Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Uliambiwa na nani kuwa kama mtu ukiwa upinzani huwezi kusema mazuri ambayo yanafanywa na wana ccm? Wewe unadhani bila ya wana ccm hii miziki yote iliyowekwa humu jamvini ilivujishwa na nani toka serikalini.

Mimi kama kuna mtu anafanya kazi nzuri Tanzania atapata support yangu hapa hata kama mtu huyo ni mwanaccm. Wapinzani wengi wako nje ya serikali na hawawezi kupata kila kitu kinachoendelea huko.

Kumbuka kuwa hapa hatupiganii vyama mkuu bali masilahi ya nchi yetu. Mtu yeyote anayepigania masilahi ya nchi yetu anapata support hapa JF kama kawa - awe mpinzani au mwana ccm.

Wajitokeze na waondoke huko!

HAKUFAI TENA...WESHAROGWA!

Mama alikuwa akipiga kelele kweli..Lakini ukisikiliza kwa makini unakuja kugundua kuwa ETI ANATAKA PESA ZA EPA ZIRUDISHWE!

PESA ZISHARUDISHWA TENA LABDA ZOTE NA NDIO MAANA WALIFANYA SIRI KUTOWEKA HADHARANI IN DETAILS!

HAKUKUWA NA JIPYA ALILOSEMA MAMA WA WATU ALIYETOKEA KWENYE VYOMBO VYA HABARI AKIONGEA KWA MACHUNGU HUKU ANACHOSEMA NI TOFAUTI!

KWANZA SERIKALI ISHAZITAKASA NA HIVYO KUWATAKASA WATUHUMIWA!

ALICHOTAKIWA MAMA KUSEMA NI....YES CCM TUNA TATIZO LA UFISADI NA WALIOMO WACHAFU WATOLEWE WAFIKISHWE KWENYE MKONO WA SHERIA!
 
Nimesema HAWEZI KUJIKAMATA YEYE MWENYEWE FISADI.
Mbona unatwist?

Wakati mwingine inabidi ukumbushwe kuwa uko JF. Hapa unashikwa kwa maneno yako mwenyewe. Ulichosema ni hiki hapa:

jmushi1 said:
AWAKAMATE WAMILIKI WOTE WA BANK M...Kina Sanjay Kumar,

K Bhasker Narayan, Noble Azania Investments ltd,Napster Group Incorp. Inayomilikiwa na ndugu za Ballali pamoja na wanasiasa wengine.

Sunjay Mehta na Vimal Mehta ambao ni kaka na kisheria tayari hiyo Bank M ilitakiwa iangaliwe kwani ni MAFisadi!

Allied & Equity Gen.Zen Advertising, BV holdings ltd,V&B Assoc ltd, New Malallaln mining co ltd, Navy cutt tobbaco ltd, Bora Apts, Noble motors ltd, Noble Azania grp
 
Wajitokeze na waondoke huko!
HAKUFAI TENA...WESHAROGWA!
Mama alikuwa akipiga kelele kweli..Lakini ukisikiliza kwa makini unakuja kugundua kuwa ETI ANATAKA PESA ZA EPA ZIRUDISHWE! PESA ZISHARUDISHWA TENA LABDA ZOTE NA NDIO MAANA WALFANYA SIRI KUTOWEKA HADHARANI IN DETAILS! HAKUKUWA NA JIPYA ALILOSEMA MAMA WA WATU ALIYETOKEA KWENYE VYOMBO VYA HABARI AKIONGEA KWA MACHUNGU HUKU ANACHOSEMA NI TOFAUTI!
KWANZA SERIKALI ISHAZITAKASA NA HIVYO KUWATAKASA WATUHUMIWA!
ALICHOTAKIWA MAMA KUSEMA NI....YES CCM TUNA TATIZO LA UFISADI NA WALIOMO WACHAFU WATOLEWE WAFIKISHWE KWENYE MKONO WA SHERIA!

Kumbe wewe hutaki pesa zirudishwe?
 
Wakati mwingine inabidi ukumbushwe kuwa uko JF. Hapa unashikwa kwa maneno yako mwenyewe. Ulichosema ni hiki hapa:

MWK...Ili nisipate shida ya kurudi nyuma..Nenda kule kwenye ile thread ya "Is our president corrupt?"
Huko tushamalizana...Tunasonga mbele sasa..Unless unanitega ili nifungiwe tena.
 
