Bajeti ya mshahara wa sh. 400,000

Nimependa hii
Safi
 
Hiyo 40000 ya sadaka ungetoa hapo, watu wanaotakiwa kutoa sadaka ni wale wenye surplus kwenye vipato vyao.
1. Eneo la sadaka ni kwa kadri unavyoamini na ufahamu ulionao

2. Kuliko kuitoa huku unanungunika ni bora usitoe kabisa

3. Usipoweza kutoa na kumshukuru Mungu kwa kuwapa wahitaji or in any way katika kidogo ulichonacho sasa ivi hautaweza kutoa hata ukilipwa 10m

4. Hiyo hapo juu ni bajeti pendekezi, unaweza kupanga vyovyote vile upendavyo, ila usiache kusevu

5. Naamini katika sadaka.
Huwa natafakari ambavyo Mungu ananipa neema, mwaka mzima sikanyagi hospital, ni lazima nitenge hela kwa chochote nilichonacho kama shukrani kumsaidia aliyeshindwa kumudu gharama za matibabu na penginepo

Na hata Mungu asipofanya yale niliyotarajia, bado nitatenga sadaka

6. Hatutoi katika surplus
Kama ni mkristo soma Luka 21:1 -4
v.4 maana hao wote walitia sadakani mali iliyowazidi...
Neno sadaka kwa kiswahili ni moja lkn kwa kingereza yapo maneno mengi, offering, sacrifice, gift etc

So It involve sacrifice sometimes
 
Hapo kwenye sadaka umenikosha

Lakini nimepata kitu kwenye kipengele cha nyumba isizidi 20% ya kipato chako
 
Mmmh kumbe nachezea hela

Kitu sijui ni kujinyima labda niwe sina hela

Nifundisheni ubahili please
1. Badilisha routine yako
2. Weka malengo tena ya mbali
3. Waza siku ukipoteza hiyo kazi una pa kuanzia?
4. Tafakari, Kama hausevu saivi je utaweza ukishapata familia? (In case kama haujapata)
Utaweza kulipa ada za watoto bila kukopa?
 
Mmmh kumbe nachezea hela

Kitu sijui ni kujinyima labda niwe sina hela

Nifundisheni ubahili please
ukitaka kua bahiri itatakiwa kuwa na malengo sawa na umri wako nyuma 2 times ya ulipo

Kinyume na hapo utafeli
Hua nakua na hela hadi 5m akiba
Ila sikuwahi kuzitumia hata iwaje

Sijui ni kipaji au ndivyo nilivyo sielewi
Budget yangu ni 5000 per day
Kuna wakati nnapata 50k naziweka nazitama tu
Sina ile kiwehuwehu na hela.
 
You are financially matured
 
Hebu niazime laki hii weekend imepwaya na vile huna haraka nayo June uipate
 
Hizi hesabu zako labda kama unaishi Malinyi Ulanga 😂..ila kwa Dar thats a serious joke.

Hio location utakayochota laki 4 kuifikia na kurudi kwako kila siku sio chini ya TZS3,000 na hapo unajibana bana haswaa. Ukipiga hesabu thats 90K a month pamoja na dharura za siku usafiri ukiwa mgumu, ukiondoa na jumapili zako maana lazma utapigishwa mzigo hadi jumamosi.

Kuhusu kula kama bachelor hutakuwa unapika siku zote isipokuwa ile jumamosi ambayo unawahi kutoka kazini na njia nyeupe hukai foleni mda mrefu, gari sio za kugombania. Chakula standard 2000 ukila mchana na jioni tu pamoja na chai hio ni roughly 150K ukihesabia siku ambazo hupiki maana yake haitapungua zaidi ya 130K.

Utataka uishi nyumba standard yenye chumba self na sebule. The easiest you can afford ni 150,000 kwa location za kiande. Hapo ondoa wilaya ya Kinondoni kabisa kwenye akili yako.


Mpaka kufikia hapo laki 3 na 70 hunayo mkononi. Bado hujapigwa mzinga na ndugu jamaa na marafiki, hujaweka bundle kwenye simu yako. Hapo una 30K tu ya kufanya hayo yote. Mkiona watoto wakike wanapigwa pumbu pamoja na mishahara yao ya laki 4 msishangae sana.
 
Yan ulipwe 400k bado uongeze neno standard kwenye nyumba na self

Hichi kipindi unatafuta pa kujisitiri tu wakati unafocus malengo ya mbele zaidi, ambayo kama kila kitu kimeenda sawa, na ukafanikiwa kwenye ujasiriamali utaadjust accordingly

Kwa ajili ya kujifunza, mshahara ukianzia sh ngapi hapa bongo ndo mtu ataweza kuanza kusevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…