Badala ya kujikita kuilaumu Kauli ya Rais Dkt. JPM tufanye haya....

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
37,004
2,000
1.Tuache kuwa Wanafiki

2.NGO’s zisitumie udhaifu wa Watanzania wengi kujineemesha

3.Wazazi tutekeleze majukumu yetu kiukamilifu

4.Tujikite kuwapa Elimu ya Uzazi Watoto ( Mabinti ) zetu

5.Maudhui mengi yasiyo ya Kimaadili hasa kwa Vijana na Mabinti zetu yadhibitiwe

6.Wazazi waache kuwafanya Watoto ( Mabinti ) zao mitaji yao ya kujipatia Mali

7.Jamii ielimishwe sana kuhusu madhara makubwa ya Utandawazi

Binafsi naungana kwa 100% kwa Kauli ya Kimamlaka na ya Kishujaa kabisa aliyoisema Mheshimiwa Rais wa JMT Dkt. John Pombe Joseph Magufuli jana huko Chalinze juu ya kuzuia na kukataa Wanafunzi wa Kike wanaopata Ujauzito wakiwa Shuleni.

Inahitaji umakini mkubwa sana na uwezo mkubwa wa Kutafakari kuweza kumwelewe Mpendwa Rais Dkt. Magufuli juu ya Kauli zake ambazo wengi wetu ‘ hukurupuka ‘ tu na kudhani kuwa ni ‘ dhaifu ‘ au ni ‘ mkatili ‘ au ana roho mbaya.

Namwelewa sana Rais Dkt. Magufuli na kamwe sijutii kumpa Kura yangu ya Kutukuka mwaka 2015 na narudia tena kusema kwa Kujiamini kabisa kuwa kwa muda mrefu sana baada ya Hayati Baba wa Taifa kung’atuka Madarakani sasa Tanzania imempata Rais ambaye pengine ilimuhitaji tokea mwaka 1985 kama siyo mwaka 1995 au 2005.

Kila la kheri Mheshimiwa Rais wangu mpendwa JPM na chapa kazi kwani tunakuamini, tutakuombea na tunakupenda mno.

Nawasilisha.

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,657
2,000
Chakufanya ni kwamba WAZIRI USIKA ajivue uwaziri tu kashindwa kazi

Swissme
 
Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,706
2,000
Mimi na naunga mkono hoja itakuwaje hawa wana watoto nyumbani si watawafundisha na wengine na kuonekana jambo la kawaida tu kubeba mimba ukiwa shuleni si shule zitakuwa za wazazi tu cha msingi wazazi angalieni watoto wenu kasi ya mimba kwa mabinti imekuwa kubwa tofauti na miaka ya 78 mpaka 95 sasa hv ni janga
 
johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
611
500
Mkuu.
Ingawa mengine nimekuwa na mtazamo tofauti juu ya Rais wetu lakini Kwa hili ni nimekaa kimya tangu jana nikiangalia mchango mbali mbali ila binafsi nami sina budi kuunga mkono uamuzi huu.
Naelewa katika jamii yetu hivi sasa mtu ukisimama kuongea maneno kama hayo ya jana ya MAGUFULI ni wachache watamwelewa.
Tuko katika Zama ambazo sisi hatuwezi wenyewe kuchagua jema au baya, isipokuwa miongozo iliyotoka new York au London.
Tuko Na kizazi ambacho mzazi anafurahia mafanikio ya ghafla ya mtoto wake bila kuhoji.
Tuko katika Zama ambapo wazazi wamebinafsisha mujukumu yao Kwa watu wengine, ndio maana unasikia kelelel nyingi za kupinga hoja hii.
Jana nimesikia takwimu zilizotolewa BBC kuwa kiasi cha wasichnana elfu nane hukatiza masomo kila mwaka nchini Tanzania Kwa kupata mimba.
Ni kweli kuna tatizo lakini hatuwezi kurekebisha tatizo Kwa kuongeza tatizo.
Hawa ambao leo wanatuhimiza hao waliojifungua warudi shuleni, kesho watakuja na hoja nyingine ya kuhalalisha utoaji mimba Kwa kigezo kuwa nayo ni Haki yao!
Kudai kuwa wasichana hao wana Haki huku tukiondoa akilni kuwa Haki huenda na wajibu ni kujidanganya. Kwanini hatuangalii Haki nyingine zinazokwenda sambamba na suala hilo kama vile Haki watoto wengine kupata mazingira mazuri ya kujifunza bila vishawishi vya wenzao wenye watoto na pia kwanini hatuangalii kuwa hao watoto wenye watoto wana uwezo gani wa kulea? Je kuwaruhusu kuzaa si aina nyingine ya kuruhusu watoto wa mitaani?
Hawa wazungu wakati mwingine wanatupeleka kusiko. si ndani ya mila na desturi zetu kuwa ni sifa binti kuolewa Akiwa bikra? Sasa kinachopendekezwa kina misingi gani? Kwamba tutakiuka Sheria au protokali zilizowekwa na watu Fulani, ambao Kwa hakika labda zinafaa ktk mazingira yao au wana malengo tofauti.
Sipingi matukio machache ya wanaopata ujauzito Kwa kubakwa , hizi ni kesi ambazo zinasikitisha lakini hazitoshi kuwarejesha hao katika kundi la watoto wetu. Waandaliwe mfumo mwingine wa kuwa saidia.
Nimalizie Kwa kusema kuwa tabia yetu ya kusaliti akili Na dhamira zetu kwa manufaa ya shine ya siku chache itatufikisha siko
 
