Bakhresa group mfano mzuri wa kuigwa

Mboka Manyema,

..ninachozungumzia mimi ni Bakhresa kuwapa wananchi wenzake "ndowana" wavue, siyo "samaki" wale.

..la kwanza, ingependeza kama angefungua viwanda Zanzibar na kuajiri wananchi huko.

..la pili, binafsi ningefurahi sana kama Bakhresa angesaidia katika ujenzi wa shule,zahanati,miradi maji, utunzaji misitu na vyanzo vya maji etc.
 
1. ukitakiwa ulipe kodi 100%, na wewe unalipa only 40% ya kodi unayotakiwa kulipa....then uka-get away with it.......ndio ukwepaji ninaosema hapa......mafia style anayo-conduct huyu jamaa......i wish ungeijua......

2. nenda uswazi/mtaa wa kongo uone jinsi hizo stamps za TBS, ISO na URS zinavyofanyiwa kazi....leave alone huko Malaysia/Asia kwa ujumla wake

3.Kulisha mtu chakula kibovu kuna madhara..........period..........kama hujui na unataka vithibitisho ya vifo............inabidi turudi darasani kuanza upya elimu............

Lini TRA iliwahi kumshitaki au hata kulalamika kwamba anakwepa kodi? na badala yake wanasema yumo kwenye orodha ya walipa kodi wakubwa Tanzania!
ni kazi rahisi sana kugundua kama hiyo ni orignal au feki kwenye product zake kuna registered number ya hiyo standard quality ichukue halafu ingia kwenye site ya ISO au URS angalia nani ana own hiyo, kuhusu TBS sijui lakini unaweza kuchukua ukaenda au kumtuma mtu ahakikishe.
Ni kweli zipo feki lakini siyo kwenye product za Bakhresa kwani investment yake ni kubwa kuliko risk ya fake standard.
Hivi unajua sasa kuna soko zuri sana la mapera, machungwa, maembe, mananasi etc....Huyu bwana ananunua kwa bei nzuri na kwa tons tena ni cash, hii ameanza toka alipofunga mitambo ya Juice kutoka Sweden (tetra pac) kabla ya hapo kulikua hakuna juice ya matunda halisi kutoka tanzania.
Kuhusu products mbovu mimi naona ni uzushi mtupu au chuki binafsi.
Thanks
 
Mboka Manyema,

..ninachozungumzia mimi ni Bakhresa kuwapa wananchi wenzake "ndowana" wavue, siyo "samaki" wale.

..la kwanza, ingependeza kama angefungua viwanda Zanzibar na kuajiri wananchi huko.

..la pili, binafsi ningefurahi sana kama Bakhresa angesaidia katika ujenzi wa shule,zahanati,miradi maji, utunzaji misitu na vyanzo vya maji etc.

Wewe Zanzibar unaisikia tu naona hujui kama utawala wa kule ni wa mafisadi CCM choyo ,Raza na UCCM wake alirudishwa na magodoro yake alipotaka kuyatoa msaada katika Hospital ya Mnazi mmoja(VI Lenin ) ,hivyo huyu kuhama kule Zanzibar ni sababu za choyo walichonacho watawala ,sasa ukiangalia utaona nani anapata hasara ,Bakaresa au SMZ ,bila ya shaka ni SMZ wanakosa kodi wanakosa misaada ,Bakarisa ni mmoja ambae hutoa misaada bila ya kutangaza au kujitangazia tofauti na wengine ambao huandaa sherehe na kujionyesha ,na amekaribishwa Msumbiji huko nafikiri wamempa eneo la bandari kujenga maghala na kiwanda cha kusindika mchele au mpunga kwenye magunia ,wamempa eneo kubwa tu na wanafaidika nae.
 
Katika mapambano haya ya ufisadi ambacho nchi inadhulumiwa, wafanyabiashara wanatumia nafasi yao kujitengeneza na yeye yuko upande gani? Au kwake yeye hajali kile kinachotokea nchini katika ulingo wa siasa anachojali ni kutengeneza fedha tu? Hajali dhulma ya mamilioni ya wananchi, wizi wa Benki Kuu n.k? That is all I care about.

Ndiyo maana watu kama kina Andy Chande na wenzao wako kimya. Kwangu mimi ukimya wao unapiga kelele.

