Baharia; (Ujasusi, Mapenzi na Upelelezi wa kutisha)

Duh
RIWAYA; BAHARIA

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA TATU



Watu wote walitoka na kuelekea nje ya ukumbi na kutazama kule ambako ilisemekana amejirusha, mabaharia kadhaa walikuwa wameshajitosa majini ili kuangalia uwezekano wa kumuona huyo aliejitupa majini.

Licha ya jitihada nyingi kufanyika kumtafuta, bado hawakufanikiwa na ndipo timu ya uokozi ilipopewa taarifa kutoka Dar es laam ili kufika hapo na kutoa msaada zaidi.

Wakati wa mapambazuko ndipo meli ipopiga honi kuashiria inafika ukomo wa safari baada ya kuzunguka baharini usiku mzima.

***

Vedi alishuka kwenye meli na kupita moja kwa moja hadi nje ya eneo la abiria, huko alichukua usafiri na kurudi nyumbani kwake alikokuwa amepanga.
Alipofika akaingia ndani na kujitupa kwenye sofa iliokuwa sebuleni kwake kisha akapumua kwa nguvu na kutupa viatu vyake virefu bila kujali vitakapoangukia.

Vedi alipumua kwa nguvu na kutazama juu kwa tafakuri.

Akakurupuka!

Akauendea mkoba wake mdogo uliokuwa na vitu vyake baadhi na alikuwa nao ndani ya meli.

Akaufungua na kupangua vitu kadhaa vya kujirembea pamoja na taulo ya kike ambayo aliiweka kwa dharura.

Hatimae macho yake yalipata kile alichokitaka.

Kilikuwa ni kile Kitabu kidogo cha kumbukumbu alichokichukua ndani ya kikontena wakati alipokuwa ndani ya meli.

Akakifunua!

Alikutana na mambo machache katika ukurasa wa kwanza na alipoyasoma hakuona kama ndicho alichokihitaji katika kitabu kile.

Kwanza alihitaji kujua kama kitabu kile kimeandikwa kwa matumizi sahihi ya kitabu chenyewe, yani kimeandikwa mambo muhimu ya mmiliki wake. Pia alihitaji kujua kama atafanikiwa kujua kama mmiliki aliandika jina lake na watu wake wa muhimu ikiwemo na mawasiliano yao..

Katika ukurasa uliofuata alikuta jina na tarehe.

“Banzi Kela….tarehe 06/4/2017”

Akafunua tena kurasa nyingine na alifanya hivyo ili kujiridhisha na mawazo yake.

Baada ya kusoma maelezo ya ukurasa ule akarudi tena kwenye ukurasa ambao ulikuwa na jina na tarehe na hapo ndipo alijiridhisha na fikira zake ya kuwa kitabu kile kilianza kutumika tarehe ile na yawezekana lile neno Banzi Kela ni jina na ni la mmiliki wake.

Kichwani mwake akapitisha jina hilo na umiliki wa kitabu kile.

Aliendelea kufungua kurasa moja na nyingine na kusoma yaliondikwa hatimae alifika kwenye ukurasa uliokuwa umeandikwa ujumbe maalumu kwa ajili ya mtu ambae aliamini ni mpenzi wa Banzi.

“Kwako Mamu!
Ni ukweli nakupenda sana kuliko sana yenyewe. Mamu najua unanipenda pia, ila kwa tulipofikia inabidi niwe mbali na wewe. Sio kama umenikosea la hasha ni kwa kuwa tu nataka uishi kwa amani zaidi ukiwa mbali na mimi. Hivi sasa mimi si Banzi tena ila ni marehemu mtarajiwa Banzi. Usiniulize kwanini ila kabla ya kuuliza nenda Hard Rock kwa Jezebeli anaujumbe wa matumaini yangu.” Ulisomeka hivyo ujumbe ule.

Vedi aliganda kwa sekunde kadhaa baada ya kuusoma.

Ni kawaida kwa wapenzi kuandikiana jumbe nyingi, ila ni mara chache kuandikiana jumbe za kutisha na kusononesha namna ile.

Banzi alikuwa na mpenzi anaitwa Mamu na anamtahadharisha juu ya mauti yanayotembea nae.

Mh!!

Vedi akaguna huku akijiweka sawa kwenye sofa yake.

Kwanini sasa Banzi ajitabilie kifo? Na je ujumbe ule ulimfikia Mamu mwenyewe?

Hakuwa na majibu wala wa kumjibu.

Haraka haraka akaanza kupitia kurasa moja na nyingine,alikuwa anatafuta lau mawasiliano ya huyo Mamu na aliamini kabisa mawasiliano yatakuwemo mule.

Hadi anamaliza kukipitia bado hakuwa amebahatika kuona namba yoyote ile ya simu.

Akarudia tena kupitia kwa mara nyingine, bado hali ilikuwa ile ile.

Mh!!.

Akaguna peke yake na kurudi pale kwenye ukurasa wa ujumbe wa Mamu.

Kuna kitu alikiona..

Katika ukurasa ule mwishoni kabisa kulikuwa kuna namba imeandikwa na ilikuwa ni sifuri..

Alifunua tena ukurasa mwingine na hakuona namba ila uliofuata aliona tena namba ikiwa imeandikwa na ilikuwa ni namba Saba.

Akaendelea kupitia na kuzinakili namba zile kwenye simu yake na zilikuwa ni namba kumi kwa ujumla wake.

Aisee!!
.
Vedi alishangaa akili nyingi za Banzi. Banzi alikuwa anasababu gani kuficha namba zile katika aina ile?.

Vedi alijiaminisha kabisa ya kuwa kuna kitu kilikuwa kinaendelea kwa Banzi si bure.

Akajaribu kuzipiga zile namba.

Simu haikutoka!!..

Vedi akarudia tena na hali ilikuwa ile ile.

Akatazama ntandao katika simu yake na alikuta upo chini hausomi.

Ebo!!
.
Na laini iliandika “emergency”

Aisee!!

Tatizo nini?

Hakupata wa kumjibu.

Alibaki akiwa amefadhaika.

Akajinyanyua kwenye sofa na kuelekea ndani kwake ambako alichukua ndoo ya maji na kumimina kwenye ndoo nyingine maalumu ya kuogea kisha akatoka nje na kwenda kuoga ili kuondoa uchovu wa usiku uliopita.
.

Dakika kadhaa badae alitoka na kukuta wapangaji wenzie wakiwa wamekaa vibalazani mwao, akawasabahi na kuelekea ndani kwake.

Akaanza kujiremba harakaharaka ili awahi kituo cha kusajilia laini apate utatuzi wa laini yake kisha amtafute mmiliki wa namba alioikuta kwenye kitabu cha Banzi.

Wakati anaendelea kujipara akachukua kitenzambali(rimoti) na kuwasha runinga.

Alikutana na habari ambayo ilikuwa inamalizikia ila alisikia jina lake likitajwa na kisha zikafuatia picha ambazo zilipigwa wakati mabaharia wakijitahidi kuokoa mtu aliesemekana kujitosa baharini.

Roho ilianza kwenda mbio na kushindwa kuelewa dhumuni la jina lake na picha za uokozi.

Habari iliishia na hakuambua japo maana ya kile alichokiona mwishoni.

Akarukia simu yake kwa pupa, mara akanywea kama maji katikati ya vumbi baada ya kukumbuka simu yake haisomi mtandao.

Akavaa haraka haraka na kutoka nje.
.
Ebwana eeh!

Alishangaa wadada wawili wakirukia ndani kwao kama walioona jini katikati ya kiza kinene huku wakipiga ukunga wa kuogopa.

Alisita kutoka mlangoni kwake akabaki akitizama milango ya wadada wale.

Mhh kuna nini tena?

Alijiuliza peke yake huku hisia mbaya zikianza kumwandama kichwani mwake.


“ooh no! Isiwe kweli basi” Alijisemea huku machozi yakianza kumlenga.

