Bado nina mashaka kuhusu kitabu hiki cha Biblia

Amani ya Bwana iwe Nanyi!

Nimezaliwa katika familia ya kikatoriki nikitimiza yote mafundisho ya Imani &dhehebu langu kama ubatizo komnyo,kipaimara na Ndoa.

Pamoja na hayo yote nilitaka kujifunza zaidi kwann Kuna madhehebu mengi namna hii hasa haya ya kikristo?

Nimekutaka na viongozi wa madhehebu karibia yote ya kilokole na Kila mmoja ana lake na tafisir yake. Moja ya vitu nilivyo hitaji zaidi kujifunza ni pamoja unywaji wa pombe Kwa maana Imani yangu ya au dhehebu langu halina pingamizi kuhusu unywaji pombe "KUNYWA KIDOGO LAKINI USILEWE" ukienda Kwa walokole Wana sema dhambi kubwa mno kunywa pombe

Lakin ukiangalia badhi ya maandiko kwenye bible yana halalisha unywaji wa pombe. Naanza na[emoji116][emoji116]
Mithali 31:6-7 (KJV) Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Aya nyingine [emoji116][emoji116]
1 Timotheo 5:23 (KJV) Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.

Na inasemekana hata yesu alipo hudhuria harusi ya kana alibadiri maji kuwa divai(pombe) watu wakanywa waka lewa na wakashuhudia Kwa kusema hii ni nzuri kuliko zote. [emoji116][emoji116]

Yohana 2:9-10 (KJV) Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

Pamoja na ushahidi huu maandiko lkn Kwa walokole ni tofauti kabisa Bado wanasema ni dhambi Na Bado biblia yenyewe inajipinga yaani mara ikubali hapohapo ikatae mfano
[emoji116]

Mithali 20:1 (KJV) Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.

Soma tena [emoji116]
Mithali 23:29-32 (KJV) Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

Hizi ni baadhi tu ya Aya zinazo ruhusu na kupinga kunywa pombe.

Baada ya hapo nimejifumza na wasabato Kwa muda mrefu sana Hawa watu nikihoji Kwa undani sana kwann wao waabidi jmos

Walinieleza Kwa uzuri kabisa Kila swali nililo uliza walijibu ama Kwa hakika waliniweza. Mambo niliyojifunza kwao ni siku ya kuabudu ni ipi (siwezi elezea sana hapa)

Kwanini wao hawali nguruwe,Bata, nk. Majibu nilipewa yamikini Kwa mjibu wa bible niliridhika nayo! Nikarudi Kwa walokole na dhehebu langu kuwauliza viongozi wangu wa Imani kuhusu vyakula hasa nguruwe. Ukweli usiopingika nikuwa majibu niliyopewa na ndg zangu walokole na viongozi wangu wa dini hayakutoka kwenye biblia mara nyingi ilikuwa kupondea tu nikaona isiwe tabu sana Kwa maana hata Mimi ni muumini mzuriiii tu kitimoto Alimarufu mbuzi katoriki nikaendelea kula.

Issue nyingine nikuhusu dawa za miti shamba au tiba Asili walokole Kwa madhehebu Yao wanasema ni dhambi kubwa sana na ni uchawi na ushirikina kutumia hizo dawa ukiumwa nenda hospital

Wasabato nao (waliniuzia Hadi vitabu na nilivipenda na vinanisaidia sana )wao wanasema Mungu aliumba mimea Ili itumike kama chakula na dawa.

BADO SIJAIELEWA BIBLIA
Kwann biblia au wanao kiamaini hiki kitabu Cha biblia wanatofautiana Ili Hali kitabu Chao kimoja na maana Moja ?
Nani yupo sawa na nani hayupo sahihi?

Huyu anasema Pombe ni sahihi mwingine anasema Pombe Siyo sahihi na ni dhambi anatoa na maandiko!

Mwingine anasema nguruwe ni dhambi harusiwi na anatoa na uthibitisho wa maandiko na mwingine hivohivo anasema nguruwe ni halali na anatoa na uthibitisho pia.

Je, Mkweli ni yupi?
Wengine wanadai zaka walikuwa wanapewa walawi enzi za agano la kale je wasabato wao na zaka! Zaka na wao je nao ni walawi ?

Hii bible Ina mkanganyiko sana mara watu waoane dada na kaka halafu Tena hiyo hiyo bible ije ikatae na kuamru atakae muoa dada yake au ndg yake afe!

