Badili mtazamo wako kuhusu mwanamke

Badili mtazamo wako kuhusu mwanamke

hapa kuna mdada anawindwa hapa hizo pm sijui tu. mada kama hizi huletwa ka kandoano hivi. ha ha haaa natania tu

Kuna ka damn anamtafuta huku so anapiga kampeni kwa kuwa ni msimu wa kampeni, utakuja kuniambia.

25 oct chukua weka Lowassa

cc: Bujibuji

Hii mada ingekuwa imewaponda wanawake au kuelezea mabaya ya wanawake nadhani hizi comment zingegeuka, jamani basi mara mojamoja muwe mnayaona na mazuri yetu.
 
Last edited by a moderator:
Huwez muelewa mwanamke mapaka unaingia kaburin ... Andika mwanamke kwenye vumbi halafu futa huyo ndiyo mwanamke
 
wanawake wenyewe hawa alosema Paul kuwa wasihudumu madhabauni au kuna wengine, yule mama wa kisabato alikosea sana Mungu amsamehe tu
 
wanawake wenyewe hawa alosema Paul kuwa wasihudumu madhabauni au kuna wengine, yule mama wa kisabato alikosea sana Mungu amsamehe tu

Hivi wewe wanawake walikufanya nini? Mbona hakuna la positive unaloongeaga kuwahusu?
 
Hivi wewe wanawake walikufanya nini? Mbona hakuna la positive unaloongeaga kuwahusu?

ishu ni jinsi mnavyotaka kuwa sawa na wanaume, mnashindwa kuelewa japo mnakesha makanisani, unamjua Hellen G White? ndo alosababisha yote haya
 
ishu ni jinsi mnavyotaka kuwa sawa na wanaume, mnashindwa kuelewa japo mnakesha makanisani, unamjua Hellen G White? ndo alosababisha yote haya

Kwahiyo Helen g white alisema tuwe sawa na nyie? Huko ni kujistukia tu maana mwanaume atabaki kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke tu!! Tatizo liko kwenu msitafute mchawi, kwani imekuwaje hadi wanawake watake kuwa sawa nanyi? The answer is mmepoteza nguvu na hadhi ya kiume so hatuna jinsi we have to take over kuokoa angalau familia zetu.
 
siwezi kubishana na wewe dada, haya mambo yapo kiroho sana na kila unachokiona ni mpango ulipangwa zamani tu, pengine hujui hata kwanini hata wanawake waliruhusiwa kuhudumia madhabauni wakati ilikatazwa, wewe kama unachukulia kidunia kama unavyisema hapo, basi haina shida, siku ukifanikiwa kujua siri hiyo utaelewa
 
Anyway i wanted to go deep into this ila nikaona nitaanzisha mjadala mpya wa kiimani, ila yo soooo wrong msome upya Hellen White na maandiko matakatifu then ujiondoe kwenye box uruhusu ubongo wako kudigest then utaelewa sana.
 
wala haina haja, vitu vidogo hivyo, mwenye masikio na asikie
 
BADO NAMTETEA MWANAMKE

Bado niko Dodoma, ni bahati nzuri kwamba mchana huu tumekuwa na mjadala kuhusu mwanamke. Bado kuna watu hawamwelewi mwanamke, bado wanamshusha, wanamchukulia tu kama kiumbe fulani hivi.

Nilishasema na nasema tena, unaweza kumshusha, kumdharau na kumtweza mwanamke kwa kadri uwezavyo, lakini kama unafanya hivyo fanya hivyo katika mwili, kwa namna unavyomtaza kwa macho yako hayo ya damu na nyama.....!
Lakini, linapokuja suala la kiroho, kwenye ulimwengu wa roho (ambao una nguvu kuliko ule wa mwili) mwanamke ni habari ingine, mwanamke ni zaidi ya vile ulivyofundishwa na kusimuliwa habari zake na jamii yako.

Nimemsoma mwanamke , namheshimu mwanamke, kwenye ulimwengu wa roho, mwanamke amempita mwanaume maeneo mengi sana. Badili mtazamo wako kuhusu mwanamke.

Badala useme ni nini ulichojifunza we umeishia kutoa angalizo tu!
 