Kumbe wewe hutaki pesa zirudishwe?

Pesa zirudishwe zisirudishwe tutazipata tu!
Tena kama washarudisha ndio vizuri kwani hapo ni kukiri kosa tayari!
Mwema keshasema hawezi kumkamata mtu licha ya kwamba hajahusika.
Hatuwezi kumchonganisha na bosi wake...Ila sisi tusiokuwa na maslahi na mtu HAPA NI MPAKA KIELEWEKE...REMEMBER I AM A JUSTICE MONGER!
 
MWK...Ili nisipate shida ya kurudi nyuma..Nenda kule kwenye ile thread ya "Is our president corrupt?"
Huko tushamalizana...Tunasonga mbele sasa..Unless unanitega ili nifungiwe tena.

Mushi,

Hakuna anayekutega na usiwe too much defensive. Haya yote ninayokuuliza yanatoka kwenye hii thread. Ni maneno yako mwenyewe uliyoandika. Mimi nakupa nafasi zaidi ya kufanya point yako ieleweke zaidi kwa kukuuliza kile ambacho umeandika.

Kwa nini unafikiria mimi nataka wewe ufungiwe? Itanisaidia nini mimi binafsi kama wewe ukifungiwa? Wewe umeonesha moyo wa mapinduzi hapa kwa ajili ya nchi yetu. Kwa nini nitake ufungiwe?

Siwezi kurudi kwenye topic nyingine kwa vile ninachangia kile unachoandika hapa kwenye hii thread. Elezea kile unachosema na mimi nitakuelewa.
 
Pesa zirudishwe zisirudishwe tutazipata tu!
Tena kama washarudisha ndio vizuri kwani hapo ni kukiri kosa tayari!

Kwa hiyo unakubaliana na Mama Malecela kuwa ni vizuri na ni lazima pesa za EPA zirudishwe na waliouhusika na huo wizi watajwe kama alivyosema mama bungeni?

Mwema keshasema hawezi kumkamata mtu licha ya kwamba hajahusika.
Hatuwezi kumchonganisha na bosi wake...Ila sisi tusiokuwa na maslahi na mtu HAPA NI MPAKA KIELEWEKE...REMEMBER I AM A JUSTICE MONGER!

I am glad kujua kuwa wewe ni justice monger... ... karibu kwenye game ambayo wengine hapa tumeicheza na wakati mwingine tumekimbizana na walinzi wa nyaraka za serikali waliotuona tukijaribu kuzinyofoa kwenye safe wanakozificha.

Karibu ujiunge na wanamapinduzi wenzako. Hapa ugomvi zaidi ni kwa waovu wa serikali na kazi ya pili ni kutoa ushauri wa nini kifanyike kama inalazimu.
 
Mushi,

Hakuna anayekutega na usiwe too much defensive. Haya yote ninayokuuliza yanatoka kwenye hii thread. Ni maneno yako mwenyewe uliyoandika. Mimi nakupa nafasi zaidi ya kufanya point yako ieleweke zaidi kwa kukuuliza kile ambacho umeandika.

Kwa nini unafikiria mimi nataka wewe ufungiwe? Itanisaidia nini mimi binafsi kama wewe ukifungiwa? Wewe umeonesha moyo wa mapinduzi hapa kwa ajili ya nchi yetu. Kwa nini nitake ufungiwe?

Siwezi kurudi kwenye topic nyingine kwa vile ninachangia kile unachoandika hapa kwenye hii thread. Elezea kile unachosema na mimi nitakuelewa.

Wewe unajua kikwete anapewa hishma kubwa hapa..Halafu unagangamala niseme ni nani wa kumkamata.
Sasa kama na wewe ulisoma ile ripoti ya EPA halafu hujajua kinachoendelea..Then tuna tafsiri tofauti..Na hapo ndio KAAZI KWELI KWELI...!
 
Wewe unajua kikwete anapewa hishma kubwa hapa..Halafu unagangamala niseme ni nani wa kumkamata.
Sasa kama na wewe ulisoma ile ripoti ya EPA halafu hujajua kinachoendelea..Then tuna tafsiri tofauti..Na hapo ndio KAAZI KWELI KWELI...!