Hiyo hiyo biblia yetu imesema kuua ni dhambi na atakae ua atahesabiwa hukumu!!

Baada ya kutokuilewa Sasa Nina muda wa miaka6 siendi kanisani nimegundua Kuna ubabaishaji mkubwa sana huenda waandishi Hawa Kuna mwingine alikuwa mlevi anasapoti pombe mwingine alikuwa hatumii pombe na Kwa sababu yeye hatumii Kwa sababu zake binafsi Ima ki afya au Kwa kutokupendelea anaandika pombe ni dhambi vilevile kwenye nguruwe na vingine vingi.

Marafiki zangu wengi ni wasabato na wao ktk kipindi hiko chote Cha miaka6 nimewakataza habari za biblia nimewaambia kama una habar nzuri basi niuzie kitabu Cha afya nitanunua lakini sio habar za bible ambazo hata baba yangu wa kiroho (ubatizo) hazielewi hapana Kwa kwel.
Maandiko yamezuia ulevi hayajazuia pombe.

Sasa wewe jiulize akilini mwako kuwa, ukishakunywa pombe matokeo yako ni nini kama siyo kulewa.

Na kama matokeo yake ni kulewa ni bora usinywe kabisa.

Ndiyo maana madhehebu mengi yanazuia kunywa pombe kwa sababu ukishakunywa utalewa na ukishalewa ndiyo matendo ya kutompendeza Mungu huanza.
 
Kusoma Biblia ni jambo moja, na kuielewa ni jambo jingine. Interpretation of the scriptures ndiyo kitu ambacho huwa kinapelekea mtu awe na imani sahihi au imani potofu.

Kwa hiyo naweza kusema kuwa kinacholeta confusion kwako katika hili siyo Bibliia bali ni tafsiri za Biblia kutoka kwa watu wanaosoma Biblia
 
Mungu alipo sema usile nguruwe Kwa kuwa ni najinsi Kuna uelewa mwingine tofauti na kutokula?

Walokole wanapokula nguruwe huku wakihalalisha Kwa Aya kadhaa wa kadhaa kuwa karusiwa je nani mkweli?
 
Je wewe ni mtu wa mataifa(yani tofauti na taifa la Mungu) au wewe ni mmoja wa kabila 12 za Israel...

Kama wewe ni mtu wa mataifa(yani waliokuwa hawana Mungu au wanaabudu kisicho julikana):
  • Umeokolewa kutoka huko mwanzo ambapo hukuwa na Mungu. Mpaka leo watu wa Mataifa wanamjua Mungu kwa sababu hiyo.
  • Hapo mwanzo taifa la Mungu na watu wa Mataifa walikuwa hawachangamani(utengano) mfano Kutokuoana, Hivyo Yesu alitoa hicho kilichokuwa kinatutenganisha na hivyo kutufunya kuwa wamoja.
Soma waefeso 2 : 11 - 22.

Kama wewe ni mmoja wa wana wa Israel umeokolewa kutoka katika dhambi na Leo huna dhambi wala huwezi kutenda dhambi kwa sababu kilichokuwa kinakufanya utende dhambi kiondolewa.
Mathayo 26:28
kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

Cha kuongozea, hauhitaji kufanya mchango wowote ili uokolewe bali umeokolewa kwa Neema.(waefeso 2 :8-10)

Uliokolewa kwa sababu Mungu alikupenda hakutaka uangamie yani Ufe bali aliamua akupe uzima wa milele.
Yohana 3 : 16-17

Dhambi ndio ilisababisha wewe kuhitaji kuokolewa

Bila shaka nimejibu.

Kibwagizo:
Luka 18:16-17
Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao.
Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.

Kristo Yesu awe nawe.
Kwamba dhambi ilihitaji mimi kuokolewa , okay!! Hiyo dhambi mimi ndiyo niliyoileta hapa duniani au mimi ndiye niliyeitekeleza hapa duniani? Unajua mambo mengine huwa mnaongea kimhemko sana, na ndio maana mnatengeneza kizazi chenye wasomi wengi wajinga na wajanja wengi wapumbavu.
Haya mimi nawewe tujiulize haya maswali kwanini mungu haonekani?
Kwanini mungu hakujua kuwa kuna siku dhambi itakuepo? Kwann hakujua shetan angekuja kuwa msaliti wake? Au nayeye alikosea kusikiliza au kutekeleza masharti ya mkuu wake?
 
Mungu alipo sema usile nguruwe Kwa kuwa ni najinsi Kuna uelewa mwingine tofauti na kutokula?

Walokole wanapokula nguruwe huku wakihalalisha Kwa Aya kadhaa wa kadhaa kuwa karusiwa je nani mkweli?
WAZINZI WALIKUWA WANAPIGWA MAWE HADI KUFA. JE TUENDELEE KUWAPIGA MAWE HADI WANAKUFA?
 
Kama imeandikwa kwann wasipigwe mawe? Kwahiyo Mungu wa agano jpya na agano la kale ni MIUNGU mawili tofauti?

Jibu swali nguruwe ni halali au siyo halali
 
Rejea kwenye biblia inasema nini!??

Si kila mtu ni Mkristo dada maana ya neno Mkristo ni yule mtu anaemfata Kristo(yaani anaefata mafundisho ya mitume)

Ukristo ni kujikana nafsi hako,ukristo sio kufuata matakwa ya dini au ya kiongozi wa dhehebu,
 
Umeokolewa nini? Umeokolewa wapi? Kwanini uokolewe na nani alikuingiza huko mpaka uje uokolewe? Ninani aliesababisha wewe kuhitaji kuokolewa? Au yesu yupo kama wamarekani anakugonga kwanza vita anahakikisha njaa inawashika vyema then analeta misaaada anatangaza kuwa nimewaokoa, kwahyo yesu alituletea shetan duniani jamaa akatupaka madhambi weeee then yesu akashuka akampiga,sijui katupa silaha then kasema katuokoa, huyu yesu nimsanii sanii pia kama ni hivyo, kama utapinga hoja yangu utatuambia sasa, kwann atuokoe amekuokoa na nn amekuokolea wapi na kwann?
Tukimuelewa Mungu ni jambo kuu za zuri sana!,

Tumeokolewa kwa sababu tayari tulikuwa tumeshakosa mbele za Mungu baada ya kukataa kuisikiliza sauti yake, yaani tuliasi na hukumu ya muasi ni nini? Obviously ni KIFO yaani mauti.

Na tutambue Mungu wetu sio dictator au hajatutengeneza sisi mama ma robot yaani hatuna uchaguzi kwamba anavyosema yeye ndio hivyo hapana!!,

Mungu alituumba kwa sura na mfano wake maana yake sisi pia tunao uamuzi wa kumpoke Yesu ama kumkataa Yesu yote hayo ni juu yako na wala ukimkataa Yesu Mungu hatakufanya lolote ila utakapo kufa jua iko hukumu ya milele.

Na kumbuka pia kilichotufanya tuokolewe ni upendo wa Mungu kwetu sisi alitupenda PASIPO SABABU yoyote ile na mpaka sasa anatupenda na ndio maana hataki tupotee

Ni upendo ambao hana mwanadamu wala malaika ila Mungu Mwanadamu hawezi akapenda tu pasipo sababu yoyote. Na hata akafa kwa ajili yetu sisi maana hakuna mwanadamu anaeweza kufa kwa sababu ya mwenzie au hata taifa, hakuna mwanadamu anaweza kufa kwa sababu ya adui yake lakini Yesu alifanya hivyo kwa maana nyingine Yesu ni Mungu katika mwili kama ni msomaji wa Biblia ukisoma kitabu cha Isaya kimeelezea vizuro pia na wafilipi.

Na ndio mwanadamu pekee alieweza kuishi katika kati ya watenda dhambi na hakutenda dhambi yoyote mpaka anakufa just imagine!!,

Soma Yohana biblia yenyewe inashuhudia kabisa mpka mafarisayo.

Kwahiyo dhambi iliingia kupitia mtu mmoja yaani Adamu na tunapata ondoleo la dhambi kupitia mtu mkoja yaani YESU Kristo Hallelujah!,

Nafikili kuna kitu utakuwa unaanza kukipata. Na ntakupa sababu ya kwa nini tuliasi na chanzo ni nini??
 
Kama imeandikwa kwann wasipigwe mawe? Kwahiyo Mungu wa agano jpya na agano la kale ni MIUNGU mawili tofauti?

Jibu swali nguruwe ni halali au siyo halali
Hapana kwa sasa si kuwapiga mawe tuko kwenye agano jipya yaani NEEMA yaani maana ya neema ni upendeleo usiokuwa na sababu yoyote ni sawa na mwanafunzi wa mwisho apewe zawadi ya mwanafunzi wa kwanza maana yake hakustahili.

Sasa kwa nini hatuwapigii mawe?? Rejea pale Yohana 4 soma yote juu ya mwanamke yule mzinzi utaona mwisho anamwambia yule mwanamke aondoke amemsamehe na ASITENDE DHAMBI tena hivyo katika agano hili tumeambiwa kusamehe kabisa haijalishi mtu kakosa kias gani kazini au la!!, inabiDi kusamehe tena kwa moyo wote.

Na nguruwe ni halali kabisa kula soma 1 TIMOTHEO 4:1-6 utaelewa na soma Matendo ya mitume sura ya 10 yote utaelewa
 
Tumeokolewa na hukumu ya milele ni kama mfungwa anaetakiwa kunyongwa halafu akasamehewa maana yake huyo mtu kaokolewa na hukumu ya kifo!!,
 
Kuhusu pombe, ."...alikuja Yohana Hali Wala hanywi mkasema anapepo, alikuja mwana wa ADAMU anakula na kunywa mkasema mlafi na mlevi..."

KAZI KWAKO KUNYOA AU KUSUKA.
 
Kama imeandikwa kwann wasipigwe mawe? Kwahiyo Mungu wa agano jpya na agano la kale ni MIUNGU mawili tofauti?

Jibu swali nguruwe ni halali au siyo halali
HATUNA HAJA YA KUWA NA AGANO JIPYA NA HIVYO NGURUWE HATAKIWI KULIWA
 
Amani ya Bwana iwe Nanyi!

Nimezaliwa katika familia ya kikatoriki nikitimiza yote mafundisho ya Imani &dhehebu langu kama ubatizo komnyo,kipaimara na Ndoa.

Pamoja na hayo yote nilitaka kujifunza zaidi kwann Kuna madhehebu mengi namna hii hasa haya ya kikristo?

Nimekutaka na viongozi wa madhehebu karibia yote ya kilokole na Kila mmoja ana lake na tafisir yake. Moja ya vitu nilivyo hitaji zaidi kujifunza ni pamoja unywaji wa pombe Kwa maana Imani yangu ya au dhehebu langu halina pingamizi kuhusu unywaji pombe "KUNYWA KIDOGO LAKINI USILEWE" ukienda Kwa walokole Wana sema dhambi kubwa mno kunywa pombe

Lakin ukiangalia badhi ya maandiko kwenye bible yana halalisha unywaji wa pombe. Naanza na[emoji116][emoji116]
Mithali 31:6-7 (KJV) Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Aya nyingine [emoji116][emoji116]
1 Timotheo 5:23 (KJV) Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.

Na inasemekana hata yesu alipo hudhuria harusi ya kana alibadiri maji kuwa divai(pombe) watu wakanywa waka lewa na wakashuhudia Kwa kusema hii ni nzuri kuliko zote. [emoji116][emoji116]

Yohana 2:9-10 (KJV) Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

Pamoja na ushahidi huu maandiko lkn Kwa walokole ni tofauti kabisa Bado wanasema ni dhambi Na Bado biblia yenyewe inajipinga yaani mara ikubali hapohapo ikatae mfano
[emoji116]

Mithali 20:1 (KJV) Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.

Soma tena [emoji116]
Mithali 23:29-32 (KJV) Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

Hizi ni baadhi tu ya Aya zinazo ruhusu na kupinga kunywa pombe.

Baada ya hapo nimejifumza na wasabato Kwa muda mrefu sana Hawa watu nikihoji Kwa undani sana kwann wao waabidi jmos

Walinieleza Kwa uzuri kabisa Kila swali nililo uliza walijibu ama Kwa hakika waliniweza. Mambo niliyojifunza kwao ni siku ya kuabudu ni ipi (siwezi elezea sana hapa)

Kwanini wao hawali nguruwe,Bata, nk. Majibu nilipewa yamikini Kwa mjibu wa bible niliridhika nayo! Nikarudi Kwa walokole na dhehebu langu kuwauliza viongozi wangu wa Imani kuhusu vyakula hasa nguruwe. Ukweli usiopingika nikuwa majibu niliyopewa na ndg zangu walokole na viongozi wangu wa dini hayakutoka kwenye biblia mara nyingi ilikuwa kupondea tu nikaona isiwe tabu sana Kwa maana hata Mimi ni muumini mzuriiii tu kitimoto Alimarufu mbuzi katoriki nikaendelea kula.

Issue nyingine nikuhusu dawa za miti shamba au tiba Asili walokole Kwa madhehebu Yao wanasema ni dhambi kubwa sana na ni uchawi na ushirikina kutumia hizo dawa ukiumwa nenda hospital

Wasabato nao (waliniuzia Hadi vitabu na nilivipenda na vinanisaidia sana )wao wanasema Mungu aliumba mimea Ili itumike kama chakula na dawa.

BADO SIJAIELEWA BIBLIA
Kwann biblia au wanao kiamaini hiki kitabu Cha biblia wanatofautiana Ili Hali kitabu Chao kimoja na maana Moja ?
Nani yupo sawa na nani hayupo sahihi?

Huyu anasema Pombe ni sahihi mwingine anasema Pombe Siyo sahihi na ni dhambi anatoa na maandiko!

Mwingine anasema nguruwe ni dhambi harusiwi na anatoa na uthibitisho wa maandiko na mwingine hivohivo anasema nguruwe ni halali na anatoa na uthibitisho pia.

Je, Mkweli ni yupi?
Wengine wanadai zaka walikuwa wanapewa walawi enzi za agano la kale je wasabato wao na zaka! Zaka na wao je nao ni walawi ?

Hii bible Ina mkanganyiko sana mara watu waoane dada na kaka halafu Tena hiyo hiyo bible ije ikatae na kuamru atakae muoa dada yake au ndg yake afe!

Hiyo hiyo biblia yetu imesema kuua ni dhambi na atakae ua atahesabiwa hukumu!!

Baada ya kutokuilewa Sasa Nina muda wa miaka6 siendi kanisani nimegundua Kuna ubabaishaji mkubwa sana huenda waandishi Hawa Kuna mwingine alikuwa mlevi anasapoti pombe mwingine alikuwa hatumii pombe na Kwa sababu yeye hatumii Kwa sababu zake binafsi Ima ki afya au Kwa kutokupendelea anaandika pombe ni dhambi vilevile kwenye nguruwe na vingine vingi.

Marafiki zangu wengi ni wasabato na wao ktk kipindi hiko chote Cha miaka6 nimewakataza habari za biblia nimewaambia kama una habar nzuri basi niuzie kitabu Cha afya nitanunua lakini sio habar za bible ambazo hata baba yangu wa kiroho (ubatizo) hazielewi hapana Kwa kwel.
Wewe achana na mambo mengi just amini tu Mungu yupo na muabudu kupitia mtoto wake yesu kristo.ni kichaa tu asiyeamini uwepo wa Mungu.
 
Kuhusu pombe, ."...alikuja Yohana Hali Wala hanywi mkasema anapepo, alikuja mwana wa ADAMU anakula na kunywa mkasema mlafi na mlevi..."

KAZI KWAKO KUNYOA AU KUSUKA.
Kwahiyo yesu alikuwa anagonga castle lite kama kawaida
 
Hapana kwa sasa si kuwapiga mawe tuko kwenye agano jipya yaani NEEMA yaani maana ya neema ni upendeleo usiokuwa na sababu yoyote ni sawa na mwanafunzi wa mwisho apewe zawadi ya mwanafunzi wa kwanza maana yake hakustahili.

Sasa kwa nini hatuwapigii mawe?? Rejea pale Yohana 4 soma yote juu ya mwanamke yule mzinzi utaona mwisho anamwambia yule mwanamke aondoke amemsamehe na ASITENDE DHAMBI tena hivyo katika agano hili tumeambiwa kusamehe kabisa haijalishi mtu kakosa kias gani kazini au la!!, inabiDi kusamehe tena kwa moyo wote.

Na nguruwe ni halali kabisa kula soma 1 TIMOTHEO 4:1-6 utaelewa na soma Matendo ya mitume sura ya 10 yote utaelewa
Siyo kweli huo ni uelewa wako kuhusu kula nguruwe kwingine umejibu vyema!
Nguruwe atabaki kuwa najisi milele Kwa mujibu wa biblia japo Mimi natumia kulingana na Imani yangu ya Catholic

Hiyo unayozungumzia ya Petro haikumanisha kula hao wanyama na wadudu Bali Ali Manisha kuwa ameambiwa asiwaite watu wa mataifa kuwa najisi au wachafu

Matendo ya Mitume 10:27-28 (KJV) Na katika kusema naye akaingia ndani, akaona watu wengi wamekusanyika.
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.

Hiyo ndio maana halisi alivyoambiwa Petro na sivingine hivyo kama unakula kula kivyako kama Mimi hapa ila biblia ipo palepale nguruwe ni najisi
 
Back
Top Bottom