Bakhresa kwa Makonda, Mwakyembe na Tido, na Nilichojifunza Binafsi

Huyu mzee ni mtu aliyeanza ALIF kwa kijiti. Alikuwa na kaduka kaa kuuza viatu, akaanzisha machine ndogo za kawaida za ice cream za kons. Miaka ya early 80s Kaka yangu alikuwa anafanya kazi Abu Dhabi, alishakutana naye kwenye ndege ya Air Tz, akiwa amebeba maboxi ya cons za ice cream.

Pesa zake kazitengeneza kwa jitihada nyingi na subira, kwa hivyo hawezi kuwa na woga wa wanasiasa, na katika globalization ya leo, kesha jijenga vizuri sana, hatishiki.

Pia ni mtu muungwana sana, hapendi majivuno,anasaidia masikini na wanyonge, mpenda haki
Kwahio zile propaganda hamna utajiri wa halali sio kweli?
 
Bashite hapo yupo like what...huyu mzee ananipita bila kunipa mkono hanijui mi nani?

Mzee nimependa maisha yake,pia naona ana busara mno maana hata wanae licha ya kusoma vyuo vya ughaibuni.maisha mazuri.investment za kila aina.Nyumba za kifahari na kupangilia migari ya kila aina hawana kelele kabisa.yani mtoto wa bakhresa umkite anapigana na kulumbana na mtu halafu anauliza "unanijua mi nani*?
Ukute mtoto wa bakhresa anapigana na Tid
 
Kwani ana pamba gani ya maana zaidi ya hayo matambara ya kijani?
Jamaa niliwahi kukutana nae airport sasa yupo anatembea haraka haraka alafu kumbe ana kichwa kikubwa sana,nkatamani nicheke ile pemben yake alikuwa ameambatana na walinzi wake,nikatulia.
 
Ha ha ha....ndio hapo. Hao ni binadamu kama wengine wana mambo kama binadamu wengine sema hawagongani na akina sisi.
Ila mzee mbona kuna magari ya kifahari nayaonaga yanazurura usiku wa manane tu,nadhani ndio wao.
 
Kuna video nimeiona, nashindwa tu kuiweka hapa,

ila watanisaidia wenye nayo, maana ipo sana tu mtandaoni,

inamuonesha Mzee SSB, akiingia msibani, kwenye msiba wa wafanyakazi watano wa Azam Media, kuelekea kiti kwake, anampita Katibu wa CCM ndugu Polepole, anampita Rc wa Dar es salaam, almaarufu kama mungu wa Dar, DAB, Makonda, anampita waziri mwenye dhaman na michezo habari na burudani, Mhe Mwakyembe, anasogea kwenye kiti chake anakaa, anampa mkono mzee wa pembeni yake ambaye, sura sio ngeni ila sijamtambua vizuri.

Na anaendelea na taratibu nyingine, wakati huo huo, jicho la kamera, linamtazama Mhe Mwakyembe, na Makonda, ni kama vile wanataka kutoa mkono wa pole kwa mzee, wasalimiane nae, ila wanaona tena kama itifaki itakuwa haijakaa sawa, basi wanabaki wasijue la kufanya, na yeye ni kama vile hana taimu nao, au ukute hata hajawajua. (Inawezekana kabisa akawa hawajui)

Mara anakuja Tiddo, ambaye ni mwajiriwa wake, kama Mkurugenzi wa Azam media ,mzee anasimama anamsalimia Tiddo kwa adabu na heshima.

My take :

1. Mzee anathamini Wafanyakazi wake, na kuwashobokea hao, zaidi ya viongozi wa kisiasa, ambao kwa kawaida mabosi wengi mtaani wangefanya kinyume na hapo,

2. Mzaa yupo busy na mambo yake, na hivi Magu anabadilisha badilisha mawazir na wakuu wa mikoa, ukute jamaa hata hajui in person wazir wa michezo ni nani, watu wake wanajua, kampuni zake zinajua, ila yeye in person hana muda wa kufuatilia hayo na hayana umuhimu kwake.

3. Anapenda kuishi kawaida sana
Wakati unaendelea kujifunza nakuongezea hii
tapatalk_1562942496528.jpeg
 
Tatizo wabongo huwaza vitu negative
Yule Mzee sio muongeaji hata kidogo ila ukiweka hoja mezani ndio mtajadili

Sasa mtoa maada anaropoka tu
Ametopoka Nini? Ndo kilichotokea. Hamna kificho hapo au huoni baba shombeshombe alivyoshangaa
 
Bashite hapo yupo like what...huyu mzee ananipita bila kunipa mkono hanijui mi nani?

Mzee nimependa maisha yake,pia naona ana busara mno maana hata wanae licha ya kusoma vyuo vya ughaibuni.maisha mazuri.investment za kila aina.Nyumba za kifahari na kupangilia migari ya kila aina hawana kelele kabisa.yani mtoto wa bakhresa umkite anapigana na kulumbana na mtu halafu anauliza "unanijua mi nani*?

Hawataki swaga Kama za akina Kinje boy.
 
Angekua bashite tusingelala,
Mimi naamini mtu unapokea baraka zaidi kutokana personality yako na moyo wako.
Maana kuna mtu ana Nyumba ya kawaida ila unaweza mfukuza mtu kama mwizi usiku wa manane,je akipewa ghorofa la billion atakuaje?
Kuna yule mwanae anaitwa Yusuf Bakhressa siku fulani alipita maeneo ya kazini nilishangaa jamaa ananichangamkia hadi nikajiuliza huyu jamaa ni nani mbona kama namjua si tu alinichangamkia mimi kila mtu aliekuwepo eneo lile basi kuna jamaa yeye anawafahamu watu wengi akaniambia unamjua yule nani? Nikamwambia hapana akaniambia ndo mtoto wa Bakhresa nikashangaa duuh nikauliza hivi huyu ndo yule nyumba yake iluonekana ile migari ya kifahari mwaka fulani jamaa akaniambia hewalaa,, sasa pata picha bashite ndo angekua mtoto wa huyo bakhressa ingekuaje duniani hapa
 
Haaaa haaaa alinipita hata mimi,badala ya kunisalimia kwa unyenyekevu kajipitia tu kama vile sikuwepo.Huyu Mzee ni shida labda anafikiri yeye ni tajiri kuliko mimi.
😂😂😂😂😂😂😂
 
Naam nimewahi kumuona mzee na kuongea nae kama mara 3 hivi hana makuu kabisa,
 
na sio mtu wa kujionyesha
Huyu mzee ni mtu aliyeanza ALIF kwa kijiti. Alikuwa na kaduka kaa kuuza viatu, akaanzisha machine ndogo za kawaida za ice cream za kons. Miaka ya early 80s Kaka yangu alikuwa anafanya kazi Abu Dhabi, alishakutana naye kwenye ndege ya Air Tz, akiwa amebeba maboxi ya cons za ice cream.

Pesa zake kazitengeneza kwa jitihada nyingi na subira, kwa hivyo hawezi kuwa na woga wa wanasiasa, na katika globalization ya leo, kesha jijenga vizuri sana, hatishiki.

Pia ni mtu muungwana sana, hapendi majivuno,anasaidia masikini na wanyonge, mpenda haki
 
Hivyo ndivyo wanavyoishi alpha males na watu waliopata mafanikio halisi, jali zaidi biashara yako kuliko mamlaka ya muda mfupi.
Kumbe biashara siyo ya muda mfupi? Au context ya comment yako ulitaka kumaanisha nn?
.vyote hivyo ni vya muda mkuu iwe madaraka ama utajiri, wangapi waliwahi kuwa na pesa lakn leo ni maskini?..

Sema tu siasa imeishi damuni lakn mie ningesema hv kama maoni ya mtoa mada ndo yako hvyo basi Bakhresa kakosea sana maana akitakiwa ajali utu nje ya kufanya kama maoni ya mtoa mada alivyosema !

Sote tunapita uwe bilionea uwe na madaraka gani hivyo ya nini kufanya mambo ya kumfanya mwanadam mwenzako ajisikie kutengwa hali ukijua hutaishi milele? Na hizo mali au madaraka yako?
 
Back
Top Bottom