Bakora hazimjengi mtoto kinidhamu

Kama kawaida yetu dunia ya wajuaji hii. Bwana Mungu Muumba kasema mtoto asinyimwe kiboko wewe ni nani hasa wa kupinga...
 
Ni kweli kabisa.Nina kabinti kangu 5yrs Sasa alikuwa na tabia Kila akivua nguo anatupa chini hapo kamerudi shule hapa utakuta soksi pale Sweta pale sketi,nimefundisha kwa mdomo weeee siku yake nikampa bakora zake, siku hizi yeye ndio msemaji wa familia,utasikia wewe dada weka nguo pale kwenye Tenga mama atakuchapa wewe?
Fimbo haikwepi kwa mtoto sema tu kwa kiasi na iwepo interval sio Kila siku achapwe.
 
Kati ya kitu wazazi walikosea ni kuto wachapa watoto wao
Watoto wa sikuhizi wana majibu mabaya sababu ya malezi mabaya
Nina jirani yangu ana mtoto wa kike ana miaka 10 yupo STD 5,anasoma English medium ndio hao wakutochapwa anavyolelewa utasema yai la tausi wa pale magogoni...siku hiyo mama yake kajifanye amchape mtoto kapokonya fimbo na kumrudishia mama yake viboko huku anamuuliza Kama hunipendi kwa nini ulinizaa na maneno ya shit kibao na vizungu vyao,mama yake anajifanya kapanic nikajisemea moyoni hukumchapa at early stage uje umchape keshakomaa..kifupi ilikuwa ni tukio la aibu Sana...Nilitamani nimshike yule mtoto nimnyuke fimbo uwezo sikuwa nao tu....
WITO watoto wetu wa kiswahili ni wagumu Sana sijui wenzetu wazungu ila tujitahidi tu kuwanyoosha mpaka tutapoishia tuwe tumesimama kwenye nafasi zetu
 
Muleta mada atakuwa miongoni mwa wale walio brainwashed na wanaharakati wa haki za mtoto, hawa ndo wamechangia kushuka kwa maadili ya watoto nyumbani na mashuleni.

Kwa kila baya MTU alifanyalo lazima aadhibiwe kwalo ili kujenga nidhamu na kumrejesha katika njia sahihi. Lakini pia naomba nieleweke, so kila kosa lazima mtoto aadhibiwe kwa viboko, kuna mambo mengine anahitaji kukanywa tu. Lakini tusitake ku- legitimize kuwa kutumia adhabu za viboko ni ukatili

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 


Kwanza ujue kwamba kila mtoto au watoto wanamalezi tofauti na tabia tofauti...kunawatoto niwapole mpaka mzazi anaogopa kunawatoto ni watundu mpaka kero kwa kila mgeni aingiaye katikannyumba hiyo..kunawatoto wanaiga mambo kwa watoto wengine..all in all ni mzazu mwenye akili tumamu tu ndio anajua anataka mtoto wake aweje...nakukumbusha mtoto yake ni fimbo...
Yaani mtoto lazima ajue kama nikifanya hivi nitachapwa au kunajambo linanikuta..ni fimbo tu ndio inamfanya mtoto awe na nidham..
 
Usimnyime mtoto bakora, Maandiko Matakatifu yameagiza hivyo.
Hata hivyo, inaonyesha KAMA binadamu tulio wengi huwa tuna roho mbaya kwa watoto, especially pale inapotokea kuwa siyo wa kuzaa sisi wenyewe. Kutokana na hali hii, inaonyesha kuwa mara nyingi binadamu unaweza ukamkuta anamchapa mtoto kwa prejudices zake tu na si kwa sababu za msingi, na pale inapotokea kuwa anazo sababu za msingi za kufanya hivyo, mapigo yake yanakuwa mazito mno na ambayo hayaendani kabisa na kosa husika la mtoto, na hapa ndiyo uharibifu unapotokea.

Ni fimbo iliyomwangukia mtoto kutokana na upendo tu na kwa uwiano sahihi kulingana na kosa alilofanya, ndiyo iliyo na matokeao chanya kwa mtoto husika, tofauti na hivyo fimbo kwa mtoto lazima iwe na madhara makubwa, tena sana tu!
 
Usitufokee.

Kila mmoja ana namna yake ya kumrekebisha tabia mtoto wake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…