Mimi simjui Bakhresa wala sina kitu chochote kinachonielekeza kumfikiria au kumdhania ni fisadi; ila najua ni mtu prominent ana uwezo (na wengine wamedai hapa kuwazidi watu wengine wengi tu). Kutokana na uwezo wake huo binafsi najiuliza anautumia vipi katika kubadilisha mwelekeo wa kisiasa nchini?

Jibu nililolipata hadi hivi sasa ni kuwa yeye hajali hali ya kisiasa nchini au uongozi. Anachojali ni biashara zake zinaenda powa tu. Huyu kwangu si mfano. Kwani, mwenye nguvu anapokaa kimya wakati wanyonge wanadhulumiwa basi anahalalisha dhulma hiyo.

Na hapa sisemi aitishe mkutano wa vyombo vya habari (akifanya hivyo sina tatizo) lakini he need to take a public position of where he stand on the question corruption in the country. Anything less than that wanaotaka kumuita wamuige. No I.
 
Lini TRA iliwahi kumshitaki au hata kulalamika kwamba anakwepa kodi? na badala yake wanasema yumo kwenye orodha ya walipa kodi wakubwa Tanzania!
ni kazi rahisi sana kugundua kama hiyo ni orignal au feki kwenye product zake kuna registered number ya hiyo standard quality ichukue halafu ingia kwenye site ya ISO au URS angalia nani ana own hiyo, kuhusu TBS sijui lakini unaweza kuchukua ukaenda au kumtuma mtu ahakikishe.
Ni kweli zipo feki lakini siyo kwenye product za Bakhresa kwani investment yake ni kubwa kuliko risk ya fake standard.
Hivi unajua sasa kuna soko zuri sana la mapera, machungwa, maembe, mananasi etc....Huyu bwana ananunua kwa bei nzuri na kwa tons tena ni cash, hii ameanza toka alipofunga mitambo ya Juice kutoka Sweden (tetra pac) kabla ya hapo kulikua hakuna juice ya matunda halisi kutoka tanzania.
Kuhusu products mbovu mimi naona ni uzushi mtupu au chuki binafsi.
Thanks

1. Inaelekea huelewi how the 10% plays katika chombo chetu pale TRA
2. Inaelekea mambo ya biashara/soko huria na gymnastics zake kidogo huyaelewi
3. Ungejua jinsi mwananchi anyeuza mapera or whetevr crops they grow jinsi anavyobanwa kwenye kodi na analipa kikamilifu (unlike huyo Bakhresa).......

NB: Uovu wote unaofanyika na hawa watu tuwaitao mafisadi........sisi wenyewe (in the system) tuna-facilitate wao kufanikisha uozo

Kuhusu biashara zake kuenea nchi jirani............naweza kusema thats a good way to clean the dirty money my friend.......

wanaonisoma na wafuatilie.........
 
Mboka Manyema,

..ninachozungumzia mimi ni Bakhresa kuwapa wananchi wenzake "ndowana" wavue, siyo "samaki" wale.

..la kwanza, ingependeza kama angefungua viwanda Zanzibar na kuajiri wananchi huko.

..la pili, binafsi ningefurahi sana kama Bakhresa angesaidia katika ujenzi wa shule,zahanati,miradi maji, utunzaji misitu na vyanzo vya maji etc.

Bakhresa amefungua viwanda Tanzania na sheria za Tanzania sio za majimbo kwa hiyo mapato ya serikali yanasaidia maendeleo ya nchi bila kujali ni sehemu gani yamepatikana sasa kama hayaendi zanzibar inavyotakiwa hilo litakua tatizo la serikali na sio bakhresa.
Wananchi wa tanzania wako huru kufanya kazi sehemu yoyote ndani ya jamuhuri ya Tanzania.
Ndugu yangu Jokakuu hata mimi ningependa asaidie kwenye hizo nyanja ulizozitaja lakini kumbuka kutoa ni hiyari na yeye kaamua atoe huko, ila kitu kingine ninachoona mimi kuhusu hizo nyanja ulizozitaja wapo wengi wa kutoa ukilinganisha na nyanja hii anayotoa yeye.
Thanks
 
baresa katoa ajira kibao kwa vijana bongo
nadhani labda ana misingi mizuri. lakin wait....
hivi alianza anzaje? ile migodaun ya national milling aliipatapataje? na kwa nini and who's influence kufa kwa NMC?
labda nipo kizani

Hapo mtafute Andy Chande!
 
