Bajeti yakataliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti yakataliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 12, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,521
  Likes Received: 81,905
  Trophy Points: 280
  • Wananchi wawataka wabunge kutoipitisha

  na Bakari Kimwanga
  TANZANIA DAIMA


  SIKU chache baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ya sh trilioni 13, bajeti hiyo imepingwa na viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati.

  Wadau hao wamewataka wabunge kutoipitisha bajeti hiyo kwa madai kuwa haina manufaa kwa Watanzania, bali imejaa takwimu zenye lengo la kuwapumbaza wananchi.

  Wakichangia mjadala wa kuichambua bajeti hiyo ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), uliofanyika jana katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema bajeti hiyo imejaa upotoshaji na kiini macho kwa wananchi.

  Profesa Lipumba, alisema vipaumbele vilivyowasilishwa bungeni na serikali vinakwenda kinyume na hali halisi ya matumizi ya serikali ambapo zaidi ya asilimia 53.6 ya fedha imetengwa kwa matumizi mengine.

  Alisema kitendo cha serikali kutanguliza kipaumbele cha umeme kinakwenda kinyume na azimio la Kilimo Kwanza ambacho kinaratibiwa na Wizara ya Kilimo iliyotengewa asilimia 3.4 ya fedha.

  ‘Kuna umuhimu wa kufanya mjadala wa kitaifa kuhusu bajeti kabla haijawasilishwa bungeni, huwezi kuwa na bajeti ya trilioni 13.5 huku ukitenga asilimia 14 kulipa madeni na trilioni 11 ndizo zikaendesha nchi, hakika hii bajeti haina tofauti na ya mwaka uliopita.

  “Hii ni hatari kubwa kwa serikali, iko tayari kuwasomea bajeti nchi wahisani kuliko Watanzania bajeti ya sekta ya afya imekuwa ikishuka kila mwaka hadi kufikia trilioni 1.2, ikiwa tofauti na mwaka uliopita ya trilioni 1.209, huku ni kuyaweka rehani maisha ya Watanzania wanaotegemea hospitali zetu za ndani,” alisema.

  Profesa Lipumba, ambaye kitaaluma ni mchumi, alizidi kuichambua bajeti hiyo na kusema kuwa kwa mujibu wa Waziri Mkulo, amewadanganya Watanzania ambapo inaonyesha kuwa Mtanzania anayetumia sh 641 na anaishi chini ya dola moja si maskini, ilhali maisha yanazidi kuwa magumu.

  Akizungumzia kukua kwa deni la taifa ambapo deni limeongezeka na kufikia asilimia saba, sawa na Trilioni 5.4, ikiwa tofauti na mwaka uliopita la dola za Marekani bilioni moja na milioni 500.

  Alisema bajeti hiyo si ya heshima, kwani imewasahau wastaafu kuhusu kulipwa mafao yao ambapo kwa sasa imekuwa tofauti na kinyume cha dira ya taifa kwa watu wote.

  Profesa Lipumba alionya juu ya mpango wa serikali wa kuwa na dira ya taifa, ambao hautoi tija kwa watu wake ambapo aliitaka serikali kuitisha mjadala wa kitaifa ili kuweza kupanga upya dira hiyo itakayo shirikisha watu wote nchini.

  “Sina hakika kama Rais Kikwete, ameusoma mpango huu wa dira ya taifa kwa kuwa hauelezi kwa kina matatizo ya Watanzania, kitendo cha Waziri Mkulo kushindwa kuielezea dira ndani ya bajeti hakika ni tatizo kwa nchi yetu na siasa zimetawala katika masuala ya kitaalamu,” alisema Profesa Lipumba.

  Naye Mkurugenzi wa taasisi huru ya uchumi na kijamii (ESRF), Dk. Bohela Lunogelo, alijikuta katika wakati mgumu mara baada ya kusifu mpango wa serikali kuhusu matumizi ya pikipiki za kubebea wagonjwa za matairi matatu, maarufu ‘Bajaj’.

  Hata hivyo mara baada ya kukutana na zomea zomea hiyo alilazimika kujitetea na kusema alikuwa akitoa mfano wa matumizi ya pikipiki, hali ya kuwa bajeti ni moyo wa taifa.

  Dk. Lunogelo alisema kutokana na hali hiyo matarajio ya Watanzania ni makubwa kwa serikali yao na kuvitaka vyama vya siasa kuwa na utaratibu wa kukosoa na kujibu hoja kwa kufikisha ujumbe kwa wananchi wa vijijini.

  “Ni vizuri bajeti ikawa inajadiliwa na Watanzania mapema walau kwa muda wa miezi sita kabla ya kufikishwa bungeni na hapa … bajeti itakuwa inatafsiri sasa ya kuandaliwa na Watanzania wote,” alisema Dk. Lunogelo.

  Hamadi Tao

  Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Hamad Tao, alipinga serikali kutenga sh bilioni 432 kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi ili kununulia silaha ilhali Watanzania wanakabiliwa na njaa.

  “Ninapinga na kulaani kwa nini Wizara ya Ulinzi itengewe sh bilioni 432 kwa ajili ya kununulia silaha huku watu wakiwa wanakufa njaa, kwani nchi ipo kwenye vita? Kwa hili ni kuwadhihaki wananchi wa taifa hili,” alisema Tao.

  Mbatia

  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema umefika wakati kwa Chama Cha Mapinduzi kutambua kuwa Watanzania wa zamani si wa leo.

  “Umefika wakati CCM na watawala kutambua nchi ni ya kwetu wote na kutambua kuwa bajeti ni ya Watanzania wote na si ya serikali pekee na viongozi wake, na yanahitajika mawazo mapya kwa masilahi ya taifa,” alisema Mbatia.

  Mbatia ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa mjadala huo alikionya Chama Cha Mapinduzi kwa kusoma nyakati na sura ya Watanzania wa sasa nini wanahitaji ndani ya nchi yao.

  Allan Mwaigaga, alisema umefika wakati wa kufanya vitendo kuliko maneno kwa kuwaweka kando waovu wanaoliumiza taifa.

  “Mwalimu Nyerere, alipoondoka aliacha viwanda hapa nchini kila kona na leo tunahamasishwa mradi wa EPZ huku bajeti ikishindwa kueleza namna itakavyoweza kufufua na kujenga viwanda vikubwa na vidogo hakika hili wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao wasiipitishe bajeti hii na ilirudishwe kwa wananchi ili ijadiliwe kwa kina,” alisema Mwaigaga.

  Erasto Tumbo

  Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema umefika wakati wa serikali kupunguza matumizi yake makubwa huku akiitaka Wizara ya Fedha kuacha kutenga fedha za tafrija na ukarabarti wa Ikulu kila mwaka.

  Alisema kitendo cha Ikulu kutengewa kiasi kikubwa cha fedha huku wananchi wakikosa dawa hospitalini ni kukosa uzalendo na umakini kwa viongozi, hali inayowafanya wananchi kukata tamaa ya maisha.

  Mbunge wa Ziwani (CUF) na hoja binafsi

  Katikati ya mjadala huo Mbunge wa Jimbo la Ziwani, Mohamed Zuberi Ngwali (CUF), alisema umefika wakati wa kujadili fedha za umma na hata nafasi ya wabunge wa viti maalumu, ambao hawana kazi kubwa kuliko wabunge wa majimbo.

  Alisema katika kuhakikisha anasimamia fedha za umma yupo mbioni kuwasilisha hoja binafsi bungeni, kwani wabunge hao hawafanyi kazi kubwa zaidi ya kununua hereni za dhahabu na magauni wawapo bungeni.

  “Nitawasilisha hoja binafsi ili kuhoji nafasi na kazi za wabunge wa Viti Maalumu bungeni … sisi tupo wawakilishi wa majimbo tuliochanguliwa wao wana kazi gani?” alisema na kuhoji mbunge huyo.

  Hata hivyo hadi mwisho wa mjadala huo washiriki hao waliipinga bajeti hiyo na kuwataka wabunge wote bila kujali vyama vyao kutoipitisha bajeti hiyo kwani haina jipya kwa maisha ya Watanzania.

   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jun 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Good move!
   
