Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,796
- Thread starter
- #61
Asante sanaHili jibu lake ni rahisi sana,ukirejea katika maana ya Imani. Tamko Imani ni tamko lenye asili ya Kiarabu lenye maana ya kusadikisha jambo lililo fichikana kwa moyo na kulitamka kwa ulimi na kulitendea kazi jambo hilo. Ndiyo maana tunasema Imani haiwi bila matendo.
Sasa,swali lako kwanini tunaamini kitu tusichokiona kwa sababu kitu hicho kina ishara yaani kinawasilishwa na kinacho onekana au mfano wake. Mathalani leo hii hakuna anaepinga ya kuwa njaa inauma,ila haioni lakini tunahisi,hii huitwa ishara kwayo huielezea au huonyesha uwepo wa kitu hicho ambacho ni njaa.
Lakini,akili pekee haiwezi kuelezea mambo yaliyofichikana pasi na msaada wa ufunuo. Hapa ndipo kwenye mizani ya kupima ukweli na uongo wa imani fulani.
Nakomea hapa.