Kuna hisia mbaya ilipita ubongoni mwake kuhusu habari alioona inamalizikia.

Alihisi anahusanishwa katika kifo kile cha mtu kujitupa ndani ya maji.

“Au ile maiti imetupwa majini na uchunguzi umeangukia kwangu baada ya kuacha kadi ile…” Alijikuta akitoa chozi huku akianza kupiga hatua ndefu kutoka pale alipokuwa amesimama.

Haraka yake ilikuwa ni kufika kwa kijana anaesajili laini za simu aliekuwa jirani na hapo alipokuwa akiishi.

Aliihitaji laini ili awasiliane na wazazi wake na kisha amtafute mmiliki wa namba alioipata kwenye kitabu cha kumbukumbu alichokitoa ndani ya meli.

Alitembea kwa hatua za haraka haraka na kuvuka barabara kisha akapita vichochoro viwili na kutokea sehemu iliokuwa imechangamka kidogo.

Akaangaza kidogo na kumuona kijana aliemhitaji ambae wakati huo alikuwa amezungukwa na mabinti wengine wawili waliionekana kuhudumiwa.

“Mambo!” Vedi alimsabahi kijana yule huku akimshika bega kwa nyuma na kijana yule akageuka.

Loh!

Kijana akaruka juu kama shoga lililotekenywa na mtoto.

Hakuishia kuruka tu, akapiga kelele kwa sauti huku akirusha mikono yake kama mtu anaeshambuliwa na nyuki na kitendo kile kilifanya wale mabinti waliokuwa wakihudumiwa nao waanze kutimua mbio huku wakipiga kelele bila kujua wanapiga kwa sababu gani.

Vedi alivutwaika.

Macho yake hayakubanduka kwa yule kijana ambae alikuwa amefika mbali kidogo na kugeuka huku akiwaeleza jambo watu waliokuwa wameanza kujaa kumshangaa.

Vedi alishindwa kuelewa.

Macho ya Vedi yalitua kwenye meza ya kazi ya yule kijana,aliona simu janja ya kijana yule na ilikuwa bado inaonesha mwanga kuashiria ilikuwa kwenye matumizi dakika chache zilizopita.

Akavutiwa na kile alichokiona.

Akaichukua simu ile na kuanza kusoma.

Ebana eeh!

Vedi aliishiwa akili ya kufikiri na kujikuta machozi ya kimtoka huku nafsini mwake kukiwa na sauti kubwa ya kupingana na jambo lile.

Alirudi tena kusoma na hakikuwa kimebadilika kitu.

Alikuwa anasoma katika tovuti moja ya kuwa mtu aliejurusha ndani ya maji amaekolewa na kufahamika kwa jina la Vedi Mashimo mkazi wa kisutu Dar es laam.

Kisutu ndio aliishi na hilo jina ni lake na sio jina tu hata picha zilikuwapo za kwake kuonesha yeye ndie alijitosa baharini na kupoteza maisha.

Akairejesha ile simu na kupiga hatua kuelekea nyumbani kwake; Baadhi ya watu waliomfahamu wakajiweka mbali nae.

Vedi alifadhaika kwa kitendo kile,machozi yalimtoka na mwili ulimwia uzito na kujikuta akipiga hatua za kinyonga.

Akajitahidi na kurejea nyumbani kwake, ila wakati anaingia tena, majirani zake wakaanza kupiga kelele za woga huku wakiita jini jini.

Hakuwajali akaingia ndani kwake ambako wakati anatoka hakufunga mlango.

Ebana eeh!

Ndani napo hakukuta mabegi yake ya nguo na viatu na baadhi ya picha pia zilichukuliwa huku akiachiwa mkoba tu ambao alikuwa ameuangusha uvunguni mwa meza.

Akachanganyikiwa!

Haraka akatoka nje na kuelekea upande wa pili ambako aliamini waliochukua vitu vyake ni lazima waliacha usafiri huko.

Hakuamini macho yake, aliona gari la baba yake mzazi likiwa linaingia barabara kubwa likiwa linatokea pale kwake.

