Bakhresa group mfano mzuri wa kuigwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakhresa group mfano mzuri wa kuigwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Apr 24, 2009.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Ndugu zetu wenye asili ya kiasia wanaweza kufikiri wanabaguliwa kwa kutajwa na mengi kwenye "shame list" lakini mfano mzuri wa mfanyabiashara wa Kitanzania mwenye asili ya kiasili ambaye hatujamsikia kwenye ufisadi wala kashfa ya wizi ni Bakhresa. Mimi kama Mtanzania napongeza wafaqnyabiashara wote wanaofanya biashara kihalali na ninapinga vikali ufisadi.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  sijakulewa; kwa vile hatujamsikia ina maana anafanya biashara kihalali? Kama si fisadi ni jambo jema kwani tumechoka na orodha ya mafisadi. Ila yeye anachukuliaje suala la ufisadi wa EPA na mambo mengine ya kisiasa nchini. Au yeye hajali lolote linaloendelea as long as biashara zake zinakwenda pouwa tu?

  Maana wakati mwingine mafisadi wengine wanakua na kukomaa kwa sababu watu wema wanakaa kimya! Je mtu mwema anayeuona uovu halafu hajitokezi kuupinga au kuukemea wema wake unasaidia vipi kuushinda uovu huo?
   
 3. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unalielewa chimbuko la Bakhresa ???
   
 4. C

  Chuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unataka aseme kwani yeye mwanasiasa?au ataka publicity au attentions?...hata Ngano yake ilipochomwa moto hakuwaita waandishi wa Habari. sometimes unapojua nature ya watawala walivyo ni vema kukaa kimya kuliko kupayuka.

  Acha wanasiasa wachukue role yao na wafanya biashara wawe wafanya biashara. Wakijitumbukiza ktk SIASA ndio hapo zitakapoanza siasa za kuchafuana na kuonekana ufisadi...
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du!

  Mwanakijiji kiboko!!! ku-demostrate good business governance is enough sio lazima na yeye awe anaita vyombo vya habari kama Mh. Mengi.

  Kasheshe
   
 6. O

  Ogah JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  1. Mafia wa kukwepa kulipa KODI
  2. Vyakula VIBOVU........na afya zetu.....je ni wangapi wanaugua/waliugua/wamekufa...........etc etc

  The guy is another Devil..........
   
 7. Mboka Manyema

  Mboka Manyema Member

  #7
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Alijaribu kukifadhili chama cha CUF miaka ile ya 90s na matokeo yake ni kuchomwa moto kwa ngano yake meli nzima, angalau alikua na international certificate iliyokua inathibitisha ya kuwa ngano ile ni safi na inafaa kwa matumizi ya binaadamu. baada ya hapo aliishitaki kampuni ya malaysia kwenye mahakama ya kimataifa ya kibiashara kwa kumuuzia ngano mbovu na hiyo kampuni ikaishitaki serikali ya Tanzania kwa kuchoma ngano safi, yalipoishia mimi sijui. kuanzia hapo huyu bwana hataki tena kusikia siasa za nchi hii badala yake amehamia kwenye football akijaribu kuleta upinzani kwa simba na yanga. ana mipango mizuri kwenye football ikiwa na kuanzisha kituo cha michezo kikubwa.
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145


  kitu anachokifanya mengi cha kuwashutumu hawa mafisadi ni muhimu sana kwa nchi kama TZ ambayo watu walioelimika na kuelewa ni kidogo sana.
  mafisadi njia wanayoitumia ni kukaa kimya kwa ajili wanajua watanzania watasahau na story itakwisha.
  kitu anachokifanya mengi ni kuhakikisha wa TZ hawasahau na story haiishi na ndio maana makamba anang'ang'nia kusema imekwisha.
  wafanyabiashara wa TZ waige mfano wa mengi na sio kwa ajili wao wanapata basi hawawajali wananchi wala nchi, pesa zinaibiwa wao wanakaa kimya tu....
  nchi yeyote inakuwa kutokana na wazalendo.....
  jamii iliyoelimika na ya matajiri TZ kazi yake kubwa ni vimisaada midogomidogo ili waaonekane wanasaidia, kama unataka kumsaidia mTZ kwa dhati lazima upambane na mafisadi
  baharesa amechomewa unga amekaa kimya....
  mengi amekataliwa kununua KLM Hotel na mambo kibao lakini hajakaa kimya ndio kwanza ameongeza GIA, na ana risk mambo yake mengi tu, huu ndio uzalendo.....
  wafanya biashara waliokaa kimya sio wazalendo........
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  baresa katoa ajira kibao kwa vijana bongo
  nadhani labda ana misingi mizuri. lakin wait....
  hivi alianza anzaje? ile migodaun ya national milling aliipatapataje? na kwa nini and who's influence kufa kwa NMC?
  labda nipo kizani
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo angekuwa mwana CCM machachari tungekula Chapati za ngano ya kuvunda???

  Kweli Serikali ya CCM imeoza na kujaa madudu.

  Ile kashfa ya Kununua mitambo ya kusaga ya NMC ambayo ilimhusisha Marehemu Semensi yeye Bakhressa hakuwamo??