popote pale watu tunatofautiana. wengine ni wazito katka jamii na wengine wepesi. wengine wakisema juu na chini sauti zao zitasikika

kuna mtu humu jf kwenye thread hii amesema alijaribu kuisaidia cuf wakamchomea ngano. naona mchango wake yeye alijaribu kuelekeza huko lakin akatishwa vibaya. naye akatishika. kimya. nahis hana hamu tena na kusaidia cuf au kusema against ccm yasijeyakamkuta kama ya zaman kuharibiwa bidhaa

kwa wengine wakikaa kimya wanakuwa wanaogopa machafu yao ya nyuma au ya sasa kuanikwa

tz ni yetu sote. ni yetu sisi wahasibu, wahandis, madaktari, wafanyabiashara, waandish wa habari etc.
kama kuna mambo ya ovyo yanaendelea katka tz yetu tutakuwa tumekosea sana kukiamua kuwaachia wanasiasa pekee wakemee. kama mambo hayaendi sawia wote tupige makelele kupinga
 
Wafanyabishara Watz inapendeza pia wanafungua biashara nchi zingine kama Malawi na Mozambique! Ili mradi tu pia walipe tu kodi!

Naskia EXIM baada ya kufungua tawi Komoro sasa watafungua Jibuti na na Southern Sudan! Vipi benki zetu naona bado wamelala.. NBC, CRDB, NMB..wenzao KCB wanafungua matawi Tz na Ug.. wao wanfanyaje?

Pia nimesikia Family Soap amefungua kiwanda Maputo Msumbiji..which is good!

Kokote Mtz anakowekeza ili mradi tu alipe kodi!
 
Katika mapambano haya ya ufisadi ambacho nchi inadhulumiwa, wafanyabiashara wanatumia nafasi yao kujitengeneza na yeye yuko upande gani? Au kwake yeye hajali kile kinachotokea nchini katika ulingo wa siasa anachojali ni kutengeneza fedha tu? Hajali dhulma ya mamilioni ya wananchi, wizi wa Benki Kuu n.k? That is all I care about.

Ndiyo maana watu kama kina Andy Chande na wenzao wako kimya. Kwangu mimi ukimya wao unapiga kelele.

Mimi simjui Bakhresa wala sina kitu chochote kinachonielekeza kumfikiria au kumdhania ni fisadi; ila najua ni mtu prominent ana uwezo (na wengine wamedai hapa kuwazidi watu wengine wengi tu). Kutokana na uwezo wake huo binafsi najiuliza anautumia vipi katika kubadilisha mwelekeo wa kisiasa nchini?

Jibu nililolipata hadi hivi sasa ni kuwa yeye hajali hali ya kisiasa nchini au uongozi. Anachojali ni biashara zake zinaenda powa tu. Huyu kwangu si mfano. Kwani, mwenye nguvu anapokaa kimya wakati wanyonge wanadhulumiwa basi anahalalisha dhulma hiyo.

Na hapa sisemi aitishe mkutano wa vyombo vya habari (akifanya hivyo sina tatizo) lakini he need to take a public position of where he stand on the question corruption in the country. Anything less than that wanaotaka kumuita wamuige. No I.

Mwanakijiji wacha kuchanganya pumba ,mi nakushangaa umekuwa mtu wa siasa nakumbuka zamani ulikuwa mtu wa mashairi kama sikosei :D ,lakini niwache kushangaa maana hata waimbaji na waandishi nao wanakimbilia kwenye siasa,sasa nimewahi kuwauliza baazi ya wafanya biashara kuhusiana na mwenendo wa siasa za nchini wengi walinieleza na kunisimamisha kuwa nisiendelee nazo au wao si wabunge wala hawataki kujihusisha na biashara ya siasa ,walizidi kusema siasa ni kazi kama kazi zingine hivyo mtu anaweza kufanya kazi mbili na zikamletea faida ila kwa hao niliozungumza nao walisema hawawezi kuchanganya biashara zao na biashara ya siasa ,katika siasa ni lazima uwe unatumia sana ili kupata faida na utakapojihusisha na siasa utakuwa upo katika upande mmoja ,utawala au upinzani jambo ambalo linaweza kuhatarisha biashara zako hivyo ni bora kutojihusisha na pande zote mbili ,halafu ukiwa mfanya biashara una hiari yako kusaidia au kutosaidia kwani unapopata shida au kufilisika mbebaji ni wewe mwenyewe ,hata huko kwenye public kuna watu tele tu ambao hawataki kabisa kujihusisha na mambo ya siasa ,hawaendi mikutanoni wala hawaendi kujiandikisha wala kupiga kura na mambo yao yanawaendea na mbali ya Bakharisa kuna matajiri wengi tu ambao hawataki kujishughulisha na mambo yanayojivuta katika siasa ,wao na biashara zao na wengi wa hawa utawakuta wanafuata taratibu zilizopangwa na serikali sio wa njia ya mkato ambao wanatafuta urahisi na kutafuta na kuifuata njia rahisi ni kuingilianza katika mambo ya siasa ili upate kula na wakubwa naweza kusema katika biashara za Bakaresa ameweza kuestablish well management ambayo inafanya kazi international na hii ni hatua kubwa ,sidhani kama muombaji kazi inabidi azungumze na bakaresa kwanza ndio apate kazi au uendeshaji wa sehemu zingine zinahitaji lazima bakareza atoe kibali ni kampuni ambayo ina watu waliosoma na wenye kujua nini wanakifanya ,huwezi kumfananisha bakareza na Mengi au Rostam maana wao biashara zao zimechanganyika na siasa na hata wanapotoa misaada huwa wanajionyesha na kuutangazia umma aidha kupitia vyombo vyao au vya serikali , ila Mwanakijiji unaweza kumualika na kumfuata na kumhoji juu ya hali ya nchi ili ukapata maoni yake kama unavyowafanyia vigogo wengine ,naona utakuwa umetuwekea sawa hili la yeye kuwepo upande gani ,hata unaweza kufanya mahojiano nae kwa njia ya simu ili tumsikie anamuelekeo gani ,natumai waandishi kwa hilo sio jambo kubwa.Timiza wajibu wako na sio kukaa pembeni na kulonga wakati uwezo wa kukutana nae ikiwa wewe ni muandishi ni jambo rahisi.
 
Last edited:
Hakuna siku serikali ililazimishwa kuuza NMC au mitambo yake, kilichotokea ni serikali kuamua kuuza kwa kushindwa kuiendesha. Alinunua NMC (mzizima) na akajaribu kununua NMC (kurasini) lakini alishindwa kwa njia ya tender na aliyeshinda ni mohamed enterprises.
Kuhusu mavi ukiyachokonoa yatanuka! na mimi ningependa uendelee kuyachokonoa kwa sababu unaweza ukaja na kitu kipya kwangu ambacho sikijui kuhusu Bakhresa na kikawa ni kweli, kitasaidia kwenye vita dhidi ya ufisadi. ni muhimu kuwa na refrence ya mafisadi wa zamani ili huko tuendako yasitokee tena
Thanks


Ni kweli serikali haikulazimishwa kuuza mitambo ya NMC, lakini Viongozi wenye dhamana ya kutoa maamuzi serikalini wakishirikiana na Wafanya biashara wakubwa walijenga mazingira ya kuia NMC na kuhakikisha kwamba katika zoezi la kufa kwake wanashibisha matumbo yao yasiyoshiba kama malori ya taka.
Kwamba serikali iliuza NMC kwa tenda si hoja ya msingi ya kuzuia Bharessa kucheza mchezo mchafu.
Kushindwa kununua mtambo wa pili ni kuzidiwa kete na Fisadi jingine kuliko kwamba alizidiwa na usafi wa kimaadili.

Waliifanyia hivyo GAPEX,
NBC ndo usiseme waliinyonga kwanza ife ndipo wakauza kwa bei ya njugu.
TTCL iliyo mishipaya ya fahamu ya taifa iliuzwa kwa bei sawa na kusomesha vijana kama 1000 huko UK.

Nyumba ya kifahari ya Semensi kule Kimara ilijengwa kwa fedha za MH Bhaharesa kashfa hiyo ilitolewa na Gazeti moja lililo milikiwa Mnyamwezi mmoja alokuwa akimiriki kampuni ya Bandari Interprise somebody Immanuel au Salehe sijui gazeti hilo bado linatolewa?
uchache alotia mfukoni ili anyooshe mambo haujulikani ulikuwa Tshs ngapi.

Huyo Mohamed Interprise ndo usiseme ni Jasusi wa Ibilisi muuaji mkubwa.

Ushahidi wa kimazingira ulionyesha kwamba kwa namna moja au nyingine alihusika kuua mashahidi wakuu waliowatumishi wa Maabara kuu ya Taifa katika kesi ya kulisha watanzania maandazi na chapati zitokanazo na unga wenye uvundo usiofaa hata kuliwa na hyawani.

Hivi watu wanadhani wote tuna vichwa vya karoti tumesha sahau????!!?

Wanahonga serikalini li wanunue ngano liyovunda na kuwa condemed kutoka India na kuiacha ngano safi kutoka Hang na kwingineko kule Arusha ili wapate faida ya kukata kwa nyengo na kutuacha sisi WaTZ tukiuugua kansa ya makoo na matumbo kwa kula uchafu uzaao faida nono kwao.

Ni upuuzi mkubwa kudhani Bhaharessa ni msafi tu kwa vile jina lake halimo kati ya Mfisadi wa hivi karibuni.

Njama nzima ya kuua NMC na madhumuni yake ya muda mrefu ni kuhakikisha Wafakiri wote( Watanzania) wanaendelea kununua mazao yote ya Unga yatokanayo na chochote kiagizwacho na Mohamed Inter na Azamu bila kuleta kelele mapepe na makeke.

Kama Binadamu inawezekana hawapendi kutulisha ngano ilopigwa laana huko ughaibuni,

lakini, kwa Choyo yao Izidiyo choyo ya Fisi mchoyo kuliko wote. Watu hawa hawajali kabisaaaa kama Watanzania mnakula unga utokanao na Mashonde ya Binadamu au vimelea vya magonjwa.
 
JF kiboko..kwa kweli kwa mwendo huu nadhani tunaweza kusema tanzania hakuna tajiri msafi wa kujisifia..si mchezo...kwa maoni yangu naona kama ukitaka kuwa tajiri tanzania nunua mali za serikali au imalize institution ya serikali kwa kuibinafsisha. 2010 nadhani theme ni chafua chafua tukose wote.
 
Mwanakjj naona unawataka watu wote wawe wanasiasa....na kama wafanya biashara lazima wachanganye biashara zao na SIASA kama za Mh.Mengi...either unataka kuifanya hii thread itoe "thanks" kwa Mengi anaetaka yote mawili...SIASA na BIASHARA.... otherwise endelea na msimamo wako....i do believe kukaa kimya kwa bakhresa na ana-conconcentrate na biashara zake ni much better...

Kuna msemo "concentration is one of the key of success"...Waswahili wanasema mtaka mawili moja humponyoka..."....Kama iman yako asiepayuka ktk SIASA basi nae fisadi...basi wewe nadharia nzima ya ufisad huijui au utakuwa na definition zako.

Kwa mnaosema asaidie ZNZ sijui mwataka afanye nini...ameweka MELI mda mrefu na ndio meli pekee iliyobora na haraka.nafikri Mengine Mh.Mwiba ameweka uzuri juu ya Chuki binafsi za SMZ....Meli ya SMZ taabani...kwa muda mrefu sasa.

Kuhusu Misaada jamaaa anatoa kwa wote...mwaka Jana au Juzi ametoa 400million kwa shule/Chuo cha kikristo hii habari ni public.kwa wenye muda waitafute ktk google....Misaada si muhim kutoa public....Ile ya pale K.Koo n style ya zaman ambayo sasa haifanyiki tena....Kama utaratibu wa Bakhresa ungekuwa ni kutoa misaada kwa waislam pekee, basi Mda mrefu tu wakristo wangeanza kumpiga vita.

kwa mtu anaesema kuhusu NMS...hizo bado ni tuhuma ambazo ni vigumu kuzithibitisha....otherwise wahusika waje na ushahidi. pia kama kununua Maghala yasio na chochote na we ukayaendeleze bado hapo unaonekana ufisadi..OK twendeni..

Kuhusu KODI.....kwa taarifa ambazo ninazo ni kuwa ukiwatoa TBL na TCC, yeye ndie anaefuata kulipa kodi kubwa.
Unaposema anakwepa KODI lazima ulete vigezo otherwise tutakachoona n kuwa Majungu na Chuki zisizo na msingi. kwa taarifa ingine ni mfanyabishara pekee ambae hana MIKOPO YA BANK....kwa wenye marafiki huko Mabenk mnaweza kuwauliza....ni hivi karibuni tu ameanza kujiingiza ktk Biashara za hovyo za STOCK market.....(na huko ndipo atakapopigwa DAFU LAO)

Kuhusu Ubora na watu KUFA, nafikiri wadau tuwe serious. Ushahidi huu hadi sasa haupo.kama upo, waandish wote wamehongwa wasitoe data hizo? unazo wewe Ogah peke yako?....pls kama unazo tusaidie.

Pia khs ubora nafikiri vitu ambavyo vinajadilika...kwanza inabidi tutatue tatizo la Msingi TBS....kuna matatizo Mengi ktk Ubora wa vitu vingi...na hapa si tu TBS bali hata maafisa wa AFYA wa Halmashauri wa Jiji.Binafsi ni mtu wa viwango si mchezo....the way ninavyotembea na watu tukifika ktk Mgahawa tukianza kuchambua...ni hatari..bahati mbaya ...Watz tumekuwa hatuna Viwango...na ukigomba viwangoa rafiki zako watakuona unajiona sana.

Fikeni ktk Migahawa wadau mjionee.....Huwezi amin watz hata KUOSHA VIKOMBE vya CHAI hatuwezi...vikombe vimejaa ukungu...na ukisema unaonekana wewe tatizo....same sometimes hata mikate ya bakhresa pia inakuwa mibovu..either from day 1 au sie wengine huku Tandika tulipo tunaletea ishakaa siku 2 au 3....

Bro Nenda soko la lolote ukajionee watu wanavyomwaga mchele au unga Hovyo.....Magunia hayana size...Lumbesa...hadi unajiulza TBS wako wapi?...ila TBS ukitaka uwajue Lete gari lako kutoka UK, then uone kasheshe lake....
 
Chuma,

Msimamo wako unaunga mkono Bakressa?

Kama anauza vyakula vibovu basi mie siafikiani na wewe 100%!!
 
He we vipi?

Eti tuhuma kuhusu NMC ni tetesi tu.

Tuhuma na na Kelele za Ubadhirifu wa NMC zilikuwako 1994-96 hiyo ni kama miaka 15.
Wenye miaka 30 leo walikuwa bado makinda pale Azania au kisutu wakila maandazi, Ubuyu na kubana pocket money ili wakale cone za Azam pale Kariakoo.
Wakati huohuo wengine tulikuwa ndo kwanza tumeanza kuendesha vicorola vyetu tuloagiza japan kwa $1500 CIF Dar baada ya kudunduliza kwa taabu sana vidolali hivyo kwa takribani miaka kaa 7 hivi, kwa kupata lunch ya Mazungumzo ya Yanga na Simba( kushinda bila kula)na kuishi kwenye chumba kimoja na stuli 2 huko Mtoni Kwa Azizi Ali Temeke.

Bhaharessa hana kesi ya kujibu leo hii kwa vile alisha ua soo miaka kibao.
Tunachopinga ni kumwingiza kwenye kundi la Watakatifu wakati naye ni Al-fisad.
 
Kuhusu Mohammed enterprises mimi siwezi kuzungumzia kwa sababu sijui chochote, Ila kuhusu Bakhresa tuhuma hizo ni uzushi mtupu hakuna kesi yoyote wala malalamiko yoyote kuhusu bidhaa mbovu na kwa taarifa tu hakuna unga bora Tanzania Kama wa Bakhresa na ice cream na juice na maji na karibu 50% ya watz wanatumia product za Bakhresa na hakuna malalamiko.
Lingine ni kwamba yeye Bakhresa ndie aliye leta mapinduzi katika biashara ya maji na kusababisha maji yashuke bei, alipo anzisha uhai na kuuza 150/= kwa 350ml wakati huo maji ya kilimanjaro yalikua 600/= kwa 350ml aliwahi kushauriwa aongeze bei ya maji akakataa na ndipo viwanda kama MAJI POA vikafa na kilimanjaro kushuka bei! Hivi sasa yupo kwenye mapinduzi ya juice na nionavyo mimi atafanikiwa kwani quality yake bomba na anauza 350/= kwa 300ml na maza juice inauzwa 700/= kwa 250ml
Thanks.
 
kuna mtu humu jf alianzisha thread inayoorodhesha watu 'wakwasi' lakin walio i 'screw up' tanzania.

vipi, hatuwezi anzisha thread ingine inayoorodhesha watz waliofanikiwa bila ku 'screw up' tz?

humo tunaweza ona kama bakhrehsa atakuwemo au la. kina mengi na nk.

kama mtu anamjua mtz anayeendesha shughuli zake amseme na ikiwezekana aseme amefanikiwaje etc
 
Back
Top Bottom