Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 25,245
- 60,446
Kwema Wakuu!
Sina uzoefu mkubwa wa mambo ya siasa za nchi hii. Lakini kwa akili zangu hizi ndogo nadiriki kusema kuwa kile alichotangaza Mhe. Mbowe kwamba wataandaa maandamano ya Amani januari 24 hayatafanyika.
Hayo mambo ya kusema sijui Bakabaka watafanya Usafi wala isije ikawa kisingizio.
Bakabaka hawajawahi kuwa tishio kwa Wananchi walioamua kudai haki zao za msingi. Narudia Bakabaka hawajawahi kuwa kizuizi kwa Watu walioamua kudai haki zao.
Kwa nchi yetu hatuna Watu wa aina hiyo. Na kama wapo basi kwenye laki yupo mmoja.
Nchi hii ingekuwa na Watu angalau elfu tano tuu wenye ile roho ya kudai na kupigania haki zao basi mambo mengi yangeenda. Lakini kwa bahati mbaya Watu hao hawapo.
Kwa nchi yetu hata Watu wachukuliwe Wake zao, nina uhakika hakuna wa kuandamana. Wataishia tuu kulalama chinichini. Kwani hata kupiga kelele hawana huo uwezo.
Elewa kuwa Watu wanaodai haki zao sifa yao kubwa hawaogopi Kifo. Hiyo ndio sifa yao namba moja. Na kama hawaogopi kifo maana yake hakuna wanachoogopa katika hii dunia.
Huwezi kudai haki ikiwa kuna kitu chenye thamani kuliko haki unayoidai. Huo ni ulaghai. Kujidanganya na kudanganya Watu.
Nawatakia jumapili njema.