Kikwete anapewa heshima hapa na hiyo ni lazima kwa jamii yetu. Katika jamii yetu binadamu wote wanapewa heshima wanazostahili. Sidhani kama wewe utakuwa na tatizo la kusema kuwa Kikwete akamatwe na hayo maneno yakawa tofauti na yangu ya kumtaka Kikwete ajiuzulu.

Heshima zipo na watu wanapingana bila kupigana mkuu na huu ndio moto wa JF yetu hii.
 
Mara baada ya pesa za EPA kuchotwa BOT ziliwekwa BANK M NA MAFISADI.
Huko zikaamishiwa tena kwenda kwenye benki nyingine zaidi ya 12.
Maajabu mengine ni kwamba...Hao wamiliki wa bank M ndio hao hao wamiliki wa kampuni zilizotoa pesa kwenye benki hiyo pamoja na zile nyingine zaidi ya 12.
Makampuni hayo yalichukua pesa hizo kwa kigezo kuwa zinakwenda nje ya nchi.
Huko nje ya nchi ni makampuni hewa yaliodaiwa kutokea Japan na kwingineko duniani
Ushahidi upo mchana kweupe.
Kampuni za Ndovu soap, na hiyo ya BORA apts. zilishirikiana na kufungua kampuni feki ya kijapani nayoitwa Maruben.
Hawa watu wote ni mafisadi pamoja na BODY OF DIRECTORS OF BOT.
Hakuna haja ya kumkamata Kikwete...Hao watendaji walioidhinisha malipo wakamatwe...TIME FOR POLITICS IS OVER.
 
Kikwete anapewa heshima hapa na hiyo ni lazima kwa jamii yetu. Katika jamii yetu binadamu wote wanapewa heshima wanazostahili. Sidhani kama wewe utakuwa na tatizo la kusema kuwa Kikwete akamatwe na hayo maneno yakawa tofauti na yangu ya kumtaka Kikwete ajiuzulu.

Heshima zipo na watu wanapingana bila kupigana mkuu na huu ndio moto wa JF yetu hii.

Haya mambo ya ujambazi Kikwete asiulizwe tena...Polisi MWEMA KAMATA HAO WATENDAJI WALIKIUKA MIIKO YA KAZI MSIFANYE UCHUNGUZI KISIASA MTAINGIA MATATANI NA NYIE!
FANYENI KAZI YENU!

NB:Mara baada ya pesa hizo kuwekwa kwenye hayo mabenki 12...Kuna wadhamini wengine waliozidhamini kampuni hizo hewa...MALEGESI LAW CHAMBER NI MAFISADI WALIOZITENGENEZA HIZO KAMPUNI FEKI...HAO WAKAMATWE BILA SIASA NA SAIDI MWEMA!
 
Benki ambazo zilihifadhi pesa hizo baada ya udhamini wa MALEGESI LAW CHAMBER ambao wali CONFIRM kuwa MAKAMPUNI HAYO FEKI NI YA KWELI NA HALALI...Wakisaidiana na wadhamini wa makampuni halali ya Ndovu soap,BORA APTS na nyinginezo ni hizi hapa...

1)Bank Of Barad T LTD
2)Barclays Bank LTD
3)CRDB
4)Eurafrica Bank LTD
5)EXIM BANK
6)Kenya commercial Bank(TZ Branch)
7)NBC
8)STD CHARTERED
9)UBA...Na nyinginezo.

Wamiliki wa kampuni zilizochota pesa...Ndio hao hao wamiliki wa Benki M ambayo ilizitoa pesa kutoka BOT,na pia ndio wamiliki wa makampuni yaliyoanzisha kampuni feki za nje kwa kushirikiana na MALEGESI LAW CHAMBER pamoja na makampuni mengine yenye kukubalika kuwa ni ya halali.
Kwa mfano kampuni ya Bora Apts walianzisha kampuni feki na kuchukua hizo pesa huko kwenye benki hizo hapo juu na wakati huo huo kuwa na share kwenye benki M ambao ilizitoa hizo pesa BOT na kuzipeleka huko kwenye hao mabenki tayari kwa kupigiana PANGA!
Yani wamejigawia pesa na jasho na damu la watanzania mbele za macho yetu na ya Mungu BILA HATA HAYA WALA HATA CHEMBE YA HURUMA!
 
