Kuelekea 2025 Bado sijaona Watu wa kuandamana nchi hii hata wangechukuliwa wake zao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
25,245
60,446
Kwema Wakuu!

Sina uzoefu mkubwa wa mambo ya siasa za nchi hii. Lakini kwa akili zangu hizi ndogo nadiriki kusema kuwa kile alichotangaza Mhe. Mbowe kwamba wataandaa maandamano ya Amani januari 24 hayatafanyika.
Hayo mambo ya kusema sijui Bakabaka watafanya Usafi wala isije ikawa kisingizio.

Bakabaka hawajawahi kuwa tishio kwa Wananchi walioamua kudai haki zao za msingi. Narudia Bakabaka hawajawahi kuwa kizuizi kwa Watu walioamua kudai haki zao.

Kwa nchi yetu hatuna Watu wa aina hiyo. Na kama wapo basi kwenye laki yupo mmoja.
Nchi hii ingekuwa na Watu angalau elfu tano tuu wenye ile roho ya kudai na kupigania haki zao basi mambo mengi yangeenda. Lakini kwa bahati mbaya Watu hao hawapo.

Kwa nchi yetu hata Watu wachukuliwe Wake zao, nina uhakika hakuna wa kuandamana. Wataishia tuu kulalama chinichini. Kwani hata kupiga kelele hawana huo uwezo.

Elewa kuwa Watu wanaodai haki zao sifa yao kubwa hawaogopi Kifo. Hiyo ndio sifa yao namba moja. Na kama hawaogopi kifo maana yake hakuna wanachoogopa katika hii dunia.

Huwezi kudai haki ikiwa kuna kitu chenye thamani kuliko haki unayoidai. Huo ni ulaghai. Kujidanganya na kudanganya Watu.

Nawatakia jumapili njema.
 
Nawatakia jumapili njema
Upo sahihi MTIBELI
 
Mbona watu waliandamana kwa ajili ya NCCR, CUF na chadema ya Slaa ulikuwa hujazaliwa? Ni muda kamati za Chadema kuwaita wanachama hai kutimiza majukumu yao kwa chama na Nchi.
 
Wajinga au operatives drives za vyama vya siasa wameanza kuamka wengi wakitaka viongozi wa vyama na familia zao wawepo endapo kisago kitatokea.
 
Mbona watu waliandamana kwa ajili ya NCCR, CUF na chadema ya Slaa ulikuwa hujazaliwa? Ni muda kamati za Chadema kuwaita wanachama hai kutimiza majukumu yao kwa chama na Nchi.
Siasa za kweli zile. Watu walikuwa motivated na mapinduzi madogo ya kisiasa.

Sasa leo hii,unamsikia Mbowe anasema,Samia kachangia 150M .
Wiki ijayo anamnanga tena Mh. Raising.
Watu watakuelewa kwa hayo maandamano?
 
Upo sahihi hivi ndivyo Watanganyika tulivyo tengenezwa toka utawala wa kipumbavu wa Nyerere.

Nawaheshimu sana Wazanzibari katika kudai haki kidogo wao wana uhai licha ya kuteswa na kuuawa na askari wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom