Baharia; (Ujasusi, Mapenzi na Upelelezi wa kutisha)

Kudo

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,579
Points
2,000
Kudo

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,579 2,000
RIWAYA; BAHARIA

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660SEHEMU YA KUMI NA SABA

Akiwa bado ana mazonge mazonge kuhusu kile alichokisoma;mara ujumbe mwingine tena ukaingia na ulitoka kwa kweli kijana wake ambae alimpa kazi ya kufuatilia mienendo yote ya msafara ule.

"Hapa haujakaa sana....loading" hiyo ilimaanisha msafara ule haukukaa sana pale na sasa kuna sehemu unaelekea.

Boneka alishusha pumzi kwa afueni huku akipanga kufanya kitu ili ajue linaloendelea hapo Hard Rock Cafe.
.

Akatazama muda na kuonesha ilisalia saa moja muda wa kuonana na Vedi ufike.

Akatulia kwenye kiti kusubiri foleni isogee..

*****

Zedi baada ya kutoka ofisini kwao,nae hakutaka kulala na kusubiri kujua undani wa ajali ya ndege ilipotea na matabibu na wagunduzi wa tiba ya magonjwa ya akili.

Lengo kubwa walihitaji kujua kilipo kibokisi cheusi ambacho hurekodi mwenendo wa safari ya ndege. Kilikuwa hakionekani kilipo na haikujulikana kama kilipotea makusudi ama bahati mbaya na watafutaji hawakuwa makini wakati wanakitafuta.

Bado alihitaji kujua ni kwanini rubani alietakiwa kuinyanyua ndege awepo na aliekuwa kwenye ndege awe mwingine. Hilo lilikuwa linahitaji ufafanuzi na hakuna wa kufafanua zaidi ya Mbondya mwenyewe.

Alipiga moto pikipiki yake kubwa na kutumia njia zisizo rasimi na hatimae alijijuta tena amerejea nyumbani kwa rubani Mbondya jirani na shule ya msingi Ilala.

Akashuka kwenye pikipiki na kuiacha kwenye maegesho ya jengo la Nssf mafao, kisha akatembea kwa miguu hadi shuleni na akasimama kutazama upande ambao nyumba ile ilikuwa.

Akavuta hatua na kulifikia geti, kisha akabonyeza kitufe cha kengele na kusubiri.

Punde geti likafunguliwa na akakaribishwa ndani na Mama mtu mzima.

Ilikuwa ni nyumba kubwa ambayo ilistahili kuitwa ya kisasa.

Mama akataka kumpeleka ndani ila alikataa na kuomba wakae kwenye korido ya kupumzika na kulikuwa kuna sofa mbili ambazo zilianza kuchakaa.

Zedi alikaa baada ya mwenyeji wake kukaa.

"Karibu baba!" Mama alivunja ukimya.

"Bila shaka hapa ndio kwao na Mbondya!" Zedi alihoji.

"Ndio baba!"

"Mbondya ameoa?" Zedi alihoji huku akimwonesha kitambulisho bandia yule mama na kitambulisho kile kilimtambulisha kama ni mfanyakazi wa uwanja wa ndege.

"Kwani hajawahi kukwambia!" alihoji Mama..

"aah wapi mama jamaa ni msiri wa mambo yake hatari ni ngumu kujua kama kaoa au la!"

"Bado hajaoa licha ya kumshinikiza sana afanye hivyo, si waona umri wangu hivi sasa nahitaji nipate mjukuu tu." yule mama alianza kujibu kwa kumzoea Zedi na Zedi alitambua yule Mama ni mtu wa kusini kulingana na lafudhi yake.

Zedi akaona akiuliza maswali mengi yule Mama atahoji kulikoni, hivyo akaamua kutumia akili ya kijasusi kupata kile alichokitaka.

Akaingiza mkono mfukoni na kutoa bahasha ndogo na kumpa yule Mama.

"Akija mpe kadi yangu ya harusi na yeye akisoma atajua tu!" Mama akaipokea na kutabasamu..