Wafuatao ni wamiliki wa BANK M iliyoanzishwa ili kuzituliza kwanza pesa za EPA...Mpango sasa ukaendelea na baada ya kuziweka pesa hizo kwenye benki hiyo feki wakapiga mahesabu wakaona NOMA...wakaamua wazikimbizie kwenye hizo benki ambazo ni za halali kama NBC nk. kwa kushirikiana na mawakili kina Malegesi.

Walipozifikisha huko kwenye mabenki halali...Tayari zikawa na uhalali...Hapo wakajifanya eti wamekuja KU WITHDRAW UPYA...kwa niaba ya makampuni feki waliyofungua wao na MALEGESI!

Pesa ambazo zilikuwa zao huko bank M zilikuwa nahaja gani ya kuziingiza kwenye benki halali kama si umafioso huo?
Waligundua kuzitoa benki m ambayo ni feki kutawapa matatizo..Wakazibariki kwa msaada wa baadhi ya watendaji wa serikali.

Wakazichota hizo pesa na kuzipeleka nje ya nchi kusikojulikana na nyingine kunako kampeni!

Pesa zilitakiwa zikamatwe zikiwa benk M wakati ilishajulikana wazi kuwa zilienda huko kifisadi na benki yenyewe si halali!

PESA ZILIKUWA ZAO TAYARI KABLA HAWAJAZIHALALISHA NA KUZIPELEKA HUKO KWENYE BENKI HALALI..MWEMA KAMATA WATU ACHA SIASA UTAPATA TABU...NI USHAHURI WANGU WA BURE!

Wakapata msaada kutoka serikalini..Zikaamishwa huko!
Ndugu zangu tuamke!

Mwema kamata hawa watu na uache kufanya uchunguzi wa kisiasa....Kama mmeshafanya uchunguzi wa kipolisi sisi kama wananchi tunataka muanze kuwakamata hao watendaji wabovu halafu mengine yafuatie...Kina Sanjay Kumar,

K Bhasker Narayan, Noble Azania Investments ltd,Napster Group Incorp. Inayomilikiwa na ndugu za Ballali pamoja na wanasiasa wengine.

Sunjay Mehta na Vimal Mehta ambao ni kaka na kisheria tayari hiyo Bank M ilitakiwa iangaliwe kwani ni MAFisadi!

Allied & Equity Gen.Zen Advertising, BV holdings ltd,V&B Assoc ltd, New Malallaln mining co ltd, Navy cutt tobbaco ltd, Bora Apts, Noble motors ltd, Noble Azania grp
 
Mii nataka kujua wabunge wangapi wa CCM waliopiga kura ya hapana? otherwise yale makelele yalikuwa ni changa la macho tu kama wamepiga kura ya ndio
 
ccm ni chama cha zamani.....kinajua nini kifanye kichukue audience yote.
makelele ya epa wakati wa bajeti yalituchanganya watanzania. tukajua kweli ccm safari hii kumekucha.
hata kura zinatoka.......hakuna kura ya NO wala ya abstain iliyotoka upande wa chama tawala. kazi kweli kweli
 
Mkuu nyangumi,
Swali ni tofauti kati ya kuabstain (walikofanya wapinzani) na kupiga kura ya hapana. Otherwise ninaelewa namna siasa inavyochezwa so sitegemei jibu la kiufundi zaidi ya jibu la kisiasa.

We hang the petty thieves and appoint the great ones to public offices hiyo ndio faida tunayoivuna sasa ,tungojeeni miaka mitano ijayo.
 
EPA yatikisa Bunge

2008-06-21 10:05:07
Na Boniface Luhanga, Dodoma


Wabunge wa CCM wameaswa kutogawanyika kuhusu suala la mafisadi waliochota fedha za Benki Kuu Tanzania (BoT) kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo, bungeni jana, Bi. Anna Abdallah (Viti Maalum-CCM) alisema hakuna mbunge anayeogopa kuzungumzia suala la ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (EPA) na kwamba halipaswi kuwagawa wabunge.

