Bajeti ya mshahara wa sh. 400,000

Kuna mwenzako ameanzisha uzi kuwa waajiriwa wana maisha mazuri kuliko wafanyabiashara.
Sasa wewe muajiriwa kwa mwezi pesa ya kula unatumia elfu 80 sasa hapa c utakuwa unakula mataka taka?
 
Kwa hiyo pesa bado unapiga hesabu za sadaka tena? yaani hapo hata kula yako itakuwa ni ya kuunga unga tu. Ni vyema kwa hiyo pesa usipie hizo hesabu za kuinvest kwanza, kwani utaishi kwa taabu sana. Hizo hesabu utazianza ukishakuwa stable kwenye kipato chako. Yaani hata wazazi hutokuwa unawatumia hata 50K kwa mwezi, na bado umetenga 40K ya sadaka?. Huna hata bwana wadogo watakupiga hata mizinga ya vocha tu?
 
Bajetiii ni kwamba unaish singo mkuu. Subiri uwe na spouce au spouces na watoto au na tegemezi wengine.
 
Sasa kwa mfano dar Nyumba ya Familia hupati bila kuwa na 500k au zaidi..
Lets say Kipato changu ni 2.6M..
20% ni 500k..
Na ni nyumba ya kawaida sana..
Hiyo maybe kama unazungumzia mtu bachelor na sio mwenye Familia kweli inafanya kazi
Goba unapata nyumba kubwa na nzuri kwa hiyo pesa
 
Lete mapendekezo mkuu wote tuna jifunza hapa

Imagine unalipwa 400k for 5 yrs
Kumbuka Baada ya muda, may be ndani ya 3yrs utapata familia
Utasubiri mpaka lini

Trust me, kusave ktk kipato kidogo ni maamuzi magumu sana mwanzoni, lkn utaenjoy baadaye

Sadaka, ni kulingana na unavoamini
Ninaamini ipo baraka katika kusaidia wengine wenye mahitaji hata ukiwa na kipato kidogo

Hata wazazi unaweza kuwapa sadaka, ni shukrani yako kwa Mungu
 
Kuna mwenzako ameanzisha uzi kuwa waajiriwa wana maisha mazuri kuliko wafanyabiashara.
Sasa wewe muajiriwa kwa mwezi pesa ya kula unatumia elfu 80 sasa hapa c utakuwa unakula mataka taka?
Waajiriwa wapo madaraja tofauti
Kuna wanaoanza na mshahara 1.2m huyu hatateseka sana kama wa 400k

Kuna wanaolipwa 6m, 10m+

Kwa hiyo inategemea, alikuwa anaongelea wa ngazi ipi
 
Mkuu naomba maelezo kidogo hapa kwenye utt amis vipi ni segment gani ni nzuri zaidi kuchagua unapoweka?

Vipi wakati unatoa pesa yako hakunaga mashaerti mengi mengi kama kufatilia nccf?
Pitia website yao kupata uelewa mpana
Au nenda kwenye ofisi zao kama upo dar, mwanza arusha

Kwa uwekezaji wa chini
Tumia mfuko wa ukwasi/liquid

Kutoa ni anytime kupitia mawakala wao nchi nzima ambao ni benki ya crdb

Mzigo unatua kwenye akaunti yako ndani ya siku 3 tangu ulipojaza fomu ya kutoa
 
Labda ukapange nje ya mji kama vikindu huko lakini mjini kama Magomeni,Sinza,Ilala n.k hapo hutoboi
Mwenge mataa hapo opposite na efatha unapata chumba cha 50k, mabibo pale unapata kwa chumba 60k, kigogo

Unless kama unataka yenye uzio, madirisha aluminium, chini tiles, gypsum, mlango grill
Utakwama
 
Waajiriwa wapo madaraja tofauti
Kuna wanaoanza na mshahara 1.2m huyu hatateseka sana kama wa 400k

Kuna wanaolipwa 6m, 10m+

Kwa hiyo inategemea, alikuwa anaongelea wa ngazi ipi
Hao wanaolipwa hizo pesa ni wachache sana tofauti na hawa wa madaraja ya chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…