Bado nakupenda sana

Bado nakupenda sana

Joined
Nov 25, 2019
Posts
9
Reaction score
2
BADO NAKUPENDA SANA :06
anafanya mishe gani maana alikuwa hashauriki kifupi mtu wa kuchagua kazi,
Nilipokuwa sijamjibu alisema "mama, umeninunia mwanao, Nisamehe basi na wewe siunajua mimi nakupenda zingine mbwembwe tu. " "Sawa nimekusamehe usiku mwema. "Nilimjibu ili akate simu kwani nilihisi ananipigia kelele lakini kabla sijakata alisema "Mama mwanao mpaka sasa sijala na sijui ata nakula nini, nifanyie mchakato basi mama yangu nitakufa njaa kipenzi changu, najua huwezi kubali nilale njaa, nisaidie mke wangu. " Sikuelewa machozi yametoka wapi, nilijikuta nalia bila kutoa sauti na nikasema "hivi utabadilika lini, kwahiyo mimi ndiyo mama huruma siyo, yaani nilijuwa tu utanipigia kujifanya umekosa ili uombe pesa, kutwa ukiwa na wanawake zako unawatunza ila hapa ndiyo chuma ulete, mimi ndiyo ninasehemu nazichota nakupa uwapelekee, pesa zako aaaah Ney anazo hawezi Tumia ila zangu mimi ninayepata taabu hujui hata natoa wapi ndiyo tamu sana sasa leo utalala njaa. " niliongea na kukata simu, nilipokata tu alituma ujumbe uliosemeka "pleeeaseee baby, am really sorry nitumie basi. " alizidi nitia hasira nikawaza nifanye nini ikabidi nimpe block yaani nimfungie namba asinipate kwa wakati ule. Nilipokuwa nafanya hayo sikuwa nimewasha data, na nilijisemea "nilikosea mtajia namba nini mbona Hansy hapigi" nilijikuta natamani kuwasiliana na Hansy kwani mpenzi wangu mimi alikuwa kwikwi kavu, nilitamani ningechukua namba yake pia lakini ndiyo haikuwa tena hivyo nikawasha data.........
Screenshot_20191204-132724.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom