Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,843
Marehemu ni nani?
Marehemu ni mtu aliyekufa na asiyeweza kufufuka tena.
Je, marehemu ana kauli na utashi?
Laa! laa hasha! Marehemu hana kauli wala utashi wa yale yatokeyo baada ya kifo chake
Je, kifo ninini?
Kifo ni hali ya roho kutengena na mwili. Vitu hivi viwili ndio hutengeneza uhai na utambulisho, vikitengena hivi kila kimoja huenda njia yake. Utengano huo ndio tunaita kifo na kifo huleta ufu wa mfu ambaye ni marehemu.
Marehemu mfu hupewa majina tofauti kulingana na hadhi yake katika jamii inayomzunguka, majina hayo ni kama mwendazake au hayati au mtwaliwa!
Umauti ni hali ileile ya kufa ambayo huzaa neno kifo. Kifo ama umauti ni wa kimwili si wa kiroho! Roho haifi bali kifacho ni mwili uharibikao baada ya roho kutengana nao.
Maisha yako tangu kuzaliwa mpaka kufa, hutengeneza simulizi na kila simulizi moja huacha alama hasi au chanya. Alama unazoacha ndio hutengeneza kumbukizi za muda mfupi ama za muda mrefu lakini si za milele. Baada ya kifo cha mtu mwanadamu simulizi yake hufikia tamati na kitabu chake hufungwa.
Hakuna jipya tena! Kama marehemu mfu hayati mwendazake alipatia basi alipatia na kama alikosea baasi alikosea. Ama la kama alipatia na kukosea kwa asilimia zake, hakuna popote kifutio cha kufuta makosa yake ama mazuri yake! Hakuna popote tena penye fundi mahiri na vitendea kazi kamili vya kurekebisha ama kusahihisha mapungufu yake.
Kinachobaki ni simulizi katika mizania ya haki. Je, itaelemea wapi!? Huko itakapoelemea basi tambua ndipo ilipo 'legacy' yako! Hii haichakachuliki wala haipambiki. Ipo kama ilivyoundwa na mhusika katika maisha yake. Ikiwa ni almasi mchangani itang'aa tena bila hata mwanga kizani na ikiwa ni uzuri wa mkakasi bado itajidhihiri hata penye kiza totoro.
Hivyo basi tunaaswa tusiishi vivuli vya wafu. Wafu ni uvundo unukao sana hata ukiusiliba na mapambo vya thamani kubwa bado utabaki kuwa uvundo na utanuka tuu mpaka utakapooza na kupotea kabisa.
Tusiishi vivuli vya wafu kwakuwa havina sauti tena, na hata roho zao zikiwa na sauti bado hazina vivuli kwakuwa hazimo kwenye mwili jumba uliolala kwenye uharibifu.
Haukuongezei hata nukta ya hatua kwa kukivika mataji na kukiwashia taa zing'aazo sana kivuli kisichoonekana tena. Kisicho na sauti tena! Kisichosikika tena.
Hivyo basi simama sasa usonge mbele, ukitengeneza simulizi zako kwa kujifunza kutoka kwa waliokwisha lala moja kwa moja. Legacy yako iko mikononi mwako ni juu yako kuiunda utakavyo! Ya mwendazake ni yake ishakamilika. Usihangaike nayo. Hutaweza kuibadilisha na haitabadilika.