Bi. Abdallah alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu Bi. Anna Kilango Malecela (CCM-Same Mashariki) atoe wito kwa wabunge wenzake kutoogopa vitisho katika kuzungumzia suala hilo ili mradi wanasimamia ukweli na haki.

Bi. Abdallah alisema kimsingi hakuna mbunge anayeogopa kulizungumzia hilo isipokuwa wanatofautiana katika kulisema.

``Baadhi wanalisema kwa madoido huku wengine tukilisema kwa upole lakini wote hatuogopi wala kutishwa ndani ya Bunge,`` alisema.

Hata hivyo, alisema vyombo vya habari, hususan magazeti, kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakichangia kuwa ndani ya Bunge kuna mtafaruku kuhusiana na sakata la EPA.

Alisema wabunge wote wana lengo moja la kuhakikisha kwamba, wanakemea vitendo viovu vinavyofanyika ndani ya jamii.

Aidha, mbunge huyo pia aliishauri serikali kuvitumia vikosi vya ujenzi vya majeshi ya JKT, JWTZ, Polisi na Magereza katika kujenga nyumba za taasisi hizo badala ya kuwatumia wazabuni kwa lengo la kubana matumizi.

Bi. Abdallah alisema haoni mantiki kwa serikali kutumia wazabuni kujenga nyumba za taasisi hizo huku kukiwepo na vikosi vya shughuli hiyo ndani yake.

Kuhusu suala la Tanzania kukemea vitendo vinavyoendelea nchini Zimbabwe, Mbunge huyo alisema Tanzania imechelewa kutoa tamko hilo.

Bi. Abdalla alisema si busara kuendekeza mambo yanayoendelea kutokea nchini Zimbabwe kwa sasa hasa kwa kuzingatia kwamba, Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

``Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe) anapaswa kuambiwa (ukweli) pale anapofanya tofauti,`` alisema.

Juioni jana wakati akifanya majumuisho, Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo, alisema kwamba Serikali inasubiri ripoti ya Timu iliyoundwa na Rais ndipo inaweza kuwa katika nafasi ya kulizingumzia suala hilo pamoja na hatua za kuchukua.

Aidha alisema pesa hizo za EPA si za BoT wala serikali bali wafanyabiashara ambao wengi wako nje ya nchi ama walikufa.

Bajeti ilipitishwa jana na wabunge wengi wa CCM na kwa upinzani aliyeipitisha ni John Momose Cheyo. Bajeti ambayo hupitishwa kwa wabunge kusema `Ndiyo`ama `Hapana` wabunge wengi wa upinzani walisema `abstantion` wakimaanisha hawakubali wala hawakatai.

Wakati huo huo, Simon Mhina anaripoti kwamba Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, amekanusha uvumi kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho iliyokutana mjini Dodoma hivi karibuni ilizima kujadiliwa kwa hoja za EPA pamoja na sakata la Richmond.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Bw. Makamba, alisema ni kweli hoja za kuwashughulikia mafisadi zilizuka ndani ya kikao hicho, lakini yalitolewa maelezo ya kina yaliyohusu umuhimu wa kutolijadili, lakini kamwe halikuzimwa.

Akifafanua, alisema si kweli kwamba CCM inawaogopa watu wanaoitwa mafisadi, lakini ni vema vyombo husika vyenye madaraka kwa mujibu wa nchi vikaachiwa kushughulikia tatizo la mafisadi.

Alisema kitu ambacho CCM inaweza kukifanya ni kuwashauri wale wanaotuhumiwa waachie madaraka ili kukisafisha chama na serikali yake, jambo ambalo limekuwa likifanyika.

Bw. Makamba, alisema CCM ni chama cha siasa na sio dola, japokuwa ndicho kimeunda serikali.

``Hatutaki kuingilia kazi ya serikali, tuhuma za ufisadi iwe EPA, Richmond au sijui vijisenti, zote hizo zinashughulikiwa na vyombo vya dola. Hii siyo kazi ya Halmashauri Kuu, hii sio siasa,`` alisema.

Alisema kama watuhumiwa wangekuwa wameshtakiwa kwenye vikao vya chama, hapo CCM ingewajibika kuchunguza, lakini kwa vile tuhuma hizo zimeanzia nje na zingine bungeni ni busara sheria ikachukua mkondo wake.