  Yakhe!! Au kwa vile ni mavi ya kale hayanuki ati??

  Alifanya ufisadi siku nyingi wengi wakiwa watoto wadogo wenye uwezo wa kulilia Koni zake tukuliko kutafakari kulikoni.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Aishkrimu za BARESA
  kali hiyo hehe we acha tu!
  dah lakini humu watu wana data mpaka naogopa maana inawezekana hata data za baba yagu mnazo nyie au tuseme sidhani kama mna data zangu za last moth nilipopigwa faini (burgained) ya kuendesha bila kufunga mkanda.
   
 12. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi Pongezi zinasahau ukweli kwamba, National Millings Ilikufa katika mazingira ya kutatanisha.Na ukiangalia kiundani,Ghala nyingi za Backresa ni mali za National ,Millings before.

  Pili Before hujampongeza Backresa you need to know the shareholders in his Company. Kwasababu ubaweza ukajikuta mafisadi wamejificha humu na ukashangaa. Kama unakumbuka Vodacom kabla hatujajua kuwa Rostam alikuwa ni moja ya Vinara.

  Mwisho kama tukijua actual shareholders na tukagundua he is doing cleam business kweli yeye ni mfano wa kuigwa.
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  haya
  ndo baresa huyo
  Hivi baba akiwa fisadi anaweza kumuambukiza mwanae?
  wikend njema wakulungenge
   
 14. Mboka Manyema

  Mboka Manyema Member

  #14
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hakuna siku serikali ililazimishwa kuuza NMC au mitambo yake, kilichotokea ni serikali kuamua kuuza kwa kushindwa kuiendesha. Alinunua NMC (mzizima) na akajaribu kununua NMC (kurasini) lakini alishindwa kwa njia ya tender na aliyeshinda ni mohamed enterprises.
  Kuhusu mavi ukiyachokonoa yatanuka! na mimi ningependa uendelee kuyachokonoa kwa sababu unaweza ukaja na kitu kipya kwangu ambacho sikijui kuhusu Bakhresa na kikawa ni kweli, kitasaidia kwenye vita dhidi ya ufisadi. ni muhimu kuwa na refrence ya mafisadi wa zamani ili huko tuendako yasitokee tena
  Thanks
   
 15. Mboka Manyema

  Mboka Manyema Member

  #15
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  wakati wewe unasema hivyo serikali kwa upande wake inasema ni mmoja wa walipa kodi wakubwa Tanzania (yaani yupo kwenye top 10)
  Product zake nyingi zimethibitiswa na TBS na ISO na URS
  naomba uthibitisho wa mtu mmoja aliekufa kwa sababu ya Bakhresa Product.
  Thanks
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,054
  Trophy Points: 280
  Mboka Manyema,

  ..inaelekea unafahamu kidogo kuhusu huyu Mzee wetu Bakhresa.

  ..naomba kuuliza amesaidia nini kwao Zanzibar[pemba na unguja]? unaweza kubainisha mradi wowote wa elimu,afya,au maji, ambao amesaidia huko kwao?

  ..Bakhresa amejitanua kibiashara mpaka Mozambique,Uganda,na Malawi. naomba kufahamishwa kama Bakhresa ana investments zozote za maana ndani ya Zanzibar.

  NB:

  ..wa-Zenj wanalalamika kwamba Tanganyika inawatia umasikini. hawamuoni mwenzao alivyofaidika kibiashara huko Tanganyika na sasa yuko ame-expand kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki.
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  1. ukitakiwa ulipe kodi 100%, na wewe unalipa only 40% ya kodi unayotakiwa kulipa....then uka-get away with it.......ndio ukwepaji ninaosema hapa......mafia style anayo-conduct huyu jamaa......i wish ungeijua......

  2. nenda uswazi/mtaa wa kongo uone jinsi hizo stamps za TBS, ISO na URS zinavyofanyiwa kazi....leave alone huko Malaysia/Asia kwa ujumla wake

  3.Kulisha mtu chakula kibovu kuna madhara..........period..........kama hujui na unataka vithibitisho ya vifo............inabidi turudi darasani kuanza upya elimu............
   
 18. Mboka Manyema

  Mboka Manyema Member

  #18
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 21, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Huko Zanzibar yupo ndugu yake ambaye anaendesha biashara zake. investments zake zipo karibu Tanzania nzima yaani Product zake utazikuta mikoa mingi, kama hujakuta ice cream basi unga au juice au japo maji na ana agents karibu miji yote mikubwa east africa.
  Kwenye suala la misaada yeye ameegemea zaidi kwenye tasisi za kidini hasa ya kiislamu na ndio maana misaada yake mingi hutoka mwezi wa ramadhani, na hiyo inatokana na imani yake inavyotaka kwamba kwanza annze kusaidia ndugu zake halafu waislamu wenzake halafu wengine.
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ni Mtuwaje mzuri sana wa sadaka siku ya ijumaa nje ya nyumba yake
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  basi na yeye aje kujitolea kuisupport JF kifedha kama si fisadi...sio anakimabilia kuagawa ijumaaa kwa wahh.......................
   
Loading...