enoah

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
271
500
Swala la wanafunzi wa kike kubeba ujauzito ni jambo ambalo linapaswa kupigwa vita, elimu ni muhimu kusaidi watoto kujitambua, Ukiwa shabiki wa MTU kila alisemalo kwako litakuwa sawa tu, Nianze na kusema uamuzi wa kuzuia watoto kuendelea na masomo Mara wanapojifungua sio wa busara na hauja tazama kwa maslahi mapana ya taifa, haitozuia watoto kutokupata mimba bali itachochea watoto kutoa mimba na baadae kupelekea vifo kuongezeka taifa litanuka damu tusitegemee mafanikio. Elimu ni jambo la msingi kwa Mtoto wa kike na wa kiume pia hasa kwa taifa maskini na lenye wasomi wachache kama Tanzania. Wakati mwingine watoto wanaendeshwa na foolish age kufikia huko. Namuomba mheshimiwa rais alitafakari upya wanaoathirika ni watoto wa maskini wasiojua hata nini maana ya kutumia uzazi wa mpango
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
37,004
2,000
Mghaibuni mpinzani ameshapinga huko insta.....Anataka watoto wetu wadonyelewe then waende kunyonyeshea class
Katika Watu very ' hopeless ' duniani nadhani huyo ' Mghaibuni Mpinzani ' atakuwa anaongoza Mkuu. Nikushauri tu acha kupoteza muda wako kumsikiliza kwani Yeye kila uchao anachokiweza ni Kujisifia tu kuwa ana Masters Degree lakini kumbe ni Omba Omba wa Kutukuka huko alipo Ng'ambo. Huku Bongo wapo Watu walioshia tu Darasa la Saba lakini wana maisha mazuri na maendeleo hata kumzidi Yeye.

Halafu ukimtizama vizuri na kwa uwezo wa Saikolojia utagundua kuwa hayupo vizuri Psychologically na anahitaji Counseling kubwa sana vinginevyo hayuko mbali na kuwa Mwendawazimu / Mtambo. Kama umegundua siku hizi 99% ya ' taarifa ' zake huwa ni za matango pori ( uwongo tupu ) na Watu wanamlisha makusudi ili azidi ' Kuporomoka ' Kiumaarufu lakini Yeye hata hajishtukii.

Mpeni pole sana Mkuu.
 
areafiftyone

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
7,405
2,000
1.Tuache kuwa Wanafiki

2.NGO’s zisitumie udhaifu wa Watanzania wengi kujineemesha

3.Wazazi tutekeleze majukumu yetu kiukamilifu

4.Tujikite kuwapa Elimu ya Uzazi Watoto ( Mabinti ) zetu

5.Maudhui mengi yasiyo ya Kimaadili hasa kwa Vijana na Mabinti zetu yadhibitiwe

6.Wazazi waache kuwafanya Watoto ( Mabinti ) zao mitaji yao ya kujipatia Mali

7.Jamii ielimishwe sana kuhusu madhara makubwa ya Utandawazi

Binafsi naungana kwa 100% kwa Kauli ya Kimamlaka na ya Kishujaa kabisa aliyoisema Mheshimiwa Rais wa JMT Dkt. John Pombe Joseph Magufuli jana huko Chalinze juu ya kuzuia na kukataa Wanafunzi wa Kike wanaopata Ujauzito wakiwa Shuleni.

Inahitaji umakini mkubwa sana na uwezo mkubwa wa Kutafakari kuweza kumwelewe Mpendwa Rais Dkt. Magufuli juu ya Kauli zake ambazo wengi wetu ‘ hukurupuka ‘ tu na kudhani kuwa ni ‘ dhaifu ‘ au ni ‘ mkatili ‘ au ana roho mbaya.

Namwelewa sana Rais Dkt. Magufuli na kamwe sijutii kumpa Kura yangu ya Kutukuka mwaka 2015 na narudia tena kusema kwa Kujiamini kabisa kuwa kwa muda mrefu sana baada ya Hayati Baba wa Taifa kung’atuka Madarakani sasa Tanzania imempata Rais ambaye pengine ilimuhitaji tokea mwaka 1985 kama siyo mwaka 1995 au 2005.

Kila la kheri Mheshimiwa Rais wangu mpendwa JPM na chapa kazi kwani tunakuamini, tutakuombea na tunakupenda mno.

Nawasilisha.

Mkuu asante kwa bandiko lako.Ni Kweli kwamba ni mtu tu anayefikiri kwa kina anayeweza kuelewa maamuzi ya Rais wetu mpendwa.Ila niseme na kuongeza pia kuwa ni yule tu ambaye ana elewa maana halisi ya huu utitiri wa vi-NGO na jinsi dunia inavyo endeshwa ndiye tu anayeweza kumuelewa vizuri zaidi Rais.The world is not about what you see and here,there is more to it than that!
 
Siyabonga101

JF-Expert Member
Mar 8, 2016
2,430
2,000
Leo umenena Kama mwanasaikolojia mbobezi ulietukuka na kusadikika mkuu. Watakuja mapopoma hapa na kukengeuka kama kawaida yao. Lakini ukweli utasimama na kuwavua nguo upenuni kama zile Voicenotes za Mh. Ayatollah Mboweini.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
37,004
2,000
Leo umenena Kama mwanasaikolojia mbobezi ulietukuka na kusadikika mkuu. Watakuja mapopoma hapa na kukengeuka kama kawaida yao. Lakini ukweli utasimama na kuwavua nguo upenuni kama zile Voicenotes za Mh. Ayatollah Mboweini.
Akhsante na Shukran sana Mkuu. Tupo pamoja. Nimependa mno ulivyojua kuyatumia vizuri maneno ya ' uliyetukuka ' kisha ' mapopoma ' na ukamalizia na ' kukengeuka '.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom