Acha mzaha wewe, unataka kusema kwa mfano marekani wakitaka kufanya any serious undertaking kama vile kujenga Hospitali ya umma au kwenda vitani wanatembeza bakuli kwa wanamuziki? Na kodi wanazolipa raia je zitaafana kazi gani?
Ukweli ni kwamba ni serikali ya Tanzania tu inayohamasisha watu wachangie kila kitu, kuanzia madawati mpaka ujenzi wa madarasa na shule wakati kodiza wananchi zinatumbuliwa na kuvimbisha matumbo ya watu wasio hata na shukurani. Tulijitolea kwa hali na mali enzi zile za Mwalimu kujenga kwa kuchangia nguvukazi kwa sababu hata ungewatazama machoni viongozi wa wakati ule unapata ujumbe wa wao kuwa "Serious", Je, leo ni kiongozi yupi unaweza kumidentify ndani ya CCM ati ana uchungu na fedha ya walipa kodi? Hapa ndipo ninapowaunga mkono CHADEMA katika hoja kwamba ni jukumu la serikali kupanga na kutumia kodi kwa ajili ya maendeleo yetu na si kuhamasishwa kujitolea kisha fedha iliyokusudiwa kwa kazi husika kuvimbisha matumbo yasiyoshiba ya hawa jamaa wavaa magwanda ya kijani.