Bajeti ya mshahara wa sh. 400,000

Bajeti ya mshahara wa sh. 400,000

Ukiwa unalipwa 400k na huna familia, yan home alone
Mchanganuo pendekezi huu hapa
Utanishukuru baadae

100,000 Akiba (weka utt)
40,000 Sadaka
80,000 Kodi ya nyumba
80,000 chakula
50,000 usafiri
50,000 mahitaji mengine

Sadaka,
unamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa wahitaji au popote unapoamini

Kodi
Haipaswi kuzidi 20% ya kipato chako

Chakula
Haipaswi kuzidi 20%
Hemea kwa jumla
Weka stock ya vyakula kama dagaa, hulali njaa

Usafiri
Panga karibu na eneo la kazi
Au sehemu ya gari moja

Akiba weka utt
Ukifikisha hata 600,000, weka mpunga stock, ni gunia kumi hizi

Lazima uwe bahili hasa, nidhamu sana

Ongezea kama kuna kitu nimeacha
Au tupe uzoefu zaidi tujifunze
Fungua duka genge..hapo unapoishi..ukitoka kazini..unakaa hapo...kuendelea kupiga hela....
 
Ukiwa unalipwa 400k na huna familia, yan home alone
Mchanganuo pendekezi huu hapa
Utanishukuru baadae

100,000 Akiba (weka utt)
40,000 Sadaka
80,000 Kodi ya nyumba
80,000 chakula
50,000 usafiri
50,000 mahitaji mengine

Sadaka,
unamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa wahitaji au popote unapoamini

Kodi
Haipaswi kuzidi 20% ya kipato chako

Chakula
Haipaswi kuzidi 20%
Hemea kwa jumla
Weka stock ya vyakula kama dagaa, hulali njaa

Usafiri
Panga karibu na eneo la kazi
Au sehemu ya gari moja

Akiba weka utt
Ukifikisha hata 600,000, weka mpunga stock, ni gunia kumi hizi

Lazima uwe bahili hasa, nidhamu sana

Ongezea kama kuna kitu nimeacha
Au tupe uzoefu zaidi tujifunze
Nimeanza kazi juzi tu na nalipwa hyo hyo..nahs mungu alikutumia unifundishe jambo..shukrani
 
80000 mwez mzima unakula nn mkuu embu tueleze
Unga 5kg
Mchele 10kg
Mafuta 3 ltrs

Kinachobaki unabalansishia kwenye mboga: matembele, msusa, dagaa, biringanya, ngogwe
Nyama/samaki mara moja kwa mwezi, kama bajeti itaruhusu

Hemea maduka ya jumla kama vile pale Kawe, kwa muyama one (kwa wale wa Dar, ikiwa ni karibu kwako)

Na hakikisha unapika nyumbani, sio kula mgahawa
Kama itakulazimu kula mgahawani, tafuta chimbo cheap

Kumbuka hii ni sacrifice ya muda tu

Ukishaanza kuinvest akiba kidogo unayojiwekea, mwaka wa pili na kuendelea hali itakuwa na ahueni kiasi
 
huvai
huna ndugu/jamaa
huumwi

80k unakula nini?

Pendekeza mkuu
Kwenye 400k
Ndugu unashauri tuwape sh ngapi
Na kuvaa tuweke bajeti kiasi gani

Tupunguze item gani

Ukiwa kwenye hichi kipindi, unahitaji nguo chache nadhifu ambazo utavaa jwa kipindi kirefu

Hela unayoweka akiba inagawanyika mara mbili
50% Emergency
50% Investment

Kama huna bima, ugonjwa ni dharura
 
Back
Top Bottom