GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,651
- 109,047
bNimekuwa nikiwasikia Wanaume wengi sana wakisema hii sentensi ambayo nainukuu hapa " Nimezaa Watoto wawili " na Wanaume wengi sana huwa wanaisema hii katika maeneo mbalimbali na hata katika Familia zetu hii kauli imekuwa ikisikika mno ila kwa binafsi yangu naona kama vile ina ulakini.
Kipi ni Kiswahili sahihi hapa kwa Mwanaume kusema kama akiwa ana Watoto?
a) ' Nimezaa Watoto wawili '
b) ' Nimejaaliwa Watoto wawili '
c) ' Nimebahatika kupata Watoto wawili '
d) ' Mke / Mpenzi wangu kanizalia Watoto wawili '
Nitashukuru nikielimishwa juu ya hili ila na Watu wa BAKITA ( Baraza la Kiswahili Tanzania ) watusaidie katika hili kwani kwa Sisi Watu wa Mikoa ya Pwani huwa tunashtuka sana pale tukiwa tunawasikia Wanaume wenzetu hasa wale ' Wakuja ' kutoka mingine wakisema tena bila wasiwasi kabisa huku wakitiririka na kuserereka kwamba ' wamezaa Watoto wawili '.
Nawasilisha.
shemeji aushi vitukuko.unaogopa kuzaaaNimekuwa nikiwasikia Wanaume wengi sana wakisema hii sentensi ambayo nainukuu hapa " Nimezaa Watoto wawili " na Wanaume wengi sana huwa wanaisema hii katika maeneo mbalimbali na hata katika Familia zetu hii kauli imekuwa ikisikika mno ila kwa binafsi yangu naona kama vile ina ulakini.
Kipi ni Kiswahili sahihi hapa kwa Mwanaume kusema kama akiwa ana Watoto?
a) ' Nimezaa Watoto wawili '
b) ' Nimejaaliwa Watoto wawili '
c) ' Nimebahatika kupata Watoto wawili '
d) ' Mke / Mpenzi wangu kanizalia Watoto wawili '
Nitashukuru nikielimishwa juu ya hili ila na Watu wa BAKITA ( Baraza la Kiswahili Tanzania ) watusaidie katika hili kwani kwa Sisi Watu wa Mikoa ya Pwani huwa tunashtuka sana pale tukiwa tunawasikia Wanaume wenzetu hasa wale ' Wakuja ' kutoka mingine wakisema tena bila wasiwasi kabisa huku wakitiririka na kuserereka kwamba ' wamezaa Watoto wawili '.
Nawasilisha.
Mama mdogo hivyo tusemeje sisi?Mwanamme hazai bali anasababisha mimba. Anayezaa ni mwanamke.
Mkulu amesema tufyatue nadhan hii ndio sahihi zaidKwa mujibu wa Ngosha ni Kufyatuwa.
Mtoto akizaliwa mseme, mke au mpenzi wangu amejifungua mtoto wetu.Mama mdogo hivyo tusemeje sisi?
Mm wananikera kwa kweli....eti samaki zile.Kwani ukimwambia mtu nimezaa watoto wawili ushaona mtu hajaelewa? mbona ninyi msiojua kiswahili fasaha mnasema ng'ombe zetu, badala ya ng'ombe wetu, zimezaa, badala ya wamezaa? na wenye kujua lugha tunawaangalia tu...
HahaWajita bhana!