Bajeti sasa yamtegemea Lady Jay Dee

Huo ndio ubunifu na si kungoja bajet ya serikali tu. Jee, wewe unaifanyia nini nchi yako? Badala ya kungoja kufanyiwa wewe!

Eti wanalaumu. Nna hakika hii ni njia nzuri tu na ni sera ya ccm ya kuhusisha wananchi na serikali katika kutimiza malengo haraka.

Nyie msiyependa kufanya na mkae mngoje kufanyiwa.

Bila shaka utakuwa na matatizo makubwa sana ya uelewa.

wananchi wamejichangisha sana tangu 1985 lakini serikali haijawekeza chochote kuhakikisha hospitali hiyo inakamilika.

kanisa katoliki waliomba wakabidhiwe majengo yale wayakamilishe na hospitali iweze kuhudumia wananchi lakini serikali ikakataa kwamba iko tayari kuikamilisha, sasa kuikamilisha kwenyewe ndio kutegemea lady jd awajazie bakuli wakati wanatoa misamaha ya mabilioni.

kweli ukiwa ccm ama mshabiki wa ccm akili yako inakuwa imbalanced.

Nakushangaa wewe uliye balanced unashindwa kuelewa kuwa hata hilo kanisa linangoja michango ya bakuli na ruzuku za serikali. Unanchekesha!

Duhh kweli ukiona mtiririko wa haya majibu unaweza ukajikuta unashangaa lakini sababu ni weekend inabidi tutoe benefit of doubt

Nadhani Faiza hapa issue ni kwamba serikali isingebisha na kusema kwamba inao mpango wa kukamilisha hospitali, huenda hii hospitali ingeshakamilika; lakini walisema kwamba wako tayari kukamilisha...

Therefore inashangaza kuona kwamba mbinu yao ya kukamilisha hili jengo ni Fund Raising..., ambayo haina guarantee ya kupata fedha za kutosha hence ubishi wao na uvivu wao wa ku-take action umepelekea delay
 
Acheni ushamba jamani, mbona hata nchi zilizoendeleazinatumia wakija Lady jay dee wao kuchangisha hela? sasa kinachowafanya mshangae ni nini?
 
Makisio ,takwimu na data hakuna? Hivi hiki si kikao cha bajeti inakuwaje hakuna figures. Au mleta mada kuna vitu umeruka?

  • Ni shilingi ngapi zinatakiwa?

  • Ni shilingi ngapi zinatapatika wakimshirikisha jay dee?

Nilitarjia kwa waziri mjibu swali au mbunge muuliza swali wajifunze kutoa data na takwimu sio majibu na maswali yapo yapo tu.
 
Acheni ushamba jamani, mbona hata nchi zilizoendeleazinatumia wakija Lady jay dee wao kuchangisha hela? sasa kinachowafanya mshangae ni nini?

Mkuu kwahiyo imechukua serikali miaka takriban zaidi ya 15 kupata wazo la kuchangisha pesa kwa kutumia wanamuziki??, na hapa ni baada ya kukataa msaada wa kanisa...

Hivi kweli wewe hushangai hapo?
 
ni aibu. halafu waziri kama huyo akitoka bungeni anaingia kwenye li-vx la V-8 full kiyoyozi kwenda 'kulitumikia' taifa! ni aibu bado yupo kazini. kwa majibu hayo alistahili kujiuzulu on the spot. hii inafanya uwachukie watumishi wote wa serikalini uwaonao kwenye hivi VX manake wanakuwa tu kodi zetu na hawana walifanyalo!
 
Nakumbuka hiyo hospitali ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi wa mkoa wa Mara tena kwa lazima mnamo mwaka 1985.

Watenadji wa serikali za vijiji chini ya usimamizi wa wakuu wa wilaya walikuwa wanapita nyumba hadi nyumba, mtu mmoja hadi mwingine ili kuhakikisha kwamba hospitali inajengwa.

Wananchi wengi sana walihamasika wakajitolea mali zao hususan ng'ombe, mbuzi, kondoo na vyakula kwa ajili ya kukamilkisha kazi hiyo. Nakumbuka hata wale waliokuwa na uwezo mdogo walikamuliwa kwa nguvu, wasiojitolea walikamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa vitu vyao mbalimbali alimuradi tu hospitali ijengwe. Ni mwaka 1985 mimi nikiwa kijana mdogo sana wa darasa la pili hadi hii leo hospitali hiyo haijakamilika, imebaki magofu.