 3. k

  kiche JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  wabunge wa ccm ni vichwa vya panzi,na hata wale wenye akili ni kama hawana,wameshaathiriwa na utetezi wa chama badala ya utetezi wa wananchi,wanatetea hata jambo likiwa ni la kipumbazu!!,mfano hoja ya Lissu kuhusu mahakama katika bunge lililopita!,wameshindwa kuelewa kuwa watu tusio na vyama ni wengi kuliko walio kwenye vyama.
  wabunge hao walivyo wa ajabu bajeti hii itapita huku wakizomea wale wa upinzani! na kwa vile ni watu wa posho najua itaanza safari ya kuzunguka nchi nzima kuitetea!!!!!,ila naomba wajue kuwa hakika yana mwisho.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kumbe wabunge wa viti maalum kazi yao ni kununua hereni na magauni......hahahahaaaaa
   
 5. k

  kiche JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hilo halina ubishi,hata spika alishatoa angalizo katika uvaaji wao,tatizo naloona hapo ni jinsi mfikisha hoja alivyoifikisha na nafasi aliyonayo bungeni,hao wanunua hereni atakuwa nao kwa miaka 4 na nusu iliyobaki,sina uhakika mahusiano yatakuwaje na ikizingatiwa kuwa watanzania wengi hatupendi kuambiwa ukweli!!.
   
 6. h

  hans79 JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  kama itapitishwa ndo uwe mwisho wao kutenda mambo kipuuzi,tuandamane nchi nzima kupinga upuuz huo hata kuwazomea wale walohusika.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wachache wanafanya kazi nzuri sana, lakini wengine huishia kuwa chak'la za watu tu
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  hawa wabunge wa ccm nina uhakika wataipitisha.
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Kelele hizi zitasaidia sana japo hazitabadilisha msimamo wa wabunge wa ccm
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  "Chama kwanza...."
   
 11. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ila nijuavyo mimi wataipitisha kwa uwingi wao ila wakae wakijua madhara yake ni kama cancer kwani inaua mdogomdogo.
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuona kichwa cha habari nikajuwa hili litakuwa Tanzania Daima.

  Tanzania Daima si linajulikana la nani.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wewe ni sawa na kikundi cha matarumbeta...kazi yao huwa ni kupiga tu hayo madude na mwisho huwa ni getini ...katu hawaingii ukumbini.....
   
