Kurunzi
Platinum Member
- Jul 31, 2009
- 10,175
- 11,571
Watu wawili wamefariki papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya huku nyumba kadhaa zikiharibiwa kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea kwenye banda la kuchomelea vyuma chakavu, Mtaa wa Magomeni, Wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, amethibitisha kuwa tukio hilo la kushtusha lilitokea Agosti 31 na Mlipuko huo unadaiwa kutokea baada ya mmoja wa waathirika kujaribu kukata kipande cha chuma, na kusababisha mlipuko uliokuwa na nguvu kubwa.
Kamanda Morcase amesema mbali na kusababisha vifo na majeraha, mlipuko huo pia umeharibu baadhi ya nyumba zilizokuwa karibu na eneo la tukio, na kusababisha hasara kubwa ya mali na pia imeleta taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ili kubaini chanzo kamili cha mlipuko huo.
Kamanda Morcase amesema kuwa taarifa kamili itatolewa hivi karibuni baada ya uchunguzi kukamilika.