Wasaalam.
Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha wa 2025/26 itasomwa tarehe 27 Mei, 2025.
Karibuni kwa ufuatiliaji.
Ahsanteni sana.
Ahsante sana.
Hivi mheshimiwa waziri zile gharama za mama kujifungua hospital za serikali wizara yako huwa inalipia au ni bure tu?
Kuna mkanganyiko hasa kwa wananchi wanapoambiwa kwamba kujifungua hospital za serikali ni bure. Mfano mama anapojifungua na kuandikiwa baadhi ya dawa wengine hugoma kununua kwa madai kwamba kila kitu ni bure.
Kwa nini msiliweke hili wazi kabisa kwa wananchi kwamba mnachogharamia ni kujifungua tu na si gharama zote zitakazoongezeka? Hii itawaondolea lawama watoa huduma za afya kwamba wanafanya kinyume na utaratibu.
________________________________
Mheshimiwa waziri, naamini utaongelea haya miongoni mwa mengine mengi kwenye bajeti yako hapo 27 May 2025:
(1). Suala la watoto wa mitaani. Siku hizi kuna watoto wengi sana wa umri wa kwenda shule wanarandaranda mitaani hasa kwenye miji na majiji. Watoto hao wapo mitaani na wanajiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya, matendo maovu, nk. Ni muhimu kuwa na mkakati maalumu wa kushughulikia suala hili kwa ajili ya taifa la kesho.
(2). Wafanyakazi wa ndani: kuna unyanyasaji na ukatili unaofanywa kwa baadhi ya hao wafanyakazi wa ndani hapa nchini na nje ya nchi. Nategemea kusikia wizara yako imejipanga vipi kukabiliana nalo kwa mwaka unaoanza.
Nakutakia kila la kheri mheshimiwa waziri.