(mungu alisema tuishi nao kwa akili) ni wajanja sana hasa kwenye kutunza siri hawajambo haki ya mungu usitake mechi na wao lazima wakushinde tuu hasa kuchapwa nje. we muheshimu usijikute unajua kufatilia sana. nasema hivi maana imewahi nitokea na pia kuna manzi wa mtu na mla na anasema hana mtu ana namba 3za simu wakati wa usiku hapatikan. mchana anapatikana nishamsoma na jamaa wake namjua huwa wanagombana kila siku. ila sabab jamaa namjua kwa kumheshimu nikaamua kujinasua hapo. inshort wanawake ni wauaji tambua hawalazimishwi na wakipenda wamependa kweli amini hivi hata uwe na ngoma kama alikupenda atakupenda hadi anaingia kaburiuni.
ila kwa uchunguzi ni hatari mno hawa wanafaa kuwa C.I.A nataman sana wawe wanatumika kwenye uchunguz. hasa kwa wanaume maana sisi ni dhaifu kwao. wao kwa wao wanajuana. huwa napenda sana mechi zao hasa wanapogombana. ni wavumilivu sana pia hawapendi kuwa na mashaka moyoni pamoja na uvumilivu wao ukiwaboa tuu au akifanya kitu gani kibaya au kufeli mtihani watatafuta faraja yoyote ili mradi awe na amani hata kumwbato ili kupunguza maumivu na ndo maana hawafi mapema katika familia nying wababa ndo wanatangulia. stress zinaua wanaume kwan hawaju namna ya kuzitoa au kuzipunguza. wanawake wanapendelea sana wawe na amani moyoni.
kwa kweli hivi viumbe ni hatari sana.
but i will hit one of chick na hasira sana coz hii ni battle na sitakubali nishindwe lazma damu imwagike au nimtie jeraha ambalo hatalisahau maisha yake. maana hakuna namna sasa.
kwan nini tutawaliwe indirect na hivi viumbe? kwan tukijifunza vitu ambayo wanavifanya hatuwez???
 
Kuna wakati humu nilipata kuzungumza na wajumbe wawili watatu humu kwa faragha, nafikiri maudhui ya mashiriki yangu kwa wao hapa yana msaada-- nitadodosa kidogo tu, zaidi fuata kiungo husika ili kuifikia akaivu yangu ya vidokezo facebook...

++++

Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi seh. I

5 Septemba 2011 saa 12:15 asubuhi
Kutoka: Mwongozo Hai kuelekea Uhuru Halisi

(Iliandikwa kwa rafiki kama mchango wa mawazo na kwa uchochezi wa fikra)

Pendo lililobarikiwa dada MwKT,

Siku kadhaa nyuma ulileta habari jukwaani juu ya ‘Kuanzishwa kwa "un-women" – kaeni mkao wa kula' katika jukwaa la siasa.

Nilipendezwa na habari hii na hasa kwa kuzingatia mapenzi yangu juu ya mabadiliko yenye kuleta kheri katika jamii niishiyo na ulimwengu kwa ujumla. Ni jambo lenye kupendeza kutambua harakati za watu mbali mbali na kujaribu kuunganisha maono ama kufanya fikra tunduizi.

Amko la wanaharakati katika kutunga na kupelekea taasisi kama chombo chenye kuongezea kwenye ushawishi, utendaji chini ya mamlaka, mifumo na utekelezaji wa mipango ama maelekezo; linavutia wote walio na dalili za kuamkia huko kimwelekeo wa fikra na imani lakini pia zaweza kuvuta ukosoaji wa kiudhanifu-yaani juu ya dhahania ya mpango mzima vile kusema, filosofia ama asili ya mwongozo wake na misingi ya ustawishi wa jitihada.

Kwanza kabisa nitambue ‘unene' na uzito wa michakato uliopo katika vyombo vya kimataifa na utengeneaji wake. Itifaki zake ni namna ya mifano yenye kufafanua mifumo na taratibu katika kuratibu matukio kulingana na makutano ya watu na michakato. Na hivi nitambue msuko wa chombo kama namna ya mipaka na mamlaka juu ya mambo yake na tena kwa muktadha wa kufanyika kwake.

Ujio wa chombo hichi kwako umekusukuma kupenda kuwaatarifu wanajamii wenzako; maana yake: uwezekano wa fursa mbali mbali--ajira, na mipango ya maendeleo. Na vile vile umepata kusema : hivyo havitaweza kuja kwenye sahani ya dhahabu… Kisha ukazungumza juu ya ‘nafasi za juu'… Halafu ukataja mjumuisho wa mataifa na hivi kuonesha kutambua msukumo wa nguvu ya uwezo na ushawishi kulingana na sehemu watu watokayo kmf Amerika ya Kati, Scandinavia na nchi nyingine za Afrika katika ugombeaji wa nafasi za kazi na labda vile vile kumaanisha vyeo vya usimamizi na utendaji pia.

Pia ukazungumza dokezo la kukabiliana na adha ya shughuli kwa kutaja umuhimu wa watarajiaji nafasi kudumu kukesha katika jitihada kwa kufuatilia kwa makini nyenendo za michakato ya uanzilishi.

Nikushukuru kwa angalizo na kushiriki habari na wenzako kama mimi na wengine.

Niliingie neno la leo kwa kutanabaisha jambo kuhusu ulimwengu wa kuona mambo kwa kiini cha usababishaji na matokeo yake.

Tumezoea kuona mipango ikipangwa na jitihada kusukwa na matokeo kuainishwa ili kuelekeza sura ya utendaji na utekelezaji. Binadamu toka zamani hadi hii leo tunaona upangiliaji wa mambo ni kama sanaa inayoweza kufanywa kamilifu ijapokuwa matokeo yake si kwamba daima huwa ni hivyo. Kuna vitu vinaweza kupangilika lakini mara kadha wa kadha mashauri juu ya watu ama jamii si yenye kupangilika na kujitosheleza bila mikingamo ama kadhia ya namna fulani kujitokeza. Labda hii tuseme inatokana na ukweli kwamba binadamu ni kiumbe chenye uwezekano wa fikra binafsi na utashi na hivyo haiwezekana kuwakundisha watu pasipo ridhaa na makubaliano na wao wenyewe kwa wakati.

Basi katika ulimwengu wa makubaliano kuna yale ya juu juu na kuna yale ya ndani. Vivyo hivo kuna kuona mambo kwa sura ya juu juu na kuona mambo katika sura ndani. Naam, vile vile kuchukulia jambo kwa sura ya nje na kuchukulia mambo kwa sura ya ndani. Uhusiano wa mambo ya ndani na yale ya nje ndiyo hujaa kuzaa uthabiti wa makubaliano na labda pia kusema, umadhubuti wa jitihada kulingana ufananikaji wa dhamira. Hata hivyo, kupo kuridhika na mambo ya nje bila kuchunguza misingi yake; na hata tena kwa namna kama hiyo; kutotambua athari za matokeo kwa kutozingatia uasili wa jambo lenyewe kwa uzima wake. Haya mawili hujitokeza hasa katika maisha ya mwanadamu kwa kutoangalia/ujisahau wake wa mashauri yaandamayo dhamira zake kwa wakati hadi wakati.

Na hivi leo ningependa kuzungumzia nafasi ya Tekinokrasia katika ustawi mpya kwa wanadamu katika zama hii mpya.

Nimechagua mchango wako toka jukwaani kujenga usuli wa shauri langu la leo kwako na kwa wadau wengine; kwa kuwa wanawake katika zama hii wanachukua sura takatifu ya michakato ya jamii na ustawi. Na hivi udadavuaji wa utata wa hali ya ustawi wa jamii unachipukia na kuanza kwa kumuelewa mwanamke na sifa ya kike ya uumbaji wote--jambo lililosahaulika katika nidhamu na uelewa wa wanadamu wa leo.

Katika hali ya juu juu shauri lako juu ya uanzishwaji wa baraza la wanawake-umoja wa mataifa, umelenga hasa fursa za ajira na labda kwa upande mwingine usiowazi ni shauku yako ya chombo hiki cha wanawake na kwa ajili ya wanawake. Kuangalia upande wa ajira-- na hapa umewakumbusha hata wanaume pia kutazamia nafasi; kulinikumbusha mashauri juu ya uchumi na siasa-na miye nikapata hamu nije kushiriki na wewe na wengine fikra tunduizi mintarafu vyombo vya jamii na nafasi yake katika kuchochea ama kuleta mabadiliko.
....

https://www.facebook.com/notes/10150299946054421/

++++

Haya mawaidha yanaweza kusaidia na mengine ya kuingiliana:

Kutoka: Mwongozo hai kuelekea Uhuru Halisi seh. IV

5 Septemba 2011 saa 12:25 asubuhi
Husimulika kwenye simulizi la 'mwanzo' jinsi mwanamke alivyodanganyika na 'nyoka'... Husemwa katika kisa: nyoka alimfuata mwanamke akamwambia: eti, umeambiwa usile matunda ya 'mti wa katikati'? Naye mwanamke kwa haiba yake yake ya kitoto kuhakiki hivyo na kubayanisha zaidi angalizo la ada ya 'mauti' itakayojiri endapo watakula. Lakini nyoka akamwambia kama vile kusema--kula tunda kutawapa ujuzi wa mema na mabaya na wao watakuwa kama mungu na hilo ndiyo wamezugwa... Naye mwanamke akaja kuyaona matunda ya mti wa katikati ni yenye kufurahisha na kupendeza 'machoni' akayachuma na kuyala na kumpa na mwenzie mwanaume wakala wote... Ndipo ghafla wote wakajishtukia wapo uchi... wakaona aibu.

Kisa cha mwanamke ni kielelezo cha ukweli mmoja kuhusu fahamu za mwanadamu. Wanawake wako karibu sana na maumbile yao kuliko jinsi walivyo wanaume. Na hivi wanawake pia wapo karibu na mazingira na kuvutika kupendezwa na faraja zake. Na ndivyo hivyo hivyo wanawake wamefanyika juu ya miili yao; mwanaume ni mtu ambaye jinsi ya kwanza ya 'kumjua' mwanamke ni kwa misukumo ya udadisi. Mfanyiko wa mwanamke kimaumbile huzidi mashauri yake yote yenye jinsi ya 'unyoofu' ulio ni kawaida ya nidhamu yake kiakili. Mwili wa mwanamke hujibainisha na ule wa kiume kwa maumbo yake yenye mviringo, na hali mwanaume ni mwenye maumbo nyoofu. Amkaribiapo mwanamke, mwaume udadisi wake huweza kuchukua sura ya kugusa na kupapasa kwa kuwa jinsi hivyo hutafuta kuaarifika na 'siri' za umbo la mwanamke... Lakini mwanawake wanajinsi tofauti ya akili ifanyavyokazi inayojitofautisha na jinsi ya kiume. Wanawake ni watu saikolojia ya undani kwa kuanzia; na wanaweza kubakia hivyo maisha yao yote. Mwanamke asiyejua mume toka kuzaliwa kwa mfano, ikiwa hataingiliwa na misukumo ya milazimisho toka nje anaweza kubaki ni bikira maisha yake yote na wale yeye asione ajabu. Kwa kuwa wanawake ni wenye kujifurahisha mawazo na ndoto zao za ndani na hata kuzimwagilia na kustahimilisha ndani ya tumbo hilo hilo la ndoto. Ndoto za mwanamke zisipoingiliwa na kukatishwa zinaweza kubakia ni uwezekano tu. Na ndivyo ndoto za mwanamke 'hukamilishwa' na 'nia' kutoka nje ili zijekuzaa matunda. Ni kama vile katika simulizi ya kisa cha Binti mfalme aliyelala usingizi kusubiri busu la mwanamfalme ili aaamke na kufanya harusi yenye mwanzo wa furaha ya milele kufuatia. Na ndivyo wanaume hufanyika kwa saikolojia ya nje ambayo ndiyo hasa hudhahirisha 'nia';-- ya kupanda vilima na kushuka mabonde, kukata vichaka na kutandua bui bui walioizunguka kasri; kuingia ndani na kumkuta binti mfalme mzuri aliyelala usingizi; kumbusu na nakujikuta ndiyo kamwamsha.

.....

https://www.facebook.com/notes/10150299967634421/

++++

Women and the 21st Century
That is nice dear sister.

immortalize women... Well, in this 21st century you women will do wonders of restoring and healing this world...

The more we men are going to be truly dignified, we are going to leave governance to women by two thirds of governmental key positions and organs... We ought to reside in Educational streams and direct involvement in technologies and works to enhance human shelter and prosperity.

If fact 'partial' immortality of man is through grace of the womb of woman. We are going to honor the new born--for through them we will hope and fathom for the brighter future and assurance of new vehicle of souls' expressions... and you will forget about the veils of weddings--for celebrating life is giving thanks and cherishing women's fertility and spirit...

In this 21st century Men we shall be the light and you are going to be the instrument of the Holy Breath of the whole life... And this is how life is meant--with this right understanding new values, new ideals and new institutions are going to be enshrined then we will learn how to Praise the spirit of all life.

For God touches us through the hands of a woman... Illuminates us through the mind/ideal and eye of a man .

***

Sure... and just now I was going through that part in which you were asked about 'reincarnation' in igbo society--do you know that this is going to be proven as a fact and that so much will be discovered some years to come?

It is going to be one of the most significant clinches in social engineering and the world culture and I was happy when I found out some African tribes dig this... My late grandmother used to say I look so familiar -- resemble someone she had known and he was deceased long ago before I was born... She even started to call me by his name... And that is my other name--'Magawa', the giver...

Source: http://www.facebook.com/photo.php?fbid=4215023826134&set=a.1565878479156.77455.1601221845&type=1

++++
 
Nikuulize je YESU wakat anawaambia watu juu ya kifo na ufufuo wake aliwaambia wanawake pekee au la? Kama ni wote kwanini mwanamke ndie alikuwa wa kwanza kwenda kaburin na kufanikiwa kujua kuwa YESU AMEFUFUKA? Je wanaume walikuwa wapi? Kama sio walikuwa wanahangaika na utaftaj rizk za kiduniani! Hivo mwanamke anaweza kuwa mzuri sana kwa mume au mtu yoyote afanyae mazuri, vivo hvo atakuwa mbaya sana kwa mume au mtu afanyae mabaya! mean katika ndoa/uhusiano, maisha ukionesha mambo mabaya ye atakuwa mbaya zaidi na ukiwa mzuri atakuwa mzuri zaidi! Hii ni kwasababu mwanamke tangu mwanzo adi sasa ndie anae shika na kutenda kwa kadri ya biblia inenavo na ndio maana akapewa uwezo wa akili kali sana na MUNGU,,,

SASA we kazana kumuandalia mabaya mwanamke huku MUNGU nae anampa mbinu kali zaidi! Na si kwamba ni upendeleo la hasha tatizo same guyz wanapenda wafanye visasi wao wakati atoae NA apangae ni MUNGU!
Kuwa mpole ishi Mungu atakavyo na si binadamu watakavyo utawapenda wanawake na kuwafurahia kama wanaume wengne wanavowafurahia.
(mungu alisema tuishi nao kwa akili) ni wajanja sana hasa kwenye kutunza siri hawajambo haki ya mungu usitake mechi na wao lazima wakushinde tuu hasa kuchapwa nje. we muheshimu usijikute unajua kufatilia sana. nasema hivi maana imewahi nitokea na pia kuna manzi wa mtu na mla na anasema hana mtu ana namba 3za simu wakati wa usiku hapatikan. mchana anapatikana nishamsoma na jamaa wake namjua huwa wanagombana kila siku. ila sabab jamaa namjua kwa kumheshimu nikaamua kujinasua hapo. inshort wanawake ni wauaji tambua hawalazimishwi na wakipenda wamependa kweli amini hivi hata uwe na ngoma kama alikupenda atakupenda hadi anaingia kaburiuni.
ila kwa uchunguzi ni hatari mno hawa wanafaa kuwa C.I.A nataman sana wawe wanatumika kwenye uchunguz. hasa kwa wanaume maana sisi ni dhaifu kwao. wao kwa wao wanajuana. huwa napenda sana mechi zao hasa wanapogombana. ni wavumilivu sana pia hawapendi kuwa na mashaka moyoni pamoja na uvumilivu wao ukiwaboa tuu au akifanya kitu gani kibaya au kufeli mtihani watatafuta faraja yoyote ili mradi awe na amani hata kumwbato ili kupunguza maumivu na ndo maana hawafi mapema katika familia nying wababa ndo wanatangulia. stress zinaua wanaume kwan hawaju namna ya kuzitoa au kuzipunguza. wanawake wanapendelea sana wawe na amani moyoni.
kwa kweli hivi viumbe ni hatari sana.
but i will hit one of chick na hasira sana coz hii ni battle na sitakubali nishindwe lazma damu imwagike au nimtie jeraha ambalo hatalisahau maisha yake. maana hakuna namna sasa.
kwan nini tutawaliwe indirect na hivi viumbe? kwan tukijifunza vitu ambayo wanavifanya hatuwez???
 
Mwanamke ana akili saana..kubembeleza umbembeleze then haitoshi umpe pesa. Haitoshi tena anahaki ya kusema haitoshi. Kazi kweli kweli
 
Kuna wakati humu nilipata kuzungumza na wajumbe wawili watatu humu kwa faragha, nafikiri maudhui ya mashiriki yangu kwa wao hapa yana msaada-- nitadodosa kidogo tu, zaidi fuata kiungo husika ili kuifikia akaivu yangu ya vidokezo facebook...

++++

++++
Nimekupigia saluti
 
Back
Top Bottom