Baharia; (Ujasusi, Mapenzi na Upelelezi wa kutisha)

RIWAYA; BAHARIA

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI NA NNE

-----------

Ahsubuhi ilimkuta Boneka akijiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda ofisini kwake,licha ya mkewe kumzuia hapa na pale ila mwishoni alitoa sababu ambazo ingekuwa si rahisi Nyamizi kumkatalia.

Alipomaliza kufunga tai yake akainama na kumbusu mkewe ambae alikuwa amelala chali akimtizama.

"Relax my love" Boneka alimwambia mkewe kisha akachukua mkoba wake na kutoka.

Safari yake ilimfikisha hadi karibu na viwanja vya Gymkana, akashuka kwenye gari na kushika kichwa mara mbili kisha akatokea kijana mmoja na bila kuuliza akapanda kwenye gari aliofika nayo Boneka na kuondoka nayo. Boneka akaanza kutembea kwa miguu na wala hakupiga hatua nyingi ikatokea gari yenye vioo vyeusi na kusimama, alipanda na safari ikaanza.

Ndani ya gari hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya dereva na kawaida huwa dereva hasalimiani ni abiria wake na wakisalimiana basi kutakuwa kuna tatizo na linahitaji ufumbuzi wa haraka.

Safari yao ilikuwa ni ya kimywa hadi walipofika kwenye karakana moja ya magari mabovu; gari ikaingia na kisha Boneka akashuka na gari iliomfikisha pale ikaondoka.

Pale akaingia sehemu maalumu akabadilisha nguo na kuvaa fulana nyeusi na suaruali ya jinzi kisha akapanda pikipiki kubwa na kuondoka hadi posta,akapaki na kuelekea kwenye ofisi za chuo cha fedha, hakupanda kuelekea ofisini badala yake alipita upande mwingine na kutokea kwenye nyumba nyingine nzuri na ya kifahari huku kwa mbele kukiwa kuna milango ya biashara.

Ilikuwa ni ngumu kujua ile ni ofisi ya kitengo muhimu na si nyumba ya bilionea yeyote hapo mjini na hata wapangaji wa milango hiyo hawakuwahi kumuona mmiliki zaidi ya kuelekezwa akaunti ya kulipia pango kila muda unapofika.

Na kila mfanyakazi aliehusika na ofisi hiyo ili afike hapo ni lazima apitie njia kadhaa ambazo ni lazima akutane na vijana wa ofisi ile ambao ni maalumu kwa kufuatilia nyendo ili kuwa na uhakika wa safari yake bila kufuatiliwa lengo likiwa ni kulinda usiri wa ofisi ile nyeti.

****

Boneka alijikuta ni yeye peke yake aliekuwa amechelewa kuwasili.

Vijana wote waliotakiwa kuwapo ahsubuhi ile walikuwapo, akiwemo Ziga; Zedi na Haji Makame huku Mwinyi Kisoda na Kobelo wakiwa wapo mbali na nchi hii kwa kazi maalumu pia. Honda alikuwa bado anaugulia hospitali na hali yake iliridhisha.

"Ndoa tamu, yani siku mbili tu umenona shavu aisee" Haji alimtania Boneka na wote walijikuta wakicheka kwa furaha huku wakipeana mikono.

Baada ya utani wa hapa na pale Zedi ambae alikuwa kiongozi wa timu ile aliwaomba waende chumba cha majadiliano.

Na walienda wote waliokuwa pale.

Faili kadhaa zilisukumwa upande aliokuwa amekaa Boneka na Boneka alizipitia kwa haraka haraka na aliona picha kadhaa za mabaki ya kitu kilichoungua, huku kukiwa kuna maelezo pia.

Alipomaliza kusoma aliinua macho na kuwatazama wenzie.

"Miezi kama mitano hivi nyuma,kulitokea ajali ya ndege ya shirika letu, ambayo ilikuwa ikitoka Dar kwenda Mwanza." Zedi aliweka kituo na kuwatazama wenzie kisha akaendelea..

"Na katika ndege ile kulikuwa kuna madaktari bingwa wa tiba za magonjwa ya akili na walikuwa wamepata dawa ya kutibu vichaa ambao huwa hawatibiki na walienda huko kwa ajili ya uzinduzi wa dawa hiyo; lakini bahati mbaya ndege yao ilipotea kwenye rada dakika chache tu baada ya kupaa na baada ya siku mbili ilipatikana ikiwa imeanguka kwenye pori la la akiba la Inara huko Njombe" Zedi akameza kidogo mate na kuwatazama wenzie na aliporidhika na usikivu wao akaendelea.

"Mwanzo tulihisi ni ajali ya kawaida ila kuna mambo yaliofanya hadi jambo hili lilifika mezani kwetu badala ya vyombo husika. Ndege hii ilipasuka vipande na watalamu wanasema ilipasuka kwa bomu dogo lililokuwa ndani ya ndege, lakini pia kibokisi cheusi (black box) cha kufuatilia mwenendo wa ndege na kurekodi kilipotea na hakikuonekana, lakini kubwa zaidi ni kuwa ulipatikana mwili mmoja tu wa rubani na miili ya matabibu watatu haikuonekana ilipo hadi leo, hii inamaanisha hawakuwemo ndani ya ndege" Zedi alisema na kuwatazama wenzie ambao bado walikuwa wanamtazama kama hawamjui.

"Guys;swali la kujiuliza hapa ni kuwa watu hao wapo wapi? Bomu lilitegwa saa ngapi na kwa nini mawasiliano yalikatika?" Zedi alihoji.

Watu wote walikaa kimya kila mmoja akitafakari lake.

Boneka akainua macho!

"Afu hii ni ndege binafsi na kama ingeruka kutoka Dar basi ili ifike mwanza bila kituo ingepita anga la Dodoma sio?" Boneka alihoji na hapo wote wakamtazama, aliongea kitu muhimu sana ambacho mwanzo hakikutiliwa maanani..

"Sasa anga la songea ilifuata nini? Na tena karibu na Nyasa huko kama ukilifuata hilo pori bila kwenda songea!" Boneka aliongeza tena.

"Inashangaza kidogo hii" Ziga alidakia huku akiandika kwenye karatasi.

"Hapo napo kuna ukakasi mkubwa si mchezo" Haji aliongeza huku akiweka mikono kichwani.

"Hili linachanganya na ninaomba tuliweke pembeni kidogo na tusikie jambo jipya kutoka kwa bwana harusi mana nae jana usiku alinidokeza kitu" Zedi alisema na wote wakamgeukia Boneka.

"wiki hii kila mtu anajua tukio gani lilikuwa linatikisa jiji; Boneka alikuwa anaoa. Lakini wakati wa kurudi kuna watu walipiga kelele kuhusu kujirusha kwa mtu ndani ya maji na taratibu za uokozi zilipofanyika alionekana ni binti ambae namfahamu mana ni rafiki wa kufa na kuzikana wa Mke wangu anaitwa Vedi." Boneka aliguna kidogo kurekebisha koo kisha akaendelea.

"Taarifa zile zilisambaa sana kama moto wa kifuu na picha zilisambazwa kila pahali na msiba ukawekwa kwao na mimi na mke wangu tukarejea nchini...jamani mwenzenu sikufaidi siku saba" Wote wakacheka kwa utani ule wa Boneka kisha utulivu ukarejea na Boneka akaendelea.

"Tulipofika nchini moja kwa moja tulienda msibani na nikaonana na wafiwa, ila mama mwenye mtoto alinambia kuwa hana imani kama mwanae kafariki, aliongea kwa hisia,nami nikaona siwezi kupuuza nikampigia mwenyekiti kamati ya mapokezi, akanipa orodha ya watu wote waliongia na kutoka, ajabu jina la Vedi lilisaini kuingia na kutoka na mwandiko ulithibitishwa na mke wangu ila jina moja liliingia tu na halikutoka nalo ni jina la binamu wa mke wangu na tulipofuatilia tuligundua kweli hajarejea nyumbani tangu alipoaga anakuja harusini kwetu. Ajabu sasa jioni ya jana Vedi alipiga simu na alionana na mke wangu na mimi nilionana na kibaraka mmoja anaefutilia nyendo za yule binti na bahati mbaya alinitoroka na kwa taarifa za awali inaonekana kuna jambo linaendelea ndani ya ile kampuni ya meli" Boneka alihitimisha.

