Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
- Thread starter
- #141
RIWAYA; BAHARIA
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA KUMI NA NNE
-----------
Ahsubuhi ilimkuta Boneka akijiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda ofisini kwake,licha ya mkewe kumzuia hapa na pale ila mwishoni alitoa sababu ambazo ingekuwa si rahisi Nyamizi kumkatalia.
Alipomaliza kufunga tai yake akainama na kumbusu mkewe ambae alikuwa amelala chali akimtizama.
"Relax my love" Boneka alimwambia mkewe kisha akachukua mkoba wake na kutoka.
Safari yake ilimfikisha hadi karibu na viwanja vya Gymkana, akashuka kwenye gari na kushika kichwa mara mbili kisha akatokea kijana mmoja na bila kuuliza akapanda kwenye gari aliofika nayo Boneka na kuondoka nayo. Boneka akaanza kutembea kwa miguu na wala hakupiga hatua nyingi ikatokea gari yenye vioo vyeusi na kusimama, alipanda na safari ikaanza.
Ndani ya gari hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya dereva na kawaida huwa dereva hasalimiani ni abiria wake na wakisalimiana basi kutakuwa kuna tatizo na linahitaji ufumbuzi wa haraka.
Safari yao ilikuwa ni ya kimywa hadi walipofika kwenye karakana moja ya magari mabovu; gari ikaingia na kisha Boneka akashuka na gari iliomfikisha pale ikaondoka.
Pale akaingia sehemu maalumu akabadilisha nguo na kuvaa fulana nyeusi na suaruali ya jinzi kisha akapanda pikipiki kubwa na kuondoka hadi posta,akapaki na kuelekea kwenye ofisi za chuo cha fedha, hakupanda kuelekea ofisini badala yake alipita upande mwingine na kutokea kwenye nyumba nyingine nzuri na ya kifahari huku kwa mbele kukiwa kuna milango ya biashara.
Ilikuwa ni ngumu kujua ile ni ofisi ya kitengo muhimu na si nyumba ya bilionea yeyote hapo mjini na hata wapangaji wa milango hiyo hawakuwahi kumuona mmiliki zaidi ya kuelekezwa akaunti ya kulipia pango kila muda unapofika.
Na kila mfanyakazi aliehusika na ofisi hiyo ili afike hapo ni lazima apitie njia kadhaa ambazo ni lazima akutane na vijana wa ofisi ile ambao ni maalumu kwa kufuatilia nyendo ili kuwa na uhakika wa safari yake bila kufuatiliwa lengo likiwa ni kulinda usiri wa ofisi ile nyeti.
****
Boneka alijikuta ni yeye peke yake aliekuwa amechelewa kuwasili.
Vijana wote waliotakiwa kuwapo ahsubuhi ile walikuwapo, akiwemo Ziga; Zedi na Haji Makame huku Mwinyi Kisoda na Kobelo wakiwa wapo mbali na nchi hii kwa kazi maalumu pia. Honda alikuwa bado anaugulia hospitali na hali yake iliridhisha.
"Ndoa tamu, yani siku mbili tu umenona shavu aisee" Haji alimtania Boneka na wote walijikuta wakicheka kwa furaha huku wakipeana mikono.
Baada ya utani wa hapa na pale Zedi ambae alikuwa kiongozi wa timu ile aliwaomba waende chumba cha majadiliano.
Na walienda wote waliokuwa pale.
Faili kadhaa zilisukumwa upande aliokuwa amekaa Boneka na Boneka alizipitia kwa haraka haraka na aliona picha kadhaa za mabaki ya kitu kilichoungua, huku kukiwa kuna maelezo pia.
Alipomaliza kusoma aliinua macho na kuwatazama wenzie.
"Miezi kama mitano hivi nyuma,kulitokea ajali ya ndege ya shirika letu, ambayo ilikuwa ikitoka Dar kwenda Mwanza." Zedi aliweka kituo na kuwatazama wenzie kisha akaendelea..
"Na katika ndege ile kulikuwa kuna madaktari bingwa wa tiba za magonjwa ya akili na walikuwa wamepata dawa ya kutibu vichaa ambao huwa hawatibiki na walienda huko kwa ajili ya uzinduzi wa dawa hiyo; lakini bahati mbaya ndege yao ilipotea kwenye rada dakika chache tu baada ya kupaa na baada ya siku mbili ilipatikana ikiwa imeanguka kwenye pori la la akiba la Inara huko Njombe" Zedi akameza kidogo mate na kuwatazama wenzie na aliporidhika na usikivu wao akaendelea.
