Bado, gharama za harusi jamani, tafadhali

Champaign jeshini zipo kwa shilingi elfu 4 na mia mbili tu kwa chupa moja. Tafuta mjeshi zama huko ibuka na chupa 10. Kinywaji mlipuko ukumbi mzima.
 
uwii nasoma kila kipengele. nacheka af naendelea tena kusoma! khaa! hamna hata kimoja cha bei hyo hapo. nkianza kukosoa ntakupa majaribu mwaya.jipige pige kwa harusi ya kawaida kabisa uwe na milioni 9
 
Wagalatia mna tabu sana, kwetu ni gharama ya pete, uturi, na sinia la pilau mke anaingia ndani...
Mnapenda ufahari mpaka mnakufuru..
Ndiyo maana ndoa zenu hazidumu

Tufurahi angalau, mambo ni mengi, hapa ninavyoandika nafahamu tupo na majadiliano pete iwe ya Tshs. ngapi, tatatata kweli ni kazi kubwa. Niombee tu nimalize maswala haya nianze maisha tofauti nisifikirie hili tena niangalie kitu kingine
 
uwii nasoma kila kipengele. nacheka af naendelea tena kusoma! khaa! hamna hata kimoja cha bei hyo hapo. nkianza kukosoa ntakupa majaribu mwaya.jipige pige kwa harusi ya kawaida kabisa uwe na milioni 9

Siyo kweli mkuu, hamna hata kimoja ni asilimia 100 umetaja. Kimoja niseme mimi price list ya kumbi pale sabasaba maonesho kuna ukumbi unaitwa Kobe umetajwa kuwa na uwezo wa kuchukua watu 300 kwa mara moja kwa bei niliyotaja, ni vema ungetaja kimoja hadi kingine. Mengine nilishayaelezea wakati tunajadili na wengine unaweza pitia uwe na hayo pia.
 
Champaign jeshini zipo kwa shilingi elfu 4 na mia mbili tu kwa chupa moja. Tafuta mjeshi zama huko ibuka na chupa 10. Kinywaji mlipuko ukumbi mzima.

Ni kweli hili? nina rafiki mmoja yupo huko.
 
+800,000 tshs fedha ya kwenda mapumziko muda wa wik 1 had 2, +500,000 fedha ya kuandaa kad za mwaliko, walinz na kamati
 
We hii harusi ya wapi. Sahani ya 7,000 ina chakula gani. Hiyo suti ya 150 000 ya aina gani? Ya kuzikia au? Suti ya kimaskini ya harusi inaanzia 500,000. Gauni la bi harusi la kukodi 300,000. Halafu hayo mapambo ya 250 000 ni ya aina gani? Fresh roses zipo au ni toilet papers. Ukumbi wa size gani? Hiyo bajeti sijui ya mkoa gani. Hapa town huoi jombaa. Hata sherehe ya comunyo hutaitendea haki.
 
Mi nakushauri hizo suti za watoto wasimamizi toa ubaki na mmoja na hapo ukienda kariakoo unapata kwa bei yako hiyo ya 25000.
 
shida ya nn kaka si upige kitu cha ndoa ya mkeka tuu au kama unaona noma sana tumia style ya BOKO HARAM... maisha yenyewe haya yanabana mbaya.

ni aibu unafunga harusi ukiwa nyumba ya kupanga hata vyumba viwili huna halafu ghalama kubwa hivi anyway Fanya UK IFA maskini haohao uliokuwa nao kwenye harusi ndio wa kwanza kusema
 
umemwambia vizuri sana ili hela zingine aanzie maisha ukipata mwanamke anataka harusi za kifahari huwa hazidumu Mara nyingi ikidumu matatizo mengi ndani yake
 
Uislam unakataza hivo vitu Vyote ulivo Orodhesha hakuna karibu katika uislam ndugu yangu

mdogo Wang ilibidi abadili dini sababu ya haya maghalama makubwa mno hela tulizomchangia zilimsaidia akaanza kujenga na saizi yupo kwake nawapenda sana waislamu hawana bwembwe kama hizi
 
Nenda kwa mkuu wa wilaya funga ya kiserikali. Gharama 0 kwani unaenda na nguo yako safi usafiri wa kawaida mashahidi 2 tu.
 
Nenda kwa mkuu wa wilaya funga ya kiserikali. Gharama 0 kwani unaenda na nguo yako safi usafiri wa kawaida mashahidi 2 tu.

Mkuu, hapo kabla nilishaongea mpaka na DAS kunipa ushauri wa namna ya kufanya hilo, tatizo ikawa ni ushirikiano kutoka upande wa pili, umekuwa ni wenyewe kabisa, wacha nipambane tu ndugu yangu.
 
mdogo Wang ilibidi abadili dini sababu ya haya maghalama makubwa mno hela tulizomchangia zilimsaidia akaanza kujenga na saizi yupo kwake nawapenda sana waislamu hawana bwembwe kama hizi

Ki ukweli, unaahirisha mambo mengi sana ikiwemo mawazo pia. Anyway, naingoja siku nimalize nianze sifuri kabisa, Mungu atanisaidia tu.
 
ni aibu unafunga harusi ukiwa nyumba ya kupanga hata vyumba viwili huna halafu ghalama kubwa hivi anyway Fanya UK IFA maskini haohao uliokuwa nao kwenye harusi ndio wa kwanza kusema

Ni kweli kiongozi, kwa sasa nimeshakwenda mbali kidogo, wacha nifanye tu, nafahamu nitaanza sifuri, nitakuja moja nitaenda mbili nitafika mbali, Mungu anisaidie anipe uzima tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…