"Kwa hiyo huyo Vedi kasema nini hadi sasa!" Zedi alihoji.

"Alikataa kumwambia lolote mke wangu kwa kuhofia kumwingiza matatizoni." Boneka alijibu.

Walijikuna vichwa.

Upele ulipata mkunaji, ila wakunaji nao walijikuna vichwa.

Kesi ngumu mezani kwao.

Kitu ambacho hawakujua ni kuwa adui wa kesi zote hizo ni mmoja.

Ni nani sasa?

-----

ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.

Whatsapp 0658564341.
 
Hadithi za kudo huwa nacheki page za mwisho km kuna neno tamati ndio nianza kusoma. Manake hachelewi kuacha watu na arosto mazima!
Si ajabu hujawahi hata kunitumia 200/! Ya vocha ama bando, ili nifikishe tamati ama kuposti kila mara hadi mwisho
 
Kwani unaelewa namba yangu kwamba sijatuma?
Basi kama unatuma na unapata na unafurahi kuniunga mkono, sikuona haja ya komenti yako.

Wenye komenti Kama zako ni wale ambao wapo tu kusubiri mtu apost wasome waende na asipoonekana basi hukimbilia kutukana ama kulaumu bila sababu ya msingi.
 
Huwa natuma mkuu sema hatutaji ni nani sababu za kiusalama
 
shukran kudoo,imeishia patamu jaman

SEHEMU YA KUMI NA TANO

Tatizo linakuja ni nini sasa kinaendelea kwenye ile meli na je tangu wahusika wagundue kuna mtu kaona siri yao bado wataendelea kufanya makosa?" Haji aliwauliza wenzie.

Hakuna aliemjibu.

"Nadhani unapaswa kuzungumza na shemeji yako vizuri ili tujue nini kinaendelea" Zedi alimwambia Boneka na Boneka alitikisa kichwa kukubali.

"Turudi sasa kwenye hili suala la hii ndege iliodondoka na tujue ni kitu gani hasa kilifanyika hapa na wako wapi hawa madaktari bingwa na tegemezi kwa familia zao" Ziga aliwakumbusha wenzie.

"Jamani tangu Chief aliponipa hii kazi, kabla sijawafikishieni, tayari nilikuwa nimepita huku na kule na tayari kuna mambo machache nilikuwa nimeyabaini" Zedi alichukua kitabu chake kidogo cha kumbukumbu na kukifunua kurasa kadhaa kisha akakipitia kidogo na kusema
"Nilifika hadi uwanja wa ndege na kutaka kujua safari ile ni nani alikuwa rubani, nikapewa jina la rubani Mbondya na nilijaribu kumfuatilia na kugundua anaishi Ilala na nilifika hadi kwake, ajabu nilikuta familia yake na niliambiwa yupo ila ametoka muda si mrefu!,sikutaka kumsubiri nikaondoka na nilikutana pia na baadhi ya wanafamilia wa matabibu wale ila familia moja ilikuwa na majibu ya mashaka kuhusu hali ya muonekano wa ndugu yao siku za karibuni." Zedi aliwatizama vijana wake tena na kuona usikivu wa hali ya juu.

"Mke wake alinambia siku za karibuni mumewe hakuwa katika hali ya kawaida, alikuwa ni mwenye mashaka mengi na hakuwahi kumwambia lolote isipokuwa alimwambia endapo polisi wakifika kwake siku moja basi awambie hali yake ya mashaka siku za karibuni." Zedi alimaliza kuwambia wenzake na kila mmoja alijisawazisha kwa namna yake alioiweza ili kuipa akili yake utulivu wa maamuzi.

"Hapa inabidi apatikane huyu rubani Mbondya ili tujue kilitokea nini hadi hakurusha ndege wakati yeye ndie alieandikwa kama mrushaji wa ndege ile" Ziga alisema na hapo kila mmoja alikubaliana na mwenzake kuhusu suala hilo la kumtafuta Mbondya.

"Okay! Hapa inabidi zifanyike kazi mbili, hiyo ya kwanza ya iwe hii na nitaifanya mwenyewe" Alisema Zedi huku akikusanya faili zilizokuwa zimetapanywa mezani.

"Na hiyo kazi ya kifamilia inabidi ifanywe na Boneka na Wewe Haji unajua unachopaswa kufanya hapa ofisini na wewe Ziga utaendelea kushugulika na hali ya Honda hospitalini ila pia utakuwapo kwa ajili ya msaada wa dharura ukihitajika,ngoja mimi na bilionea kijana tuingie mzigoni ili chief roho yake itulie." Zedi alitoa maagizo kisha wenzie wote wakakubaliana na kusambaratika kila mmoja akienda kwenye jukumu lake alilostahili kulishugulikia.

****

Boneka baada ya kutoka kwenye ile ofisi alielekea kwenye maegesho ya kulipia posta na kwa mbali aliona gari lake likiwa limepaki pale nae akaenda kulichukua huku akijua kila kitu kipo na garama za maegesho zimeshalipwa. Alipanda kwenye gari na kabla hajawasha alimpigia simu baba yake na Vedi na alihitaji kujua hali ya mkewe na alipoambiwa bado ni mbaya aliamua kuuliza utaratibu wa mazishi na wapi ilipo maiti ile.

Alipata jibu la kushangaza kidogo.

"Mwanangu kuna mambo yanazidi kumchanganya hapa" Alisema mzee Mashimo.

"Kivipi tena mzee!" Boneka alihoji.

"Hapa jana wale polisi waliochukua mwili wa mwanangu walisema wanaupeleka Muhimbili lakini ajabu ni kuwa leo naambiwa umepelekwa Mwananyamala na bila maelezo muhimu, kule ni mbali mwanangu na sijui kwa nini haukuachwa muhimbili" Mzee Mashimo alilalama.

"Ok! Yawezekana askari wenyewe wanajua sababu zao! Ila nakuomba kwa sasa sitisha zoezi la msiba na usubiri nitakuelekeza jambo badae na nitagarimikia mimi mambo yote, kikubwa Mama apate ahueni na aje kumzika mwanae," Boneka alimwambia Mzee Mashimo kisha wakazungumza mambo mawili matatu na Boneka alikata simu na bila kusubiri alipiga tena sehemu nyingine.

"Koplo imekuwaje tena" Boneka alimuuliza koplo Maganga ambae aliongoza wenzake kuuchukua mwili wa mtu aliefanana na Vedi na kuupeleka muhimbili.

"Ebana ee mi sijui kilitokea nini ila baada ya wewe kupiga simu na mimi kuja pale kuichukua maiti wala hatukufika hata hiyo muhimbili yenyewe tulikutana na gari la maaskari pale Tazara na tukaamuliwa kuwapa wale askari tulipkutana nao na tulipouliza tuliambiwa ni maagizo kutoka juu" Koplo Maganga alimwambia Boneka.

Boneka akashusha pumzi na kusema
"poa koplo fanya kazi yako nikikuhitaji nitakutafuta kwa maelekezo zaidi" Kisha akakata simu.

"Hili sasa ni tatizo kama lina maagizo kutoka juu, juu kwa nani sasa!" Boneka alijihoji mwenyewe huku akitoka kwenye maegesho...

Alipanga kuelekea Mwananyamala alihitaji kufanya uchunguzi kwa njia alizozijua ili apate kujua ilikuwaje yule mtu afanane na Vedi kiasi kile na kwa nini asipelekwe sehemu nyingine zaidi ya kwa Mzee Mashimo.

