Badala wanasiasa wawaze kuongeza miundombinu ya Afya na elimu wanawaza kugawana majimbo; shame

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
891
4,154
Wezi WA Kura mara nyingi wanakuwa wabinafsi, wanategemea kubebwa Ndipo waishi. Wapo radhi kuua ili wapate madaraka. Wapo radhi wawafunge wapinzani wao wanaokubalika ili wao wapite Bila kupingwa.

Alichofanya Gambo na Tulia nikuonyesha kile wanachofikia walafi WA madaraka kwenye majimbo yenye wananchi wengi wanaokubaliana na mawazo kinzani.

Kauli kama hii yaweza tolewa kwenye Jimbo la Kawe, Ubungo, Kinondoni, Kigoma, Hai, Majimbo ya Mtwara nk...lengo niwatu wasio na sifa wapate njia rahisi yakutawqla.

Lakini pia hii inatokana na ukweli kwamba hakuna vigezo vinavyoweza kutazamwa kwenye ugawaji wa majimbo; mwanasiasa akijisikia tayari anaamua na tume inatekeleza.

Mwisho, wabunge pamoja na fedha nyingi wanazolipwa hakuna anayewaza wananchi, wanawaza uchaguzi na gharama hata ziwe kubwa kiasi gani kwao siyo tatizo. Tuwaepuke walafi
 
Ndio hasa "legacy" ya Mwendazake.

Kama nchi sasa ndio tunavuna alichotupandia kwa miaka yake 5!

Sadly, na bado kuna mengi tu yanatugharimu leo na pengine kesho.
 
Back
Top Bottom