"Mwanzo tulihisi ni ajali ya kawaida ila kuna mambo yaliofanya hadi jambo hili lilifika mezani kwetu badala ya vyombo husika. Ndege hii ilipasuka vipande na watalamu wanasema ilipasuka kwa bomu dogo lililokuwa ndani ya ndege, lakini pia kibokisi cheusi (black box) cha kufuatilia mwenendo wa ndege na kurekodi kilipotea na hakikuonekana, lakini kubwa zaidi ni kuwa ulipatikana mwili mmoja tu wa rubani na miili ya matabibu watatu haikuonekana ilipo hadi leo, hii inamaanisha hawakuwemo ndani ya ndege" Zedi alisema na kuwatazama wenzie ambao bado walikuwa wanamtazama kama hawamjui.
"Guys;swali la kujiuliza hapa ni kuwa watu hao wapo wapi? Bomu lilitegwa saa ngapi na kwa nini mawasiliano yalikatika?" Zedi alihoji.
Watu wote walikaa kimya kila mmoja akitafakari lake.
Boneka akainua macho!
"Afu hii ni ndege binafsi na kama ingeruka kutoka Dar basi ili ifike mwanza bila kituo ingepita anga la Dodoma sio?" Boneka alihoji na hapo wote wakamtazama, aliongea kitu muhimu sana ambacho mwanzo hakikutiliwa maanani..
"Sasa anga la songea ilifuata nini? Na tena karibu na Nyasa huko kama ukilifuata hilo pori bila kwenda songea!" Boneka aliongeza tena.
"Inashangaza kidogo hii" Ziga alidakia huku akiandika kwenye karatasi.
"Hapo napo kuna ukakasi mkubwa si mchezo" Haji aliongeza huku akiweka mikono kichwani.
"Hili linachanganya na ninaomba tuliweke pembeni kidogo na tusikie jambo jipya kutoka kwa bwana harusi mana nae jana usiku alinidokeza kitu" Zedi alisema na wote wakamgeukia Boneka.
"wiki hii kila mtu anajua tukio gani lilikuwa linatikisa jiji; Boneka alikuwa anaoa. Lakini wakati wa kurudi kuna watu walipiga kelele kuhusu kujirusha kwa mtu ndani ya maji na taratibu za uokozi zilipofanyika alionekana ni binti ambae namfahamu mana ni rafiki wa kufa na kuzikana wa Mke wangu anaitwa Vedi." Boneka aliguna kidogo kurekebisha koo kisha akaendelea.
"Taarifa zile zilisambaa sana kama moto wa kifuu na picha zilisambazwa kila pahali na msiba ukawekwa kwao na mimi na mke wangu tukarejea nchini...jamani mwenzenu sikufaidi siku saba" Wote wakacheka kwa utani ule wa Boneka kisha utulivu ukarejea na Boneka akaendelea.
"Tulipofika nchini moja kwa moja tulienda msibani na nikaonana na wafiwa, ila mama mwenye mtoto alinambia kuwa hana imani kama mwanae kafariki, aliongea kwa hisia,nami nikaona siwezi kupuuza nikampigia mwenyekiti kamati ya mapokezi, akanipa orodha ya watu wote waliongia na kutoka, ajabu jina la Vedi lilisaini kuingia na kutoka na mwandiko ulithibitishwa na mke wangu ila jina moja liliingia tu na halikutoka nalo ni jina la binamu wa mke wangu na tulipofuatilia tuligundua kweli hajarejea nyumbani tangu alipoaga anakuja harusini kwetu. Ajabu sasa jioni ya jana Vedi alipiga simu na alionana na mke wangu na mimi nilionana na kibaraka mmoja anaefutilia nyendo za yule binti na bahati mbaya alinitoroka na kwa taarifa za awali inaonekana kuna jambo linaendelea ndani ya ile kampuni ya meli" Boneka alihitimisha.
"Kwa hiyo huyo Vedi kasema nini hadi sasa!" Zedi alihoji.
"Alikataa kumwambia lolote mke wangu kwa kuhofia kumwingiza matatizoni." Boneka alijibu.
Walijikuna vichwa.
Upele ulipata mkunaji, ila wakunaji nao walijikuna vichwa.
Kesi ngumu mezani kwao.
Kitu ambacho hawakujua ni kuwa adui wa kesi zote hizo ni mmoja.
Ni nani sasa?
-----
ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.
Whatsapp 0658564341.