Kipindi fulani kanisa katoliki kwa kutambua uzito wa tatizo kubwa la huduma za afya kwa wakazi wa mkoa wa Mara waliomba kukabidhiwa hospitali hiyo ili waiendeleze na kuikamilisha na hatimaye iweze kuanza kuwahudumia wananchi, lakini kwa bahati mbaya sana viongozi wa ccm na serikali mkoani wakaingiza siasa za maji taka na ubinafsi na kukwamisha utaratibu wa kanisa kukabidhiwa hospitali. Hatimaye baada ya kusubiri kwa muda mrefu sana bila kupata committment ya serikali kanisa liliamua kujitoa na sasa serikali haijawekeza kiasi cha fedha za kueleweka ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo.

Ni maajabu ya karne kwamba serikali imetenga sh.100 milioni wakati mahitaji yaliyowasilishwa serikalini katika uendelezaji wa hospitali hiyo ni sh.15 bilioni kwa mwaka ili baada ya miaka mitatu hospitali ianze kutoa huduma. Sasa hapa mtu mwenye akili timamu lazima aishangae serikali kwa jinsi ilivyoshindwa kuthamini ustawi wa afya za watu wake kwa kutoweka bajeti ya kukamilisha hospitali hiyo.

Swali la kujiuliza ni kwamba, kuna ushahidi gani kwamba lady jd anaweza kusaidia upatikanaji wa walau sh.1 bilioni tu achilia mbali hizo 15 bilioni zinazohitajika? matamasha mangapi amefanya na yakaingiza kiasi kikubwa cha pesa?? kutumia wanamuziki si tatizo, tatizo ni kwa namna gani ataweza kukidhi matarajio?? hebu tutofautishe wanamuziki wa kimarekani na bongoland. Kama mtu anajihangaikia kujikusanyia kipato kwa machozi band na nyumbani lounge, tena anahudumia mwenyewe na mme wake, atawezaje kukusanya mabilioni ya shilingi? hii ni dharau kubwa ya serikali ya ccm kwa wanaMara.
 
Yote mliyosema mliyotenda... Nasonga mbele...kwani siku hazigandiiii... Lady Jay Dee... Waziri Mponda amechemka...
 
Wazo zuri sana... somethin is better than nothing... Mfanyiwe nini nyie mi CDM...mkubaaliiii??? tushawazoea
 
Akijibu hoja ya Mbunge kuhusu ni lini serikali itatoa fungu la kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Musoma ambao ulishaanza mwaka tangu 1985 kwa kuhusisha nguvu za wananchi, Waziri wa Afya Mh. Haji Mponda alilieleza Bunge jana jioni lilipokaa kama kamati ya matumizi (bajeti ya ofisi ya waziri mkuu) kwamba Serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa harambee ya kuchangisha ujenzi huo itakaowahusisha watu maarufu kama Lady Jaydee na wanamuziki wengine kutoka Marekani na kwingineko.


Hivi kweli tuna mawaziri????? Serikali haina vyanzo vya uhakika vya mapato mpaka kutegemea akina Jay Dee? Mbona wanashabikia misamaha ya kodi kama hali ya mapato ni mpaka wanamuziki wa marekani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Bajeti inapangwa kwa vipaumbele.......... hospitali sio kipaumbele.......tusubiri wanamuziki waje tuserebuke.....:dance:
 
Mbona hata Marekani wanawatumia wanamuziki wenye majina kufanya fund rising? Tuacheni unazi wa kijinga

ni kama unasema " nimeua kwa sababu rafiki yangu ameua" bila kujua kwa nini yeye ameua, tuna akili za kasuku kwelikweli.
 
Kundi la Bilal Islamic sound nasikia pia limealikwa kuimba kaswida siku hiyo, wameshaanza kufanya mazoezi ya kunoa sauti zao huku Sandali
 
Serikali zisizo na vision mambo yao ndiyo hayo,wawapitie pia original comed waende nao shame to you magamba mliochangia thread hii.
 
Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaa toka mwaka 1985 hini kali hakuna haja ya harambee punguza posho zao kumi
mpaka mbili tu.
 
