Badala ya JKT wana vyuo wafundishe Mashuleni! Huu ndiyo uzalendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Badala ya JKT wana vyuo wafundishe Mashuleni! Huu ndiyo uzalendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Sep 2, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Badala ya Maafisa wa Jeshi kuweka mipango ya kifisadi ya kutenga pesa kwa JKT Vijana wasomi wanatakiwa kuwa Wazalendo na kupelekwa kufundisha shule zote Tanzania. Kama kweli tunahitaji uzalendo ni elimu na msindi wa maendeleo atakuwa mwenye elimu zaidi!

  Hatuna majirani wanaotafuta vita na Tanzania pesa hiyo ingetumika kuwapa posho vijana wanaomaliza shule na kuweka utaratibu wa hawa vijana kufundisha kwa miezi sita.
   
 2. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Naunga mkono hoja 101%. Naongezea, iwe mwaka mwaka mmoja wa kujitolea, wapewe posho na liwe sharti muhimu la kuajiriwa katika sector nyingine serikalini au kwingineko. Hatutahitaji tena peace corps toka nje shule zote zitapata walimu, Faida ya shule za kata itaonekana.

  Kaka umenena sana. Bunge likikataa tutashangaa sana.

  Kwa hili umefunika bovu. Tanzania ina hitaji wazalendo kama wewe wenye fikra pana na nzito ambazo inahitaji mtu asiwe na uzalendo ili azipinge.

  Wanajamii frm wote naomba tuunge mkono hoja hii na ipelekwe bungeni.

  The best time is the present time.
  Lets duit tanzanians.
   
 3. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Faida ya hili kwa maendeleo ya taifa la leo iko wazi sana kuliko ya watu kujitolea JKT.

  Ikiwezekana vyeti vizuilwe mpka wamalize mkataba wa mwaka mmoja kujitolea mashuleni.

  Badala ya kupeleka rasilmali kuanzisha JKT, rasilimali hizo zielekezwe kwenye miundo mbinu ya shule zetu zote, maabara, nyumba za walimu,vitabu,magari nk.
  Tutapiga hatua kubwa ya ajabu katika elimu na ajira.
   
 4. B

  Balozi Chriss Senior Member

  #4
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja.....Peace corp ni wapelelezi wale,bora tujipeleleze wenyewe...
  Ila kwa mwendo wa kuhongana sutu kweli wazo lako watalitilia maanani?
   
 5. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wakuu hii ishu ni nzuri sana, mimi mwakajana baada ya kumaliza chuo niloorganize wana vyuo mbalimbali na nilipata dadi ya wanafunzi kama 200 hivi na wao waliomba wapewe hela ya chakula nauli na nyumba na baada wanapoondoka wapewe token of thanks walimu wakuu walikiubali kutoa chakula, nyumba na token ila nikaomba wapewe na nauli za kwenda na kurudi kituo atachopangiwa kutoka chuo anachosoma nikawaomba baadhi ya wabunge wafadhili hii kwa kweli ilishindikana nikawanapigwa kiswahili mpaka tukakata tamaa.

  Wakuu wa shule walikiubali kutoa token of thanks amount yake unknown but doesn't matter. Issue ikawa nauli. Wanafunzi wengi sana wa vyuo wanapenda sana kujitolea ila hawapati support kutoka kwa viongozi wao wa nchi. Bila shaka mnajua tunapomaliza mihula tunakuwa tunapigika sana na ingekubali nilipanga iwe endelevu na target ilikuwa ni shule za kata.

  Labda tuanzishe nguvu kazi kutoka hum jf ili kuwasaidia wadogo zetu Taifa letu linazidi kupoteza mwelekeo kweli kielimu.

  Nawasilisha
   
 6. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati nikiingia JF huwa natoka na raha mikno mfukoni na kamluzi ka mbaali. Naunga mkono hoja. Great thinkers! Hii iwe kauli mbiu ya siku ya vijana Tanzania.

  Kwa wale waliopitia JKT miaka hiyo kulikuwa na udhalilishaji wa kutosha hasa kwa dada zetu. Hil mkubali ama mkatae lakini wahanga wapo watashuhudia. Vijana wanaweza kutatua tatizo hili na pia naamini kuwa katika kila kata kuna wasomi wa vyuo mbalimbali hii nayo itapunguza gharama maana watahudumia watu wa kwao na kuinua kiwango cha ufaulu wa mtaa wao.

  Nyumbani ni nyumbani tu.
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri ila linahitaji upembuzi yakinifu, maana si wote wanaomaliza kidato cha sita wanaweza kuwa walimu. Tusipoangalia tutakuwa tunapeleka manyang'au wa ngono kwenye shule zetu na kutuharibia watoto wetu wa kike mashuleni.

  Kufundisha kuahitaji maandalizi ya kitaaluma na kimaadili kama kweli tunahitaji kukuza elimu. Binafsi sioni kama hili wazo lina tija kwa sababu zifuatazo
  1. Ili mtu aweze kufundisha mwenzake anatakiwa kuwa na taaluma ya anachokifundisha au awe na uwezo kujisomea kuelewa na kuwa na uwezo wa kumuelekeza mwanafunzi. Wanafuzi wengi wa kidato cha sita wanakuwa wamejikita zaidi kwenye masomo ya A-level ili kufaulu mitihani yao na hivyo kujikuta elimu ya O-level wakiipa kisogo kwa miaka yao yote ya A-level. Mtu huyu kumrudisha kufundisha O-level itahitaji awe na uwezo wa ziada kujikumbusha yale aliyoyaacha O-level kwa muda mfupi.
  2. Unapompeleka Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita ambaye bado ana element za uanafunzi, kwa wale tuliopitia shule za mchanganyiko na single sex at different stages tunajua nini kitaendelea kama mtoto wa kiumeunampatia darasa lenye watoto wa kike kufundisha. Unakuwa unawa-expose watoto wa kike kwenye hatari ya kujiingiza kwenye mapenzi na walimu watoto wa kiume
  3. Je unawapeleka kufundisha baada ya matokeo yao ya kidato cha sita kutoka au kabla?, Je matokeo yakitoka na kukuta mwalimu mtoto amepata daraja la sifuri wakati alikuwa anawafundisha watoto yale anayodhani ni sahihi kumbe uwongo huoni atakuwa amerudisha nyuma elimu?
  Mi nafikiri wanafunzi wa kidato cha sita wapelekwe sehemu watakazofanya kazi ambazo si za kitaaluma wakati wakisubiri matokeo yao,kazi ya taaluma inahitaji kuwaandaa si kazi ya kumpa mtu kama anapiga debe au akajaze nafasi iliyo wazi ya kufundisha hata kama anafundisha upupu.

  Ni kweli kabisa kuna baadhi ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita ni wazuri sana na wanapofundisha shule wanaeleweka sana kwa peer wenzao ila hawa ni wachache na huwezi kuchagua hawa na kuwaache wengine kama lengo ni kuwapatia wanafunzi waliomaliza kidato cha sita nafasi za kufundisha.

  Unless uniambie kuwa uwe unafanyika usaili wa kuwatambua walio wazuri ambao wapo ila je gharama za kufanya hivyo na kuwapeleka JKT zipi zinazidi?.
   
 8. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Nadhani mtoa mada amesema ni wanaomaliza vyuo, hawa wamepevuka sana na wakipata semina elekezi ya wiki moja katika centers watakazo pangiwa wanaweza kufundisha masomo ya sekondari bila mashaka yoyote. Ni utaratibu na nia ya serikali tu. Kila graduate atapangiwa masomo yanyoendana na field yake.

  Engineer-fizikia,hesabu,ufundi nk

  Daktari- biologia,kemia nk
  nk nk nk nk nk.

  Tutapiga hatua.
   
 9. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tanzania inabidi tuache sera za kinafiki kama hii ya mikopo. Hakuna Mtanzania hata JK ambaye amelipa deni lake la shule lakini kila siku tunaita mikopo!!. Kwasababu ya wazi kwamba wana vyuo wengi hawatalipa pesa ya mikopo na JKT si nzuri kwa wakati huu mgumu wana vyuo wote waliopata mikopo ya vyuo wafundishe. Hata kama wasipolipa madeni watakuwa wamewekeza kwa wadogo zao. Korea ya kusini wanaita walimu national builders kwasababu ushindani mkubwa wa sasa duniani ni wa technologia na si vita. Tanzania haiwezi kuendelea kama haitafikiria kisasa
   
 10. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  Angeanza kwanza ridhiwani kufundisha, halafu wanachuo wengine wafuate.
   
 11. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  SIAMINI KAMA UMESOMA HOJA YA MWANAJANVI,wewe unasema form six, yeye kasema waitimu wa vyuo au hii ni hoja yako mupya?
   
 12. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Naunga hoja kwa mikono miwili bwe duh.Ndugu zangu tatizo la kutokuwepo walimu wakutosha Tanganyika unawezekana kabisa kama watawala watakuwa makini.Angalia ili la TP vyuo vyote wanafanya kitu hicho wakati mmoja kitu ambacho kinafanya walimu wa TP kurundika kama utitiri,mfano shule inapokea walimu wanafunzi 49 alafu wanaondoka wote kwa pamoja.Inatia kinyaa mpaka mtu anapewa stream moja afundishe hv kweli inaingia akili?Pili vyuo vingi vinawapangia walimu wa TP mjini tu na kuacha shule za vijijini bila kupata walimu alafu wakitoa ajira wanawapanga watu vijijini mwisho watu hawaendi serukali inaanza kulaum kuwa walimu wanakimbia vituo vya kazi wanasahau kuwa wanasababisha wenyewe kwani wakati wa field hawapelekwi huko ili wayazoee mazingira ya huko.Yote yawezekana kufanya lkn hawa nyinyiemu hawawezi fanya kitu hiyo,lets wait till 2015.
   
Loading...