wimbi la mbele
JF-Expert Member
- Jan 4, 2011
- 647
- 266
hivi sasa hivi standard bajet ya harusi ambayo si kubwa na modest ni kiasi gani?
naomba mchakato tafadhali
naomba mchakato tafadhali
hivi sasa hivi standard bajet ya harusi ambayo si kubwa na modest ni kiasi gani?
naomba mchakato tafadhali
Kanisani inafungwa BURE !! [/SIZE][/B].
naombea nikipata wangu basi tusiwaingieze au nisimuingize gharama,tutafunga kanisani tutarudi nyumbani na kulala baaasi
Kwani baada ya harusi, kazi ni kulala baaasi???:confused2:
naombea nikipata wangu basi tusiwaingieze au nisimuingize gharama,tutafunga kanisani tutarudi nyumbani na kulala baaasi
Ndugu ya Harusi ni nzuri sana ..na pia najua uko excited sana... Lakini kama atatokea mtu na kuniambia nirudie tena harusi yangu..nitafanya kila njia niepuke gharama na pia nikubali lawama, kashfa na kila kitu kwa manufaa ya baadaye ya familia yangu.
Unless otherwise, uchumi wako uko imara sana, au umezungukwa na mtandao wa mafisadi ambao wako tayari choma moto hela ambazo hawana uchungu nazo ..Please go with my advice..hebu fikiri ..miaka kumi ijayo unaweza kuwa na familia, watoto watataenda shule n.k. Kwa nini hizo hela usizifanyie namna..
Ningekushauri kuwa fanya harusi ya bei ya chee sana kama symbolic, utamaduni au kuwa karibu na familia & marafiki.. na sio lazima uamishe ukoo mzima toka kule kwenu..kwa watani zangu.....yaani..kikubwa ni ukumbi wa bei rahisi, kama unayo plot ushwahilini weka tent ...vyakula vya kawaida na madoido ya kawaida....yaani kwa fanya harusi ya kichovu kwa lugha nyingine... kwangu mimi maximum ningeweka less than 5 million..au chini ya hapo kutegemea wigo wa watu wanaokuzunguka.. lakini kumbuka si lazima kumwalika kila mtu..
Najua kuwa watu watachonga sana eti ..lazima nichangiwe..kama mimi niliwachangia watu..si lazima wao wanichangie.. nitawapa mwaliko at vey short notice kama symbolic ili wanichangie kidogo..sina haja ya kuwaumiza na ugumu huu wa maisha..kikubwa waje kwanye hivyo vikao visivyozidi 4..sitampa ndugu yangu yeyote au rafiki haiki na jukumu la kuburuta vikao viwe virefu ili watu wanywe sana na wachangie sana uchakavu..vikao vifupi na maana yake ni just kuwa pamoja kimawazo, symbolic na kuonyesha nawajali ndugu na jamaa.. muda uliobaki waendelee na shughuli zaooo na walee familia zao..
Anyway.. in short napinga sana matumizi makubwa ya harusi kwa watanzania wasio mafisadi kwa kisingizio eti,,jamii haitanielewa ..wakati jamii yenyewe yetu Watanzania , ndugu, jamaa ni wachovu na masikini kama walivyo asilimia kubwa ya watanzania..kumbuka wewe Bwana Harusi na wife wako mtarajia ndio waamuzi..na ndio mtakao face reality baadaye...hata yeye aepuke hizo Vikitchen party vya gharama,...Najua watu wanaweza piga lakini ..wakitaka sherehe wasitumie kizingizio cha harusi yenu...kumbuka nyinyi maharusi mnaweza amua kufunga harusi basi kama wanataka sherehe wafanye bila wewe..
Anyway, Najua hapa kuna wana JF watao argue..lakini kumbuka hayo ni mawazo yangu..labda kwa sababu mimi ni zumbukuku..
naombea nikipata wangu basi tusiwaingieze au nisimuingize gharama,tutafunga kanisani tutarudi nyumbani na kulala baaasi
sasa je,kutafuta watoto kama sio kulala utawapataje...?:becky::becky:
Wewe yako umefanya bure maana usiongee tu kuongeza mudaKanisani inafungwa BURE !!
Gharama zingine unajitakia mwenyewe.
Ukumbi 500,000/=
chakula na keki na champagne 2,000,000/=
vinywaji 2,000,000/=
mc & music 400'000/=
video camera & steel picture 400'000/=
Transpot 300,000/=
Total 5,600,000/=
Harusi ikizidi pesa hiyo basi wakati wewe unakwenda honey moon na mwenyekiti wa kamati ya harusi ujuwe anakwenda showroom kununuwa gari lake kutokana na michango ya harusi yako. kila kila kitu hapo wanakidoubble price.
N:b, Hiyo ni bajeti ya harusi ya wageni 400.
Anaebisha hilo basi na yeye ni mmoja wa wanufaika wa wizi wa michango ya Harusi, vitu sio vigumu kivile ila watu wanaweka maslahi sana.