Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,977
- 30,168
Wadau,
Kuna Bahati Nasibu mpya imeingia inaitwa TATU MZUKA. Sina uhakika ni kampuni gani hasa inayochezesha hii Bahati Nasibu ila kila nikiiangalia uchezeshaji wake naona kabisa kuna kitu hakiko sawa. Bahati nasibu hii huchezwa kwa Mchezaji kuotea namba zake 3 na kuweka Dau (Stake) kisha Wachezeshaji nao watatoa na wao namba zao 3.
Mshindi hupatika na pale Ikitokea Namba 3 zote za Mchezeshaji zimefanana na Mchezaji ambapo Mchezaji hulipwa X200 ya kiasi alichoweka (Stake). Na ikitokea ni namba 2 ndio zimefanana basi Mchezaji hulipwa x2 ya kiasi alichoweka (Stake). Mchezo hoo hufanyika kila baada ya lisaa/saa moja hivyo kila saa ni draw mpya.
Wasiwasi wangu ni kua Sisi wachezaji tunaanza kwanza kuchagua namba zetu 3 kisha hao wachezeshaji ndio wanakuja kutoa za kwao 3. Ina maana kuna uwezekano mkubwa kabisa wakasubiri tumeshatoa namba zetu 3 kisha wao Wachezeshaji wakakaa chini wakachagua zile namba ambazo hazijatajwa au kuchaguliwa na wengi ndio wakazema ndio namba za bahati.
Wasiwasi wa pili, au unaoungana na huu wa kwanza ni kua hatuwaoni wakichezesha hadharani, bali tunatumiwa tu meseji hivyo hatujui hata hizo namba wanazichagua kwa mtindo gani. Hatujui kama ni mashine ndio inachagua au wanachagua vikaratasi, mipira au wanafanyaje.
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha iyaangalie mapungufu haya, maana isije ikawa tunafanywa chanzo cha mapato cha wengine isivyo halali.