“aah ina maana nyumbani nao wanajua nimekufa hadi wafuate nguo zangu?” Alijiuliza huku akiwa ameweka mikono kichwani.

Vedi hakujua afanye nini katika dakika zile ili kuondoa uongo ule ambao ulikuwa unasambaa kwa kasi kama moto wa kifuu.

Nb: Maoni yako ni muhimu Sana katika kazi hii.
Karibu kwa maoni yako juu ya hiki kitu
 
Sawa
RIWAYA; BAHARIA


NA; BAHATI MWAMBA


SIMU; 0758573660


****

Wakati anafungua mlango na kutoka sebuleni;alikuwa na haraka isioelezeka, alipita sebuleni kama hakujui.


Wakati anafungua mlango ili atoke nje, wala hakupiga hata hatua moja; uso wake ulikutana na mtu ambae licha kujua ujio wake ila si kwa uharaka namna ile.

Alikutana na Boneka!

Kwa kuwa alikuwa na haraka nyingi na pia alikuwa ana kazi ya kuhakikisha anamchelewesha akifika; alijikuta anapata mshituko mkubwa kiasi hadi kitabu alichokuwa ameshika kikidondoka chini.

"Aah karibu komredi" Jay alisema kwa kubabaika baada ya kumuona Boneka.


"Vipi komredi kwema lakini!" Boneka alihoji huku akiinama kukiokota kile kitabu.


"aaah ni kwema... Aah karibu.. Afu hiki kitabu.." Jay aliongea kwa kurukia maneno bila kujua alitaka kuongea nini wakati huo.

"Hebu tuingie ndani komredi, inaonekana haupo sawa kabisa" Boneka alimwambia huku akimshika mkono Jay ili waingie ndani.


"Hapana komredi, wewe ingia afu nisubiri nakuja!" Jay aliongea huku akijinasua mikononi mwa Boneka na kwa kasi aliondoka.

Boneka alibaki akishangaa mambo yale.
Na Jay alikuwa anawahi kuona wale jamaa zake watamfanya nini Vedi na kwa haraka zake akajikuta anasahau kuchukua kile kitabu cha kumbukumbu mikononi mwa Boneka..


Boneka alibaki akikitazama kile kitabu, kisha akaingia ndani na kuona kama Vedi atakuwepo ama la.


Aliita mara kadhaa bila kuitikiwa, akachukua simu yake ili apige.


Simu ikaita kidogo ikapokelewa na Vedi.


Boneka hakusikia mtu akiongea, ila alisikia kama sauti ya mtu anahema na kukimbia kwa kasi.

Alijitahidi kuita bila mafanikio ya kuitikiwa.

Aliendelea kusikia hekaheka za mbio na mara simu ikakata.


Boneka alishindwa kuelewa yanayoendelea.
Alishindwa kujua kama mbio za Jay zilikuwa ni kumuwahi Vedi au vipi na je wamegombana hadi kufikia kutimuana namna ile?

Hata!

Nae akatoka kasi huku akiwa na kile kitabu na alielekea njia aliohisi Jay alipitia..


Mbio zake zilimfikisha barabarani, lakini hakuona mtu wala dalili ya mtu au watu kushangaa jambo fulani.

Alishindwa aulize nini kwa wapita njia.

Akachukua simu yake tena na kupiga, ila wakati huu simu iliita bila kupokelewa.

Boneka alishindwa aamue lipi hasa.

Akarejea alipoiacha gari yake na haraka akapanda na kutaka kuondoka, ila alijikuta anasita baada ya kutupia jicho kitabu alichokuwa amekishika.

Alitaka kukipekuwa ili aone kama ni sahihi kutembea na kitabu cha kumbukumbu za mtu wakati hajui kina umuhimu gani kwa mtu mwenyewe.

Aliamua kukipitia ili aone kama anastahili kukirejesha ama la.

Kitu kimoja kilichomsaidia ni kuwa yeye ni mpelelezi na katika kozi za ujasusi alichofunzwa ni kutokupuuzia hisia zake hasa wakati wa mambo ya kuchanganya.