Safari yake hiyo iliibua tena jambo jingine ambalo hakulitarajia.

****

Vedi aliamka ahsubuhi na mapema ili afanye usafi na kisha aelekee sehemu ile ya Hard Rock Cafe kumtafuta Jezebeli mana aliamini kabisa Jezebeli ni mtu na atakuwa yupo pale mgahawani.

Ila hakujua ni kwanini mke wa marehemu Banzi alitazama kaunta kwa woga baada ya kutamkiwa neno Jezebeli. Je hapo ndipo ilipo hiyo Jezebeli? au huyo Jezebeli ni kitu gani au ni nani hadi Banzi amtaje kwenye kitabu chake?

Bado alimuona Jay hayupo sawa na hakutaka kuongea nae chochote ili kumpa muda zaidi pengine nae angesema kinachomsibu hadi kukutana na dhoruba ya kipigo namna ile.

Simu yake ilikuwa ikiita mara kwa mara na aliekuwa anapiga ni Nyamizi ili kujua anaendeleaje.

Tatizo Vedi hakujua ni kuwa kila alipopigiwa na Nyamizi; Jay nae alikuwa anaandika ujumbe kwenda kwa Gomba.

Na Gomba alipopokea ujumbe aliuliza Nyamizi ni nani na aliambiwa ni mke wa billionea kijana Boneka.

Gomba na Panga wakataka kujua kilichonyuma ya urafiki wao, wakaanza kutafuta taarifa muhimu kuhusu Nyamizi na kwa bahati mbaya hakuna walichokipata zaidi ya kuambiwa ni mhitimu wa chuo kikuu Dar.

Ila kazi yao haikuwa bure, walipata picha za mume wake..

Gomba alibaha baada ya kuzitambua.

"Ayaa huyu bwege ndo aliniotea jana usiku ujue" Gomba alihamaki.

"Sasa na urembo wote wa huyu jamaa alikuoteaje!" Panga alikebehi.

"Aisee yule jamaa ni mjuzi wala sio muoteaji, ni mwepesi na ngumi zake zinaujazo wa kimazoezi sio mrembo kabisa!" Gomba aliongea kwa upole huku akitafakari.

"Sasa kwa nini akuvamie? Alijua lolote au ni kwa kuwa aliona unamtazama mkewe?" Panga alihoji.

"Sina hakika kama alinivamia kwa wivu, yule jamaa alikuwa anajiamini sana na alikuwa anataka kitu zaidi kuliko kunililia wivu wa kumfuata mkewe" Gomba aliendelea kutafakari huku akimhabarisha Panga mawazo yake.

"Kwa hiyo anaweza kuwa ni mtu wa sisitimu?" Panga nae alizidi kuhoji huku mzaha ukiwa pembeni.

"Sina hakika ila kitendo cha kumuona Vedi wakati nyumbani anajua kuna maiti ya Vedi ni lazima kutampa maswali na kwa pesa yake anaweza kuleta watu wakatuadabisha..lakini yule jamaa ni zaidi ya bilionea aisee!" Bado Gomba alizidi kupambana na hisia zake.

"Kwa hiyo unasemaje?" Aliuliza Panga.

"Tumshirikishe Cholo afu nadhani inabidi Vedi auwawe kiukweli sio tena maigizo" Gomba alisema.

"Na vipi kuhusu huyu mchumba bilionea mwenye sura ya kike!" Panga alihoji.

"Tujue kwanza nyendo zake kisha tutampeleka akasilimie wafu kwanza" Gomba alijibu huku akisoma ujumbe kutoka kwa Jay.

Wanapanga kuua ila hawajui moto wa mtu wanaetaka akasalimie wafu umeshaunguza mifupa mingi hata isiotafunika. ..

Wataweza?

*****

ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.

Whatsapp 0658564341.
 
RIWAYA; BAHARIA

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI NA SITA

Gomba aliendelea kusoma ujumbe wa Jay na tena akamgeukia Panga.

"Hivi huyu dogo bado anatufaa kweli!" Gomba alihoji.

"Bado kidogo, acha tujue nyendo za yule mtoto wa kahaba afu nae tutampa zawadi yake, hatuzoeleki sisi" Panga alisema huku akipokea simu iliokuwa na ujumbe wa Jay.

----------

Vedi aliendelea na kushika hiki na kila na alipomaliza akamuita Jay mezani kwa ajili ya kupata stafutahi na kisha kila mtu aendelee na mambo yake.

Wakiwa wanaendelea kula mara simu ya Vedi ikaita na alipoangalia mpigaji ilikuwa ni namba ngeni ila aliifahamu, ilikuwa ni namba ya shemeji yake Boneka.

Walisalimiana na kujualiana hali kisha Boneka akasema...

"Shemeji badae nitakuwa na mazungumzo na wewe ila naomba tukutane hapo hapo nyumbani kwenu na pia jitahidi usitoke kwa usalama wako"

"Kuna sehemu nilitarajia kwenda ila nitajitahidi kuwahi na utanikuta " Vedi alijibu..

"Ulitarajia kwenda wapi kwani!" Boneka alihoji kwa umakini sana.

"Kuna mtu wa muhimu nilitaka kwenda kumuona hapo Hard Rock Cafe ila nitawahi" Vedi alijibu.

Walizungumza kidogo kisha wakaagana.

Jay ambae muda wote alikuwa kimya aliinua macho na kumtazama Vedi.

"Vedi hivi ukisikia nimekufa leo au kesho utafanya nini?" Jay alihoji kinyonge huku nafsi yake ikiwa na mabishano makali kuhusu mustakabali wa maisha yao.

"Nadhani ulipaswa kujiuliza ni kwanini ulinifukuza na kunipa tuhuma ila bado nipo hapa kwako najizungusha lakini pia ungejiuliza ni kwanini hujarudia tena kunifukuza baada ya kukomaa kukaa hapa kwako hivyo ukipata majibu basi huna haja ya kuniuliza hilo swali" Vedi alisema kwa hisia jambo ambalo lilimchoma Jay na hakuwa na cha kufanya. Watesi wake walimshika kubaya, alihitaji tiba ya kansa ya kuambukizwa. Likini bado Jay alijiuliza atakaa nalo moyoni hadi lini na ataendelea kumsaliti mchumba wake hadi lini. Hakupata jibu. Akatazama ukutani akaona masaa yanazidi kusogea na alianza kuhofu kuhusu dawa za kulevya alizopewa usiku uliopita ni vipi kama zitahitajika, atazipata wapi ili kujinusuru na vipi Gomba na wenzake watarejea kumpa dawa na vipi kama wakimkuta Vedi watamfanya nini?

Jay alidondosha chozi bila kujijua.

"Mpenzi najua unapitia magumu kuliko hata mimi, lakini unapaswa kunishirikisha na mimi nikushirikishe ili tujue tunaokoka vipi...Jana nilikuta umepigwa na udhoofu wa mwili na juzi nilipofika ulinifokea kama mtoto bila sababu huku ukinisingizia mambo yasioyo kuwepo, ni kipi hasa kinaendelea?" Vedi bado aliongea kwa hisia kubwa.

Jay aliyapokea maneno yale kwa uchungu mkubwa huku akishindwa kujua aanzie wapi kusema neno lolote.

Nafsini mwake alikuwa anajiuliza ni kipi afanye, alinde siri ama aanike kwa mkewe mtarajiwa watatue?

Mara akakumbuka mkwara aliopigwa na Panga kuhusu lolote atakaloliongea basi wao watalisikia popote walipo.

"Watch your back" alijionya.

"bado muda upo tutazungumza ngoja kadhia yako ipite kwanza" Jay alisema huku akinyanyuka na kuelekea chumbani.

Vedi alibaki akimtizama tu bila kusema lolote lile.

----------

Boneka aliegesha gari sehemu ya kuegesha magari nje kidogo ya majengo ya hospitali ya Mwananyamala.

Aliangaza kushoto na kulia ili kujipa uhakika wa mazingira kisha akashuka kwenye gari na kuelekea sehemu ya kusaini kwa wageni wanaoingia na akaandika alikotaka kuelekea.

Alipomaliza alielekea yalipo majengo ya kuhifadhia maiti.

Hakutumia dakika nyingi akawa amefika kwenye ofisi husika.

Akaeleza shida yake na akaomba kuona mwili wa mtu alieitwa Vedi Mashimo.

Walinzi wakaangaliana kisha mmoja akamjibu..

"Tumezuiwa kuutoa huo mwili au kuonesha ni hadi kwa kibali maalumu kutoka ngazi za juu"

Boneka alielewa nini mana ya kauli ile akakubali na kuanza kuondoka..

Lakini wakati anatoka nyuma yake alisikia kuna harakati zinaendelea, akageuka kutazama

Aliona majeneza mawili yakitolewa na kisha akaona yakipakizwa kwenye gari moja.

"ina maana waliokufa wanaenda kuzikwa pamoja au!" ajabu nyingine aliona wamama wawili tu na jamaa mmoja ndio walolioonekana kuwa wafiwa au watu wa karibu na marehemu wale.

Jamaa yule alikuwa amevaa kofia ya pama na miwani huku akipigilia na koti na suruali ya jinzi na viatu vya buti.

Zilifanyika harakati chache kisha safari ya magari matatu ikaanza huku gari la mbele likiwasha taa kuashiria kuna tatizo katika msafara ule.

Boneka akatembea haraka kuwahi gari lake huku lengo lake likiwa ni kuwahi msafara ule na hata yeye alijishangaa ni kwanini aliamua kuutilia shaka msafara ule.

Ukiachilia mafunzo ya kijasusi kutumia milango mitano ya fahamu; yeye aliamua kutumia na kuheshimu mlango wa sita wa fahamu ambao ni "machale".

Katika kozi ya utambuzi wa viashiria vya hatari basi mlango huo wa sita ulikuwa ni muhimu sana na hakupaswa kupuza.

Akawasha gari lake na kuanza kufuata nyuma.

Msafara ule ulielekea barabara ya Makumbusho.

Kabla hawajafika kona ya kuingia kituo cha magari ya abiria; Boneka aligundua kuna gari lipo nyuma yake na yawezekana alifuatwa yeye au lilikuwa ni gari ambalo lilihakikisha usalama wa ule msafara.

Akachukua simu yake na kutafuta jina fulani kisha kwa kutumia mkono mmoja aliandika ujumbe mfupi na kisha akaendelea na safari.

Walitokea barabara ya kawe na aliona msafara ule unaelekea kulia kama waenda kawe, yeye akaelekea Mwenge na kwa kutumia vioo vya kuangalia nyuma aliona lile gari lililokuwa nyuma yake ni kama limeshindwa pa kuelekea.

Boneka akatabamu.

"Hawa hawajui usuvailensi nimeufanya kabla sijafakia hiki kitengo, ngoja sasa mabingwa wa kazi wawafuatilie hadi mwisho tuone" Alijisemea huku akimalizia kuandika ujumbe kwenye simu kuelekeza njia ulikoelekea ule msafara.

"Kwa nini wamezuia ule mwili kutazamwa? Na kwa nini hakuna hao maaskari?" Boneka alijihoji.

Akiwa bado yupo kwenye foleni mara ujumbe ukaingia na alipotazama aliona moja wa kijana aliemtuma kufuatilia msafara ule ameandika ujumbe mfupi tu

"Hard Rock Cafe!" ilimaanisha ulielekea hapo na pia alikumbuka Vedi alimwambia nae anaelekea hapo.

E bwana ee!..

Boneka alichemkwa na damu huku akili ikimtembea kwa kasi, alihitaji kufanya kitu, ila mbele foleni kubwa ya magari na nyuma pia kuna mshono wa magari, atachomokaje na hakuona pa kupaki ili atumie usafiri wa boda boda.

Mh!!!!

*****

ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.

Whatsapp 0658564341.
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom