Serikali , bakita, tataki tuamke huu ni wakati wetu sasa

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,477
2,148
SERIKALI, BAKITA, TATAKI TUAMKE SASA KUMEKUCHA
Hujambo mpenzi ndugu msomaji wangu karibu katika makala Nyingine, yenye lengo lakutupa mzinduko.
Lugha ya Kiswahili kwa kwa nchi za upwa Wa Afrika mashariki ni bidhaa ambayo kama itatumika vizuri inaweza kubadili kabisa maendeleo ya kiuchumi na kupandisha kabisa hadhi ya nchi hizi za upwa Wa Afrika mashariki hasa Tanzania.
Pamoja na juhudi mbalimbali zinazo fanywa na serikali, kupitia asasi zake, Taasisi ya Taaluma za kiswahili na vyombo mbalimbali nathubutu kusema kuwa kwa upande Wa Tanzania bado tupo nyuma sana, na bado juhudi zaidi zinahitajika ili tunufaike na hii bidhaa.
TUNAKOSA UTHUBUTU:
Tunasubiri kuitwa. Tusipo itwa je? Tunakosa uthubutu Wa kwenda kuwekeza Kiswahili. Tunasubiri hadi pengine kuwe na uhitaji huko nje halafu waitwe wataalamu wawili au mmoja kwa namna hiyo tutasubiri sana.
Nataka nikupe mfano huu , Nchi ya China kwa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Hanban na taasisi yake ya Confiscius wamedhamiria kweli kweli kueneza kichina Duniani na ndiyo sababu ukienda nchi mbalimbali wamefungua matawi kwaajili ya kufundisha kichina pamoja na utamaduni Wa watu wachina, hata hivi maajuzi Mh Rais aliweka wakfu Maktaba pamoja na Kituo cha kufundishia Kichina katika chuo Kikuu cha Dar es salaam. Sisi tunashindwa wapi hata kuiga?. Licha ya hayo Vipo vituo vya Redio mfano CRI yapale Beigin ambayo hufunza kichina na husikika katika nchi za Afrika mashariki kupitia Redio washirika, Swali la kujiuliza hapa je radio zetu hazina uwezo wakufanya hivyo? Kuwepo hata kipindi cha dakika tano cha kufundisha kiswahili halafu tukafungua studio pale South Afrika au pengine tukasikika kupitia Durban FM?
Hatuna haja ya kusubiri tena hadi tuitwe kwa kupitia Mabalozi wetu waliopo nchi za kigeni tunaweza kufungua Taasisi nyingi za kufunza kiswahili na tukatoa wataalamu kwaajili ya vituo hivyo na kiswahili kikaenea zaidi, na ajira zikawepo kwa wingi huko, kwani kwasasa Nina shaka kuwa huenda tunazalisha wataalamu wasio tumika.
Wito wangu Nikwa Serikali, vyama vyote vya ukuzaji kiswahili Tanzania, Taasisi zinazo zalisha wataalamu kujadili kuhusu kuanzisha vituo vya kufunza kiswahili katika nchi za kigeni.

Vilevile kutokana na kukua kwa sayansi ya teknolojia ni wajibu wetu sasa kukikuza kiswahili kupitia tehama , nashukuru nimeweza kuona kamusi ya Tuki imeweza kuchapishwa mkondoni nijambo la kujivunia lakini hiyo haitoshi tu ningependa kuona TUKI wakianzisha duka umeme (E-shop) kwaajili ya kutoa Huduma kwa wapenzi Wakiswahili waliopo mahali popote ulimwenguni. Pia ni wakati sasa wakuanza kukipromote kiswahili kupitia mitandao, Kwanamna ya pekee kabisa napenda kumpongeza rafiki yangu Ndugu Mexece C.E.O Jamii forums kwani mtandao Wa Jamii ndio ulio andika lugha ya kiswahili Mara nyingi zaidi duniani katika mtandao. Hayo aliyasema yeye mwenyewe katika kikao kifupi tulicho kutana Jana, hiyo ni hatua kubwa sana katika kiswahili ukiacha ile ya kuingizwa katika mifumo ya micro soft 2004 ,pale lamu Kenya. Pia kutaka katiba ambayo inakitambua kiswahili kuwa lugha ya Taifa na rasmi kama ilivyo kwa katiba Mpya ya Kenya kwa 2010.
Majukumu yote ya kuhakikisha kiswahili kinakua na kutuneemesha sio ya serikali , Bakita, au Tataki pekeyake Bali ni yetu sote kila mtu kwa nafasi yake.
Mwisho na pongeza, naheshimu kila jukumu la kila mmoja wetu kuanzia serikali, taasisi na juhudi za MTU mmoja mmoja katika kuhailikisha kiswahili kinaenea kila pahali, Bila kumsahau mpambanaji Wallah Bin Wallah mwanzilishi Wa tuzo za wasta, ukipata ujumbe huu uniandikie pepe nautambua sana mchango wako. Na wengineo
Mwisho
 
Back
Top Bottom