RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 51,876
- 108,406
Kwahio zile propaganda hamna utajiri wa halali sio kweli?Huyu mzee ni mtu aliyeanza ALIF kwa kijiti. Alikuwa na kaduka kaa kuuza viatu, akaanzisha machine ndogo za kawaida za ice cream za kons. Miaka ya early 80s Kaka yangu alikuwa anafanya kazi Abu Dhabi, alishakutana naye kwenye ndege ya Air Tz, akiwa amebeba maboxi ya cons za ice cream.
Pesa zake kazitengeneza kwa jitihada nyingi na subira, kwa hivyo hawezi kuwa na woga wa wanasiasa, na katika globalization ya leo, kesha jijenga vizuri sana, hatishiki.
Pia ni mtu muungwana sana, hapendi majivuno,anasaidia masikini na wanyonge, mpenda haki