Agathadastorywriter
Member
- Nov 25, 2019
- 9
- 2
BADO NAKUPENDA SANA:08 aliendelea kupiga huku akinikera kwani ile simu yake ilipokua ikiingia niliisikia milio masikioni kwangu, lakini sikujali niliendelea kuongea na Hansy tena kwa amani zote kwani bwana yule alinichosha kipindi chote tulichokuwa pamoja, akifanya hili na mimi nafanya kile ili mradi tu na mimi nifurahi, baadae nilichoka nikabaki namuangalia tu nisijue chakufanya, nikawa ninaongea na simu nikiwaza kwamba nimfanye nini lakini na mbona nimemzuilia huduma simu anapiga Vipi, nikamwambia Hansy "Usijali Hansy, nimekusamehe ila subiri kidogo kuna jambo naliweka sawa alafu nakurudia tena" "Haina shida Ney, nasubiri. "Alijibu kiustaraabu lakini ustaaarabu wake haukunishtua sana kwani hata yule mwanaume wangu aliyekuwa akinitoa jasho, ukimuona mbona hakuna atakayekuamini Kama ni msumbufu na hakuna atakayekubali Kama anaongea maana amekaa kistaarabu mno Kama yule kijana aliyeamua kuongea na Mungu peke yake alafu baadae akanitafuta mimi ili tusaidiane maisha. Nikakata simu ya Hansy, ile nakagua simu yangu nikakutana na ujumbe "yaani tumezinguana kidogo tu tayari umepata mwaume mwingine alafu mimi unanidharau kweli Malaya ni Malaya tu, acha tabia za umalaya mwanamke wewe. " Hakuna maneno yaliniuma Kama Yale, yaani mwanaume wangu niliyekaa naye kwa mahusiano kwa muda mrefu japo tumekuwa tukigombana kwa mengi, kuna wakati nakosa lakini Naomba msamaha, anakosa lakini maisha yanaenda kwani hakuweza kuomba radhi katika maisha yake, leo ananiita MALAYA, CHOZI LA MWANAMKE NA MAISHA BILA WAZAZI sh 10000 kwa kila kitabu ila story yangu yoyote ile ni 3000 nakutumia watsup karbn