"Yani vijana mnazidi kuoa tu huku mwenzenu yeye ni kuponda raha tu, hongera mwanangu" Yule Mama alisema huku akiipokea ile bahasha.

"Kwani anapenda sana kujirusha kweli mbona kama hatujawahi kuona hayo mambo kwake hata tukiwa na safarini?" Zedi alijikosha kwa lengo la kupata kile alichohitaji kutoka kwa Mama yule.

"Unajua yule mtoto nimemlea na kumsomesha kwa shida na wakati wote huo hajawahi kuonesha tabia mbovu hadi wakati huu ambao ameanza kupata pesa, amekuwa hanisikilizi kabisa na amekuwa akiambatana na marafiki wa ajabu tu, na kila mara amekuwa na safari ambazo hazina mpango tofauti na zamani anbapo safari zake zilikuwa kwenye ratiba wakati wote, ila siku za hivi karibuni amekuwa mlevi sana..... Mh!" Yule Mama alimalizia kwa kuguna kwa masikitiko huku akionekana dhahiri kuumia kwa tabia ile ya mwanae kipenzi.

"Ooh pole sana Mama, kwani kwake ni wapi au anaishi hapa?" Zedi alihoji kijanja lengo likiwa ni kujua hasa ni wapi atampata Mbondya.

"Hapa siku hizi ni mara chache sana kuja, japo ni lazima aje, ila kwake sio mbali na hapa ni hapo nyuma tu, yani ukitoka kwenye hilo jengo refu yeye anaishi kwenye nyumba inayofuata karibu na barabara.

Zedi alimpigisha soga za hapa na pale kisha akaaga na kuondoka na huku akiwa amejua makazi rasimi ya yule jamaa na safari yake ilikuwa ni kuelekea huko.

Hakuhangaika kutumia usafiri, bali alitembea kwa miguu tu kisha akapita jengo la Nssf na kwa mbele aliona nyumba alioelekezwa ikiwa imezungukwa na miti michache tu mirefu ambayo haikuleta kero barabarani na majirani wake.

Akavuta hatua na kuachana na milango ya biashara, hadi kwenye geti lililoonekana ndilo linalotumika kuingilia.

Akalisukuma baada ya kugundua lipo wazi.

Akaingia na aliona haikuwa nyumba kubwa ni ya kawaida tu iliopaswa kuishi kijana mwenye umri sawa na wake..
.
Kulikuwa kuna gari moja nyeusi iliokuwa imeegeshwa karibu na mlango wa kuingilia ndani.

Sauti kubwa ya muziki ilisikika na hiyo iliashiria wenyeji watakuwepo.

Akapiga hatua za kujiamini na kugonga mlango mara kadhaa bila kuitikiwa na aliendelea kusikia kelele za muziki.

Akasukuma mlango na kuingia huku akiwa makini sana.

Macho yake yakatua kwenye sofa na kuona binti akiwa amelala na kanga moja tu sofani.

Yule binti aligeuza shingo kivivu na kuona kuna ugeni ambao hakuutarajia..

Akanyanyuka kihasara hasara bila kujali kama kanga yake inaanguka ama la..

Macho ya Zedi yalitembea kwa kasi ya kimbunga na kwa haraka aliona picha za Mbondya akiwa amevaa mavazi ya kikazi na tabasamu murua usoni.

Macho yake akayarejesha kwa yule binti, na hapo akagundua vile yule dada alivyokuwa akimtizama kwa kiulizo.

Lakini sura ya yule dada ilisadifu hali fulani isio ya kawaida, uso wa yule binti ulianza kupoteza nuru ya uzuri wa asili na tayari kulianza kuonekana athari za utumiaji wa vilevi kupitiliza au uraibu wa dawa za kulevya au pombe kali.

Zedi alikaa taratibu huku yule dada akiwa hajahangaika hata kupunguza sauti ya radio iliokuwa juu kupitiliza na ilikera kusikiliza.

Mezani aliona kitenzambali(rimoti) akachukua na kupunguza sauti ya radio kisha akauliza.

"Mbondya nimemkuta?"

Yule binti alitikisa kichwa kukataa..

"Yupo wapi kwani!"
Zedi alihoji tena.

"Kwani umeenda Hard Rock Casino umemkosa?" yule binti alijibu kwa swali huku akipinda midomo kuashiaria alikereka na swali hilo.

"Kwani ndo anakopatikana siku zote!" Zedi alihoji."kwani wewe wa wapi hadi uusijue bwana Mapesa yupo huko muda huu, wewe mgeni hapa mjini bila shaka!" yule binti aliongea kwa kushushua.

Zedi alielewa yule dada ni kahaba wa mjini ambae hana nidhamu wakati wa kuongea.

Lakini alijiuliza tangu lini rubani hugeuka kuwa bwana mapesa?

Alimtizama yule binti kwa tuo kisha akawaza kufanya jambo pale ndani.

Akasimama na kutoa pesa mfukoni kiasi cha laki moja hivi na kumpa yule dada.

"Nimekutamani, naomba unichetue kidogo niondoke basi!" Zedi alisema huku akisogeza zile pesa.

Yule dada akasimama huku akiacha kanga yake ikianguka bila kujali na kubaki mtupu huku akijichekesha kibwege.

"Au bwana Mapesa kakutuma unijaribu wewe" yule binti aliongea huku akizipokea zile pesa.

Zedi akamsogelea na kuwa kama anataka kukumbatia hivi,ila kwa kasi akampiga kwa kutumia upande wa kiganja karibu na sikio na yule binti alilegea na kupoteza fahamu.

Zedi akamlaza kwenye sofa kisha akamfunika na kanga na kisha akazima radio na kisha akaanza kupekua hapa na pale.

Aligusa kila mahali ndani ya sebule ile bila kupapata chochote.

Akaamua kuelekea chumbani huku tahadhari ikiwa mbele kama tai.

Akasukuma mlango na kuingia.

Alikutana na chumba safi chenye samani za kisasa hasa kitanda na kabati.

Alitizama hapa na pale na akaona suruali ya kike ikiwa imetupwa chini, bila shaka ilikuwa ni ya yule binti.

Akaikota na kuikagua mifukoni.

Alitoka na vitu viwili ambavyo havikumpa shida kuvifahamu.

Kimoja kilikuwa ni kete ya unga wa dawa za kulevya, lakini kingine ilikuwa ni kadi ya kuingilia casino na pia kulikuwa kuna jina la kasino ile.

"Hard Rock Casino"

Akavirudisha kwenye suruali na kuiacha chini.

Alikagua hapa na pale na hatimae aligota kwenye droo ya kitanda.

Ikamgomea!

Akaichunguza vyema kisha akatoa funguo moja kwenye mfuko wake, funguo ile haijawahi kushindwa kufungua kitasa chochote kile.

Akaipachika na kitasa kikaachia.

Macho yake yalikutana na kadi nyingine tena..
Akaisoma na kadi ile ilikuwa na majina mawili.

"Hard Rock Cafe na Hard Rock Casino" ilimaanisha mgahawa na kasino vyote ili uingie ni lazima utoe kadi.

Zedi aliguna baada ya kumaliza kusoma kadi ile na macho yake kuyarejesha kwenye droo ile.

Noti nyingi za dola ya kimarekani zilikuwa zimepangwa vyema kwenye ile droo.

Lakini pia aliona kitu kingine cha ziada...

Aliona visa ya kusafiria ikiwa imeambatanishwa na pesa zile.

Akaivuta kutoka nayo, akaisoma na kuona nchi kadhaa ambazo mbondya alitarajia kuzifikia ama visa ile ilimruhusu kuzifikia. Lakini alipondelea kukagua aligundua Mbondya alipanga kusafiri siku chache mbili zijazo kwa kutumia ndege ya abiria na tayari alikata tiketi iloonesha anaelekea falme za kiarabu..

