Badala ya wahitimu kupelekwa JKT wapelekwe VETA

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
Na Gaspary Charles

SERIKALI imekuwa ikitumia gharama nyingi sana kuwapeleka wahitimu wa kidato cha VI kila mwaka kujiunga na mafunzo ya muda mfupi kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini ukiangalia kwa jicho la ziada ni kama mpango huu licha ya nia yake njema kuwafundisha uzalendo vijana dhidi ya taifa letu lakini pengine mpango huu haujawa na matokeo mazuri kwa vijana wengi kutokana na mazingira ya sasa.

Ikumbukwe tupo katika nyakati ambazo Ujasusi wa Kiuchumi umeshika hatamu na kushikilia mizizi yote ya Dunia ambapo ili uweze kumudu mapambano yake taifa halihitaji tu kuwa na idadi kubwa ya vijana Wazalendo bali idadi kubwa ya vijana wenye uwezo mkubwa kiujuzi na kielimu ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili na kuzigeuza kuwa fursa kwaajili ya kukuza uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.

Ili kuweza kufikia huko dunia nzima inapambana kuhuisha mifumo ya elimu kwa kuifanya kuwa ni elimu saidizi kwa taifa kupitia kuwekeza zaidi kwenye ujuzi ili vijana waweze kukabili kasi ya dunia na kuondokana na elimu tegemezi.

Wakati ambapo wadau wa elimu wanahanikiza mabadiliko ya mtaala wetu wa elimu, ni muhimu suala la UJUZI kupewa kipaumbele zaidi katika mifumo yetu ya elimu ili kuweka fursa kwa taifa kuwa na idadi kubwa ya vijana wenye UJUZI kisha ELIMU ambapo kwa pamoja vitasaidia kupunguza mzigo kwa serikali dhidi ya wimbi kubwa la wahitimu tegemezi.

Ukisikiliza hoja za wanaohitaji mabadiliko ya mtaala wa elimu nchini wanadai mfumo wa elimu tulionao hauandai vijana KIUJUZI na kuwa na uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya soko la dunia badala yake ni elimu inayojenga vijana wasomi tegemezi kwa serikali bila kuwa na uwezo mbadala.

Bahati mbaya sana baada ya vijana kuhitimu wanaporudi mtaani hukutana na hali tofauti ya walichojifunza na wanapopata shida ya kukabiliana na mahitaji ya soko la dunia, lawama zote zinaelekezwa kwao kama mizigo isiyokuwa na uwezo wa kuziona fursa zilizopo huku tukisahau kwamba tatizo linaanzia kwenye mfumo wetu.

Badala ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kupelekwa JKT ni bora ukawekwa mpango ambao utalazimisha wahitimu wote Kidato cha IV & VI kabla ya kuendelea na ngazi nyingine ya elimu wajiunge kwanza kozi fupi kwenye vyuo vya UFUNDI ili wapate ujuzi kulingana na mahitaji yao.

Hii itasaidia kujenga taifa imara lenye vijana walio na UJUZI, MAARIFA na UWEZO wa kukabiliana na changamoto za kijamii hata baada ya kuhitimu vyuo na baada ya muda litapunguza sana kelele za sasa kwa serikali kubeba mzigo wa ajira kwa kila msomi.

Wasalaam,
#GMdadisi
 
VETA ina replace vipi malengo ya JKT, kwani kuna kijana anazuiwa kwenda VETA kupata ujuzi anaouhitaji?
 
Lengo la kupitia jkt ni kupunguza migomo ya vyuo vikuu ndo maana unasikia siku hizi watu hawagomi mwanajeshi hagomi akigoma anapewa adhabu za kijeshi
 
Wangepunguza muda wa JKT wawapeleke kwenye vyuo wasome Utalii ambao kila sehemu pana mbuga au Kilimo kuliko kuhangaika na hayo mambo wanakua wakakamavu ila hawana mbinu za kukabiliana na maisha...adui yetu ni umasikini bado mnawafundisha ulinzi ili waje walinde vyuo badala ya kuwafanya waongeze uzalishaji...
 
Na Gaspary Charles

SERIKALI imekuwa ikitumia gharama nyingi sana kuwapeleka wahitimu wa kidato cha VI kila mwaka kujiunga na mafunzo ya muda mfupi kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini ukiangalia kwa jicho la ziada ni kama mpango huu licha ya nia yake njema kuwafundisha uzalendo vijana dhidi ya taifa letu lakini pengine mpango huu haujawa na matokeo mazuri kwa vijana wengi kutokana na mazingira ya sasa.

Ikumbukwe tupo katika nyakati ambazo Ujasusi wa Kiuchumi umeshika hatamu na kushikilia mizizi yote ya Dunia ambapo ili uweze kumudu mapambano yake taifa halihitaji tu kuwa na idadi kubwa ya vijana Wazalendo bali idadi kubwa ya vijana wenye uwezo mkubwa kiujuzi na kielimu ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili na kuzigeuza kuwa fursa kwaajili ya kukuza uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.

Ili kuweza kufikia huko dunia nzima inapambana kuhuisha mifumo ya elimu kwa kuifanya kuwa ni elimu saidizi kwa taifa kupitia kuwekeza zaidi kwenye ujuzi ili vijana waweze kukabili kasi ya dunia na kuondokana na elimu tegemezi.

Wakati ambapo wadau wa elimu wanahanikiza mabadiliko ya mtaala wetu wa elimu, ni muhimu suala la UJUZI kupewa kipaumbele zaidi katika mifumo yetu ya elimu ili kuweka fursa kwa taifa kuwa na idadi kubwa ya vijana wenye UJUZI kisha ELIMU ambapo kwa pamoja vitasaidia kupunguza mzigo kwa serikali dhidi ya wimbi kubwa la wahitimu tegemezi.

Ukisikiliza hoja za wanaohitaji mabadiliko ya mtaala wa elimu nchini wanadai mfumo wa elimu tulionao hauandai vijana KIUJUZI na kuwa na uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya soko la dunia badala yake ni elimu inayojenga vijana wasomi tegemezi kwa serikali bila kuwa na uwezo mbadala.

Bahati mbaya sana baada ya vijana kuhitimu wanaporudi mtaani hukutana na hali tofauti ya walichojifunza na wanapopata shida ya kukabiliana na mahitaji ya soko la dunia, lawama zote zinaelekezwa kwao kama mizigo isiyokuwa na uwezo wa kuziona fursa zilizopo huku tukisahau kwamba tatizo linaanzia kwenye mfumo wetu.

Badala ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita kupelekwa JKT ni bora ukawekwa mpango ambao utalazimisha wahitimu wote Kidato cha IV & VI kabla ya kuendelea na ngazi nyingine ya elimu wajiunge kwanza kozi fupi kwenye vyuo vya UFUNDI ili wapate ujuzi kulingana na mahitaji yao.

Hii itasaidia kujenga taifa imara lenye vijana walio na UJUZI, MAARIFA na UWEZO wa kukabiliana na changamoto za kijamii hata baada ya kuhitimu vyuo na baada ya muda litapunguza sana kelele za sasa kwa serikali kubeba mzigo wa ajira kwa kila msomi.

Wasalaam,
#GMdadisi
Sema mtaala wa JKT uhusishe mafunzo ya ujuzi pia
 
Back
Top Bottom