 14. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Vipi tena TZDaima? Nilimsikia Mh. Mbowe mwenyewe akiisifia hii bajeti na kwamba angefuatilia mikakati ya utekelezaji, angalieni msijekuwa mnacheza ngoma ya watu wengine!
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135  Ndugu Mwanakijiji
  ,
  Kwanza ulinishituwa kwa kichwa cha habari lakini niliposoma posting nilianza kujiuliza hivi tulitegemea nini iwapo lengo la siasa ya Tanzania ni kugombea madaraka? Katika hali hiyo haitotokea hata siku moja kwa wanaotaka kuingia madarakani wakasifu kile kilichofanywa na walio ndani ya utawala.
  Nashangaa kuwa wanasiasa wetu wanataka matakwa yao yawemo ndani ya matakwa ya chama tawala huku hawako tayari kwa serikali ya umoja. Niaminivyo mimi ni kuwa kwa lengo lile lile la kutaka madaraka juu ya wananchi chama tawala kinajaribu kufanya kila kiwezacho kuhakikisha kuwa Bajeti itawafurahisha walio wengi ili kuendelea kupewa ridhaa ya kuendelea kutawala. Tofauti ya chama tawala na Serikali yake kulinganisha na vyama vinavyogombania nafasi hiyo ni kuwa Chama tawala kina kazi ya Kujenga wakati wapinzani wameegemea katika kubomoa jitihada za chama tawala.
  Hivi vyama huwa viko hata kabla ya kuwasilishwa bajeti na huwa hawana kazi yoyote wanayoifanya katika suwala la Bajeti isipokuwa kungojea kutowa makosa ya bajeti hiyo na hapo ndio bajeti mbadala hufuata. Hii Mwanakijiji huoni kama kutanguliza gari la farasi kabla ya farasi ? Kama lengo ni kuwafaidisha wananchi basi vyama hivi na asasi mbalimbali wangetowa mapendekezo yao mbele kabla ya kutengenezwa bajeti. Tumekuwa tukiona kila mwaka bajeti mbadala ya upinzani lakini hazijawahi kutumika hata siku moja. Hii haileti logic iwapo lengo ni kwa mwananchi la kama lengo ni hili linaloonekana la kuleta confussion kwa ajili ya political gain basi wananchi hawana budi kuendelea kuwapa ridhaa MAGAMBA kuliko wale wasioangalia maslahi ya wananchi.
  Tunaposema nchi ni yetu sote na kukitaka chama tawala kitambue hivyo huku tukiachilia hao hao kupanga bajeti peke yao na baadae ndio tutowe makosa, hatuwa ambayo haiwezi kulisaidia Taifa huwa tunakinzana na kauli zetu. Pengine tukikubali collective responsibility itatufanya tukose kitu kimoja kinachosaidia kuleta confussion kwa wananchi hivyo ndio tunaamuwa kujifanya tuna uchungu wa wananchi pale kelele zetu zitasikika na kuonekana kuwa tuna uwezo kuliko tukitowa mapendekezo yetu katika kuhakikisha kuwa bajeti itamsaidia mwananchi.
  Haya tukiangalia haya ya uwakilishi hewa unaosababisha matumizi yasio ya lazima tunajikuta kuwa hata hawa wanaoitwa wapinzani hawajali matumizi mabaya kama wanavyodai. Angalia hawa CHADEMA wanapotosha watu kwa kutumia malipo ya posho wakiacha suwala la wabunge wa upendeleo. Wana faida gani hawa bali ni upotevu wa hizo hela wanazojidai kuwa zinapotezwa. Lakini kwa vile huu mtindo wa vitu maalum ndio uliowapa CHADEMA uwezo wa kuwa na sauti basi wako tayari kunyamaza na kusahau zile kelele zao za kuokoa pesa za wananchi. Hili pia linaoonekana kwa Wabunge kutoka upande wa pili wa Muungano, ambao kikatiba wana mambo machache ambayo wangepaswa kuyashughulikia katika Bunge. Badala yake wanalipwa na kuhudhuria siku zote na hata kuwemo ndani ya kamati ya mambo yasiyo ya Muungano. Hivyo nyinyi mnaojidai mna uchungu na hali zinazosababisha umasikini hamuyaoni madudu haya au kwa vile yanasaidia kutafuta uhalali wa kisiasa mnanyamaza kimya?
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nafikiri uhusiano hautokuwa mbaya kama wale wanaopendekeza hizo fedha za hereni kuondolewa!
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sasa kwanini haya marashi yao wasiyapendekeze kabla Magamba hawajapanga hiyo bajeti? Hasa tukichukulia maanani kuwa ikishapangwa basi piga uwa inapitishwa? Haka kamchezo juu yetu wananchi kinatakiwa kifikie kikomo. Waache kutumia maafa yetu kwa faida ya umaarufu wa kisiasa.
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Jun 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nilipenda saana the program jana ulivyokua for ilinipa picha ya jinsi Watanzania walivyosukumwa na kuona they are a part of decision making katika masuala yanayohusiana nao na hasa mambo ya bajeti, ingawa most members walikua wakitoka nje ya maada na wengine kuongea kwa kuiga tu kua mradi kasimama mbele ya TV na kutamka kua bajeti haifai…. the important thing ni kua most walotoa mada kama wahusika walisikiliza ujumbe ulifika.

  Simkubali kivile Mbatia for my own reasons but I loved alivyohitimisha, ilikua kweli tupu na wala si chembe za kisiasa, aliongea kama mzalendo wa kweli Mtanzania anavyotakiwa awe/aongee.. nafikiri he has changed my mind on my kutomkubali. Most wengine ilikua propaganda tu za kisiasa… hadi inachosha… for once mtu kusimama na kua mzalendo si mwanasiasa ni Vigumu! All in all big up kwa TCD… Message I believe has been delivered!

  Pia ilinigusa suala (ambalo ilikua nje mada ya budjet) kua viti maalum kwa ajili ya akina dada/mama haina maana wala umuhimu wowote! Viti maalum ni muhimu saana… ila simlaumu huyo mbunge kwa mawazo na msimamo wake hou… maana kweli kabisa hao wadada wa viti maalum hata mimi mwanamke mwenzao sijaona bado nguvu yao au mchango wao… labda yawezekana ni sababu ya vigezo walochaguliwa ikawa ina contradict na uwezo wao wa kufanya kazi…

  Katika the whole kipindi, nilisikitika the number of women participants….
  Naona majukumu yametubana mno hasa ya kupanga budget za nyumbani!
   
 19. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na kuwastarehesha wale waliowakingia kifua ili wachaguliwe
  Si unajua walio wengi ni vigoli wa waheshimiwa!!!!!!!

   
Loading...