Alifunua kurasa ya kwanza, alikutana na jina la Banzi Kela na hakukuwa na maelezo mengine zaidi.

Aliendelea kufunua na kukutana na ujumbe ambao ulimpa hisia za ajabu kichwani.

Ujumbe ule ni ambao Vedi aliukuta na ilikuwa ni ujumbe unaomhusu Mamu; lakini katika ujumbe ule kulikuwa kuna kuasa jambo fulani la hatari.


Ujumbe ule ulimtaka Mamu akae mbali na watu wabaya endapo yeye akifa bila kuonana nae...

Boneka aliona kabisa ujumbe ule ulimlenga Mamu na ulitoka kwa Banzi; sasa iweje kitabu kile kiwe mikononi mwa Jay?..


Aliendelea kukifunua na hapo alikutana na kitu alichokitilia shaka.

Kila baada ya kurasa kadhaa aliona kuna namba imeandikwa chini.

Alichukua simu yake na kuzipiga zile namba.

Ajabu ziliita!


"Samahani ndugu!" Boneka aliongea baada ya upande wa pili kukaa kimya.


"Nani!" Iliunguruma sauti kavu ya kike.


"Samahani! Nimepata hizi namba kwenye kitabu fulani cha kumbukumbu!" Boneka alisema huku akiaacha sentensi ikielea hewani.


"Diary? Ya nani!" Sauti upande wa pili iliuliza.

"Banzi Kela!" Boneka alijibu kiufupi.

Alisikia upande wa pili ukipumua kwa kasi kama mtu alieona nyoka mkubwa.


"Najua unataka kuonana na mimi na hicho kitabu kama kimefika kwako basi ukionana na mimi ni kujitia matatizo tu, ila naomba uniletee tafadhali" Mamu alisema bila kujua mpiga simu atapokeaje hiyo taarifa.


"Uko wapi?" Boneka alihoji.


"Tukutane Hard Rock Cafe!" Mamu alijibu huku akikata simu.


Boneka alishangaa ni mara ya tatu anasikia neno Hard Rock Cafe katika mazingira tofauti.

Mara ya kwanza aliambiwa na Vedi ya kuwa anaenda hapo; mara ya pili aliambiwa na kijana wake ya kuwa msafara alioona unatoka hospitali uliingia pale na kutoka n mara ya tatu anaalikwa kuonana hapo na mtu ambae alihisi ndie Mamu.

"Kuna nini hapo Hard Rock Cafe?" lilikuwa ni swali bila jibu.

Aliendelea kugeukia kurasa zingine na hapo alikutana na kurasa moja ambayo ilimfanya atokwe jasho.

Kurasa ilikuwa na maelezo yenye maneno na namba bila ufafanuzi wake.

"Hizi code zimeandikwa kwa ugumu hasa!" Boneka alijisemea huku akijitahidi kuzifungua bila mafanikio.

Alirudia kusoma code moja wapo.

"N1820H=DR KUSEKWA" hapo alijaribu kuzungusha kichwa bila majibu.


Aliishia kuambulia jina la Dr Kusekwa.

Mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake akafungua,ulitoka kwa Mamu.


Mamu alikuwa amemwandikia ujumbe kumwelekeza muda ambao walistahili kukutana.

Ilisalia nusu saa tu ili ufike muda huo.

Boneka aliweka pembeni kitabu kisha akawasha gari na kutoka kwa kasi kuwahi huko alikotakiwa kuwapo ndani ya muda huo.

*****

Safari yake ilikuwa ni ya kupita njia zisizo rasimi na baada ya dakika arobaini alifanikiwa kufika pale Hard Rock Cafe akiwa yupo nyuma kwa dakika kumi.

Haraka akaegesha gari lake na kuingia ndani ya mgahawa huku akitumia ujanja mwingi kuzugusha macho yake bila kumstua mtu ambae angelikuwa anamfuatilia.