"Kaacha kazi?" Zedi alijihoji bila majibu.
.

Zedi hakutaka kwenda kwenye kampuni aliofanyia kazi Mbondya ili kujua kinachoendelea ili kuepuka kuharibu harakati zake.

Alichukua ile hati ya kusafiria kisha akaiweka mfukoni na akarudisha vitu kama alivyovikuta na kufunga kisha akatoka. Lengo likiwa ni kumharibia safari..

Hawezi kusafiri bila hati ile.

Zedi akatoka sebuleni na kukuta bado yule binti hana fahamu, akachukua pesa yake na kuondoka.

*****

ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.

Whatsapp 0658564341.
 
Kudo

Kudo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
1,579
Points
2,000
Kudo

Kudo

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
1,579 2,000
RIWAYA; BAHARIA

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660

SEHEMU YA KUMI NA NANE

***

Zedi alipitia kwenye maegesho akachukua piki piki yake na kuondoka huku kitu pekee alichokuwa anakiwaza ni Hard Rock Cafe na Hard Rock Casino.

Alihitaji kujua mengi kuhusu hizo sehemu lakini pia alihitaji kukutana na Mbondya p.a.k bwana Mapesa.

Kazi anayoifanya ni kazi ambayo ina pesa nyingi ila haiwezi kuwa kazi ya kumpa vibunda vile vya dolali na pia kazi anayoifanya msingi mkuu ni kutokuwa mlevi wa kila muda, hiyo ni kwa usalama wake na abiria anaowabeba pale anapohitajika, sasa ni ajabu kusikia Mbondya ni mlevi wa kupindukia hadi Mama yake analalama.

Lakini pia alijiuliza kuhusu aina ya mtu aliemkuta nyumbani kwa Mbondya.

Mtumiaji wa dawa za kulevya, lakini pia alikuwa na kete kwenye nguo zake na kikubwa yule ni kahaba.

Je Mbondya hakujua hilo au nae ni mtumiaji? Lakini kwanini safari iliomhusu hakwenda na kwanini bado hajaripoti kazini tangu kuanguka kwa ile ndege? na inaonekana muda wote hakusafiri, kwanini asafiri hivi karibuni sasa!

Yalikuwa ni maswali bila majibu.

Pikipiki iliendelea kuburuza barabarani.

Alijikuta anamhitaji sana Mbondya kuliko hata kumhitaji mtu alienyuma ya mchezo ule,mana kumpata Mbondya ni hatua kubwa ya kumfikia mtu alie nyuma yake.

****

Boneka alikuwa bado yupo kwenye foleni huku muda wa kuonana na Vedi ukiwa unakaribia..

Akasikia ujumbe ukiingia kwenye simu.

Akaufungua!
.

Ulitoka kwa Vedi na alimjulisha tayari anamsubiri.

Vedi nae baada ya kutuma ujumbe alienda chumbani kwa lengo la kujilaza kidogo ili walau apate kupunguza kidogo mawazo yake kwa kijiusingizi kitakachomchukua.

Mara Jay akaingia.

"Nilisikia una mgeni badae kidogo sio!" Jay alihoji.

"Ndio na anakuja muda sio murefu" Vedi alijibu.

"Ok sawa!" Jay alisema huku akitoka chumbani na kwenda sebuleni.

Jay alipokea ujumbe ambao ulimwelekeza ya kuwa ajitahidi Vedi asionane na Boneka na hiyo ni baada ya Jay kutoa taarifa ya Vedi kutembelewa na Boneka pale kwake.

Na alipokea ujumbe huo uliosisitiza ajitahidi wasikutane.

Atafanya nini, hilo ndilo alilohitaji kufanya na kujiuliza.

Aliona akimtaka watoke itakuwa ngumu sana kwake July alias akizingatia ya kuwa siku za karibuni wamekuwa hawana maelewano mazuri kabisa.

Akazidi kuwazua bila jibu.

Mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake.

"Muda wa kupata dozi unakaribia, hivyo mwambie aje hapa nyuma ataona gari jeusi alifuate na atakuletea. Ila baada ya kuhakikisha huyo bwana katoka hapo" Ulikuwa ni ujumbe wa Panga.

Akimtuma kwa kawaida sio rahisi Vedi kwenda na atakuwa na kiulizo, jambo ambalo litasababisha Boneka amkute hapo.

Jay akaanza kujinyonga akiwa amekaa kwenye sofa, alijinyonga mithili ya mtu anaepitia mateso makali ya maumivu ya tumbo.

Alipoona juhudi zake hazimvutii Vedi; ikabidi atoe miguno ya maumivu na hila zake zilifanikiwa.

Vedi alisikia ile miguno, akatoka haraka ili kujua kulikoni.

Alikuta Jay anaugulia maumivu huku akiwa ameshika tumbo na kutumbua macho kama mgonjwa anaekaribia kukata roho.

"Shida nini tena jamani!!" Vedi aliuliza kwa mashaka huku akihangaika kumshika hapa na pale.

"Tumbo linaniuma sana na kitu kimebana kifuani" Jay alizungumza kwa tabu kidogo.

Vedi akakurupuka ili kuwahi kuchukua dawa za tumbo ambazo huwa wanaweka ndani kwa dharura.

"Tafadhali naomba nisikilize kwanza" Jay alimwambia Vedi baada ya kuona anataka kutoka na kumwacha.

Vedi akarejea kumsikiliza.

"Kuna jamaa zangu hapo nyuma wana gari jeusi, tafadhali nenda wambie waje mnipeleke hospitali"

Vedi hakutaka kusubiri, akatoka ndani mbio na kuelekea nje kuelekea usawa alioelekezwa.

Alipotoka tu, ni wakati huo ambao Jay alinyanyuka na kwenda chumbani kuchukua simu yake na kuwasiliana na Panga.

"Naombeni msifanye kitu kibaya huyo binti jama!" Jay aliwandikia huo ujumbe.

"Sasa kagua vitu vyake, kuna kitabu kidogo cha kumbukumbu, tunaomba ukichukue na utoke nacho nje" Panga alimwandikia Jay.

Jay akahaha kukitafuta hicho kitabu huku roho yake ikiwa inahangaika na kichwa chake kikipita kwenye tanuru la fikira kujua kitu gani wale jamaa watakifanya kwa Vedi.

Roho ilimsuta ila hakuwa na la kufanya, alihitaji kufanya linalowezekana ili Vedi asiingie matatizoni.

Atafanya nini wakati ameshamtuma kwa wabaya wake.

"ooh shiit!" Alijisemea huku chozi la usaliti likimdondoka,hakika alipitia hali ngumu.

Mikono yake inayotetemeka iliendelea kuhangaika kupekua mikoba ya Vedi.

Hatimae alikipata kitabu kile kikiwa kina kalamu iliobanwa pamoja nacho.
.

Akaanza kutoka ili akipeleke kama alivyoelekezwa.

Lakini alisita kidogo alipofika kwenye mlango wa chumba chake.
.

"Kama hiki nikiwapa ndo watatuua itakuwaje?".Jay alijiuliza bila kupata majibu..

Akajikuta akiwa na maswali mengi kuliko majibu,huku akiwa amekishikilia.
.

Akaamua kutoka ili apeleke!...

Kitu ambacho haukujua ni kuwa kikifika mikononi mwa Panga; wao watakuwa hawana thamani tena.

Hilo hakujua kamwe!
..

*****

ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.

Whatsapp 0658564341.
 
moneytalk

moneytalk

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
4,431
Points
2,000
Age
27
moneytalk

moneytalk

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2017
4,431 2,000
Jaman kudoo

Forum statistics

Threads 1,294,033
Members 497,789
Posts 31,162,957
Top