``Wengine walisema mafisadi wafukuzwe ndani ya chama. Jamani hawa ni watuhumiwa, tuwafukuze halafu tukifika kwa wananchi waliowachagua tukawaambie tumewafukuza viongozi wao kwa sababu zipi?`` Alihoji.

Bw. Makamba, alikiri kwamba katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana hivi karibuni, baadhi ya wajumbe walitaka chama kikemee wakubwa wa serikali ambao baada ya kujiuzulu kufuatia tuhuma za ufisadi, wafikapo kwenye majimbo yao wanalakiwa kwa nderemo na wapiga kura wao.

Katibu huyo alisema wajumbe hao walikuwa hawajaelewa dhana nzima ya kujiuzulu, kwamba ni \'kuwajibika` lakini kamwe sio kukiri kosa.

``Kujiuzulu ni moja ya sifa za ustaarabu na uadilifu, sasa hawa waliojiuzulu, kisha wapiga kura wao wakawapokea, bila shaka wamewapokea kwa sababu ya ustaarabu waliouonyesha,`` alisema na kuongeza ``Hawa bado ni wabunge, na wengine ni wajumbe wa Halmashauri Kuu, hatuwezi kuwanyima haki zao za kisiasa na kikatiba eti tu kwa sababu wametuhumiwa.``

Kuhusu madai yaliyotolewa kwamba katika kikao hicho, wajumbe walisema kwamba wanataka CCM kama ile aliyokuwa anaongoza Mwalimu Nyerere irejee, Bw. Makamba, alisema Mwenyekiti Jakaya Kikwete ameshairejesha.

Alisema sifa moja ya CCM ya Nyerere ilikuwa kukaa pamoja na kujadili matatizo ya kila mtu, kukosoa na kisha watu wote wanatoka kwa umoja.

``Ndicho kilichotokea juzi, kila mjumbe alitoa dukuduku lake, mwenye kulaani ufisadi alifanya hivyo, mwenye kumlaumu Makamba alifanya hivyo na baadaye tukafikia majumuisho kisha tukakubaliana. Hii ndo CCM ya Nyerere ambayo tuliapa kuwa tutasema kweli daima, fitina kwetu ni mwiko,`` alisema.


Bw. Makamba, alisema kama kuna mjumbe aliyeacha kutoa hoja yake kwenye kikao hicho na kulalamika kwenye vyombo vya habari, amekiuka kiapo cha CCM.
  • SOURCE: Nipashe

Kwenye higlight especially nyekundu...Utangundua usanii si tu wa ki zecomedy...Bali wa kimafia!
Kama ni kweli vyombo vya dola vimepewa majukumu...Then ni kwanini Mwema hakamati watu?
Uwajibikaji gani huo Kikwete na Makamba wanaousema kwa niaba ya ccm?
Kujiuzulu ni kuwajibika bila kuwa na makosa...Je wenye makosa wamekamatwa?
 
Kuunda tume nyingine ya EPA wakati polisi walitakiwa wakamate watuhumiwa mara baada ya ripoti za ukaguzi wa mahesabu si siasa hizo?
Kusema hawa watu ni safi na huku wamejiuzulu kwa kshfa za ufisadi kuna manufaa gani kwa wazalendo?
Ama Makamba na Kikwete ni vichaa?
 
Nilposema ccm bye bye kuna watu hawaamini hivyo na wanadhani kuna atakayekuwa na uwezo wa kupambana na Mkapa na kina Chenge huko kwenye chama kabla hata hawajahojiwa!
Ni vigumu kufanya hivyo kwani EPA NI UJAMBAZI WA ccm.
 
CCM na ufisadi ndoa yao itadumu milele!

ban.nundu.jpg
Deus Bugaywa

NI wazi sasa kwamba kile kinachosemwa kuhusu CCM na hatima yake kutokuwa ya kutia matumaini si tena habari za mitaani, ni suala ambalo liko wazi na dhahiri hata kaka wenye chama chao hawataki kuuikiri ukweli huo.
Na zaidi sana kutokiri kwao kwamba mambo si shwari ndani ya chama chao ni moja ya dalili za wazi kwamba huu ni mwanzo wa mwisho wa chama hicho kikongwe katika historia ya siasa ya nchi hii na bara la Afrika.
Ukiangalia kwa makini taarifa zilizotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari tangu kuanza kwa kikao kinachoendelea cha Bunge na fununu kwamba kwamba lipo kundi la wanachama wakongwe wa chama hicho waliokuwa na mkakati wa kushawishi wabunge wa chama hicho wawasafishe watuhumiwa wa Richmond.
Pia kuibuka kwa tuhuma za ushirikina bungeni na yaliyojiri kwenye kikao cha NEC ya CCM na wabunge wake, na habari zilizoandikwa kama matokeo ya kikao hicho, haihitaji kuwa Thomaso kujua kwamba uko mkono unaoiandikia CCM ukutani kwamba ‘Mene mene tekeli na peres’ yaani ufalme wake sasa umekwisha.
Baada ya kikao cha NEC na wabunge kila aliyekuwa na shaka na ukali wa wabunge wa CCM wakati wa kujadili ripoti ya kamati ya Mwakyembe sasa amethibitihsa hofu yake hiyo, kwamba hizo zilikuwa ni mbio za sakafuni ambazo mkiambiaji wake hata awe na kasi kama ya mwanga, jeuri yake inaishia ukingoni - haifiki mbali.
Msomaji mmoja wa safu hii aliwahi kuniandikia wakati wa vurugu hilo lililosababisha waziri mkuu wa wakati huo kujiuzulu kwamba ‘ndugu mwandishi hiki kinachosemwa na wabunge wa CCM sasa ni ngoma ya watoto haikeshi, ufisadi siku hizi ndiyo mhimili wa CCM, kujidai wanaupiaga vita ni kama wanajipiga vita wenyewe, wataweza?’ Wakati huo nilimwambia kila kitu lazima kiwe na mwanzo na mapinduzi yanapoanza huwa kuna mstari mwembamba sana katikati ya hali ya zamani iliyozoeleka na hali mpya ya kimapinduzi inayoanza kuzaliwa, kiasi kwamba unaweza usione tofauti, kwa hiyo huo huenda ukawa mwanzo wa CCM kujivua gamba lake.
Kokote aliko msomaji huyu najua wala hakushangaa kusikia matokeo ya kikao cha chama kinaamua kurejea kwenye jadi yake na kuwatakasa watuhumiwa wa ufisadi, kwamba kuitengeanisha CCM na ufisadi unaoendelea nchini ni kazi kubwa.
Tunaambiwa hata wale ambao tuhuma zao wala hazihitaji kuwa mhitimu wa kilichokuwa chuo cha kijasusi cha Patrice Lumumbe huko Urusi, kujua kwamba kulikuwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kukiuka maadili ya kawaida kabisa uongozi.
Na hapo ndiyo ule mwisho unapokaribia, kwamba kikao hicho kama vilvyokuwa vilivyotangulia vilivyokuwa na lengo la kuleta mshikamano katika chama, kimesaidia kuongeza uadui miongoni mwa wanachama wake wakongwe na viongozi waandamizi kiasi kwamba nyufa zilizopo sasa sina shaka hata mweyekiti wake, Rais Kikwete, anaweza kuzuia zisiendelee kukua na kupanuka achilia mbali kuziziba kabisa.
Inapofika mahali chama kikongwe chenye viongozi wazoefu, kama viongozi wake wa ngazi ya mwenyekiti wa kamati ya maadili ya chama ya taifa, anamwambia Spika wa Bunge lenye wabunge wengi wa CCM na Spika huyo anatoka CCM, kwamba ni mzushi anaongoza Bunge kizushi, ujue anguko kuu haliko mbali.
Na hizi tunazoziona hadi huku nje ni ishara chache tu kwamba sasa hivi kuna CCM mbili, bila kujali wennyewe wanafunika kombe vipi, hata kama watasingizia kwamba ndio kukomaa kwa demokrasia, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba mambo ndani ya chama hicho yanakwenda msege mnege.
Kama tulivyojuzwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba pamoja na mvutano uliotokea ndani ya kikao hicho cha NEC na wabunge juu ya nini chama kifanye kwa watuhumiwa wa ufisadi, na mwenyekiti kuishia tu kutoa kauli laini ambazo kila kundi linaitafsiri kwamba ilikuwa ni kijembe kwa upande mwingine, si ishara nzuri ya kiuongozi, hii inatoa mwanya kwa watu kuanza kuamini kwamba hata mwenyekityi wake sasa kuna watu au kundi analoliogopa ndani ya chama.
Hakuna ubishi kwamba kusafishwa au (kujisafisha?) kwa watuhumiwa wa kashfa za Richmond na EPA ndani ya CCM, si suala ambalo limekuja kibahati bahati, huo ni makakati ambao umeandaliwa na wahusika siku nyingi, kwa ujuzi mkubwa na gharama kubwa.
Kwa hiyo, ndiyo kusema kwamba CCM mengine ya chama hicho sasa hayategemei sana itikadi yake na mfumo wake wa kutendaji au kimaadili, isipokuwa ujanja wa baadhi ya wanachama wake wanaoweza kufanya ‘maarifa’ na kuwafanya wajumbe wawaunge mkono katika kile wanachokitetea hata kama kinasigana na maadili na miongozo ya chama hicho.
Wanaoshinda kwa ‘mbinu’ na maarifa yao katika hoja moja wanatoa mwanya kwa kundi lililoshindwa nalo kujiandaa na kupanga mikakati ya kuja kuwapiku wengine, ilimradi ni mashindano ya madaraka na kunyemelea nani atakuwa mpangaji anayefuata wa mambo pale Magogoni.
Kwa kufanya hivi viongozi wa chama hiki wamewasahau wananchi, wako bize wanapigana vikumbo vya kuwania ukubwa, katika vikao vyao vingi vya hivi karibuni kwenye kila hoja nyeti, mwananchi na mwanachama hana nafasi ukisikia ametajwa ni katika hali ya kujihami kwamba ‘wananchi wameamka’ kwa hiyo mwaka 2010 chama kinaweza kuwa na kazi kubwa kushinda.
Kusahauliwa huku kwa wananchi ndiko kunakopaswa kutumiwe na Watanzania kuona na kukijua hasa chama hiki kinachoitwa cha mapinduzi, kina sura gani na viongozi wake wana mweleko na malengo gani na watu wa taifa hili.
Kwa kuamua kuwakumbatia mafisadi, CCM inatuma salamu kwa wananchi kwamba chenyewe kinaangalia watu wake kwanza, ikumbukwe CCM ina wenyewe na wenyewe ni wao, na chama hakiko tayari kuwaona ‘wanapata tabu’ hata kama wanatuhumiwa na nini.
Ni jukumu la wananchi kuamua kusuka au kunyoa - chama ndiyo hivyo kimeamua kufunga pingu za maisha na ufisadi, kwa kwamba yaliyounganishwa na NEC, wananchi kwa maana ya Bunge lao lisiyatengue.
Mbele ya CCM hata Bunge si lolote si chochote, kwamba hata kama Bunge limejiridhisha kwamba kweli hawa ni watuhumiwa, lakini kwa kuwa wanachokifanya ni kile kinachoitikadiwa na chama chao, acha Bunge lisema na ‘lizushe linavyoweza kuzusha’, lakini ndoa ya CCM na watu wake hata kama ni watuhumiwa hawana ruksa kuivunja.
Chama (kipande kimoja cha chama) ndiyo hicho kimeamua kuchukua ufisadi, je, kundi la wakereketwa linalodhani mwenendo wa mambo ndani ya chama hicho si wenyewe litakwenda njia ipi? Ni suala la kusubiri na kuona.
Lakini kitu kimoja ni dhahiri kwamba kwa kila kitendo na kila neno wanalosema CCM linashabikia mtu ambaye machoni pa umma anaonekana hana sifa hata za kuwa balozi wa nyumba kumi, kwa kukosa nidhamu na uadilifu wa kiuongozi, ni hatua moja ya taratibu lakini yenye nguvu na ya uhakika kuelekea kwenye kaburi lake.
Mungu ibariki Tanzania!
drbugaywa@yahoo.com
0734 449 421
 
Back
Top Bottom