Morogoro Road ___ Uswazi.Com
Bagamoyo Road ___ Ushuani.Com
Fursa Kibiashara ___ Morogoro Road
Maisha Tulivu na Uwekezaji ___ Bagamoyo Road
Kelele Nyingi ___ Morogoro Road
Utulivu kama Wodi ya Upasuaji wa MOYO ___ Bagamoyo Road
Nunua Eneo uje uliuze baada ya miaka mi 5 au ujenge frem za biashara/Nyumba za Biashara ___ MoroGoro Road
Nunua Eneo Uje uishi Baadae huku ukiwa na utulivu wa NAFSI ___ BAGAMOYO ROAD
Binafsi nimedokoa Kote na sababu nakwambia haya nilishawahi kuwa na eneo Mlandizi nilinunua 600k 2021 nmekuja Uza kwa 20m mwaka Jana 2025 (nlieka kajumba ka kulindia kiwanja tu room 3) eneo la heka 2 tu.
Nikatoa 10m ikabaki 10m nikanunua tena eneo huko huko Porini ndani ndani.
Sasa hivi eneo nililopo Heka ni 4m na mimi nlinunua kwa 1m (8 acre)
Bagamoyo Huku ndio Ntazeeekea na Kufia, na bei za Bagamoyo ni nzuri.
KWA BEI :
MOROGORO ROAD ___ BEI JUU
BAGAMOYO ROAD ___ BEI CHINI (na itakua chini zaidi ukiuziwa eneo na MZAWA sio haya makampuni) japo hata makampuni bei zao n rafiki sana ACRE 1 wanaanzia 1.5m mpk 2m na unalipa kwa instalment.
Kama pesa ipo usichukue sehem 1 Chukua POTE...
HATA 20 X 20 Morogoro road sio ndogo baadae ni pesaaaa (hakikisha umepoint pazuri pakujenga nyumba za biashara na frem sio sehem ya kujenga nyumba tu)
Ila ukienda Bagamoyo Road usijibane Kama unazomba Zomba maeneo makubwaaaaa...
Binafsi naogelea kwenye BONGE moja la PORI sijui hata ntafanyaje akili za Kufuga ndio zimekuja Juzi.
Yote kwa Yote...Popote Kambi Ardhi haimtupi Mtu
MUHIMU : NUNUA ENEO KWA MTU SAHIHI OTHERWISE UTAKUJA KUJUTA NA KUCHUKIA UWEKEZAJI ARDHINI.