Kwenye meza moja kulikuwa kuna mwanamke alievaa suruali ya bluu na shati jeupe na mkoba aliuweka juu ya meza huku akiendelea kuperuzi na simu janja yake.

Kwa kubahatisha; Boneka nae alienda kukaa pale pale.

Akajaribu kuita jina alilohisi ndo la mtu aliempeleka pale.

"Mamu!!"

Yule mwanamke alitikisa kichwa kukubali.


Boneka alipumua kwa afueni.


"Niite Boneka!"


"Kitabu kipo wapi, nakiomba tafadhali" Mamu alisema huku akijaribu kuzuia sauti isifike meza za jirani.


Mhudumu nae hakuwa mbali, alifika na kupokea oda kisha akaondoka.

"Nadhani tuna mengi ya kuzungumza afu nitakupa hicho kitabu" Boneka alisema.


"Nakwambia haya kwa kuwa sitaki kukujua na ninaona u mtu mwema tu bila hata kukuuliza" Mamu alisema huku akimtizama usoni.


"Kila ambae huwa anaonana na mimi kuzungumzia hiko kitabu, maisha yake ni mafupi, sijui kilichomo ila nimekisikia mara kadhaa na kila aliekipata ni lazima anipigie, hivyo sasa ni vizuri nikiwa nacho mwenyewe pengine nitaokoa wengi" Mamu alisema huku dhahiri akionekana kuwa mbali kihisia.


"Kwa nini unahisi kinakuhusu hicho kitu!" Boneka alihoji.

"Banzi Kela; huyo ni mchumba wangu japo naweza kusema ni alikuwa mchumba wangu!"


"Kwanini unasema alikuwa, kwani sasa sio mchumba wako?"

"Mtu wa mwisho kuwa na hiki kitabu alinambia Banzi si mtu tena ila ni maiti tayari na hapo kwenye maiti ndipo alipokipata hiko kitabu!"

Boneka alimakinika kidogo.


"Alikwambia amemuona wapi na kina nani waliomuua?" Boneka alihoji.

"Wewe ni askari?" Mamu nae alihoji.


Boneka alibabaika kidogo huku akijiuliza kama ni sahihi yeye kumwambia kazi yake..

Boneka alikumbuka moja ya sheria za mpelelezi ni kuwa wazi panapobidi ili ili kupima uzito wa jambo lililombele yake.


"Ndio mimi ni askari" Alijibu.


"Umepataje hiko kitabu"

"Kuna binti ni ndugu yangu na tulikubaliana tu...." Boneka hakumalizia kauli yake alikatishwa na Mamu.


"Usiniambie binti Mashimo nae kauwawa" Mamu alihamanika kidogo.


"No! Sina hakika kama ameuwawa ila kwa asilimia zote naamini yupo hai ila ni bahati mbaya tu mi nilikutana na hiki kitabu, japo sijamkuta hapo"


Mamu alishusha pumzi kwa afueni.

"Ok! Banzi alikuwa ni mpenzi wangu na karibuni tungefunga ndoa, ila wiki kadhaa kabla ya ndoa alibadilika huku kila mara akinambia anahisi yupo hatarini kwa mambo fulani ambayo aliyaona" Mamu alinyamaza baada ya mhudumu kufika.


"Alikwambia anaogopa nini?"


"Hapana! Ila alinambia kama akifa, basi Diary yake ina majibu yote.....na bahati mbaya amekufa hiyo diary haipo kwangu na maiti yake sijaiona hadi sasa!" Mamu alifuta chozi kwa mgongo wa kiganja chake.

"Banzi alikuwa na kazi gani kwani!?"


"Banzi alikuwa ni Baharia!; alikuwa mpishi kwenye meli ya Serengeti Marine na ndiko maiti yake ilikoonekana!" Mamu alijibu kinyonge huku akijitahidi kuzuia chozi lisidondoke.


"Kwa hiyo unahisi ndiko alikoona hayo yaliomuua?" Boneka alihoji..


"Wakati fulani aliwahi kunambia tuje kwenye mgahawa huu, na tulipo fika alinambia mashaka yake yanaanzia hapa na hapa ndipo kifo chake kilipo!" Mamu alisema kwa uchungu mkubwa.


"Kwanini hapa!" Boneka alihoji.

"Hata mimi nilimuliza kama wewe ila alinambia neno ambalo sikulielewa hadi leo"Mamu alisema.


"Neno gani!?" Boneka alihoji huku akiwa makini na anachotarajia kusikia.


"Jezebeli!" Mamu alijibu.


"Ndo nini sasa!" Boneka alihoji.

"Hata mimi sijui na wewe ni askari nadhani unastahili kujua sasa" Mamu alisema huku macho yake yakiwa upande wa kaunta ya pale mgahawani.


"Nadhani hiko kitabu kipo pahali sahihi, hivyo nitakihitaji ukimaliza shida zako. Mume wangu amekufa na kafia Serengeti Marine" Mamu alisema huku akichukua mkoba wake na kuanza kuondoka.
.
Boneka alibaki akimtizama tu namna alivyoondoka.

Boneka aligeukia kahawa aliokuwa ameagiza.

Akasonya baada ya kugundua imepoa..
.
Akasimama na kuacha pesa mezani kisha akaanza kuondoka, mara akasikia kelele upande wa barabara.

Akapiga hatua kubwa kuwahi, akaona umati unasogea katikati ya barabara.

Nae akawahi kuona kilichotokea.

"ooh my God" Boneka alijisemea baada ya kuona mwili wa mwanamke ukiwa umelala chini huku damu ikisambaa.

Alikuwa ni Mamu!

Watu walikuwa wanalaani gari iliomgonga Mamu.

"Kagongwa makusudi huyu binti " Boneka alijisemea huku akijitahidi kupangua watu na akamfikia Mamu.

Aliinama na kumgusa; Mamu alikuwa anahema kwa mbali sana.

Boneka akaomba msaada wa wasamaria wanuwahishe hospitali.

Mamu alitulia kimya katikati ya dimbwi la damu.


Waliamua kumnyamazisha, na Boneka alikubali kwamba; tatizo linaanzia Hard Rock Cafe.

Jezebeli! Ni nani au ni nini?"


******


AHSANTENI WOTE MNAOENDELEA KUNUNUA RIWAYA HII KILA UCHWAO NA POLE KWA WOTE AMBAO MNASHINDWA KUFANYA HIVYO KWA SABABU KADHAA AMBAZO ZIPO NJE YA UWEZO WENU.

NAMI LENGO LANGU NI KUONA WAPENDA RIWAYA ZANGU WANASOMA RIWAYA ZANGU BILA KUKOSA.

HIVYO BASI KUANZIA SASA RIWAYA HII INAPATIKANA KWA TSH 1000/= TU BEI INAYOWEZWA NA KILA MTU.

WASILIANA NAMI 0758573660 KWA MALIPO YA M-PESA

0658564341 KWA MALIPO YA TIGO PESA

0624155629 KWA MALIPO YA HALOPESA.

NAMBA ZOTE JINA NI BAHATI MWAMBA.

WHATSAPP NI 0658564341.

KARIBUNI
 
Je, umekuwa shabiki wa riwaya zangu kwa muda mrefu?

Je umekuwa ukinunua riwaya zangu kila mara?

Basi ofa ipo kwa ajili yako!

Wasiliana nami whatsapp 0658564341.

Nimepoteza mawasiliano yenu yote!

Hivyo kunikumbusha ni muhimu
 
Aiseee buku buku zinanihusu, Baharia, urith wa Gaidi, Mpango wa Congo
 
Je, umekuwa shabiki wa riwaya zangu kwa muda mrefu?

Je umekuwa ukinunua riwaya zangu kila mara?

Basi ofa ipo kwa ajili yako!

Wasiliana nami whatsapp 0658564341.

Nimepoteza mawasiliano yenu yote!

Hivyo kunikumbusha ni muhimu
Mzee Baba nakutumia punde unipe ya Baharia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom