko wa waislamu na kuleta matatizo makubwa ambayo athari zake si kwa waislamu tu bali nchi nzima. Pia BAKWATA inajulikana kwa ufisadi katika miradi yake na raslimali zake. Swali muhimu kujiuliza ni nini kinachozuiwa hii taasisi isirekebishwe na mfumo mpya ? kila mtu anajua waislamu na wengineo kuwa kuna umuhimu wa Bakwata kubadilishwa na katiba yake kuundwa upya ili iweze kufanya kazi yake inavyotakiwa kwa maslahi ya waislamu na Tanzania kwa ujumla. Muhimu BAKWATA mpya lazima iwe ya kidemokrasia ,iendeshwe kwa kanuni na UWAZI .
 
Ndugu, hii ishu ya BAKWATA, imekua kama jinamis!! waislam baadhi hawaitaki na kigezo ni kuwa ipo close na serikali!! Lakini kiundani ni kwamba BAKWATA ile ya mwanzo na uongozi wake, wameshindwa kufanya mabadiliko kwenda na wakati, idadi ya waislam imeongezeka, dunia imebadilika, wale mashekhe wamebaki rigid. Mabadiliko kwenye uislam yamepata nafasi, hivyo nchi za kiarabu, maana ndo zenye ushawishi na dini hiyo, zimeibuka na makundi, mfano ushia, answar sun nk umekua na kujitanua, hivyo bakwata ikajikuta haiweza kumeza mabadiliko hayo yote!!

Kuna watu hawataki bakwata, lakini hawaji na njia mpya ya kutatua tatizo wamebaki na maneno tena yale ya viongozi waliokataliwa na kisha kuizushia bakwata mabaya, bila jema hata moja, naamini ina mema yake.

Je Bakwata ndo tatizo? Jibu langu hapana, katika dini hii misikiti yote ni mali ya watu flan, ama aliye ujenga, au imamu wa pale au au....., hivyo organization structure ya uislam ipo ngumu kiasi. Mfano shekhe wa wilaya hana sauti na mamlaka ya kuchagua maimamu wa misikiti katika misikiti iliyopo eneo lake, na mkoa n,k nini madhara yake? hamna mwenye kumtii mwingine. shekhe mkuu hawezi mkanya/ adhibu au kumfukuza, shekhe/imamu wa mkoa, wilaya, au kata.
Hivyo yake kila msikiti umekuwa independent hivyo kufanya individual decisions, wakati mwingine zina kwanza Bakwata as organization.

Nini kifanyike? kuvunja Bakwata siyo suluhu, ila kuimodern ma kure-organize ikiwa na kureform institution ili iendane na wakati ni muhimu sana!! tatizo nani anafanya hivyo? je TAMPR, MAULAMAA, wasomi n.k wanafanya nini? nao walalama!!! ajabu na kweli!!! Kosa ambalo leo limefanywa ni kuwa na vitasisi vingii, vidogo vidogo vya kislaam kisha vina bishana venyewe, kisha vinatoa maoni kwa niaba ya waislam wote, ingawa wengine hawavitambui.

Nani aliunda BAKWATA jibu lake siyo suluhisho, BAKWATA ifanye kazi zake kwa ufanisi hilo ndo suluhisho!!, we never walk the dead, otherwise we shall never stop complains.
Sp
 
Je Bakwata ndo tatizo? Jibu langu hapana, katika dini hii misikiti yote ni mali ya watu flan, ama aliye ujenga, au imamu wa pale au au....., hivyo organization structure ya uislam ipo ngumu kiasi. Mfano shekhe wa wilaya hana sauti na mamlaka ya kuchagua maimamu wa misikiti katika misikiti iliyopo eneo lake, na mkoa n,k nini madhara yake? hamna mwenye kumtii mwingine. shekhe mkuu hawezi mkanya/ adhibu au kumfukuza, shekhe/imamu wa mkoa, wilaya, au kata.
Hivyo yake kila msikiti umekuwa independent hivyo kufanya individual decisions,
Usizungumzie usichokijua!...huu ndio ushauri wangu kwako.
 
Mhh usizungumzie kuundwa hata kuendeshwa linaendeshwa na nani? kwa maana mtaji wa kuiendesha Bakwata unatoka wapi? ukijua hutabaki ukisubiri amri au chochote toka kwa Sheikh wa Bakwta na ndio maana tunapotaka kufanya mapinduzi Bakwata serikali kwa gharama yoyote huilinda
 
lakini kwani kuna mtu amekatazwa kuunda "bakwata" nyingine nje ya hii? au kwani ni lazima kila muislamu kuwa bakwata? kama huipendi si ujitoe tu na uanzishe yako kama ponda.
 
tatizo bakwata hawataki uchaguzi ili waislam wapate fursa ya kumchagua kiongozi wanaemtaka,viongozi wote wa bakwata wapatikane kwa kupigwa kura hili ndo suluhisho la matatizo yote

hilo litakuwa la pili,la kwanza ni serikali kuiacha BAKWATA iwe TAASISI HURU YA KIDINI,pia itoe mapindikizi yake ili waislamu waamue hatima ya TAASISI YAO.
 
Mhh usizungumzie kuundwa hata kuendeshwa linaendeshwa na nani? kwa maana mtaji wa kuiendesha Bakwata unatoka wapi? ukijua hutabaki ukisubiri amri au chochote toka kwa Sheikh wa Bakwta na ndio maana tunapotaka kufanya mapinduzi Bakwata serikali kwa gharama yoyote huilinda

Mkuu kujua waundaji ni mzizi wa tatizo then tufike huko kwenye kuiendesha
 
hili ndiyo tatizo la waislamu, wakisaidiwa wanalalamika(NYERERE ALIWASAIDIA KUWAUNGANISHA KWA KUWAANZISHIA CHOMBO BAKWATA) wasiposaidiwa wanalalamika(KIKWETE KAKATAA KUWASAIDIA KUANZISHA MAHAKAMA YA KADHI) wananungunika kila siku! KWELI HAWA NI MAJANGA!
 
hilo litakuwa la pili,la kwanza ni serikali kuiacha bakwata iwe taasisi huru ya kidini,pia itoe mapindikizi yake ili waislamu waamue hatima ya taasisi yao.

nyie ndio wakuyatoa hayo mapandikizi, serikali haina dini itayatoaje? Au serikali inaratibu chaguzi za bakwata?
 
lakini kwani kuna mtu amekatazwa kuunda "bakwata" nyingine nje ya hii? Au kwani ni lazima kila muislamu kuwa bakwata? Kama huipendi si ujitoe tu na uanzishe yako kama ponda.

tatizo kila kitu wanahitaji msaada wa serikali bado hawajatambua serikali haina dini!
 
Bakwata ilianzishwa na Nyerere kule iringa baada ya mwl kutoka tabora kuzungumza na wazee wa kikatoliki.

Bakwata haikuanzishwa kwa nia ya kuwasaidia waislam kwa namna yeyote, hata mzee ruksa analijua hilo.
 
Ruhusa hiyo haipo kwenye hii nchi, hukitaka kuunda itaibuka mizengwe wala usijue ilikoanzia mpaka mushindwe.
 
ni ugomvi wa sadaka na vitega uchumi, nani aliwaambia waislamu wakitaka kumuabudu huyo allah lazima wawe na baraza

Niliomba mods kwa watu kama hawa wenye kashfa kwa wengine wapewe likizo.kama unaona hujui cha kuchangia unakaa pembeni tu....
 
hili ndiyo tatizo la waislamu, wakisaidiwa wanalalamika(NYERERE ALIWASAIDIA KUWAUNGANISHA KWA KUWAANZISHIA CHOMBO BAKWATA) wasiposaidiwa wanalalamika(KIKWETE KAKATAA KUWASAIDIA KUANZISHA MAHAKAMA YA KADHI) wananungunika kila siku! KWELI HAWA NI MAJANGA!

ukimjengea mtu nyumba unampa aishi kwa matakwa yake si kwa matakwa yako
 
tatizo kila kitu wanahitaji msaada wa serikali bado hawajatambua serikali haina dini!

hapa hatulaumu kama unavyotaka wewe hapa tunajadili waundaji wa baraza hilo na kwanini serikali iwe na mikono yake mpk leo
 
Bakwata ilianzishwa na Nyerere kule iringa baada ya mwl kutoka tabora kuzungumza na wazee wa kikatoliki.

Bakwata haikuanzishwa kwa nia ya kuwasaidia waislam kwa namna yeyote, hata mzee ruksa analijua hilo.
mkuu ni kweli alianzisha BAKWATA na kama waislamu wanavyo amini mpk ni kuwa halikuwa na malengo ya kweli na uislamu wenyewe,tukubali makosa ya NYERERE KWANINI tusisaishe ili bakwata iwe chini ya watu husika na kwa malengo mazuri ya wahusika wenyewe
 
tatizo kubwa wanakosa hierchial ya kiuongozi ndio maana leo utasikia shehe bungo, kundecha mara mkuu wao ponda kasema hili juu ya mufti n.k.

naomba wakajifunze mfumo.mzuri wa.utawala na uongozi kutoka kanisa katoliki.
 
Back
Top Bottom