Akijibu hoja ya Mbunge kuhusu ni lini serikali itatoa fungu la kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Musoma ambao ulishaanza mwaka tangu 1985 kwa kuhusisha nguvu za wananchi, Waziri wa Afya Mh. Haji Mponda alilieleza Bunge jana jioni lilipokaa kama kamati ya matumizi (bajeti ya ofisi ya waziri mkuu) kwamba Serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa harambee ya kuchangisha ujenzi huo itakaowahusisha watu maarufu kama Lady Jaydee na wanamuziki wengine kutoka Marekani na kwingineko.


Hivi kweli tuna mawaziri????? Serikali haina vyanzo vya uhakika vya mapato mpaka kutegemea akina Jay Dee? Mbona wanashabikia misamaha ya kodi kama hali ya mapato ni mpaka wanamuziki wa marekani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu niliposikia yule waziri anajibu zile pumba nilitaka kuvunja hata TV.............Kwa hakika baraza la mawaziri la sasa lina vilaza wengi mno......angalia hawa........

  1. Haji Mponda
  2. Omari Nundu
  3. Mkuchika
  4. Nagu
  5. wasira
  6. Lukuvi
  7. Kawambwa
  8. to infinite..............
 
Wazo zuri sana... somethin is better than nothing... Mfanyiwe nini nyie mi CDM...mkubaaliiii??? tushawazoea
Mmmh sioni haja ya kuhusisha msimamo wa kichama katika kujadili hoja hii. Udhaifu uliopo ni kwa waziri kuonyesha mpango uchangiaji wa wananchi kwa matamasha yanayohusisha wasanii. Wengi wetu tunahisi kwamba serikali inatakiwa ije na mikakati ya kutumia vyanzo madhubuti kupata fedha. Hivi ukishalipa hao wasanii na maandalizi kwa pesa ya viingilio na "uchakachuaji" uliopo ni kiasi gani kitabaki kununulia vitu vitakavyoifanya hospitali iwe ya rufaa? Nahisi hapa lazima tukubali "usanii" katika jibu la waziri na namna ya kisanii ya kufanikisha lengo. Kwa kifupi waziri amemtoa mbunge njiani ili lipite na kwakua wanajua Muheshimiwa mkuu wa kaya anahusudu sana mambo ya kuwashirikisha wasanii kama aliyetajwa na waziri basi kombe litafunikwa na mwanaharamu(swali) atapita. Kwa mkakati huo hakuna cha hospitali ya rufaa hapo hadi 2020
 
Akijibu hoja ya Mbunge kuhusu ni lini serikali itatoa fungu la kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Musoma ambao ulishaanza mwaka tangu 1985 kwa kuhusisha nguvu za wananchi, Waziri wa Afya Mh. Haji Mponda alilieleza Bunge jana jioni lilipokaa kama kamati ya matumizi (bajeti ya ofisi ya waziri mkuu) kwamba Serikali ipo kwenye mchakato wa kuandaa harambee ya kuchangisha ujenzi huo itakaowahusisha watu maarufu kama Lady Jaydee na wanamuziki wengine kutoka Marekani na kwingineko.Hivi kweli tuna mawaziri????? Serikali haina vyanzo vya uhakika vya mapato mpaka kutegemea akina Jay Dee? Mbona wanashabikia misamaha ya kodi kama hali ya mapato ni mpaka wanamuziki wa marekani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hapa hakuna mawaziri ila wala hela za wananchi. Je kama wakitumia posho zao ambazo wanazipigia debe zisiondolewe mbona kwa mwaka mmoja tu hiyo hospitali ikatakuwa imefika mbali karibia kumalizika? hawaoni kuwa kwa hilo watakuwa wamesaidia kuokoa maisha badala ya yale maneno ya hovyo ya muhishimiwa mmoja kuwa " hizi fedha zina matumizi mengi, ukitoka mlangoni unakutana na wapiga kura wako unawagawia"
 
Fund raising Tanzania!!!KUna fund raising ilifanyika 2009,ikijulikana kama white ribbon fundraising ikiongozwa na first lady pale moven pick,ilikuwa aibu tupu.Super model naomi campbell ndo alikuwa mgeni rasmi.Mwisho wa siku walifanikiwa kuraise 10,000 usd,kiasi ambacho nafikiri hakifikii hata gharama za kumleta naomi...what a shame!!sasa jay dee si ndo wataraise 10,000 tzs au?
0e1b71c85425d16b_2.jpg
http://www.google.co.tz/imgres?imgu...=572&gbv=2&tbm=isch&ei=y28PTtTXGszusgaZkv2IDw
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom